RPC Kinondoni aruka kuwa hakwenda kuzuia mkutano wa Nape ila alikwenda kuweka ulinzi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,883
FB_IMG_1490346824839.jpg
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Susan Kaganda, amesema kuwa yeye hakutoa maelekezo ya kuzuia mkutano wa aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye pamoja na Waandishi wa Habari Jana Protea Hotel.

Akifafanua kupitia kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm mapema Leo asubuhi, Susan amedai yeye kama Kamanda hana mamlaka ya kuingilia biashara binafsi (Protea Hotel), na alikwenda pale kuhakikisha Usalama unaimarika zaidi na si vinginevyo.

"Protea ni private Hotel sio Mali ya Serikali, ile ni Biashara huru kamanda hawezi kuzuia, lakini nilikuta Waandishi wengi pale na alipata fursa ya kuongea nao.

" Mimi kazi yangu ni kusimamia Usalama wa Raia na Mali zao, mkutano unanihusu ukiwa wa Hadhara" alisema RPC Susan.

Alipoulizwa kuhusiana na kipande cha 'Picha Jongefu' (video) inayomuonyesha mtu anayedhaniwa kuwa Askari akimtolea silaha Nape Nnauye, amesema hawezi kuliongelea swala hilo kwa sasa mpaka uchunguzi utakapokamilika kwa maana kipande hicho hakionyeshi Sura ya mtu Huyo.

"Jeshi la Polisi tunawafundisha Askari wetu kutumia nguvu kwa namna wanavyokutana na Mazingira, Sikuwepo sikuona nilielezwa na ndio maana nilikwenda nikamuuliza Mh uko sawa akanijibu yuko Salama.

" Lakini kama kuna Silaha imetumika kama ambavyo nimeona kwenye vyombo vya Habari tunalifanyia Uchunguzi, sikuwepo eneo la tukio picha ile inaonyesha KISOGO, kuwa mtulivu tunachunguza" Alifafanua.
 
Kwa mtindo huu wa blah blah za viongozi wa jeshi la polisi ni wazi watanzania wamekosa imani na jeshi la polisi kwani ni jeshi la kulinda watawala tu sio jeshi la kulinda raia na mali zao.

Jeshi la polisi limepoteza sifa na uhalali katika utendeji na majukumu yao.
 
waliwaomba usalama, mbona vikao vingine wanafanya na usalama hakuna mambo yanaenda, hii nchi aisee, anyway mshaamua mngemuuma mngekana kuwa sio askari,
 
Kwa tamko hilo usalama wetu uko rehani. Kwa hiyo inawezekana hata kuwa hilo jamaa lilikuwa jambazi. Polisi wa kawaida walikuwa pale, kazi yao ilikuwa ipi! Sitaki kusikia ujinga huu. Bila shaka Mwigulu amemsikia.
 
View attachment 486125 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Susan Kaganda, amesema kuwa yeye hakutoa maelekezo ya kuzuia mkutano wa aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye pamoja na Waandishi wa Habari Jana Protea Hotel.

Akifafanua kupitia kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm mapema Leo asubuhi, Susan amedai yeye kama Kamanda hana mamlaka ya kuingilia biashara binafsi (Protea Hotel), na alikwenda pale kuhakikisha Usalama unaimarika zaidi na si vinginevyo.

"Protea ni private Hotel sio Mali ya Serikali, ile ni Biashara huru kamanda hawezi kuzuia, lakini nilikuta Waandishi wengi pale na alipata fursa ya kuongea nao.

" Mimi kazi yangu ni kusimamia Usalama wa Raia na Mali zao, mkutano unanihusu ukiwa wa Hadhara" alisema RPC Susan.

Alipoulizwa kuhusiana na kipande cha 'Picha Jongefu' (video) inayomuonyesha mtu anayedhaniwa kuwa Askari akimtolea silaha Nape Nnauye, amesema hawezi kuliongelea swala hilo kwa sasa mpaka uchunguzi utakapokamilika kwa maana kipande hicho hakionyeshi Sura ya mtu Huyo.

"Jeshi la Polisi tunawafundisha Askari wetu kutumia nguvu kwa namna wanavyokutana na Mazingira, Sikuwepo sikuona nilielezwa na ndio maana nilikwenda nikamuuliza Mh uko sawa akanijibu yuko Salama.

" Lakini kama kuna Silaha imetumika kama ambavyo nimeona kwenye vyombo vya Habari tunalifanyia Uchunguzi, sikuwepo eneo la tukio picha ile inaonyesha KISOGO, kuwa mtulivu tunachunguza" Alifafanua.
HIVI nape ni nani? naomba unikumbushe, nimesahau
 
usicheze na kazi maalumu yle jamaa alishasoma kwa umakini kamera ziko ndipo akachomoka faster na alihakikisha hakosei
Kwaakili yakawaida unataka kusema wale waliokua wanamtoa yule jamaa hawakumuona,na ile hadhira yote haikumuona,haya majibu niyakumwambia mtu ambaye hayuko determined kumtafuta yule jamaa.Nina uhakika jamaa aktaka kutafutwa anapatikana haraka sana,hata mimi mwenyewe nikipewa hiyo kazi nampata.
 
Back
Top Bottom