ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 42,727
- 49,419
Habari za Leo mdau.
Rostam Aziz mfanyabiashara mashuhuri Tanzania amesema ni ghali zaidi kuagiza bidhaa baina ya Nchi za Afrika ambazo ziko jirani kuliko Kuagiza bidhaa hizo hizo Ulaya,Asia au India.
Rostam alikuwa akizungumza kwenye utiaji saini wa Ujenzi wa mradi wake wa uwekezaji Nchini Kenya.
Rostam amesema Nchi za Kiafrika zinathamini zaidi wazungu kuliko kujithamini wenyewe.
My Take.
Hivi Waafrika tulirogwa au Kuna shida mahali? Kwa nini tunashindwa kuweka mazingira ya Intra-Afrika Trade ambayo itakuza ustawi wa watu Wetu na kufanya tupate uchumi Kwa haraka na kuwa na sauti kwenye majukwaa ya Kimataifa?
Yaani tatizo Huwa ni gani kwenye hizi Nchi zetu? Leo hii ukitaka usafiri wa kwenda West Afrika lazima uende Dubai nk ndio utapata usafiri wa kwenda huko..
Kuna mtu mmja alipata soko la bidhaa za kahawa nk West Afrika ila gharama za usafiri ni kama kutoka Tanzania kwenda Marekani Sasa huu upuuzi Hadi lini?
Maelfu ya watu wa Afrika wanakimbia Bara hili sababu za ujinga wa kama hivi,napenda kufahamu shida hasa ni zipi Hadi inakuwa ngumu Kwa Nchi za Afrika kuwa na mtengamano wa biashara?
Mwisho Afrika itabadili Vyama na Vyama Watawala huyu na yule ila bila kukata mzizi wa fitina wa mambo yanayokwamisha maendelea na Biashara tutaishia kupigana na kuuana hakuna Maendelea yeyote.mfano ni huko Nigeria, Ghana,Kenya,Malawi ,Zambia nk.
Binafsi ndio maana Huwa naunga mkono Rais yeyote kutoka chama chochote ambae ana mtizamo wa biashara na Huwa napinga sana Watu wenye mitizamo ya kijima na Kijamaa..
Namkubali Rais Samia Kwa sababu hii na namponga Mwendazake Kwa sababu ya sera za Kijima.Nadhani Kila mtu anaona tofauti ya Sasa na miaka 5 iliyopita.