TRL
Treni hizi zitasimama kwenye vituo sita (6) vifuatavyo:
Stesheni ya Dar es Salaam, Kamata, Buguruni kwa Mnyamani, Tabata Matumbi, Mabibo na Ubungo Maziwa. Kila treni itakuwa na mabehewa sita yenye uwezo wa kubeba abiria waliokaa na wale waliosimama takriban 1,000 kila safari.
TAZARA:
vituo vya Dar es Salaam, Kwa fundi umeme, Yombo, Kwa Limboa, Lumo Kigilagila, Barabara ya Kitunda, Kipunguni B, Moshi Bar, Majohe, Shule ya Sekondari Magnus, Mwakanga, Chimwaga, Maputo, Mtoni relini, Kwa Azizi Ali relini hadi Kurasini. Kuanza kwa usafiri huu kutachangia kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam na kuwezesha watu kufika katikati ya jiji haraka zaidi.
Kwa utaratibu huu inakisiwa kwamba treni hizi mbili zitaweza kusafirisha watu takriban 16,000 kwa siku kwa safari 8 asbi na 8 jioni
Izi project kuanza rasmi october 2012
Source:hotuba ya bajeti ya wizara 2012/13
Ministry of Transport, Tanzania - Publications | Waziri wa Uchukuzi awasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2012-13
Chukulia kila kipanya kinabeba abiria 20 mpaka kumaliza route moja, utagundua makadirio ya route 800 za vipanya zimeondolewa kwa siku. Kama kila kipanya kinafanya wastani wa trip 10, utagundua huu mpango utaondoa vipanya kama 80 hivi kwa siku ya kawaida.Idea nzuri lakini watu 16,000 ni wachache sana kwa treni ya siku nzima kuna kitu hakiko sawa hata gharama za kuilipia treni haita cover.
Nampongeza sana Mwakyembe, na pia namtahadharisha awe makini sana hasa na uhai wake. Rizwani juzi kaingiza trailer 50 na 100 zipo njiani.
kwa sababu wanaolengwa siyo wenye magari! As a matter of fact nadhani itachangia zaidi ongezeko la magari jijini Dar. Think about it.
Yule ambae yuko mbezi au kimara, anasogea na usafiri wa kawaida mpaka Ubungo, anapanda tren sio kila mtu imfikie kwake wamejaribu kurahisisha. Kwa wale wa Kawe kuna boti itapita baharini.Kwa hiyo hizo treni zimetengenezwa kwa ajili ya wakazi wa huko tabata, wale wa mbezi kawe mikocheni msasani obay imekula kwao sio
Yule ambae yuko mbezi au kimara, anasogea na usafiri wa kawaida mpaka Ubungo, anapanda tren sio kila mtu imfikie kwake wamejaribu kurahisisha. Kwa wale wa Kawe kuna boti itapita baharini.
Sasa hizo trailer zitabeba abiria wangapi toka kati mpaka ubungo? Au tueleze hizo tela zina manufaa gani hapa
Chukulia kila kipanya kinabeba abiria 20 mpaka kumaliza route moja, utagundua makadirio ya route 800 za vipanya zimeondolewa kwa siku. Kama kila kipanya kinafanya wastani wa trip 10, utagundua huu mpango utaondoa vipanya kama 80 hivi kwa siku ya kawaida.
Swali la msingi ni kwenye collateral damage ambalo linaweza kufanya watu waanze kufitiniana.
Kama kila abiria akilipa Tsh 500, mapato kwa siku ni kama 8 milioni hivi. Je kati ya hizi ni ngapi zitarudi kwenye mtaji na ngapi zitawezesha uendeshaji wa kila siku. Labda tutaambiwa bajeti ijayo na hapo shaka lako la msingi litajibiwa.
Niambieni, Gongolamboto na Mbagala hakutakuwa na usafiri huu?.
Hii kitu inatumiwa sana kwenye miji ya wenzetu.
Well done JK