RPC Gilles Moroto: Tunasikitishwa na dereva wa Tundu Lissu kutoonyesha ushirikiano kwa jeshi hadi sasa

Huu ni upuuzi mtupu,katika maandamano,huwa mnasema intelligencia imewaonyesha kutakuwa na uvunjifu wa amani,
Sasa kama hamuwezi kufanya upelelezi,kwa sababu tu,majerui wa tukio hajatoa maelezo,basi hamfai kuendelea kula mishahara bule,mtakuwa ni viraza kweli kweli,huyo dereva,angepoteza maisha(God forbid) kwenye tukio,inamaana kesi ingekuwa imefika mwisho?hebu fanyeni kazi,acheni porojo porojo,
Ulimwengu wa sasa watu wanajua mengi kuhusu law enforcement,kwahiyo msituletee mapicha picha,
Hata kama political elites wa nchi hii,wamewatisha kwamba msilifuatilie sana suala hili,toeni sababu zingine,sio hizi za darasa LA kwanza,kwamba mnasubili ushirikiano,wa driver,mnaiabisha taaruma yenu,na utu uzima wenu,
 
Hivi polisi hawaruhusiwi kukuhoji kwa njia ya simu? Maana kama ni maelezo yanaweza yakarekodiwa pamoja na kuandikwa atakaporudi ataweka sahihi yake tu kama atakuwa anakubaliana nayo.
Kuna shuruti na nguvu hutumika wakati mwingine sasa kwa simu utabanwa je?
 
3. Death Row Records was very uncooperative with the police after 2Pac's death. They hardly told the police anything! In many occasions, the police and newsreporters couldn't even find people on Death Row Records to question. Here's another interesting fact... ABC interviewed Suge Knight after the shooting of 2Pac. He was asked, "If you knew who killed 2Pac, would you tell the police?". Suge then replied "Absolutly Not".

-Sio kweli kwamba hakufanywa suspect, ila alikuwa akivikwepa vyombo vya usalama kama afanyavyo huyu dereva wa lissu:D

Hahaha! Daah! Hata Suge Knight aliyekuwa akiendesha gari alilokuwemo Tupac siku ya kushambuliwa hakufanywa suspect right away na police. Kamateni suspects mnawafahamu acheni usanii.

Wameshaona ni issue ya motomoto na wakijaribu kukamata watuhumiwa, watakuwa wanaenda kinyume na mkuu wa nchi.
 
Hawa wanaujua ukweli halafu hawataki tu kutoa ushirikiano ili serikali ionekane ndio inamakosa, polisi sijui wanasubiri nini wasimkamate wakati sharia ipo wazi kabisa.
Mawazo ya wapumbavu wa kitanzania bwana, na wewe hapo ndio umeshafanya reasoning!? Mh nchi ina wajinga hii sijui chanzo chake ni kipi.
 
Can you testify that Magufuli is behind all this? .

Umesoma kweli nilichokiandika? Nimekwambia kauli zake alizozitoa zinatosha kumfanya awe mshukiwa namba moja. Sasa ingekuwa ni kazi ya Mahakama kuamua kama yeye kashiriki kutaka kumwua Lissu. Ila kwa kauli zake tu, anakuwa ni prime suspect kwenye nchi zenye watu wa kujielewa na taasisi huru za polisi, uchunguzi, haki na mahakama.

NB: naona umekwepa kujibu maswali yangu mengi tu. Nimekuuliza specific questions kutokana na yale uliyoyaandika, kama vile unavyosema ati hili si tukio la kwanza la wanasiasa kupigana risasi n.k.
 
3. Death Row Records was very uncooperative with the police after 2Pac's death. They hardly told the police anything! In many occasions, the police and newsreporters couldn't even find people on Death Row Records to question. Here's another interesting fact... ABC interviewed Suge Knight after the shooting of 2Pac. He was asked, "If you knew who killed 2Pac, would you tell the police?". Suge then replied "Absolutly Not".

-Sio kweli kwamba hakufanywa suspect, ila alikuwa akivikwepa vyombo vya usalama kama afanyavyo huyu dereva wa lissu:D
Hapana! Hiyo ya kufanywa suspect ni baada ya uhusiano wao na gangs kuwekwa wazi na ukweli kuwa walimshambulia mmojawapo wa rival gangsters wakati wakitoka kwenye pambano la Mike Tyson. Pia Suge alisema hivyo kuwa hata angekuwa anamfahamu muuwaji asingemtaja, ni kwasababu gangs hawana ushirikiano na polisi, na pia inaondoa street credibility kwasababu ni sawa na ku "rat". Wao huwa wanaamuwa kudeal na issue kimtaa na kulipiza badala ya kwenda polisi.

Kumbuka ilikuwa ni crips vs the blood kama sikosei ndo zilikuwa rival gangs in LA. Na ndiyo maana kukawepo na retaliation kwa Biggie Smalls kuuwawa.
 
Hivi polisi hawaruhusiwi kukuhoji kwa njia ya simu? Maana kama ni maelezo yanaweza yakarekodiwa pamoja na kuandikwa atakaporudi ataweka sahihi yake tu kama atakuwa anakubaliana nayo.
Over 70% ya maongezi ni body language; sio mara zote huwa watu wenye mafunzo ya communication skills wanaweza baini uongo ata bila ya kuwaambia (lakini body language reveals a lot)

Kuna kesi iliwahi tokea UK watoto wawili wenye umri wa miaka 10 kupotea; katika TV interview tu ya BBC school care taker alikuwa anaojiwa kawaida baada ya kuonysha majonzi mwishowe akatabasamu.

Hilo tu polisi walichukua inawezekana anaongopa na ndio kiliwafanya wamfuate na kumchukulia kama main suspect mpaka conviction ya murder.
 
Kwa hiyo dereva wa muhimu kuzidi wale FFU waliokua Geti kubwa la kuingilia ndani pale Area D wasifanye watanzania wapumbavu kiasi hicho
 
Dereva na lissu ndio mashahidi namba moja as walikuwepo kwenye tukio.... lissu yupo icu but dereva is physically ok, anapochelewa kutoa statement ndio jinsi anakwamisha upelelezi, kwanza sasa tunajuaje kama cdm wanampanga ili atakachoongea kiegemee upande mmoja n not the whole scenario o ni vipi kama atasahau minor details ambazo zingekua crucial to the whole investigation??

Ushaona wapi Polisi wa nchi moja wanaenda kufanya kazi ya kipolisi inayohusu nchi yao nchi nyingine (unless its a multinational crime) na hapo polisi wa Interpol wanahusika ... kama ni kuzitambua izo nissan o watuhumiwa wapelekewe kenya. Jaribu kufikiria kireality kidogo sio kimuvi muvi.

Na wale FFU waliofungulia Gari likaingia Ndani likafanya uhalifu then wakalifungulia likatoka acheni kufanya watanzania wapumbavu
 
Dereve ni shahidi muhimu katika hili. Kitendo cha chama shindani kuendelea kumtia" kizuizini" dereva huyo ili hasihojiwe na vyombo vya usalama na uchunguzi nchini kinachelewesha taratibu za kuwanasa waliohusika na tukio hilo.

Pia hii inaweza kutoa tafsiri mbaya kwa chama hicho shindani ya ni halisi ya kumshikilia kwa nguvu dereva huyo (sidhani kama aliomba kupewa ushauri huo wa kisaikolojia). Kiweledi chama shindani kinatakiwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vyetu maalumu vya kiuchunguzi.
Hakuna tafsiri mbaya.

Huyu mtu ameona mvua ya risasi na mtu akikutwa na mauti.
Ni tukio baya sana kuona mtu wa karibu yu karibu kupoteza maisha

Dereva anahitaji msaada wa afya, kwa wasiojua wanadhani ni suala rahisi tu
Wengine wanataka kufanya kitu cha kawaida, si tukio la kawaida hata kidogo

Pili, chama chake kimemchukua badala ya kumtelekeza. Wameeleza yupo Nairobi

Busara zinasema wamesha ji commit, wanajua alipo na wamezungumza kwa niaba yake. Ni suala la muda kuna ''wadhamini' atarudi na asiporudi wataulizwa

Tatu, kusema CDM wamezuia asihojiwe ni yale yale ya Kamanda 'ajitokeze, aripoti n.k''

Huyu hahojiwi si mtuhumiwa. Ni mtu aliyekuwepo anayeweza kueleza na si kuhojiwa. Kuhojiwa tayari kunamfanya awe mtuhumiwa, kwa lipi?

Kinachotanguliwa si ''kumjengea hofu''

Nne, Kamanda alitakiwa awasiliane na ndugu, marafiki na chama chake.

Katika hilo,jambo la kwanza ni kuhakikisha ana afya njema .

Mtu anaweza kuathirika kisaikolojia akashindwa kutoa maelezo ya maana, ni 'mgonjwa'
Alichofanya ni kumwita kwa amri, na tuhuma za 'kwanini aongee..., kwanini hivi na vile'

Hilo linamjengea hofu akiwa na hofu tayari na ni mbinu dhaifu

Katika tukio dereva amekuwa TL, kumfanya kama mhusika kunaongeza mashaka

Ndiyo maana independent investigator ni muhimu, tayari kuna mashaka kama unayoeleza


Dunia inapopiga kelele si jambo la kupuuza
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto ameeleza kusikitishwa kwao na kitendo cha dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kutokufika polisi na kutoa maelezo yake.

Kamanda Muroto amesema hayo leo Jumatano wakati akijibu swali la upelelezi unaendeleaje kuhusu tukio hilo.

Amesema upepelezi unaendelea kuhusu tukio la Lissu kupigwa risasi na watu mbalimbali wanaendelea kuhojiwa wakiwemo wamiliki nane wa gari aina ya Nissan ambazo zilikamatwa kuhusiana na shambulizi hilo.

“Wamiliki wa gari tumewahoji na tunapogundua hakuna muunganiko wowote basi tunaachana nao maana hakuna haja ya kuendelea kuwashikilia au kushikilia gari hizo,” amesema.

Hata hivyo Kamanda Muroto amesema anasikitishwa na kitendo cha aliyekuwa dereva wa mbunge huyo wakati wa tukio kutoonyesha ushirikiano kwa jeshi la polisi.

“Tunasikia yupo nje ya nchi na hadi leo hajaitikia wito wa kufika polisi kupata maelezo yake ambayo yangesaidia katika upepelezi wa tukio hilo.”

Chanzo: Mwananchi

Pamoja na kwamba anapata psychotherapy, lakini inawezekana anawaogopa polisi kwa usalama wake.

Siyo kila wakati ukali na amuri zitafanya kazi.

Aliwaona wauaji na inawezekana ni watu wa karibu na ninyi kwa hiyo inawezekana perceptions zake ni kwamba mnamwita kwa kumkebehi kwamba mnawajua wauaji. Lakini pia inawezekana anaogopa kuangukia mikononi mwa hao hwao wauaji, especially kama anajua wako juu ya polisi.

Inawezekana anahofu na usalama wake kama Roma Mkatoliki.

Anaweza kuwa na wasiwasi na ninyi kama vile Watanzania wengi wako na hiyo wasiwasi na ninyi.

Mlilpewa taarifa nyingi za kufuatiliwa kwa lisu tena kwa dispatch, hamkufanya lolote.

Tundulisu alipigwa dodoma. MLifahamu kwamba mnahitaji kupeleleza, driver wa Lisu alikuwepo lakin hamkuonyesha kumhitaji wala kujua hali yake.

Ni ngumu kuelewa.

Ni vizuri mkamsubiri ajitibu kwanza kama binadamu. Si mnyama. Ni binadamy ana damu na nyama. Sasa kwa kuwa mmeambiwa anaumwa, mwacheni apone halafu atakuja kuwaletea hizo taarifa. Uhai wake kwanza.
 
Polisi bana Usanii tupu kama ni shaidi No1 vp mnamtafuta baada ya saa zaid ya 30 na wakati upererez ulianza wakat ulele?Vp lkn Walinzi wa Naibu Spika na Wa Geti la Kuingia kwenye Nyumba hizo wamewapa Ushaid wowote maana Risasi zaid ya 30 hawakuzisikia ukizingatia Ulinzi wa Naibu ni Wa uhakika

Sent using Jamii Forums mobile app

upelelezi ndugu, sio upererezi, haujawahi kusoma magazeti ya Tanzania?

mnaudhi sana, kiswahili hauwezi, kiingereza hauwezi,

ebu kuweni serious watanzania na lugha yetu hii, ni aibu kukosea vitu basic kama hivi
 
polisi wanamtaka derevea aliyekuwa anaendesha gari la lissu awasaidie ili wawapate wale waliomshambulia mh lissu. cdm mnabisha kuwapa angalie wa meja jeneral mstaafu. kawasaidia haraka sana wamepatikana watuhumiwa au washukiwa. msibishane na polisi nyie. polisi akikwambia we umekufa unatakiwa ukazikwe basi kubali tu tukupeleke ukazikwe.

usibishane na wataalamu wa hayo mambo .nyie wapeni huyo dereva ili wawapate walimoshambulia maskini mtanzania wa watu mh tundu antipasi lissu. wapeni msibishe. madereva huwa waa ujuzi wa kutambua wahalifu. acheni ubishi usio na sababu.
 
Kweli kabisa mkuu, tunaweza mpoteza Lisu kwasababu ya wajinga wachache wanajifanya wanajua kuliko hali halisi iliyopo. Wangekubali dereva ahojiwe alafu Lisu apelekwe nje akatibiwe hapo Nairobi sio mbinguni ....

Umenifurahisha uliposema ukiambiwa ukazikwe kubali....hahahaaa!, hata km bado napumua itanibidi nikubali kuzikwa??
 
Mzee kwema lakini?

Mbona unaandika kwa pupa bila kutuambia madereva hua wanapata wapi hayo mafunzo ya kutambua wahalifu.

Na kama hua wanayapata, dereva wa meja na wa Lisu watapata mafunzo sawa?

Wana obligations sawa za kushirikiana na askari?

Walishambuliwa idadi sawa za risasi?

Au mmoja hakushambuliwa?

Au haujala mpaka sasa hivi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom