Rostam si wakulaumiwa yeye pekee yake bali Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam si wakulaumiwa yeye pekee yake bali Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chalamino, May 26, 2011.

 1. C

  Chalamino New Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu watanzania, chama cha mapinduzi kimemtumia Rostam aziz kwa muda mrefu katika kupora mali zetu, ili chama hicho kujipatia fedha za kuendeshea shughuli mbalimbali za kichama. Toka enzi za mkapa Rostam ametumika sana mpaka enzi za JK. Pesa nyingi za uchaguzi, CCM wamekuwa wakimtumia huyu mtu ili kupata fedha kwa ajiliya kuwalaghai wananchi wakitumia unyonge and umasikini walio nao . kwa hiyo viongozi wote waliochaguliwa kupia chama cha mapinduzi ukianzia Rais, wabunge and madiwani si halali. Ndiyo maana Rostam na wale wenzake hawawezi kufukunzwa kabisa ndani ya CCM eti ni mafisadi. CCM wasipende kutudanganya, maana wote ndani ya CCM wamefaidika na Ufisadi. Makampuni mengi ndiyo yalio chota pesa EPA ( External Payment Arrears) ndiyo yaliyomwingiza JK madarakani. Yote hayo makampuni yalikuwa yakiongozwa na kinara Rostam. kwa hiyo Rostam ametumika kama wakala wa CCM kwa kupewa tenda na mikataba isiyo ya kihalali ili kukipatia chama hicho pesa.
  NInawambia muda wa siku 90 au 120 hakuna atakaye fukuzwa ndani ya chama hicho kikongwe.Hata hivyo JK amempa Nape kazi ya kuwafukuza mapacha hao, kazi ambayo hata YeYe mwenyewe imemshinda. kwa hiyo nape ajue kwamba JK hampendi, amempa nafasi hiyo ili kumuua kisiasa na nape alivyo na mawazo mafupi na mwenye tamaa na madaraka akakubali tu bila kuangalia athari zake kwake yeye. kwam hiyo Rostam na wenzake wameitwa magamba ni pale walipoguza uwenyekiti wa JK. kwa hiyo ndugu watanzania wenzangu, viongozi wa chama hiki si wema na waadilifu maana kalibia wotekatika kutukandamiza na kupola mali za nchi yetu ambayo tulipaswa kunufaika wote. Tuwe makini na viongozi hawa wazalimu walio na roho ya korosho.
   
Loading...