Baada ya wananchi wiki iliyopita kuandamana kwa kumkataa mwenyekiti wa kijiji aliyeteuliwa na CCM kukabidhiwa ofisi, hatimaye leo mkurugenzi wa wilaya pamoja na mkuu wa wilaya ya Kilosa wamemteua na kumtangaza mwenyekiti wa kijiji katika kituo cha polisi cha Ruembe K2, badala ya kwenda kumtangaza kwa wananchi.
Nimeongea na wananchi wa Ruaha wanasema huyo ni mwenyekiti wa kijiji wa polisi na si wa wananchi.
Nawasilisha.
Nimeongea na wananchi wa Ruaha wanasema huyo ni mwenyekiti wa kijiji wa polisi na si wa wananchi.
Nawasilisha.
Muda si mrefu uliopita, Viongozi wa CCM chini ya Mkuu wa wilaya ya Kilosa wamemtawaza Ndugu Kisaluni kuwa mwenyekiti wa kijiji, kinyume na Kanuni za uchaguzI wa serikali za mitaa. ZoezI hilo limefanyika mbele ya zaidi ya polisi 50 katka kituo cha polisi Ruhembe.
Tangu uchaguzi ufanyike kwa kumuengua mgombea wa CHADEMA bila sababu, wananchi wameapa kumkataa mwenyekiti huyo wa CCM kupitia mkutano mkuu.
Hata hivyo kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa mitaa, tayari siku 7 zimepita tangu tarehe ya uchaguzi 28/04. hivyo mwenyekiti huyo hana uhalali.
DURU ZA NDANI zinasema kawaida kiwanda cha sukari hutoa mamilion kwa maendeleo na hivyo CCM wamefanya juu chini kumweka mtu wao ili wapige pesa. Nitawa-update.
SOURCE: Me