Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,728
- 2,259
Madudu ya kiutendaji, uhuni na ujambazi sasa yanafnywa na MAAFISA WA POLISI!!!!Kwa sisi ambao ingalau tumepitia JKT, tuliopata mafunzo kamili ya infantria miaka kabla tu ya Vita ya Kagera, matukio ya miaka ya karibuni yanatutia wasiwasi sana na hili jeshi letu la Polisi.
Malamiko madogo madogo ya utesaji, ubambikaji kesi, hata wizi na rushwa yalianza kuwa malamiko ya kawaida ya wananchi.
Watu walianza kusituka na matukio makubwa;
1.kuuwawa kwa makusudi wachimba madini wanne toka Morogoro. Polisi na hadi RCO Zombe akasema ni majambazi. Uchunguzi zaidi ukathibitisga kuwa ni uporaji uliofanywa na Polisi.
Maafisa polisi walipanga na kutekeleza uhalifu.
2. Kuuwawa kwa mchimba madini huko Mtwara , tukio hili limetonesha kesi hiyo ya Zombe na watuhumiwa ni maafisa wandamizi wa Polisi mkoani Mtwara.
Maafisa Polisi walipanga na kutekeleza uhalifu.
3 Huko Tanga nako wananchi wamelalamika watu kuuwawa na Polisi.
4. Tukio la kijana Hamza kulipiza kisasi na kuua vijana wadogo wa Polisi. Inasemekana alidhulumiwa madini na hao vijana wadogo wa polisi. Suala halikuwa independently investigated.
5. Kesi ya Freeman Mbowe nayo imeonyesha dalili za ubambikaji.
Polisi walio fungua kesi kujikanyaga kitoto hadi kufikia tabia za primary scholl ambapo mwanafunzi mtukutu anakimbilia chooni kukwepa adhabu za Mwalimu.
Maofisa waandamizi kwenda chooni au kujidai wanaumwa kila wakibanwa na maswali ya kisheria yanayowahusu moja kwa moja.
Tunaishukuru serikali kwakuliona tatizo la aibu ya hao maafisa wa polisi na kuondoa mashtaka mahakamani.
6. Tuje sasa suala la RPC Wankyo Nyigesa.
Afisa Wankyo bila aibu na kujizuia kiafisa, anatamka waziwazi kukitaka cheo cha Mkuu wa Jeshi la Polisi.
Haijawahi tokea ukosefu wa nidhamu kwa afisa wa Polisi kukejeli na kudharau afisa mkuu wa polisi, Polisi No 1.
Kwa tuliopitia mafunzo serious ya jeshi, hata kama ni JKT miaka hiyo, huyu RPC Wankyo moja kwa moja anapelekwa Court Martial.
Na pengine tukio hili si la kushangaza sana ukifikiria matukio tuliyaona na ukosefu mkubwa kwa uaminifu na weledi hasa kwa maafisa wa Polisi, wengine wakifanya uhalifu wa kupanga-kula njama.
Tatizo limeota mizizi na inabidi serikali itazame kuanzia kiini cha tatizo.
Polisi wanakuwa recruited kindugu.
Polisi wanateteana kwenye uhalifu.
Polisi vile vile wamekuwa wakitumika na wanasiasa.
Ilistua sana kuwa Polisi waandamizi hawajui PGO.
Matatizo ya Polisi ni ya muda mrefu na si ya viongozi wa sasa, wameyakuta ila yameota mizizi
CCM nayo imeona tatizo hilo na kukubali kwamba kuna haja ya kufanya mabadiliko kiutendaji ndsni ya Polisi.
Tuchukue hatua sasa kabla jeshi la Polisi halijawa halitawaliki.
Hatuna jeshi la polisi.