Mfamaji
JF-Expert Member
- Nov 6, 2007
- 6,631
- 1,926
Nilimsikiliza Kamanda wa polisi Arusha akihojiwa na Radio Sunrise jioni na alisema hivi.
AICC walikataa uwanja wao usitumike kuaga miili ya waliouwawa juzi Jumamosi kwa hiyo polisi waliwekwa eneo hilo kuzuia CHADEMA wasitumie uwanja huo kwa shughuli hiyo kwa kuombwa na AICC.
My take.
AICC walikataa uwanja wao usitumike kuaga miili ya waliouwawa juzi Jumamosi kwa hiyo polisi waliwekwa eneo hilo kuzuia CHADEMA wasitumie uwanja huo kwa shughuli hiyo kwa kuombwa na AICC.
My take.
- Uwanja huu wa soweto ulitumika kwa muda wote wa kampeni na vyama vyote toka mwazo.
- Uwanja huu ulitumika tarehe 15 June siku bomu lilipolipuliwa hapo hapo uwanjani na kuuwa watu na kujeruhi wengi.
- Hata jana uwanja huo ulitumika na ulinzi ulikuwa wa JWTZ. Wananchi waliambiwa leo wataaga miili hiyo na hakukuwa na kizuizi cho chote.
- Iweje leo mkurugenzi wa hicho kituo akataze usitumike kuaga marehemu?
- Je asingekataa maafa ya leo yangetokea?
- Je hakuna uhusiano kati ya KAaya huyo mkuu wa AICC ambaye ni gamba chovu kuhusika na mpango mzima ?
- Je kamanda Sabas hakuona umuhimu wa kuwashauri hao AICC waruhusu uwanja utumike kwa kuwa ulishatumika muda wote na leo ndio likuwa hitimisho.
- Kaaya uje huku utambie kwa nini ulikataza uwanja usitumike siku moja wakati ulisharuhusu muda wote wa kampeni. Nahisi unahusika moja kwa moja na hicho ndicho alichoimanisha Kamanda Sabas.