Rubani Anapowaambia Abiria Anzeni Kusali..

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20




Utafanyaje kama ukiwa kwenye ndege halafu rubani anawatangazia ndege imepata hitilafu angani na kisha kuwataka muanze kusali.

Huku akiwa na wasiwasi wa kutua salama kwa dharura, rubani wa ndege aina ya Boeing ya shirika la ndege la Iran la Aseman Airlines aliwaambia abiria wake kuwa ndege hiyo imepata hitilafu na abiria waanze kusali sala za mwisho.

Ndege hiyo ilikuwa imepaa toka uwanja wa ndege wa Tehran na ililazimika kugeuza na kurudi uwanjani hapo baada ya dakika 45 angani.

Zengwe la ndege hiyo lilianza hata kabla ya ndege hiyo kupaa wakati safari ya ndege hiyo ilipochelewa kwa takribani masaa sita kutokana na hitilafu kwenye ndege hiyo.

"Rubani aliwatangazia abiria, ndege imepata hitilafu na inatubidi turudi Tehran, kwahiyo tafadhali anzeni kusali", alisema abiria mmoja wa ndege hiyo.

Iran imekuwa na rekodi mbaya ya ndege zake kuanguka ndani ya miongo michache iliyopita na ajali nyingi za ndege nchini humo huhusisha ndege zilizotengenezwa nchini Urusi.

Vikwazo vya kiuchumi walivyowekewa Iran na Marekani vimesababisha Iran ishindwe kununua spea za ndege zao za zamani aina ya Boeing na Airbus na kusababisha wategemee zaidi ndege zinazotengenezwa nchini Urusi.

Mwezi julai mwaka huu, ndege ya shirika la ndege la Iran la Caspian Airlines ilianguka na kuua watu wote 168 waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

 
Kila moja atanena kwa lugha ambayo anafikiri na kuamini lugha hiyo inasikika na kueleweka na mizimu, mungu, malaika etc ambao wapo huko tusikokujua ambako wafu tu wanakujua kupoje.........!
 
Kwa uzoefu wangu kwenye mambo ya ndege, Si kawaida sana kwa Pilot kutangaza kitu kama hicho kwa Abiria, its too unproffessional!

Katika hali yoyote ile ya ajali pilot au mhudumu hatakiwi kuwaambia abiria katika hali itakayowastua, bali kuna lugha maalum za kuwajulisha abiria, na cha msingi kabisa ni kuwataka wafunge mikanda na kuwataka wakae katika mkao fulani, ambao kitaalamu unaminimize sana uumiaji katika ajali za ndege!
 
uwiiiiiiiiiiiiii sitaki hata kuwaza hapa ,nadhani nitakata roho before anything happen
 
mi nadhani kuna kitu inaweza kugonga chupi kabla hata sijaanza hiyo kusali ...hahaaaa
 
Kwa uzoefu wangu kwenye mambo ya ndege, Si kawaida sana kwa Pilot kutangaza kitu kama hicho kwa Abiria, its too unproffessional!

Katika hali yoyote ile ya ajali pilot au mhudumu hatakiwi kuwaambia abiria katika hali itakayowastua, bali kuna lugha maalum za kuwajulisha abiria, na cha msingi kabisa ni kuwataka wafunge mikanda na kuwataka wakae katika mkao fulani, ambao kitaalamu unaminimize sana uumiaji katika ajali za ndege!
wewe huwajui waarabu nini yaani ni machizi
 
ahahhahahahhahahha kitu gani manake vingi tu vinaweza gonga

ndugu NYANI, mbona unaulizia jibu!! Tafakari tu utajua ni kitu gani kitagonga. Tukirudi kwenye mada, kwa uzoefu wangu wa usafiri wa anga, rubani na hata watumishi wa kwenye ndege hawapaswi kuwaeleza abiria kuhusu uhalisia wa dharura kwani inaweza tokea fujo ikawa ni madhara juu ya madhara. Huyo pilot wa iran alichemsha!!!
 
Back
Top Bottom