RPC Gilles Moroto: Tunasikitishwa na dereva wa Tundu Lissu kutoonyesha ushirikiano kwa jeshi hadi sasa

Sasa hapa ndo umuhimu wa kuwaleta wale Scotland Yard au FBI unapoonekana kwa maana hawa local investigators wako more compromised by the state who is also the main suspect in this matter.

Ina maana hakuna leads zingine wanazoweza ku-apply kwa wakati huu kama namba za lile gari, walinzi wa eneo husika au ni watu gani waliathiriwa na constant criticisms by the victim.

Kinachoonekana hapa ni "Cover Up Exercise" zaidi, huku kutokuwepo kwa Driver has only provided an excuse to justify the cover up plan. Nothing more, although this will only help them for a while.
 
Achana nao .

Lakini wajue wanatengeza mazingira ambayo nayaifanya serikali ijitoe kwenye hili suala.

Kikawaida tuu tukio kama lile lilipaswa kuripotiwa polisi.

Lakini yawekana hadi leo hakuna taarifa ya malalamiko au maeleizo kutoka kwa waathirika.

Tunaona kweli kuwa lissu alishambuliwa ila hakuna ushirikiano.

Trust me. Hii ishu itaisha kama ya nape.
Kwani matamshi anayotoa Lissu mpaka anakamatwa mara kwa mara ni nani huwa anariport polisi?

Kwa taarifa yako hata mtu asipotoa taarifa bado serikali itamfikisha mahakamani na itasimama kama jamhuri.
 
You are the one to re-think..

Tatizo CDM wanacheza mchezo bila wachezaji wa Akiba..vitu vingine wana create wao vinawarudia.

Juzi, Sirro alisema kitu cha msingi sana kama ulimwelewa mkuu.

Sirro aliuliza ""kama lissu alikuwa anafuatiliwa kwanini hakuja polisi kutoa taarifa? Ni kituo kipi Lissu alienda kutoa taarifa? ""

Lissu aliitisha press tuu akasema kuna watu wanamfutilia..hakwenda polisi.

Sasa umeona namna ambavyo CDM wanawapa polisi mwanya wa kujifanya hawajui kinachoendelea Hata kama wanajua mchongo mzima?

Leo hii Lissu amepigwa Risasi akiwa na Dereva wake. Hakuna alieenda polisi kutoa taarifa ikiwa na Lissu ama ni dreva (watu ambao ndio walikuwa kwenye Tukio) . Na hadi sasa hakuna aliyehojiwa..

Sasa kama huamini polisi wao watafanya wanavyojua kwa makusudi kabisaaaaa....afu last days wanakuja kuwaruka kirahisi tuuu.

Watasema walifanya jitihada zao , ila wahusika hawakuwepo .

File closed...yaani Easy kihivyo tuu, kama makonda ambavyo aliikimbia kamati ya Nape...Sheria zitawalinda tuu.

Ni mtazamo tuu mkuu.
Acha kujitia upofu, katika matamshi ya kufuatiliwa na kutishiwa aliyatoa pamoja na matamshi ya bombardier. Mbona walichambua na kuchukua ya bombardier na kumkamata kuwa ametoa maneno ya uchochezi? Inamaana yale ya kutishiwa maisha waliona hayawafai? Halafu kama hakuriport mbona walimkamata na kumfungulia kesi? Nani aliripoti kwa jeshi la polisi kuhusu uchochezi na akashindwa kuripoti hayo ya kutishiwa maisha?

Hata wafurukute vipi hii aibu haifichiki na double standard inaonekana wazi kama ya mbuzi
 
Kauli hiyo haiwezi kuwa ya Kamanda, Kwani anabembelezwa KUTOA USHIRIKIANO kwanini Haijatumika nguvu ILI KUSAIDIA POLISI
 
M/kiti wao kaloa jasho sana kutoa maelezo leo.
Mpk sasa mil 200+ ishakwenda endeleeni kuchanga watu wa ufipa na mihemko yenu
Hahahaha mkuu, usimwamshe Alie lala, acha mipopima iendelee kuchangia tu, halafu watukuja kulalamika hapa hapa subiri,,

Watu wanajua kutumia fursa acha kabisa.
 
Kwenye hili kwa maoni yangu vyombo vyetu vya Ulinzi &Usalama vimechemka, naongelea dereva wa Tundu Lisu, iweje atakiwe kuhojiwa hlf atoroshwe nje ya nchi na waliomtorosha wapo hapa nchini tena wanafanya press conference?

Hii ni dharau kubwa sana kwa nchi yetu kwa maoni yangu, Serikali ilipaswa itumie nguvu kuitaka Serikali ya Kenya imrudishe kwa nguvu huyo Dereva na kumkabidhi, tuna makubaliano na nchi ya Kenya na hili linawezekana, tuache kuchezeana kwenye maswala ya nchi, Nchi siyo Familia yako, nchi ni maisha ya watu zaidi ya Milioni 40, kilichotokea ni kama vile mimi nifanye uhalifu hlf Askari wanitafute ndugu yangu anichukuwe na kunikimbiza nje ya nchi, ni wapi huu ujinga unafanyika?

Arrest warrant itolewe na huyu dereva arejeshwe nchini kwa nguvu acheni mchezo, mambo ya sijui albadir mara malipo sijui hapa Duniani huo ujinga haujawahi kujenga nchi, kamata huyo mtu hata kama yuko wheel chair arudishwe hapa, ...


Teh teh teh teh teh teh teh
 
Moroto na sarakasi endelea tuu mkuu Dodoma ilivyo Ndogo zipigwe risasi zaidi ya 30 hakuna hata police aliesikia mpo busy na drama kwa Dereva...
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto ameeleza kusikitishwa kwao na kitendo cha dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kutokufika polisi na kutoa maelezo yake.

Kamanda Muroto amesema hayo leo Jumatano wakati akijibu swali la upelelezi unaendeleaje kuhusu tukio hilo.

Amesema upepelezi unaendelea kuhusu tukio la Lissu kupigwa risasi na watu mbalimbali wanaendelea kuhojiwa wakiwemo wamiliki nane wa gari aina ya Nissan ambazo zilikamatwa kuhusiana na shambulizi hilo.

“Wamiliki wa gari tumewahoji na tunapogundua hakuna muunganiko wowote basi tunaachana nao maana hakuna haja ya kuendelea kuwashikilia au kushikilia gari hizo,” amesema.

Hata hivyo Kamanda Muroto amesema anasikitishwa na kitendo cha aliyekuwa dereva wa mbunge huyo wakati wa tukio kutoonyesha ushirikiano kwa jeshi la polisi.

“Tunasikia yupo nje ya nchi na hadi leo hajaitikia wito wa kufika polisi kupata maelezo yake ambayo yangesaidia katika upepelezi wa tukio hilo.”

Chanzo: Mwananchi
Hamkua na nia ,kwani aliondoka saa ngapi nchini acheni kutufanya wajinga wa fikra
 
Naomba kujuzwa kama serikali hawahusiki na shambulio la Lissu!

Ivi inamaana dereva wa Lissu angefariki kwenye shambulio la Lissu wangefanyaje uchunguzi kama kauli zao za kusema kuwa wanamaubiri dereva wake ili kwanza wamuhoji?

Kwa intelejensia yao waliyonayo mpka sasa wameshindwa kujua wahusika?
 
Habari wakuu,kwanza naomba nianze na kulaani kitendo cha uhalifu wa kutumia silaha dhidi ya mh lissu.Pia naomba kupongeza juhudi za haraka zilizochukuliwa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuchunguza jambo hilo ili wahalifu wabainike na kufikishwa katika vyombo husika licha ya dharau na kebehi zinazofanywa dhidi yao eti hawana imani na vyombo vyetu vya ndani wanataka vyombo vya nje.

Pia na laani kwa nguvu zote kitendo cha mh mbowe na dereva wa lissu kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika naomba vyombo husika kuchukua hatua katika hilo kwani issue ya lissu ni ishu ya kosa la jinai hivyo kitendo walichokifanya ni kosa la jinai.Dereva wa lissu ndo shahidi namba moja kwani yeye ndo aligundua anafatiliwa akawaona wahalifu na anadai anawajua wahalifu sasa kitendo cha mbowe kumzuia kwenda kuhojiwa na kumficha nairobi sijui kinamaana gani? je mnategemea vyombo husika vitafanyaje kazi ilihali kuna baadhi ya watu wanazuia mashahidi kutoa ushahidi muhimu utakaowezesha kufanikisha uchunguzi kwa kiasi kikubwa?
Je mbowe anafaharibu uchunguzi kwa maslahi ya nani?

Mwisho naomba vyombo husika viwaburuze mahakamani mbowe na dereva wa lissu kwa kosa la kutotoa ushirikiano kwa vyombo vyenye mamlaka
 
Hivi kama kweli polisi walikuwa na nia na huo uchunguzi na kila wakipiga intelijensia yao inaonesha kuwa dereva wa Lissu ni muhimu wangeshindwa kumpata?.Ukweli ni kwamba hili suala hata mtoto wa chekechea huwezi kumdanganya.
 
Hivi kama kweli polisi walikuwa na nia na huo uchunguzi na kila wakipiga intelijensia yao inaonesha kuwa dereva wa Lissu ni muhimu wangeshindwa kumpata?.Ukweli ni kwamba hili suala hata mtoto wa chekechea huwezi kumdanganya.
watampata vipi wakati kafichwa nairobi
 
Wafanye haraka wanangoja nini hadi wakumbushwe?? Muda wote wako wapi hao police wasimkamate Freeman kama kweli yy ndo kakwamisha kesi au upelelezi.Tangu muda Lissu anakua attacked dereva alikuepo na alikwenda Nairobi late hours.After all Nairobi sio mbali why police wasifanye contacts na Interpol ili dereva awe arrested?? Vitu vingine ni upuuzi hata kuvijadili.
 
Back
Top Bottom