Rostam nusura ajiumbue | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam nusura ajiumbue

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 2, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,818
  Likes Received: 83,216
  Trophy Points: 280
  Na Alfred Lucas

  Mwanahalisi~Maslahi ya taifa Mbele

  MFANYABIASHARA na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz amesitisha uchapishaji magazetini wa taarifa yake ya kukana tuhuma za ufisadi.

  Taarifa iliyokuwa inakwenda kwa njia ya tangazo, ilikuwa inakana kuhusika kwake na kampuni ya kufua umeme kwa njia ya upepo ya Wind East Africa Limited.

  Kampuni hii inatuhumiwa kupora ardhi ya wananchi katika kijiji cha Kisasida, mkoani Singida na taarifa zinasema tayari watu wameanza kuhamishwa kwa nguvu kama inavyofanywa kwenye maeneo yenye migodi ya madini mbalimbali.

  Taarifa zinasema uhamishaji watu kwa nguvu unafanywa kwa msaada wa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Parseko Kone.

  Hata hivyo, madai hayo yamekanushwa vikali na Kone akisema, "Mimi sijaenda huko na wala si kazi yangu kuhamisha watu. Kuna watu hapa wanafanya siasa na wanadhani kwamba mimi ni kikwazo katika kufanikisha malengo yao."

  Alisema, kampuni zinazodaiwa kugombea eneo awali zilikuwa kampuni moja. "Hizi kampuni awali zilikuwa moja. Zimegawanyika kutokan na sababu zao binfasi," alisema Kone katika mahojiano na gazeti hili kwa njia ya simu.

  Wananchi waliohojiwa katika eneo anapotaka kujenga mradi, wamesema kampuni ya Wind East Africa Limited haijawahi kuwalipa hata senti tano kama fidia.

  Tayari kampuni ya Rostam imepewa mkataba na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kwa njia ya upendeleo. Wameingia mkataba bila kuwa na miliki ya ardhi.

  Hata hivyo, katika taarifa yake aliyositisha uchapishaji wake, Rostam anamtuhumu mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa kuwa anampakazia kwa kudai kuwa anamiliki kampuni ya Wind East Africa Limited.

  Taarifa hiyo (MwanaHALISI inayo nakala), inasema anazushiwa na kwamba hahusiki na kampuni hiyo, bali imekuwa kawaida ya Dk. Slaa na washirika wake kumchafua yeye kwa kumpachika tuhuma zinazomhusisha na kampuni zilizokumbwa na kashfa za ufisadi.

  Dk. Slaa anamtuhumu Rostam kuwa ni fisadi mkubwa, na kwamba ni mmiliki wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited iliyochota zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Hata hivyo, Rostam hajakana kumiliki Kagoda.

  Rostam pia hajakana taarifa zilizohusu andishi la wakili wa Mahakama Kuu, Bhydinka Michael Sanze kuwa aliitwa na Rostam ofisini kwake 50 Mirambo, jijini Dar es Salaam , kusaini nyaraka zilizowezesha Kagoda mabilioni kutoka BoT.

  Katika andishi hilo la wakili Sanze, Rostam anatajwa kuwa ndiye kinara wa mpango wa kuchota mabilioni ya shilingi kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya BoT akitumia Kagoda.

  Ni katika andishi hilo ambamo Rostam anadaiwa kuwahusisha rais mstaafu Benjamin Mkapa, katibu mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula na aliyekuwa Gavana wa BoT, Dk. Daud Ballali.

  Wakili Sanze anaeleza kuwa Rostam, Peter Noni na Bered Malegesi walimthibitishia (yeye Sanze) kuwa Rostam alikuwa kwenye kikao ambapo Mkapa alitoa maelekezo kwa gavana Ballali kutoa fedha hizo kwa Rostam, kupitia Kagoda, kwa ajili ya shughuli za uchaguzi ndani ya CCM.

  "Rostam mwenyewe alisema, ‘system yote inajua,'" anaeleza Sanze. Hata katika taarifa aliyotaka ichapishwe katika vyombo vya habari, Rostam hakukana Kagoda.


  Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Karatu juzi, Dk. Slaa alisema ana uhakika kampuni ya Wind East Africa Limited ni mali ya Rostam akishirikiana na aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa.

  "Sikiliza bwana. Hii ni kama Kagoda. Kwenye nyaraka za usajili hakuna wanapoonekana. Lakini katika baadhi ya nyaraka nilizonazo, wanaonekana wamesaini vitu mbalimbali na kutumia anuani ya kampuni ya Rostam wakati wa kusajili.

  "Nawasubiri wakane. Nitawaumbua maana nimejiandaa kikamilifu. Mimi si mtu wa kukurupuka na Rostam anajua hivyo," anasema Dk. Slaa.

  Anasema bado anaamini kuwa hakuna mgongano wa maslahi, isipokuwa ufisadi unaofanywa na Rostam Aziz na rafiki zake, wakisaidiwa na mkuu wa mkoa wa Singida.

  Dk. Slaa anasema akina Rostam wanataka kuzalisha umeme wakati hawana eneo. "Hicho ndicho chanzo cha ugomvi wao na Dk. Mwakyembe (Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Kyela)."

  Alisema, "Nimekwenda Singida. Naufahamu vema mradi unaodaiwa. Nimeongea na wanakijiji Singida na viongozi wao. Kina Mwakyembe wanataka kuwakomboa wananchi, lakini kina Rostam wanataka kuwakandamiza.
   
 2. T

  Tofty JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2009
  Joined: Nov 6, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duh! Kaazi kweli kweli!!!
   
 3. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nchi ya wenyewe...
   
 4. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tutafika tu mkuu maana hawajaanza leo hao watu!!
   
 5. A

  August JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  Hivi August Mrema wa TLP si aliwahi kuja na Mpango wa mradi wa Umeme wa Upepo akapigwa Chini. Sasa hawa wa CCM wanapewa.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,599
  Likes Received: 18,608
  Trophy Points: 280
  Sasa kidogo na mimi ndio naanza kupata picha ya ugomvi wa King Maker na Dr. Harry. issue siyo conflict of interest ni conflict ya kimaslahi. wote wanamiliki kampuni za kufua umeme majina karbu yafanane. mmoja ana eneo hana mkataba. mmoja ana mkataba hana eneo.
  kwa maoni yangu, wote ni mafisadi.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hili Riburushi kwa nini mnalionea aibu jamani?
  Mnataka atutawale hadi kwenye familia zetu?Jamani inauma sana mi ngoja niende kwa bibi Swanga nampiga na kombora kali afie mbali atatunyanyasa mpaka lini?Kama mmeshindwa mi namloga.
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  hili wazo!
   
 9. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  rostam- inakuwaje mtu ana eneo alafu anao mkataba?

  mwak - yule mwenye eneo ajafanya chochote kibaya, ni kama wewe kuwa na shamba la mahindi
   
 10. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Na bado, mwaka huu tutasikia mengi.

  Infwakti huyu jamaa hayuko peke yake bali ametangulizwa na wanasisiemu wengine wasiopenda kujulikana kwa maslahi ya kisiasa.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,599
  Likes Received: 18,608
  Trophy Points: 280
  Baba Fidel, utakolalia, wenzio ndio wameamkia, nini S'wanga, wenzio wamekesha 'Mlingotini'.
   
 12. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2009
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona watu wengine hawatajwi amabo wanausika?
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,599
  Likes Received: 18,608
  Trophy Points: 280
  Bongo, kwanza unapata tenda(mkataba) ndipo unatafuta eneo. hii picha ilivyo japo Dr. Harry hakusema, mwanzo walikuwa wote, yeye akajitoa, wakaanzisha kampuni yao, wakakimbilia Singida kwa wananchi, wakapata eneo. Wenzao wakamwaga rupia, wakapata mkataba na kuamini watamwaga tena rupia kupata eneo.
  Kwa lugha nyingine, Dr. aliwazungunguka wenzake na sasa anapiga kelele kutafuta public symphathy. Mwisho wa movie, wote ni mafisadi, ila atakae cheka kweli, ni atakaecheka mwisho.
   
 14. senator

  senator JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2009
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Mdau umenena nukta hapo..hapa tunashuhudia mafahari wawili wanataka kuzichapa ila sitegemei kama nyasi zitaumia labda mahafahari hao kutoana ngeu wenyewe kwa wenyewe
   
 15. D

  Dina JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Hawa watu bwana, yaani wana mikataba mpaka ya wajukuu zetu....kweli tumekwisha! Hivi ni kweli kabisa kuwa there nothing that can be done? Na hakuna mtu yeyote wa kuwanyooshea kidole! Manake kama kelele tumepiga kweli kweli, lakini no reaction at all...
   
 16. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2009
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Tanzania presidential candidate accused of receiving foreign funding


  --------------------------------------------------------------------------------


  Member of Parliament for Igunga Constituency has to be honoured by the Ruling Party, CCM as he has facilitated JK to enter the State House. Read the story below:-
  Dar es Salaam, Tanzania (PANA) -

  Tanzania's controversial opposition leader, the Reverend Christopher Mtikila alleged Friday that ruling Chama cha Mapinduzi (CCM) presidential candidate Jakaya Kikwete had used funds from Iran to defeat his opponents at the party's recent convention.

  The Chairman of the Democratic Party claimed at a press conference that the Iranian government through Tanzanian MP Rostam Aziz, had funded Kikwete's campaign for over 10 years.

  The press conference was held ahead of a meeting by eight opposition parties to plan a common strategy against the CCM in Tanzania's October elections.

  Mtikila alleged that the Iranian government had set aside a substantial amount to prop presidential candidates in countries where the Asian country has economic interests.

  Aziz, a Tanzanian of Iranian extraction is representing Igunga constituency in Tanzania's Union Parliament on the platform of the CCM.

  Mtikila did not say how much Aziz had allegedly received from the Iranian government for Kikwete's presidential campaign, but cited Tanzania's uranium deposit as possible motivation for the alleged assistance.

  He said the Iranian government could not have given Aziz money for nothing: "they must be harbouring interests in Tanzania."

  This is the second time that Aziz, Kikwete's campaign manager, would be accused of securing foreign funds for Kikwete's presidential campaign.

  Last April, London-based journal, Africa Confidential claimed that he had been given two million US dollars by the Oman government as campaign funds for Kikwete.

  Kikwete, Tanzania's Foreign Affairs and International Co-operation Minister had vowed to sue the journal over the report, but since his nomination as CCM presidential candidate in May, he has said nothing about the report.

  The London journal has challenged him to go to court insisting it has overwhelming evidence to back its claims.

  There was no immediate reaction to Mtikila's allegations from either Aziz or Kikwete.

  Dar es Salaam - 16/09/2005

   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Apr 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Sasa nini nifanye niende Malawi nini maana mizizi ya Malawi nayo safi sana....
   
 18. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe una interest zako binafsi hapa! Sijamsikia Rostam akisema chochote, mbona Dr. tu ndio ana confidence ya kuongea na wananchi? Doesn't that ring a bell? Au ndio amekupigia simu umsemee nini?
   
 19. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #19
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Fidel80, mimi nadhani uchawi haupo Tanzania!

  Kwani kwa jinsi tunavo nyanyasika ndani ya nchi yetu kama kuna mtu ana teknologia hii kwanini asishughulike na hiyo lisiti ya watu 50 wanao imaliza nchi?, Yaani hata kwa kuwapiga upofu tu walau!
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sasa ndio tunaelekea kule ambako tutaanza kuona mgongano wa maslahi
   
Loading...