RPC Shana aapa kutumia 'dog style' kumkamata Muuaji

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Sakata la Mwanaume,Moses Palangyo mkazi wa kijiji cha Kilinga Wilayani Arumeru kumuuwa kinyama kwa shoka mwanamke anayedaiwa kuwa mke wake, Mary Richard Mushi(24) limechukua sura mpya Mara baada ya jeshi la polisi mkoani hapa kuapa kumsaka mtuhumiwa huyo uvungu kwa uvungu nyumba kwa nyumba na kumtaka ajisalimishe akiwa hai popote alipo.

Akiongea na Vyombo Vya Habari ofisini kwake,mkuu wa jeshi hilo Mkoa wa Arusha,Jonathan Shana amesema kuwa kitendo kilichofanya na mtuhumiwa huyo ni cha kinyama na halikubaliki na kumtaka mtuhumiwa huyo popote alipo ajisalimishe kabla jeshi hilo halijatumia nguvu kubwa kumsaka.

"Nawahakikishia polisi tumeingia kazini tutamkamata mtuhumiwa muda sio mrefu ,tutatumia style ya dog kunusanusa na kama yupo juu ya mti tutatumia nyani style kufuata alipo na kama yupo pangoni tutapiga mpaka atatoka" amesema Shana

Kwa mujibu wa kamanda Shana ,tukio hilo limetokea Jana Majira ya SAA NNE asubuhi huku chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika huku taarifa za awali zikiwa bado zinatatanisha .

Kamanda ameeleza kuwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo waliohojiwa na polisi wamedai kuwa wapenzi hao walikuwa na mgogoro wa kifamilia na kupelekea Mke kukimbilia kwa Wazazi wake huku taarifa zingine zikidai huenda ni wivu wa mapenzi.

Amewataka wananchi kusaidia kumfichua mhalifu huyo na kwamba iwapo kama kuna MTU atakuwa amemficha atachukuliwa hatua Kali za kisheria.

Katika hatua nyingine kamanda Shana ameeleza hali ya utulivu imetawaka katika Mkoa wa Arusha katika kipindi cha sikukuu ya X mass na kwamba wananchi wamesherehekea bila kuwepo kwa matukio ya uvunjifu wa Amani.
 
Hapo sawa lukeni sarakasi zote lkn namhitaji mtuhumiwa.Awe mzima ama amekufa
 
Ukute mchzi now yupo zake kwa mromboo anatafuna minofu ya mbuzi huku akipuliza tarumbeta ya Serengeti lite ya bariiidi mbwa akija kumfikia anakutana na mifupa tuu daaaaadeq...😄🚶🏿🚶🏿🚶🏿
 
Akiongea na Vyombo Vya Habari ofisini kwake,mkuu wa jeshi hilo Mkoa wa Arusha,Jonathan Shana amesema kuwa kitendo kilichofanya na mtuhumiwa huyo ni cha kinyama na halikubaliki na kumtaka mtuhumiwa huyo popote alipo ajisalimishe kabla jeshi hilo halijatumia nguvu kubwa kumsaka

Nilidhani habari itasema "akiongea kutoka unakofanyika msako..." kuongea kutoka ofisini ni blabla
 
Niliposikia dog style, kuna vitu vingi sana kama nyota nyota vimeniijia kichwani mithiri ya Kofi la uso, ila nimebaki mdomo wazi baada ya kusoma

Sent using Jamii Forums mobile app

Ulifikiri kamanda anataka kula tunda "kimasihara"! Mabaharia bwana! Nimekuwa nikiwasoma sana mabaharia wangu kwenye ule uzi wenu wa kula tunda kimasihara! Huwa mnafunguka kwelikweli!!
 
"Nawahakikishia polisi tumeingia kazini tutamkamata mtuhumiwa muda sio mrefu ,tutatumia style ya dog kunusanusa na kama yupo juu ya mti tutatumia nyani style kufuata alipo na kama yupo pangoni tutapiga mpaka atatoka" amesema Shana

Nimesikia kutoka magazetini kuwa polisi watatumia mabomu ya machozi kumkamata muuaji
 
Back
Top Bottom