RPC Arusha Ajivua Vurugu za Polisi leo. Asema ni AICC Wanahusika

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,631
1,925
Nilimsikiliza Kamanda wa polisi Arusha akihojiwa na Radio Sunrise jioni na alisema hivi.

AICC walikataa uwanja wao usitumike kuaga miili ya waliouwawa juzi Jumamosi kwa hiyo polisi waliwekwa eneo hilo kuzuia CHADEMA wasitumie uwanja huo kwa shughuli hiyo kwa kuombwa na AICC.

My take.
  1. Uwanja huu wa soweto ulitumika kwa muda wote wa kampeni na vyama vyote toka mwazo.
  2. Uwanja huu ulitumika tarehe 15 June siku bomu lilipolipuliwa hapo hapo uwanjani na kuuwa watu na kujeruhi wengi.
  3. Hata jana uwanja huo ulitumika na ulinzi ulikuwa wa JWTZ. Wananchi waliambiwa leo wataaga miili hiyo na hakukuwa na kizuizi cho chote.
  4. Iweje leo mkurugenzi wa hicho kituo akataze usitumike kuaga marehemu?
  5. Je asingekataa maafa ya leo yangetokea?
  6. Je hakuna uhusiano kati ya KAaya huyo mkuu wa AICC ambaye ni gamba chovu kuhusika na mpango mzima ?
  7. Je kamanda Sabas hakuona umuhimu wa kuwashauri hao AICC waruhusu uwanja utumike kwa kuwa ulishatumika muda wote na leo ndio likuwa hitimisho.
  8. Kaaya uje huku utambie kwa nini ulikataza uwanja usitumike siku moja wakati ulisharuhusu muda wote wa kampeni. Nahisi unahusika moja kwa moja na hicho ndicho alichoimanisha Kamanda Sabas.
 
If that is true, then this Kaaya man should be put to task. Hakuna aliye juu ya sheria.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Elishilia Kaaya, Walikutupa kura za maoni arumeru mashariki last year, leo unakubali tena wakutumie??

Sijaonaga mmeru wa hivi. Shtuka kama kina Sarakikya.
 
Huyo Kaaya atafutwe aseme alikuwa na sababu gani za msingi asituletee ujinga na itikadi zake za ccm
 
Elishilia Kaaya, Walikutupa kura za maoni arumeru mashariki last year, leo unakubali tena wakutumie??

Sijaonaga mmeru wa hivi. Shtuka kama kina Sarakikya.



Hata cku moja hata Mi cjawahi ona Mmeru janga kama huyu!
Shwain sana Kaaya!
 
Hata kama alikataa bado polisi walitakiwa kutumia busara ili kuepusha majanga yasiyo na lazima.Ninadhani kwenye Katiba ya nchi inayokuja inabidi mtu yoyote anayetaka kuingia kwenye jeshi hilo awe na minimum qulification ya Advance level education na pass mark zisizopungua division three ili tupate polisi wenye weledi na wanoikiria zaidi na kwa haraka kabla hawajapiga mabomu ya machozi hovyo.
 
Kiukweli hakukuwa na sababu yoyote ya kutumia nguvu kubwa kuzuia kusanyiko katika uwanja huo wa SOWETO haswa ikizingatiwa kusudio la kuutoa yaani kampeni zilizokuwa zihitimishwe kwa uchaguzi.,uchaguzi haujafanyika na watu hawa ni wahanga tayari katika uwanja huo."UTU NA USTAARABU WA MWAFRIKA,MTANZANIA UWAPI?Ujamaa na udugu kwishney???
 
Kweli mkuu kama walionyesha ushirikiano muda wote wangemalizia kabisa na hiyo shughuli ya kuaga, ukiona hivyo wanatumiwa pia hakuna kitu kibaya kufanya maamuzi huku mna hasira maana wakati mnakubaliana hakuna kujiuliza kiundani kuhusu mpango wenu kiundani zaidi kwa kuangalia angle zote
 
Leo ni habari moto moto tu jeiefu raha

Imekuwa poa kweli leo maana wiki nzima JF nilikuwa naipata kwa kwiki kiasi nikitaka kufungua uzi inakuja BAD 400 inatokea blunk page but kuanzia leo naona mambo poa na habari moto moto kwa kwenda mbele
 
Hivi AICC ni shirika la mtu binafsi au la serikali? Kama ni la serikali linatoa wapi mamlaka ya kuzuia uwanja usitumiwe na watanzania ilihali ni mali ya watanzania?
 
Kama huu uwanja ulikuwa unatumika siku zote kwenye kampeni,kwa nini leo wagome uwanja usitumike?
 
​
1016222_709997279026534_467189810_n.jpg
 
Imekuwa poa kweli leo maana wiki nzima JF nilikuwa naipata kwa kwiki kiasi nikitaka kufungua uzi inakuja BAD 400 inatokea blunk page but kuanzia leo naona mambo poa na habari moto moto kwa kwenda mbele

Mkuu nilidhani tatizo hilo nilikuwa nalipata peke yangu kumbe ni wengi jf!.. Kweli sasa mambo safi!
 
Waziri Mkuu Mizengo pinda amesema bomu lililotumika kuulia wanachadema limetoka CHINA...

Hivi lile gamba lililoenda china kupata mafunzo ya ukakamavu na kurudi na kofia yenye nyota ya kikomunisti halihusiki hapa?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom