Rubani wa ndege ya ATC No. TC103 airudisha ndege parking baada ya kuhisi tatizo kwenye runway

From Sir With Love

JF-Expert Member
Sep 13, 2010
2,076
3,797
Kwanza nitoe pongezi kubwa sana kwa rubani wa ndege ya ATC No. TC103. Huyu rubani mzungu ameonesha yeye sio risk taker. Hii ndege imeshindwa kutake off mara mbili na akaamua kuirudisha kwenye parking ili aweze kufahamu tatizo.

Hii ndege ilikuwa iondoke hapa Mwanza saa nne kasoro usiku huu wa tarehe 20/03/2019 na ilitakiwa kufika Dar saa tano kasoro usiku.

Hongera Rubani kwa kuligundua tatizo mapema.

Kunradhi naandika kama nakimbizwa.

............................................................................................................................................
UPDATE:
10:36 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu naye imebidi ashuke kama abiria wengine.

.........................................................................................................................................
UPDATE:
23:00 Tukaruhusiwa kuingia kwenye ndege tena. Kuna baadhi ya abiria walikataa kuendelea na safari na hivyo ikabidi mizigo yao ishushwe.

23:05 Rubani mkuu Captain Graham alituhakikishia kwamba hakutaka kupaa akidhani kuna tatizo. Alituhakikishia asilimia mia moja kwamba tatizo lililokuwepo lilihusu sensor na tatizo limetatuliwa.

23:26 Tukaondoka Mwanza airport kuelekea Dar.

00:43 Tukatua Dar na kuelekea majumbani.

Nimshukuru Mungu muumba Mbingu na Nchi kwa utukufu wake. Namshukuru pia Captain Graham na wafanyakazi wote wa ndege kwa kuwa makini.

ATCL idumu, Rais John Pombe Magufuli piga kazi ila liache fao la kujitoa kwenye ajira liwepo.
 
Kwanza nitoe pongezi kubwa sana kwa rubani wa ndege ya ATC .TC103. Huyu rubani mzungu ameonesha yeye sio risk taker. Hii ndege imeshindwa kutake off mara mbili na akaamua kuirudisha kwenye parking ili aweze kufahamu tatizo.

Hii ndege ilikuwa iondoke hapa Mwanza saa nne kasoro usiku huu wa tarehe 20/03/2019 na ilitakiwa kufika Dar saa tano kasoro usiku.

Hongera Rubani kwa kuligundua tatizo mapema.

Kunradhi naandika kama nakimbizwa.
Kwan bado ina suka mzungu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom