RPC Mwanza elewa kuwa vikao misibani haviepukiki na ni vya muhimu sana

Mkuu msibani sio sehemu ya kuongelea siasa sasa kama mnaeneza chuki na uchochezi mnataka mchekewe au
Niliona siku moja igogo yaani msiba ulitokea 17/2/2017 wakaja kukaa mwezi wa Pili 18/2/2018 nikashindwa kuelewa huu msiba au mini cha ajabu yanayohubiliwa sio msiba bali ni siasa tupu mara tunamtaka wenje...
 
Bob anataka ccm amzike ccm mwenzake tu na vice versa..
hataki mchangamane misibani!
 
Kwa mara ya pili kunaripotiwa taarifa za polisi Mwanza kuvamia na kutawanya watu misibani kwa maelezo kuwa kuna hisia viongozi wa CHADEMA wanatumia misiba hiyo kufanya vikao vya siasa.

Ninachotaka kumwambia RPC huyo wa Mwanza ni kuwa anafanya kosa kubwa sana kuongeza huzuni na simanzi misibani hasa kwa wafiwa, ndugu jamaa na marafiki.

Mtu anapofariki au kunapokuwa na misiba huwa kuna kuwa na vikao mbali mbali msibani au hata nje ya msibani kuangalia namna ya kumsitiri marehemu. Mbali ya vikao vya wanandugu, jamaa na marafiki, huwa kuna kuwa na vikao mbali mbali vya vikundi au taasisi tofauti kulingana na nafasi aliyokuwa nayo marehemu wakati wa uhai wake.

Mfano kama marehemu alikuwa ni mwanaccm au chadema siyo ajabu kukuta viongozi na wanachama wa chama husika wamekaa pamoja msibani au nje ya msiba kuangalia namna watavyoshiriki katika kufanikisha mazishi ya mwanachama wao. Na kwakuwa aliyefariki alikuwa mwanachama wao au kiongozi wao lazima watakuja wakiwa wamevaa sare za chama chao na hata huwa tunaona jeneza linafunikwa bendera ya chama husika katika sehemu ya kumuenzi marehemu.

Vivyo hivyo kama marehemu alikuwa mwanakwaya kikundi cha kwaya kinaweza kusasanyika msibani hapo au kanisani kuangalia namna watakavyochangia kufanikisha mazishi hayo. Kama alikuwa ni kwenye SACCOS fulani hao nao watakaa kuona namna watakavyochangia kufanikisha msiba huo. Kama alikuwa mwalimu au mwanafunzi halikadharika kutakuwa na vikao kulingana na mipango ya taasisi husika. Hatimaye ndipo utasikia kwenye matangazo wakisema labda marehemu alikuwa mwanachama na kiongozi mwaminifu wa CCM ua CHADEMA hivyo chama kimetoa mfano jeneza na kosta moja kwaajili ya kusafirisha mwili wa marehemu. vikundi vingine utasikia vinatangaza kutoa chakula, maji, PA, maturubai, pesa taslimu na hata ahadi ya kusomesha watoto wa marehemu au kumalizia nyumba ya marehemu. Pia vikundi au taasisi mbali mbali hutoa salam na pia wasifu wa marehemu kulingana walivyomfahamu na kuishi naye au kufanya kazi naye katika taasisi au kikundi chao. Haya yote yanafanyika na kufanikiwa kulingana na wanavikundi husika kukusanyika na kujadiliana na kisha kukubaliana kuhusu michango yao kwa mpendwa wao.

Kama nilivyosema wanaweza kufanya vikao vyao msibani au hata kwenye baa kulingana na jinsi watakavyoona inafaa. Tumeona CCM wakizika na pia tumeoana CHADEMA na vyama vingine vikizika watu wao. Na nina imani kuwa CHADEMA walikwenda kwenye misiba hiyo kwakuwa marehemu au mfiwa au wafiwa ni wanachama wao. Ninaamini kama misiba hiyo ingekuwa inahusiana na wanachama wa CCM, CHADEMA wasinge kwenda kichama. Sasa sijaelewa kwanini RPC wa Mwanza haelewi haya na anatumia vibaya askari kufanya vurugu misibani. Hata kama wataongea siasa hakuna dhambi kwa kuwa aliyekufa ni mwanasiasa au ni ndugu wa mwanachama wao. Naomba huyu RPC ajifunze kuwa mtu mzima na kuwaacha watu wawazike watu wao hata kama watakuwa wanaimba au wanacheza au wanakunywa pombe hiyo haimhusu. Aache kuchokoza wananchi wanapokuwa katika shughuli zao za kijamii. Sijaona kabisa mantiki ya kutawanya watu misibani. Mbona watu huwa wanaongea habari za mpira, nyimbo, sinema na utani misibani sasa kuna kosa gani kama aliyekufa ni mwanamichezo?

Polepole anazunguka nchi hii anavyotaka huku akifanya maandamano na mikutano ya siasa hatujasikia polisi wakiwatawanya kwa kufanya shughuli hizo za kisiasa lakini CHADEMA wanachukuliwa kama sio raia wa nchi hii. Hawatakiwi kufanya chochote hata kushiriki katika misiba! Tengenezeni tu hasira mioyoni mwa wananchi. Hayo mabomu na bunduki mnazoringia wamenunua wananchi wenyewe ili mzitumie kuwalinda sio kuwafanyia vurugu wanapokuwa katika shughuli zao na sio kuwajeruhi au kuwa uwa bila hatia kama mlivyofanya kwa Mwandishi David Mwangosi kule Iringa na Akwilina Akwilini kule Dar es Salaam. Kuna siku hayo mabomu na risasi havita fyatuka ndipo mtatafuta pa kukimbilia msipaone. Kwanini mnawafanya baadhi ya raia wa nchi hii kama wao ni second class citizens huku wengine mkiwanyenyekea na kuwafanya wao ndio first class citizens?
CCM huenda kichama na mavazi yao wao wanafuata taratibu kufanya siasa msibani, tatizo la Chadema in kutofuata taratibu na kupata kibali cha kuhudhuria msiba.
 
CCM huenda kichama na mavazi yao wao wanafuata taratibu kufanya siasa msibani, tatizo la Chadema in kutofuata taratibu na kupata kibali cha kuhudhuria msiba.
Kwahiyo kuhudhuria Msiba mpaka upate kibali sio
 
Misiba ya kichochezi ilijaa siasa na vurugu hatuitaki hapa mwanza ,mwanza uwe mji salama
Kama na babu yako angekuwa na busara kama zako,hadi sasa tungekuwa chini ya malikia.

Kwa hiyo msibani kuwe na maongezi maalum,mikao maalum na wahudhuliaji maalum,haya ndugu.
 
Back
Top Bottom