Mahitaji
Kwa ajili ya supu
Namna ya kutaarisha
Mahitaji
Michango ya wadau
Kwa ajili ya supu
- Viazi 4 vikubwa katakata round
- Nyanya 2 kubwa katakata
- Kitunguu maji 1 kikubwa
- Kitunguu saumu 1 tablespoon...
- Tangawizi 1 tablespoon..
- Bizar ya pilau 1/2 teaspoo.
- Mdalasini 1/2 teaspoon
- Curry powder 1/2 teaspoon (sio lazima)
- Nyanya ya kopo 1..
- Pilipili mboga 1
- Karot 1
- Chumvi kiasi
- Limau 1
Namna ya kutaarisha
- Kaanga viazi vikiwiva weka pembeni..
- Katika sufuria kaanga kitunguu maji Kwa dakika 10
- Weka pilipili mboga na karot
- Kaanga vikivaribia kuwiva weka nyanya kaanga vizuri
- Weka nyanya ya kopo na limau
- Ikiwiva weka viazi vichanganyike na rosti...taratibu viazi visivurugike
- Epua
Mahitaji
- Samaki wa vipande
- Pilipili ya kuwasha kiasi upendacho
- Pilipili manga 1 teaspoon
- Tangawizi 1 teaspoon
- Kitunguu saumu 1 teaspoon
- Chumvi kiasi
- Safisha vizuri samaki wako
- Mueke viungo vyote...muaxhe 30 min _-1 hour ili akolee viungo
- Weka pan yako mafuta
- Kaanga samaki
- Akiwiva weka kwenye bakuli lako la mchuzi mimina roasti ya viazi juu yake...
- Tayari kwa kuliwa.
Michango ya wadau
----Da #farkhina asante kwa mapishi, mie hupika sana mbatata jap hupenda kuzila na rosti la nyama ila leo nimejifunza style mpya!
Nauliza pale mwanzoni viazi unavikaanga na mafuta si ndio au sijaelewa??nimependa upishi huu
Miye huwa nakaanga rosti vizuri halaf viazi sikaangi huviweka baada ya rosti kukaribia kuiva kisha nikafunika hadi vyote vikaiva.ila ntajaribu hii style ya kukaanga kwanza viazi nimeipenda
farkhina weekend hii nataka nipike hii kitu...
Kwa kuongeza ladha katika hiyo roast ya viazi kwa wale waliopo TZ unaweza ukaongeza Onga Mchuzi Mix katika rojo la roast na wale wa mamtoni basi mnaweza kutumia chengachenga za Beef au Chicken bouillon(sina uhakika km s'markets za TZ wanayo hii)...