RPC wa Dodoma, Afande Muroto aituhumu JamiiForums kwa kupotosha taarifa za kifo cha Sheikh Rashid Bura

Dot zimesha someka
1. Aliwahi fanyakazi ofisi ya CAG

2. Anahusika katika taasisi ya Dalai Islamic center ambayo hata CAG mstaafu yupo.

3. Kabla ya kifo alikuwa safaarini kuhudhuria kwenye kikao cha tasisi yao ambacho CAG mstaafu alikuwepo ambaye naye ilisemekana alitekwa baada ya kutoka kwenye kikao hicho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kesi kama ya Costa del sol iliyoleta sintofahamu baada ya baba na wanae kufia kwenye swimming pool



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mwenyeezi Mungu ailaze roho ya marehemu peponi na amsamehe madhambi yake. Poleni ndugu najamaa wote mliopatwa na habari za kusikitisha sana.
 
Nijuacho kuna damu za watu si zakuzichezea chezea kabisa tena hasa hawa watu wa dini nakupindisha pindisha sababu ya vifo vyao, hamjui tu Mwenyezi Mungu anaudhika kiasi gani, haya mambo yote malipo yake huja maradufu wala haina haja ya kuongea sana.
 
Pascal Mayalla,
Mkuu nakuelewa sana na mada au uchambuzi wako. Ila nina mashaka na weledi wako wa kusimamia haki. Katika hili umekuwa upande mmoja sana maana sijaona ukiuliza maswali kama hayo kwa upande wa washutumiwa ambao ndio sisi humu JF, nipashe na wengineo. Je, ukweli wa taarifa zetu upo kwa kiwango gani? Je, tunaruhusiwa kuegemea katika single source? ni nani alithibitisha kutoka kwenye eneo la tukio yale yote yaliyoandikwa kwenye vyombo vya habari kabla ya taarifa ya polisi? Kwanini tunang'ang'ania sisi tu ndio tupo sahihi na si wengine?

Sina shaka kabisa na mapungufu mengi yaliyomo kwenye ripoti ya polisi sababu aliitajika daktari atoe taarifa ya kitaalam isiyoacha shaka. Lakini hili hali halalishi taarifa ya JF iwe sahii.
Jf kwa kiasi kikubwa imekuwa kama ulimwengu wa "Kambale". Hakuna mtu wa kuangalia ubora na ukweli wa taarifa na mbaya zaidi huwa tunaamini taarifa ya mwanzo tu, zinazofuata haziaminiwi hata zikiwa na ukweli. Na humu ndani kuna makundi kivyama. Hili linanipa ukakasi sana katika kujadili mambo ya kitaifa.
Samahani kama nimekukwaza.
 
Kimbinyiko hizi zenye System Charger au zipi?

Halafu toka anatoka Dar hakuwasiliana na Familia yake...
Msomaji ni alikuwa anasoma ila mwili unakataa alichokuwa anasoma.
Kubabatiza maneno yani maneno na mwili vinaenda pande mbili tofauti.

Nyakati zao za kukusanya kwa wote wanayotenda hayo maovu..ila pia nyakati za wanaoonea zikifika.

Njia na kipimo kitakuwa kama hicho wanachotumia.

Muda tu ..2020
 
Hapa ndio Muroto anapo angukia pua. Kijana wa marehemu amekataa version ya Muroto na kusisitiza kuwa mwili wa Mzee wake ulikutwa hauna nguo na una dalili ya majeraha. Labda kama nae amezushiwa kusema hivyo, vinginevyo taarifa ya polisi ina walakini na JF ina msingi wa kuleta taarifa iliyoletwa.

Nafikiri Jeshi letu la Polisi kwenye uwazi na ukweli (in Mkapa's voice) wana matatizo makubwa hadi wanafungua kesi ambazo hazipo, wanatoa reporti ambazo si sawa.
Wewe mchchezi! Dalili ya majeraha ni nini.
Mlianza na pro.. asadii kuwa katekwa akaharibu mwenyewe!
Mmekuja kwenye huu mkasa napo mmeshindwa! Tunajua mnakesha na kulipwa posho ili kuleta machafuko! Mtapata taabu sana.
 
Mkuu Nguruvi3,
Kwanza naunga mkono hoja.
Kunapotokea kifo cha utata, taarifa ya polisi ilipaswa kuishia kwenye kuthibitisha mwili umepatikana, ukiwa amekufa na daktari amethibitisha kifo .

Baada ya hapo taarifa ya kifo kimesababishwa na nini haikupaswa kutolewa na police bali daktari, tena kwa vile mwili ulifanyiwa post mortem, hata familia walipaswa kushauriwa wasizungumzie mwili umekutwajwe (bila nguo, na majeraha, umejaaje) kabla ya forensic report ambayo familia ndio hupewa na kuwa na disclosure liberty.

Marehemu kukutwa bila nguo sio uthibitisho wa crime wala mwili kukutwa na majeraha hayo matatu kwa mujibu wa mtoto wa marehemu pia sio uthibitisho wa crime kama uchunguzi wa forensic ungethibitisha hayo majeraha ni ya nini na ya lini maana mwili umekutwa ukiwa umekaa 3 days dead body in a room, hivyo there is a chance majereha hayo yalikuwa inflicted on dead body baada ya kufariki natural death.

Kitu ambacho sijasikia kikitajwa kwenye kifo hiki ni ambacho mimi nakihisi ni kuwa huyu Marehemu alitoka Dar kwenye mkutano ule ule wa CAG Mstaafu. Ulikuwa ni mkutano wa nini, ulijadili nini, waliohudhuria mkutano ule wajitokeze waseme marehemu alichangia nini kwenye mkutano ule ili tuweze ku connect the dots kama kilikuwa ni kifo cha kawaida or else.

Kwenye uwezo wa polisi wetu na serikali yetu kufanya baadhi ya mambo, unafahamika na niliisha wahi kuuzungumza hapa

Haya mambo ya Ma RPC kutoa taarifa za urongo kwenye media na kutuona sisi wananchi wote kama ni watoto wa darasa la pili, pia niliisha wahi lizungumza humu kwa kumshauri IGP Sirro asiwaache ma RPC waropokaji kama hawa kulichafua jeshi letu safi la polisi

Hili la kifo hiki linahitaji maelezo ya ziada ili lieleweke.
Kwa vile Jamiiforums tumetajwa kwa kushutumiwa kwa uzushi, nashauri uongozi wa jf usikubali na tusikae kimya, hata kama aliyeleta taarifa hizo mwanzo ni just an ordinary member, lakini baada ya tuhuma kwa jf, ni ama huyo member awe equipped kwa kuwa linked na members humu wenye uwezo wa kufanya IJ wamuelekeze cha kufanya ili kuisafisha jf, au jf imtume member mwingine mwenye credentials za kufanya hayo makitu na ukweli ukibainika, ni kamanda Muroto kumpumzishwa tuu kwa uropokaji.

P
Taarifa haiwezi kutolewa na Daktari kwani hawawezi kusema uongo na ni kinyume na maadili yao
 
Hizi sura tayari naona wabunge 11 wa jamhuri ya muungano 2020, na mmoja ni raisi wa zanzibar
20200102_144800.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom