Ruby yenye thamani ya bil 276 ilisafirishwa kimagendo huko Dubai? Serikali haina taarifa ilifikaje

Serikali imelala usingizi mali mpaka inafika nchini dubai Serikali haina habari? Ama kweli Serikali ya Mama Samia ilikuwa imelala usingizi fofofof.Waziri wa Madini, Hafai kuongoza Wizara ya madini itabidi atumbuliwe na kupelekwa Mahakaman.



Download
720
 
Kufika siyo hoja kubwa, suala ni wachimbaji wazawa na serikali kujua thamani ya madini.

Elimu hii ni adimu na muhimu sana inatakiwa wachimbaji wazawa na watu wote waliopo ktk mnyororo wa madini yanapopita kuifahamu vyema na ndipo nchi na mwenye mgodi atapata value for money "halali" ya soko la dunia katika kila hatua ya soko.

SimuJanja, vituo vya televisheni kama TBC kurusha vipindi maalum vinavyozungumzia sekta ya madini aina za madini, uchimbaji , kuongeza thamani na bei za soko la dunia kila baada ya saa 24 n.k vingeongeza uelewa wa wachimbaji, wauza na wanunuzi wa ndani thamani ya Vito hivyo na hivyo kama somo la uraia wananchi wangeelewa umuhimu na thamani ya madini mbalimbali bila kusahau kujipatia faida sahihi ya soko.
Mzungu hawezi ruhusu hii kitu bwashee...tupate uelewa kwenye madini ili tuanze kusumbua tena.
 

Rare 8,400 carat rough ruby lands in Dubai for auction, estimated at $120 million​

Tala Michel Issa, Al Arabiya English​

Published: 12 April ,2022: 11:54 AM GSTUpdated: 12 April ,2022: 12:02 PM GST
One of the world’s biggest rough rubies has landed in Dubai to mark the launch of the new Callisto Collection by SJ Gold and Diamond, the Swiss firm said in a statement on Tuesday.

The rough Ruby, mined from the Central Tanzanian village of Winza, Mpwapwa Dodoma will make its first public appearance in the market at the Waldorf Astoria in Dubai Financial Center (DIFC) on Friday.

SJ Gold and Diamond, established in Dubai since 2017, will display the record-breaking rough ruby gem called ‘Burj al-Hamal,’ or ‘Aries’ in English.

After the holy month of Ramadan, the Ruby will be auctioned off to buyers in the United Arab Emirates. The rare gem has been estimated to go for a minimum of $120 million.

Weighing in at a whopping 8,400 carats and 2.8 kilograms in weight, the Burj al-Hamal will be unveiled by the event’s guest of honor and the renowned Hollywood actor, Tamer Hassan.

“The launch of the Callisto collection in Dubai represents a groundbreaking moment for the company in its journey to becoming one of the world's leading Metal and Mineral Asset Management Firm, managing a total of 4 billion dollars in assets, ranging from exclusive gemstones and gold,” said SJ Gold and Diamond Managing Director Patrick Pilati.

“This is the first time we are introducing our crown jewel of the collection. Unveiling this one-of-a-kind stone to the public for bidding, is a clear continuation of our dedication to showcasing the best of the best in the UAE,” added Pilati.

The Callisto collection, named after the famous Arcadian Nymph of Greek Mythology, includes millions worth of hand-picked white and yellow cut and uncut diamonds along with the 12 unique rubies, weighing 236,000 carats.

Each rough ruby, coming in diverse sizes, will be featured in the Callisto collection’s logo, tethered together with gold lines to form the collection’s very own constellation

Source : Rare 8,400 carat rough ruby lands in Dubai for auction, estimated at $120 million
The rough Ruby, mined from the Central Tanzanian village of Winza, Mpwapwa Dodoma
 
April 20, 2022

WATATU MBARONI KWA TUHUMA ZA KUTOROSHA MADINI​




Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila akizungumza na waandishi wa Habari namna walivyojipanga kudhibiti utoroshaji wa madini mkoani humo.

Na Costantine Mathias, Simiyu.

WATU watatu wamekamatwa kwa tuhuma za utoroshaji wa madini ya dhahabu katika wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu yenye uzito wa gramu 10, huku Mkuu wa mkoa huo David Kafulila akivitaka vyombo vya Ulinzi na Usalama kuimarisha ulinzi maeneo ya migodi.

Kafulila amewataka Idara ya Madini kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi na kufanya ukaguzi maalumu kwenye migodi yote mkoani humo kwa kuwakamata wote wanaojihusisha na utoroshaji wa madini

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo jana (aprili 19, 2022) wakati akiongea Jeshi la Polisi pamoja na Waandishi wa habari, katika kituo cha polisi Bariadi mara baada ya kuwahoji watuhumiwa waliotorosha madini katika mgodi wa Dutwa uliopo Bariadi.

‘’Najua nyie mmetangulizwa, nawatafuta walioko nyuma yenu, mkiwataja mtapata nafuu na msipowataja mtakuwa kafara…watajeni watu wanaowatuma katika mambo hayo, RPC hakikisheni mnafanya ukaguzi maalumu na naamini vyombo mnajua jinsi ya kufanya’’ alisema Kafulila na kuongeza.

"Hawa ambao wamekamatwa tunataka waione rangi ya Rais Samia, kamateni wote kwa sababu hatuwezi kuruhusu hiyo mianya iweze kuwepo, vikosi kazi vilivyoundwa na watu wa usalama hakikisheni mnazibadilisha’’ alisema.

Kwa upande wake Ofisa Madini Mkoa wa Simiyu Mhandisi Amini Msuya alisema walikamata gramu 10.4 mbichi, baada ya kuchomwa zilibaki gramu 7 ambazo zilikuwa hazieleweki zinakoelekea na kwamba watu hao walikamatwa kwa taarifa za kusafirisha dhahabu hizo kwenda nchini Kenya.
Alisema wanashirikiana na vyombo vya usalama kuhakikisha wanafanya uchunguzi kwa watu hao ili kupata mtandao wa utoroshaji wa dhahabu kwa lengo la kuuvunja mtandao huo na pia wanatoa elimu kwa wafanya biashara waweze kufuata taratibu za biashara ya madini

"Tunafanya uchunguzi kwa watu hawa ili waweze kutupa taarifa, kwa sasa bado ni washukiwa na lengo kubwa ni kuuvunja mtandao katika mkoa wa Simiyu….tunatoa elimu na vikao mbalimbali na wafanyabiashara dhahabu, wafanye biashara katika masoko ya dhahabu ili tuone mwenendo wa soko la dhahabu’’ alisema Mhandisi Msuya.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa polisi Shadrack Majisa alisema jeshi la polisi liko tayari kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kudhibiti utoroshaji wa madini na kwamba wataendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo ya migodi.

Awali Yunis Masuke (ambaye ni mtuhumiwa wa utoroshaji wa dhahabu) alisema yeye ni msimamizi wa mwalo na kwamba alikamatwa kwa tuhuma za kuuza dhahabu grami 10.4 kwa Prisca Seni ambaye naye pia ameshakamatwa.

Naye Gamaya Makoye mlinzi wa mgodi wa EMJ alisema alikamatwa baada ya Yunisi Masuke na Prisca Seni kuuziana dhahabu huku yeye akiwa ni mlinzi wa eneo hilo.

Ofisi ya Madini kwa kushirikina na vyombo vya Ulinzi na Usalama, vinawashikilia Yunis Makoye, Prisca Seni pamoja na Gamaya Makoye wakishukiwa kutorosha au kuuziana dhahabu yenye uzito wa gramu 10 kinyume cha sheria ya madini.
 
Ukipata mchongo piga haya mambo ya wanasiasa tunadanganyana hata uwaulize sa hz watoto wao na mambo yao mengi wanafanyia nje Kwa sababu wao ndio kundi la kwanza linaloongoza kwa kujinufaisha na rasilimali za Nchi huu sio Uungwana hata kidogo

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Kilo moja ya rubby inauzwa TZS billion 657

CONVERSION OF CARAT TO GRAMS

1 carat = 0.20 grams
Therefore 8400 carats -=420 grams= 0.42 kg

Hii rubby haifiki hata nusu kilo, lakini bei yake ni billion 276. Kwa hiyo kilo moja ya rubby inauzwa billion 657
 
Mbona bado, chini ya huyu Mmakunduchi nchi italiwa mpaka basi
Amalizie kipindi chake cha mpito atoke zake huko, huu upuuzi ukilelewa utatuletea hasara kubwa. Tatizo la kuwapa uongozi watu majizi ndio matokeo yake hayo. Nonsense
 
The rough Ruby, mined from the Central Tanzanian village of Winza, Mpwapwa Dodoma will make its first public appearance in the market at the Waldorf Astoria in Dubai Financial Center (DIFC) on Friday.

Halafu kila kukicha tuko ughaibuni kuomba misaada, aibu ya karne
 
Kilo moja ya rubby inauzwa TZS billion 657

CONVERSION OF CARAT TO GRAMS

1 carat = 0.20 grams
Therefore 8400 carats -=420 grams= 0.42 kg

Hii rubby haifiki hata nusu kilo, lakini bei yake ni billion 276. Kwa hiyo kilo moja ya rubby inauzwa billion 657
Mbona wanasema ina kilo 2.8?
 
Amalizie kipindi chake cha mpito atoke zake huko, huu upuuzi ukilelewa utatuletea hasara kubwa. Tatizo la kuwapa uongozi watu majizi ndio matokeo yake hayo. Nonsense
Kwani imeshathibitika kuwa imekwenda huko kipindi yeye akiwa madarakani?
 
Mbona hii ajabu sasa, madini ya pesa ndefu kama hii yalichimbwa hapa nchini kwetu na kusafirishwa Dubai


24 April 2022

SAKATA LA RUBY DUBAI, BITEKO AJIBU - "YAPO MAWE MENGINE 25, WATANZANIA WANA HAKI YA KUWA NA HASIRA"



Waziri wa Madini Doto Baada ya Kufatilia Jiwe Moja La Ruby Linalotalajiwa Kupigwa Mnada baada ya Ramadhan, Amesema Imegundulika Kuna Mawe Mangine ya Madini Tofauti 25 Yapo Marekani ......

Source : Global TV online
 
29 April 2022
Bungeni
Dodoma, Tanzania

MBUNGE KISHIMBA AIBUKA NA HOJA YA BEI YA DHAHABU NA VITA YA UKRAINE NA URUSI




Mbunge Jumanne Kishimba atoa elimu ya madini bungeni leo ili serikali na maofisa wote wapate ufahamu juu ya soko la dunia la madini linajiendesha vipi
 
Back
Top Bottom