The Royal Tour ya Rais Samia ni wazo zuri lakini…

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
ROYAL TOUR NI WAZO ZURI LAKINI...

Nimetafakari sana kabla sijaandika maneno haya. Nina wazo gumu na mkono wangu hauna uwezo wa kuandika wazo langu kwa usahihi. Huu ni ulemavu wa wengi. Unachokitaka unakijua lakini kukiandika kwa usahihi huwezi.

Huku vijijini ukipata mgeni wa kulala, unamwandalia chumba. Wakati mwingine chumba cha kulala ndiyo stoo. Unachukua mashuka na vitenge unafunika visivyohusika. Mgeni analala na baadaye anaondoka bila kujua vilivyofunikwa na vitenge. Anafurahia ukarimu na kuahidi kurudi. Mgeni akikaa sana, kuna hatari ya kujua yaliyofunikwa.

Royal Tour ya Mama ni wazo zuri. Siku hizi kibaya na kizuri vyote vinajitembeza. Usipojitembeza utadoda.

Lakini Royal Tour inahitaji usuluhishi na mambo yetu ya chumbani yaliyofunikwa kwa vitenge. Wageni wakija wakayafunua, TUTAAIBIKA. Tumefunika haya:

1. Uhuru wa habari HAKUNA. Mama ananadi nchi, huku nyuma Msigwa anafungia magazeti. Watalii hushamiri penye uhuru wa habari. Serikali iache kuwa mhariri wa magazeti, redio na televisheni. Atakayekashifiwa aende mahakamani. Taifa lenye mtazamo mmoja si kivutio cha watalii.

2. Uhuru wa Kisiasa HAKUNA. Hata chama tawala hakiko huru kufanya siasa. Bila uhuru wa kisiasa Taifa linageuka kuwa TALIBAN STATE. Mtutu wa bunduki una thamani kuliko katiba na mahakama.

3. Haki za Binadamu HAKUNA. Bila haki za Binadamu, wanawake si sawa na wanaume, weusi si sawa na weupe na matajiri si sawa na Maskini. Tumeona watu wanahoji HANGAYA kuwa Chifu kwa sababu tu, hana ndevu! Bila haki za Binadamu, ROYAL TOUR ni pipa lililotoboka. Halihifadhi maji.

4. Usawa mbele ya sheria HAKUNA. Matokeo yake, wenye madaraka wana haki zaidi mbele ya sheria kuliko wasio na madaraka. Hili ni tanuru la machafuko kwa sababu kuna wanaoamini haki iko mikononi mwao. Tunaishi kwa utulivu si kwa amani.

5. Uhalali (legitimacy) HAKUNA. Kukubalika hutokana na uhalali. Tuna mfumo wa utawala unaopungukiwa na uhalali. Ulipita bila kupingwa, ulipigiwa kura bila kuchaguliwa, ulichaguliwa bila kukubaliwa na uliapishwa bila kuhalalishwa. Hili ni deni la dhamiri. Halilipiki kibinadamu. Mungu tu ndiye Pay Master. Inatisha kukutana naye mubashara. Katiba Mpya yaweza kupunguza kero hii.

Haya 5 na mengine madogo madogo ni mazito kuliko Royal Tour. Tuchague kati ya kupata wageni watakaokuja na kuahidi kurudi tena na wale watakaokuja na kuapa kutorudi tena.

Tukisafisha nyumbani, watakuja na kuahidi kurudi tena. Tusiposafisha, hata wenyeji wataondoka. Dhuluma haivumiliki.

Askofu Bagonza

A2E0DE6D-C98F-41FB-AD18-B554371366C1.jpeg
 
Ben Saanane alipotea wananchi walikaa kimya.

Vyama vya upinzani haviruhusiwi kufanya mikutano yeyote ile na wananchi pia wanachama wake. Wananchi wamekaa kimya.

Huwezi kuwa kiongozi hata wa mtaa kama wewe si mwana CCM. Wananchi wamekaa kimya.

Kura feki ziliokotwa na uchaguzi kuchakachuliwa. Wananchi wamekaa kimya.

Tuendelee kukaa kimya mpaka Masiah atakaporudi.
 
ROYAL TOUR NI WAZO ZURI LAKINI.

Royal tour Nzuri lakini haikupasa kiongozi wa nchi kupuuza matatizo mengi ya wapinzani kupigwa, kuzuiwa mikutano huku yeye akizunguka na kuaminisha Mabeberu kuwa kuna demokrasia wakati wana mabalozi, wanaona mitandaoni nk.

lakini pia, kuna mengi tu, hii ROYAL TOUR hatuja ambowa fedha zilipotoka, nani anakagua, nani kapewa tenda, tenda ilipatikanaje? kuna kashfa kubwa itakuja kuliko EPA NA ESCRWO

Nimetafakari sana kabla sijaandika maneno haya. Nina wazo gumu na mkono wangu hauna uwezo wa kuandika wazo langu kwa usahihi. Huu ni ulemavu wa wengi. Unachokitaka unakijua lakini kukiandika kwa usahihi huwezi.

Huku vijijini ukipata mgeni wa kulala, unamwandalia chumba. Wakati mwingine chumba cha kulala ndiyo stoo. Unachukua mashuka na vitenge unafunika visivyohusika. Mgeni analala na baadaye anaondoka bila kujua vilivyofunikwa na vitenge. Anafurahia ukarimu na kuahidi kurudi. Mgeni akikaa sana, kuna hatari ya kujua yaliyofunikwa.

Royal Tour ya Mama ni wazo zuri. Siku hizi kibaya na kizuri vyote vinajitembeza. Usipojitembeza utadoda.

Lakini Royal Tour inahitaji usuluhishi na mambo yetu ya chumbani yaliyofunikwa kwa vitenge. Wageni wakija wakayafunua, TUTAAIBIKA. Tumefunika haya:

1. Uhuru wa habari HAKUNA. Mama ananadi nchi, huku nyuma Msigwa anafungia magazeti. Watalii hushamiri penye uhuru wa habari. Serikali iache kuwa mhariri wa magazeti, redio na televisheni. Atakayekashifiwa aende mahakamani. Taifa lenye mtazamo mmoja si kivutio cha watalii.

2. Uhuru wa Kisiasa HAKUNA. Hata chama tawala hakiko huru kufanya siasa. Bila uhuru wa kisiasa Taifa linageuka kuwa TALIBAN STATE. Mtutu wa bunduki una thamani kuliko katiba na mahakama.

3. Haki za Binadamu HAKUNA. Bila haki za Binadamu, wanawake si sawa na wanaume, weusi si sawa na weupe na matajiri si sawa na Maskini. Tumeona watu wanahoji HANGAYA kuwa Chifu kwa sababu tu, hana ndevu! Bila haki za Binadamu, ROYAL TOUR ni pipa lililotoboka. Halihifadhi maji.

4. Usawa mbele ya sheria HAKUNA. Matokeo yake, wenye madaraka wana haki zaidi mbele ya sheria kuliko wasio na madaraka. Hili ni tanuru la machafuko kwa sababu kuna wanaoamini haki iko mikononi mwao. Tunaishi kwa utulivu si kwa amani.

5. Uhalali (legitimacy) HAKUNA. Kukubalika hutokana na uhalali. Tuna mfumo wa utawala unaopungukiwa na uhalali. Ulipita bila kupingwa, ulipigiwa kura bila kuchaguliwa, ulichaguliwa bila kukubaliwa na uliapishwa bila kuhalalishwa. Hili ni deni la dhamiri. Halilipiki kibinadamu. Mungu tu ndiye Pay Master. Inatisha kukutana naye mubashara. Katiba Mpya yaweza kupunguza kero hii.

Haya 5 na mengine madogo madogo ni mazito kuliko Royal Tour. Tuchague kati ya kupata wageni watakaokuja na kuahidi kurudi tena na wale watakaokuja na kuapa kutorudi tena.

Tukisafisha nyumbani, watakuja na kuahidi kurudi tena. Tusiposafisha, hata wenyeji wataondoka. Dhuluma haivumiliki
 
Mama ama anajishauri au anashauriwa vibaya, changamoto ya utalii Tanzania siyo 'kutangaza vivutio' Duniani. Kuna sehemu Duniani hawajui Tanzania ni moja ya sehemu zenye vivutio? Serengeti, Mikumi, Kilimanjaro, Zanzibar n.k vinajulikana sana.

Changamoto kubwa ni gharama za utalii kwa wageni na ukilitimba wa huduma kuanzia pale Airport hadi Mbugani. Ndiyo maana watalii wakija siyo wote baadae watatamani tena kurudi Tanzania. Hili la Mama Hangaya kuzurura ku-shoot a film siyo baya bali siyo hitaji muhimu kimkakati katika kukuza utalii wetu.

Umeandika vitu vya msingi sana.
 
gharama si tatizo ila wazungu wapo makini sana, hawezi lipa dola zake zitumike kuuwa watu kama Tundu lissu, akwilina, na wengine wengi.
 
Back
Top Bottom