Roth ira ni nini na je unajua siri iliyojificha nyuma yake??

abcd123

Member
Nov 6, 2015
6
3
Wadau habari za mihangahiko.
Nimebahatika kusoma kitabu ambacho kinaelezea financial discipline and opportunities nikaona kitu kinaitwa Roth IRA je wewe wakijua??

Baada ya kusoma zaidi nikagundua kuwa ni kiasi cha hela ambacho mtu unaamua kukiwekeza katika mfuko flani wa pensiion au taasisi yoyote na iko hivi:

1.Hela unayoweka ndio inakatwa kodi hapo hapo
2.Hela unayotoa haikatwi kodi

Mfano ukiweka million 2 inakatwa kodi hapo hapo lakini ile hela inavyoongezeka thamani kwa wewe kuiwekeza humo hautakatwa kodi.

sasa cha ajabu nimejaribu kuulizia baadhi ya mifuko ya pension na mabank wanasema hiyo kitu ndo wameiskia kwako nikasema hii kweli kazi aisee.

Je nani humu ana idea na hii kitu maana nimeipata baada ya kusoma hiki kitabu kinachofundisha siri za utajiri while working.


Napatkana instagrame:adolphkato
Email: adolphkato86@gmail.com
 
Mkuu umenichekesha sana....uliposema hao wahusika hawajui....kitu kikubwa hapo tasisi zetu si wabunifu sana...wangechukua ilo wazo na kulifanyia utafiti....au hata kupendekeza ktk sera na sheria za kifedha....
 
Sasa jana tarehe 21/02/2017 nikaamua kwenda bank physicaly. Kwa kweli nimeamini Tanzania hii watu sio watafiti. Eti wakaniambia niende EWURA ndo huwa wana accounts kama hizi sasa nikawauliza kama wako na accounts hizi kwani wanafungulia wapi si ni Bank???? wakabaki wameniangalia tu sasa walikuwa watu wazima nikaona nisije kuonekana mbaya nikaondoka nitaendelea kufuatiliya mpaka nipate majibu
 
Sasa jana tarehe 21/02/2017 nikaamua kwenda bank physicaly. Kwa kweli nimeamini Tanzania hii watu sio watafiti. Eti wakaniambia niende EWURA ndo huwa wana accounts kama hizi sasa nikawauliza kama wako na accounts hizi kwani wanafungulia wapi si ni Bank???? wakabaki wameniangalia tu sasa walikuwa watu wazima nikaona nisije kuonekana mbaya nikaondoka nitaendelea kufuatiliya mpaka nipate majibu
Itakuwa haikuwa kwenye syllabus walizosoma. So unajua sisi watanzania tunasoma ili tufanye mitihani.
So hayo mambo mengine yanapuuzwa
 
ROTH IRA & 4O1K ni Accounts za Wamarekani ambazo zina benefits fulani za kodi ili kuwasaidia watu angalau wajitengenezee Uhuru wa Kifedha au ku Create utajiri. Kibongo bongo mabenki yanachojua ni kukamua watu kwa miriba kibao - Maana walikuwa wanafanya biashara na serikali, kwahiyo wewe kapuku mwenzangu unapoenda benki wanakuona kama kinyago na ili kukukataa kistaarabu wanakuambia riba 45%
 
Mambo ya vitabuni na bongo wapi na wapi.
Hapa tupeane dili za kuchoma mahindi na kuchukua viazi mviringo Uyole ndio angalau kwa mabaali tunaweza kuelewana
 
Back
Top Bottom