King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 51,632
- 68,561
Mipango mbali kutekeleza mbali ccm tafuteni hela zenu ndio muweke hyo miradi sio mnaplan nyingiiii kwa kutegemea hela sa wavuja jasho(wanachama wa nssf/ppf)
tulipiga kelele sana kuwa mradi wa mabasi hauwezekani UMEWEZEKANA.......sasa tunapiga kelele kuwa hilo la treni haliwezekani MWAKYEMBE na timu yake WANAANZA KUONYESHA WANAWEZA
Sisi TUNAONGEA wao WANAFANYA........mwisho wa siku tutasema wameiba kura kwa sababu mikutano yao haijazi watu....KUMBE WENZETU HAWAONGEI KWA MIDOMO BALI VITENDO
Mipango mbali kutekeleza mbali ccm tafuteni hela zenu ndio muweke hyo miradi sio mnaplan nyingiiii kwa kutegemea hela sa wavuja jasho(wanachama wa nssf/ppf)
hakuna mtu anayekataa kuwa mabasi yaendayo kasi (kama ni kweli) na treni zitasaidia kwa muda kupunguza msongamano. Ila sio suluhisho la muda mrefu. Nigeria ni moja ya nchi zenye mfumo wa mabasi hayo lakini hali ya usafiri Lagos bado sio nzuri. Wale wenye umri uliosogea kukaribia mafao watakumbuka enzi zile UDA ilikuwepo yenyewe. Baadaye ilipozidiwa marehemu Sokoinne aliruhusu dala dala (wakati huo nauli ilikuwa shs 5) tatizo la usafiri likapungua sana. kwa vile hatukuwa na mipango endelevu tatizo likarudi pale pale kwa kiasi kikubwa. Hili litatatua kwa mwaka mmoja halafu tutarudi pale pale. Kutatua tatizo hili lazima ulitatue kwa jicho la uchumi mkubwa (macro economy). 1. treni kwa vile zinapita chini zitasababisha msongamano zaidi wa magari kwa vile njia zitafungwa mara kwa mara. (kumbuka network yake haikufikishi unapotaka kwenda. Mfano nakaa Tegeta nataka kuwahi mechi uwanja wa taifa nafikaje?
2. foleni zingine zinasababishwa na magari mabovu yanayofia njiani, kutokuwepo vituo/nadhamu kwa dala dala matokeo yake wanasimama barabarani na ujenzi usiozingatia maegesho unaoendelea.
kwa sababu wanaolengwa siyo wenye magari!
Pongezi kwa Mwakymbe umethubutu ni hatua nzuri ya kupambana na msongamano wa magari.
Mwakyembe adai Sh317.7 bilioni zinatosha bajeti yake | Send to a friend |
Saturday, 04 August 2012 10:44 |
Boniface Meena,Dodoma WAZIRI wa Uchukuzi,Dk Harrison Mwakyembe amesema Sh 317.7 bilioni alizoliomba Bunge kwa ajili ya bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2012/13 zinamtosha hata kama kuna watu wanasema kiasi hicho ni kidogo. Alisema ili wizara yake iweze kutekeleza majukumu na malengo yake katika mwaka huu wa fedha kiasi hicho kinatosha kuitoa sekta ya uchukuzi ICU. Dk Mwakyembe alisema hayo juzi wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2012/13. "Bajeti hii mimi inanitosha kwani sekta ya uchukuzi ilikuwa ICU,"alisema Dk Mwakyembe. Alisema kati ya fedha hizo Sh 64.9 bilioni zitakuwa ni za matumizi ya kawaida na Sh252.7bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. "Fedha za matumizi ya kawaida zinajumuisha Sh37.0 bilioni za mishahara ya watumishi na Sh27.8 , fedha za matumizi mengineyo,"alisema Dk Mwakyembe. Alisema fedha za miradi ya maendeleo zinajumuisha Sh189.7 bilioni ambazo ni fedha za ndani na Sh52.9 bilioni fedha za nje. Wakati Dk Mwakyembe akiomba kiasi hicho cha fedha, Kamati ya Bunge ya Miundombinu imesema, wizara hiyo imetengewa fedha kidogo ikilinganishwa na mahitaji halisi. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba aliliambia bunge kuwa wizara ya uchukuzi ni miongoni mwa wizara chache zinazoweza kuchochea ukuaji wa uchumi kwa haraka kwa kuwa fedha inayowekezwa katika wizara hiyo inakwenda kuzalisha fedha zitakazotumika kuboresha sekta nyingine. "Pamoja na ukweli huu, wizara hii imetengewa fedha kidogo ikilinganishwa na mahitaji halisi kwani mwaka wa fedha 2011/12 ilitengewa jumla ya Sh167.9 bilioni baada ya Bunge kushinikiza fedha za maendeleo ziongezwe katika sekta ya reli na bandari,"alisema Serukamba. Alisema Serikali iliahidi kuongeza Sh95 bilioni na hivyo fedha za maendeleo kufikia jumla ya Sh262.9 bilioni lakini hadi kufikia Mei mwaka huu fedha za maendeleo zilizotolewa ni jumla ya Sh96.7 bilioni sawa na asilimia 57.6 ya fedha ambayo bunge liliomba kutaka iongezwe. |
tulipiga kelele sana kuwa mradi wa mabasi hauwezekani UMEWEZEKANA.......sasa tunapiga kelele kuwa hilo la treni haliwezekani MWAKYEMBE na timu yake WANAANZA KUONYESHA WANAWEZA
Sisi TUNAONGEA wao WANAFANYA........mwisho wa siku tutasema wameiba kura kwa sababu mikutano yao haijazi watu....KUMBE WENZETU HAWAONGEI KWA MIDOMO BALI VITENDO
mbn bagamoyo road sioni route
Ni njia rahisi tu BabaDesi - kuwa na sheria/kanuni nzuri na utekelezaji wake. Kwa wenzetu wanakofuata sheria (na ustaarabu), mabasi yana mlango wa kuingilia na kutokea), wala hakuna konda au mpiga debe; unalipa kwa dereva anakupa tiketi au kutumia kadi maalumu ya malipo.....Mimi najiuliza jinsi watakavyoweza kudhibiti wadandiaji wa njiani watakaokuwa wanataka kusafiri bure kwenda/kutoka mjini kwa kutumia treni hizi ambazo zitakuwa haziendi kasi sana..
Kuna tatizo kwa huduma bora ya usafiri kuwalenga waso magari?
Kuna tatizo kwa huduma bora ya usafiri kuwalenga waso magari?