Rubani huzingatia sana kitu kinachoitwa flight plan kabla hajarusha ndege

Boeing 757

JF-Expert Member
May 18, 2020
288
612
Upangaji wa ndege (flight plan) ni mchakato wa kutengeneza mpango wa ambao rubani anaufuata kuelezea safari ya ndege inayopendekezwa kufanyika ni vitu izingatie ili kufanikisha safari nzima kutoka point A kuelekea pint B.

Inajumuisha mambo mawili muhimu ya usalama: hesabu ya mafuta ambayo rubani atatumia katika safari nzima, Hii ni kuhakikisha kuwa ndege inaweza kufikia tuseme kutoka dar kwenda mwanza iweze kufika salama, pili ni kufuata mahitaji ya udhibiti wa usalama za anga , ili kupunguza hatari ya mgongano na ndege nyingine zinazopitia karibu na route iliyopendekezwa ifuatwe siku hiyo.

Kwa kuongezea, wapangaji wa safari za ndege ambao hujulikana kama flight dispatcher kawaida hupanga safari za ndege hutamani kupunguza gharama ya kuruka kwa ndege kupitia chaguo sahihi la njia, urefu njia husika, na kasi ambayo ndege itakimbia, na kwa kupakia kiasi cha mafuta yatakayotumika kwenye safari husika.

Kingine kinachozingatiwa katika mpangilio wa safari za ndege ni kitu kinaitwa Huduma za Trafiki Hewa (Air Terminal Service) hizi ni taratibu za kiusalama zinazotumia mpango uliokamilika wa safari husika wa ndege ili kuweza kutenganisha ndege na ndege zinazoruka angani. Pia katika huduma za usimamizi wa safari za ndege, ATS inahusika katika kufuatilia na kupata ndege iliyopotea, wakati wa misheni ya utaftaji na uokoaji (Search And Rescue).

Upangaji wa safari ya ndege unahitaji utabiri sahihi wa hali ya hewa wa siku husika ili mahesabu ya matumizi ya mafuta yaweze kuhesabika na athari za matumizi ya mafuta katika siku ambayo hali ya hewa ni joto sana ,baridi au kuna upepo ambao unabadilisha mwelekeo ukivuma.

Kumbuka kuwa Sheria za usalama za usafiri wa anga zinahitaji ndege kubeba mafuta zaidi ya kiwango kinachohitajika kuruka kutoka pointi A kwenda pointi B, Hii Ni kwa sababu hali siyotarajiwa inayoweza kujitokeza wakati wa safari angani ndege kuahirisha kule inakoelekea na kugeukia uwanja mwingine wa ndege ambao utatumika kama alternative .

Kwa mfano mpangilio wa safari kutoka dar kwenda mwanza uwanja wa dharura kutua ni Kilimanjaro ikiwa ndege hiyo imeleta shida angani hivyo lazima ndege iwe imebeba mafuta ya ziada kuweza kuifikisha Kilimanjaro.

Kwa kuongezea, chini ya usimamizi wa udhibiti wa ndege, ndege zinazoruka kwenye anga iliyodhibitiwa lazima zifuate njia zilizopangwa zinazojulikana hata kama njia hizo ni refu kama vile ndege zinazofanya safari ya moja kwa moja.

Kwa mfano ndege ya abiria inayoruka kutoka dar kwenda Dodoma haiwezi kuruka anga ya maeneo ya kambi ya jeshi Hapo Morogoro (nimesahau jina kidogo ya hiyo kambi ya jeshi) kwa sababu anga hilo limedhibitiwa na mamlaka ya air defence ya jeshi.

Ndege lazima izunguke kama inaenda Kilimanjaro au mwanza halafu ikifika tuseme maeneo ya anga ya tanga ndio inabadilisha mwelekeo na kuenda Dodoma.

Na pia ndege zinazoruka Ndani ya njia moja , lazima kuwe na mwinuko fulani kawaida hutengwa kwa wima na 1,000 au 2000 ft (300 au 610 m), kulingana na njia inayosafirishwa na mwelekeo wa kusafiri ili kupunguza uwezekano wa kugongana angani.

Kwa mfano kama barabara ya one way ambao magari yanaelekea uelekeo mmoja lazima kuna umbali wa gari na gari lazima yaweze kuachana ili kupunguza uwezekano wa kukwanguana au kugongana.

Pia Wakati ndege zilizo na injini mbili tu zinaruka umbali mrefu kupita maeneo ya bahari, jangwa, au maeneo mengine bila uwanja wa ndege, zinapaswa kutimiza sheria za usalama zijulikanazo ETOPS (extended range for twin engine operating standards) zaidi kuhakikisha zinaweza kufikia uwanja wa ndege wa dharura ikiwa injini moja itashindwa kufanya kazi.

Hivyo basi katika Kutengeneza mpango mzima na sahihi wa kuruka kwa ndege kunahitaji mamilioni ya mahesabu, kwa hivyo, mifumo ya kupanga safari za ndege hufanya matumizi kwa kompyuta ili kurahisisha mambo.

Hivyo usione safari ya ndege inaanza , kuna vitu vingi sana huzingatiwa ili kuiwezesha safari iwe salama sana NA NI LAZIMA RUBANI AUFUATE MPANGO HUU ILI SAFARI IWE SALAMA.

Mniwie radhi kwenye uandishi kama sijaeleweka.

Na pia kama sipo sahihi sehemu ni haki yako kunirekebisha na pia mwenye kuongezea nyama ni vizuri maana JF ni sehemu ya kujifunza.
 
Kwenye ndege ni flight plane, na upande wa meli kuna Voyage Plan. Hii uandaliwa kabla ya safari kuanza na utoa mchanganuo wa wapi chombo kitapita,usimamizi wakati wa safari mpaka kufika bandari nyingine.
 
Maendeleo ya Teknolojia yamefanya flight plan kupangwa na mfumo. Rubani anabaki Kama picha tu. Imefikia hatua hizi commercial flights zinaruka (na abiria ndani) bila rubani na zinatua salama tu (Pilotless flight tech). Hii Fourth Industrial Revolution inakuja Kasi, wale waajiriwa mjiandae.
 
Haupo sahihi asilimia 100 kwa sababu wataalamu wa maswala ya usafiri wa anga walishapropse kutengeneza ndege isio na rubani kwa ajili ya kusafirisha abiria.. lakini wakaja ku hitimisha wakaona hakuna abiria angepanda chombo ambacho kinaendeshwa kwa mfumo wa computer pasipo intervention ya mwanadamu...
 
Ndani ya Mada, kazi ya flight operator ni ipi,? mtalaam unaweza kunipa mwongozo hapa.
 
Lakini Teknolojia ipo tayari
 
Yes, na ndege za masafamarefu mara nyingi zikiwa hewani marubani uwa wanalala lakini abiria hawaambiwi, rubani wanaitajika zaidi kwenye landing na take off ndege ikiwa angani hawahitajiki sana.
 
Ndani ya Mada, kazi ya flight operator ni ipi,? mtalaam unaweza kunipa mwongozo hapa.
Flight dispatcher officers ndio hao wana fanya plan ya Safar, Kuna buggage handlers hawa ni wale wanaohusika na upangaji wa mizigo na mabegi ya abiria Kuna cargo master huyu anahusika na kuhakikisha mzigo umekidhi vigezo na pia umefungwa vizuri ndani ya ndege ya mzigo kabla ya kuruka. Pia kuna food and catering people hawa ndio wale wanaohusika na maswala ya kuhudumia mashirika ya ndege vyakula kwa ajili ya abiria wakiwa safarini.... Na wengine wengi tu kwa hiyo hawa kwa pamoja ni FLIGHT OPERATORS
 
Yes, na ndege za masafamarefu mara nyingi zikiwa hewani marubani uwa wanalala lakini abiria hawaambiwi, rubani wanaitajika zaidi kwenye landing na take off ndege ikiwa angani hawahitajiki sana.
Ndioilivyo Yaani.
 
Back
Top Bottom