RPC Kingai awaonya BAWACHA, Ahoji, unafanya mazoezi ukiwa umevaa fulana zilizoandikwa ''Tunataka Tume Huru ya Uchaguzi'?

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,904
Dar es Salaam. Wakati Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) likilaani kitendo cha Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam kuzuia mazoezi waliyofanya jana, leo Septemba 19, Kamanda wa Kinondoni, Ramadhani Kingai amewaonya wanachama hao akisema Polisi wana akili zaidi yao na kwamba wasiwabipu.

Kupitia taarifa iliyotolewa kwa umma leo Septemba 19, 2021 na Kaimu Mwenyekiti Bawacha, Sharifa Suleman imeeleza tukio hilo lilitokea asubuhi ya Septemba 18, 2021 ambapo Polisi hao kiume, walivamia na kusambaratisha mazoezi hayo wakidai kuwa ni "Maandamano Haramu.’’

“Mazoezi haya ni jambo la kawaida ambalo wanawake hawa wamejipangia kufanya kila wiki kwa ajili ya kuimarisha afya zao. Vitendo hivi vimekuwa vinalenga matukio yanayofanywa na Chadema pekee kwani CCM imekuwa inaendelea na matukio mbalimbali ikiwemo Jogging, mikutano ya ndani na hadhara bila kubughudhiwa kwa namna yoyote na Jeshi hilo,” imeeleza taarifa hiyo.

Bawacha imesema kitendo cha Polisi kuzuia mazoezi hayo kwa nguvu kudhalilisha raia na kwamba havitavumiliwa.

“Kila mmoja ana haki ya kuheshimu na heshima na staha. Bawacha itaendelea kuwa ya wanawake wote nchini dhidi ya vitendo vyote vya udhalilishaji na kuonewa.

Akizungumza na Mwananchi kuhusu malalamiko ya Bawacha leo, Kamanda Kingai amesema hiyo ilikuwa sio Jogging bali wanachama hao walikuwa na nia ya kufanya maandamano ya kimkakati hivyo walichukua maamuzi ya kuvamia na kuwasambaratisha.

Nitumie fursa hii kuwaonya kwa sababu walichokuwa wanakifanya wao ilikuwa ni nia ya kufanya maandamano Ulishawai kusikia wapi jogging ya chama? Kingine ,” amehoji Kingai.

Kingai amesema hiyo sio Jogging bali yalikuwa maandamano ya kimkakati na aliwaonya kuendeleza vitendo hivyo na kwamba wasiendelee kulibipu jeshi hilo kwani wanatakiwa kuzingatia taratibu za kisheria kama zinavyoeleza.
 
Kesho utaona t-shirt za jogging club flani zimepandikwa "HATUMTAKI RAIS 🧝"
 
Dar es Salaam. Wakati Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) likilaani kitendo cha Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam kuzuia mazoezi waliyofanya jana, leo Septemba 19, Kamanda wa Kinondoni, Ramadhani Kingai amewaonya wanachama hao akisema Polisi wana akili zaidi yao na kwamba wasiwabipu.
VIPI HII MIKUTANO
20210916_182401.jpg
 
Uwezo wako wa kuelewa umeishia hapo??? Kisha unajiita Mkorinto???
Tenda haki kwa maana "Laana ya Mungu haiishii kizazi kimoja..."
Nadhani ikutoshe mstari huo mmoja
Kisasi ni cha Mungu.

Haki haiwi kwa sababu inakufurahisha wewe tu,hata ile inayokuudhi ama kukusikitisha.
 
Dar es Salaam. Wakati Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) likilaani kitendo cha Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam kuzuia mazoezi waliyofanya jana, leo Septemba 19, Kamanda wa Kinondoni, Ramadhani Kingai amewaonya wanachama hao akisema Polisi wana akili zaidi yao na kwamba wasiwabipu.
Joging ni kitu kidogo sana, CCM wao wameandaa mashindano ya michezo.
 
Anataka kuzalisha kina hamza wengine maana hamza ameonyesha njia ya kudili na wakandamizaji.
Watu kusema kweli weshawachoka polisi ,nikisema watu namaanisha hata ndani ya polisi na jeshi kuna watu.
 
Back
Top Bottom