RPC Shinyanga una taarifa ya vijana watano wanaoshikiliwa zaidi ya siku 10 kituo cha Polisi Bugarama, Msalala na kuteswa kikatili?

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Kuna vijana watano wapo mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Bugarama wilaya ya Msalala wanateswa kikatili, walikamatwa siku zaidi ya kumi zilizopita wakituhumiwa kuiba TV ya hawara yake na Polisi.

Wanatishiwa kupewa kesi ya ujambazi wa kutumia silaha endapo hawatakiri kuiba hiyo TV.

Taarifa za uhakika kutoka kwa Police asiye na cheo aliyepo kituoni hapo ambaye ana hofu ya Mungu na ameumia kushuhudia ukatili huo zinadai kuwa, Police katili wanaowatesa vijana hao wamewaambia kuwa watawapeleka msituni na kuwapiga risasi kisha waseme kuwa walikuwa wakipambana na majambazi na kuwaua baada ya kuwazidi nguvu.

Nakutaarifu ili usije kupewa Report ya uongo na OCD kuwa wameua majambazi kumbe ni vijana hao.

Nyie Police wa Tanzania,mtavunja sheria hadi lini? Yaani mnawatesa Watanzania mtakavyo, ni kawaida yenu,yaani mnakamata watu bila kuwafikisha Mahakamani na mnawatesa,ndo maana sijawahi kuona Police mwenye mwisho mzuri Tanzania,wengi wenu hata mkistaafu mnataabika sana, kwa sababu mikono yenu ina Damu za watu wasio na hatia na mmeua watu wengi mno wasio na hatia.
Yaani mnashikilia watu na kuwatesa siku kumi bila kuwafikisha Mahakamani?

Ukatili gani huu?

Watanzania ndo mjue bila CCM kuondolewa madarakani mtaendelea kuteswa tu, hawa Police wanavunja sheria wakidekezwa na Serikali ya CCM.

Ila uonevu huu una mwisho, The day is coming in which you'll pay the price.
 
Umetoa taarifa vizuri sana, ilikuwa imeeleweka na nlikuwa na Imani leo leo swala hilo lingeshughulikiwa, ila ulivyoingiza U-CCM mwishoni umeiharibu kabisa taarifa husika, utashi na maadili ya mtu kazini vinabebwa sana na tabia ya ndani ya mtu. Maana hata aliekupa taarifa hiyo (polisi mwenye hofu ya MUNGU) yawezekana ni CCM pia.

Nafikiri wakuu litawafikia kwa wakat
 
Mkuu Roho,imeniuma sana,sipendi watu waonewe
 
Kwenye heading unasema wako 10.

Kwenye uzi unasema wapo 5.

Basi wewe ni muongo au pengine ndio uliuziwa hiyo tv
 
Kipi hujajielewa hapo?

Wahusika wakilifatilia hilo swala ukweli utajulikana.
 
Watanzania ndo mjue bila CCM kuondolewa madarakani mtaendelea kuteswa tu,hawa Police wanavunja sheria wakidekezwa na Serikali ya CCM.

Ila uonevu huu una mwisho, The day is coming in which you'll pay the price.
Mkuu My Son drink water , kwanza asante kwa taarifa hii, maana sasa hii ni whister blow kubwa na itafika kunakohusika, na hatua zitachukuliwa, ila sio haki kuiingiza CCM kwenye kila ovu, au baya linalofanyika na taasisi huru, simply kwasababu tuu CCM ndio chama tawala na serikali ni ya CCM.

Ingekuwa kinachofanyika kiko kwenye ilani ya CCM, na hao polisi wanatekeleza ila ya uchaguzi ya CCM ndio ungeilaumu CCM, lakini kuilaumu CCM kwa makosa ya watendaji wa taasisi independent ni kuionea bure.

Maneno haya " bila CCM kuondolewa madarakani mtaendelea kuteswa tu"
ni kama uchochezi fulani wa kujenga chuki kwa CCM. Na kwa vile namna pekee ya kukiondoa chama chochote madarakani ni kupitia sanduku la kura, na kufuatia CCM kupendwa sana na kukubalika, hakuna namna ya kuiondoa CCM madarakani kupitia sanduku la kura , hivyo uki suggest kuiondoa CCM madarakani kwa njia nyingine yoyote ni uhaini!.

Huu ndio ukweli uliopo, kubali, kataa!.
P
 
RPC Yupo Hajachukua Hatua Yoyote

Bango Moja Kiongozi Mmoja Anaondoka Kwenye Nafasi Yake Sasa DC,Ded Wapo
 
POLISI WAMEKUWA MASHETANI SANA:

JUMATANO ILIYOPITA POLISI WA IRINGA WAKIWA DORIA WALIWAKUTA WADADA WAWILI WAMECHELEWA KUFUNGA GROCERY MITAA YA STENDI KUU YA ZAMANI IRINGA MJINI. WAKAWAMATA WAKAWAPIGA WAKAWANYANG'ANYA HADI HELA ZA MAUZO. WAKAZUNGUKA NAO KWENYE GARI KUANZIA SAA 6 HADI SAA TISA WAKAENDA KUWASHUSHA NJE YA MJI MITAA YA KIHESA. HAPO HAMNA BODABODA, DALADALA WALA BAJAJI.

POLISI NI WAUAJI NA WATESAJI.

MTU KAMA ANA KOSA AFUNGULIWE MASHTAKA SIO KUMTESA AU KUPORA MALI ZAKE.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu My Son drink water , kwanza asante kwa taarifa hii, maana sasa hii ni whister blow kubwa na itafika kunakohusika, na hatua zitachukuliwa, ila sio haki kuiingiza CCM kwenye kila ovu, au baya linalofanyika na taasisi huru, simply kwasababu tuu CCM ndio chama tawala na serikali ni ya CCM.

Ingekuwa kinachofanyika kiko kwenye ilani ya CCM, na hao polisi wanatekeleza ila ya uchaguzi ya CCM ndio ungeilaumu CCM, lakini kuilaumu CCM kwa makosa ya watendaji wa taasisi independent ni kuionea bure.

Maneno haya " bila CCM kuondolewa madarakani mtaendelea kuteswa tu"
ni kama uchochezi fulani wa kujenga chuki kwa CCM. Na kwa vile namna pekee ya kukiondoa chama chochote madarakani ni kupitia sanduku la kura, na kufuatia CCM kupendwa sana na kukubalika, hakuna namna ya kuiondoa CCM madarakani kupitia sanduku la kura , hivyo uki suggest kuiondoa CCM madarakani kwa njia nyingine yoyote ni uhaini!.

Huu ndio ukweli uliopo, kubali, kataa!.
P
Mkuu Pasco, utawala wa Chama kimoja Tu umefanya Taifa liwe lemavu kabisa, ndo maana naituhumu CCM kwa sababu wamekuwa wakiongoza nchi kwa mazoea
 
Kuna vijana watano wapo mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Bugarama wilaya ya Msalala wanateswa kikatili, walikamatwa siku zaidi ya kumi zilizopita wakituhumiwa kuiba TV ya hawara yake na Polisi.

Wanatishiwa kupewa kesi ya ujambazi wa kutumia silaha endapo hawatakiri kuiba hiyo TV.

Taarifa za uhakika kutoka kwa Police asiye na cheo aliyepo kituoni hapo ambaye ana hofu ya Mungu na ameumia kushuhudia ukatili huo zinadai kuwa, Police katili wanaowatesa vijana hao wamewaambia kuwa watawapeleka msituni na kuwapiga risasi kisha waseme kuwa walikuwa wakipambana na majambazi na kuwaua baada ya kuwazidi nguvu.

Nakutaarifu ili usije kupewa Report ya uongo na OCD kuwa wameua majambazi kumbe ni vijana hao.

Nyie Police wa Tanzania,mtavunja sheria hadi lini? Yaani mnawatesa Watanzania mtakavyo, ni kawaida yenu,yaani mnakamata watu bila kuwafikisha Mahakamani na mnawatesa,ndo maana sijawahi kuona Police mwenye mwisho mzuri Tanzania,wengi wenu hata mkistaafu mnataabika sana, kwa sababu mikono yenu ina Damu za watu wasio na hatia na mmeua watu wengi mno wasio na hatia.
Yaani mnashikilia watu na kuwatesa siku kumi bila kuwafikisha Mahakamani?

Ukatili gani huu?

Watanzania ndo mjue bila CCM kuondolewa madarakani mtaendelea kuteswa tu, hawa Police wanavunja sheria wakidekezwa na Serikali ya CCM.

Ila uonevu huu una mwisho, The day is coming in which you'll pay the price.
Hizi tuhuma ni nzito sn
 
Nje ya mada,hiyo ya wakistaafu wanataabika sana nakataa,nimefika nyumbani kwa RPC mstaafu Alfred Gewe tabata mawenzi ni kama pepo duniani.Narudi kwenye mada, polisi hao vijana wakifa mtajuta kamuulizeni Bageni.
Ukiona hivyo ujue Gewe alitenda haki,si Police wote washenzi,wapo wema, japokuwa wachache sana
 
Kuna vijana watano wapo mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Bugarama wilaya ya Msalala wanateswa kikatili, walikamatwa siku zaidi ya kumi zilizopita wakituhumiwa kuiba TV ya hawara yake na Polisi.

Wanatishiwa kupewa kesi ya ujambazi wa kutumia silaha endapo hawatakiri kuiba hiyo TV.

Taarifa za uhakika kutoka kwa Police asiye na cheo aliyepo kituoni hapo ambaye ana hofu ya Mungu na ameumia kushuhudia ukatili huo zinadai kuwa, Police katili wanaowatesa vijana hao wamewaambia kuwa watawapeleka msituni na kuwapiga risasi kisha waseme kuwa walikuwa wakipambana na majambazi na kuwaua baada ya kuwazidi nguvu.

Nakutaarifu ili usije kupewa Report ya uongo na OCD kuwa wameua majambazi kumbe ni vijana hao.

Nyie Police wa Tanzania,mtavunja sheria hadi lini? Yaani mnawatesa Watanzania mtakavyo, ni kawaida yenu,yaani mnakamata watu bila kuwafikisha Mahakamani na mnawatesa,ndo maana sijawahi kuona Police mwenye mwisho mzuri Tanzania,wengi wenu hata mkistaafu mnataabika sana, kwa sababu mikono yenu ina Damu za watu wasio na hatia na mmeua watu wengi mno wasio na hatia.
Yaani mnashikilia watu na kuwatesa siku kumi bila kuwafikisha Mahakamani?

Ukatili gani huu?

Watanzania ndo mjue bila CCM kuondolewa madarakani mtaendelea kuteswa tu, hawa Police wanavunja sheria wakidekezwa na Serikali ya CCM.

Ila uonevu huu una mwisho, The day is coming in which you'll pay the price.
Loo kama taarifa hii ni ya kweli Basi hatuna jeshi la polisi bali tuna jeshi la majambazi!
 
Back
Top Bottom