RPC Shanna amwagiwa Sifa Lukuki "umefanikiwa kuzima mauaji ya wanawake"

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amempongeza kamanda wa Polisi mkoani hapa,Jonathan Shanna kwa kufanikisha kudhibiti uhalifu wa silaha yakiwemo mauaji ya wanawake yaliyokuwa yakitokea katika kata ya Olasiti na kusababisha wananchi wa kata hiyo kujawa na hofu

Gambo alimtaja Kamanda Shanna kama kiongozi mwenye weredi,mchapakazi aliyetumwa kuwatumikia wananchi wa Arusha na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kujenga umoja kwa askari polisi

"Pongezi kwa RPC Shana kwa kuchapa kazi umekuwa na weredi wa hali ya juu,umefanikiwa kuleta nidhamu kwa jeshi la polisi, huna unafiki umeleta utulivu katika mkoa wa Arusha ,umefanikiwa kudhibiti mauaji ya wanawake kule Olasiti " Alisema Gambo

Katika hatua nyingine Shanna alitoa rai kwa RC Gambo kupuuza mijadala inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwamba ameanza kampeni za kujinadi kisiasa mapema.

Awali kamanda Shanna alimhakikishia Mkuu huyo wa mkoa kwamba, jeshi hilo mkoani hapa litaendelea kufanya kazi kwa weredi na katika uchaguzi ujao halitatumia silaha zozote za moto , badala yake litalinda amani kama raia wa kawaida.

Aliwataka wanasiasa na wananchi kutii sheria bila shuruti kipindi chote cha uchaguzi Mkuu ikiwemo kufanya siasa za kistaarabu ambazo hazitavunja sheria kwani wakichokozwa hawatasita kuchukua hatua.

Katika hatua nyingine kamanda Shanna alimpongeza mkuu huyo wa Mkoa Mrisho Gambo kwa kuwa karibu na jeshi la polisi kwa kutoa mawazo ya kusaidia maendeleo ya jeshi hilo ikiwemo ujenzi wa makazi ya askari.

Ends...

IMG_20200604_131028.jpeg
IMG_20200604_131013.jpeg
IMG_20200604_131352.jpeg
 
Kama namuona kamanda Shanna anavyozipokea sifa hizo

Ova
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom