Rostam na Kikwete Dhidi ya Dokta Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam na Kikwete Dhidi ya Dokta Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kulikoni Ughaibuni, Aug 26, 2010.

 1. Kulikoni Ughaibuni

  Kulikoni Ughaibuni JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 235
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005,mfanyabiashara controversial Rostam Aziz alitumia raslimali zake nyingi kuhakikisha mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM,Jakaya Kikwete,anashinda kwa gharama yoyote ile.Na kutokana na utajiri mkubwa alionao pamoja na mbinu zake mbalimbali,mchango wake ulimsaidia sana Kikwete kuingia Ikulu,na sasa ni Rais wetu anayeomba tena ridhaa ya kutuongoza kwa miaka mitano ijayo.

  Kati ya mwaka 2005 (baada ya Kikwete kuingia Ikulu) na sasa,Rostam ameibuka kuwa kiumbe mwenye nguvu za kutisha sio tu ndani ya CCM bali kwenye siasa za Tanzania kwa ujumla.Lakini kubwa zaidi katika kipindi hicho ni kwa mfanyabiashara huyo kuhusishwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi na Kikwete na serikali yake kushindwa kuwaridhisha Watanzania kwamba "hamkumbatii swahiba wake huyo".Haihitaji kurejea namna Rostam alivyohusishwa na ufisadi wa EPA (Kagoda) na ujambazi wa Richmond.

  Mwaka 2010,yaani mwaka huu,Rostam anaelekea kurejea tena ulingoni japo si kwa wazi sana.Ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuhusika kwa mfanyabiashara huyo katika kampeni za Kikwete.Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Rostam vimekuwa vikiendesha kampeni ya chuki dhidi ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema,Dokta Wilbroad Slaa,mwanasiasa anayeonekana kuwa tishio kwa mfanyabiashara huyo na vitendo vyake dhidi ya maslahi ya taifa.

  Na kama hilo la vyombo vya habari vya Rostam kumuandama Dkt Slaa halitoi mwangaza wa kutosha basi taarifa kwamba mwandishi mwandamizi wa kampuni ya Habari Corporation (inayomilikiwa na Rostam),Muhingo Rweyemamu,anatajwa kuwa mratibu wa kampeni za Kikwete.Itakumbukwa kuwa mwaka 2005,waliokuwa waandishi waandamizi wa Habari Corporation,Salva Rweyemamu na Dokta Gideon Shoo walitumika sana kwenye kampeni hizo.Baada ya kuingia Ikulu,Kikwete "alimzawadia" Salva ukurugenzi wa habari wa Ikulu,nafasi anayoshikilia hadi sasa.

  Kama alivyo Salva,Muhingo anasifika kwa uwezo wake wa hali ya juu wa kujenga hoja.Kwa bahati mbaya au makusudi,uwezo huo pia unatumika ipasavyo kutengeneza fitna.Wengi watakumbuka namna Dokta Salim Ahmed Salim,mmoja wa wana-CCM waliokuwa wanawania kuchuana na Kikwete,alivyoundiwa zengwe kubwa na kumhusisha na kundi la Hizbu la huko Zanzibar.Inaelekea kuwa mbinu hizohizo zimeanza kutumika dhidi ya Dokta Slaa,na kuna kila sababu ya kuamini kuwa kuna mengi yatakayoibuliwa dhidi yake.

  Yayumkinika kuamini kuwa waandishi wa habari wanaotumiwa kumchafua Dokta Slaa na Chadema kwa ujumla wanafanya hivyo kwa minajili ya "kupeleka mkono kinywani".Kubwa zaidi ni sapoti ya Rostam kwa Kikwete.Wakati mwaka 2005 alijibidiisha ili kufanikisha maslahi yake binafsi ya kibiashara (na amenufaika kweli-kwa kuangalia ishu za Kagoda na Richmond/Dowans) safari hii Rostam anahaha kumzuia Dokta Slaa kwa vile anafahamu fika kwamba laiti mwanasiasa huyo wa Chadema anayesifika kwa msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi akiingia Ikulu,zama za mafisadi kutumia jeuri yao ya fedha "kuendesha serikali kwa remote control" itakuwa imefikia kikomo.

  Kwahiyo,Dokta Slaa na Chadema kwa ujumla wanapaswa kuelewa kuwa safari hii Rostam ana "special mission" ya kuhakikisha "survival (kusalimika) yake.Atatumia kila raslimali aliyonayo kuhakikisha Dokta Slaa haingii Ikulu.Anafanya hivyo akifahamu wazi kuwa rais yeyote mwenye kujali maslahi ya nchi yake "atamkalia kooni" mfanyabisahara huyo na washirika wake.

  Hata hivyo,kwa vile si fedha za Rostam au wanahabari wake zitakazopiga kura kwenye uchaguzi mkuu,bali mimi na wewe pamoja na kila Mtanzania aliyechoshwa kuona nchi yetu ikigeuzwa "shamba la bibi",ni muhimu kwa wapiga kura kusema HAPANA.Tusitoe fursa kwa watu wenye maslahi binafsi kuipeleka nchi yetu kwenye maangamizi.Na ni muhimu zaidi kutambua kuwa baadhi ya watu hao wana utata wa kutosha tu kuhusu asili ya mahali walipozaliwa.Hiyo inamaanisha kuwa "wakishaiingiza Tanzania kwenye mtaro",watakuwa na sehemu ya kukimbilia.

  KILA MTANZANIA MWENYE KUITAKIA MEMA NCHI YETU ANAPASWA KUPAMBANA NA WAHUNI WA KISIASA WANAOTAKA KUTUWEKEA MADARAKANI VIONGOZI WANAOWAMUDU NA HIVYO KUENDELEA KUTUFISADI KAMA ILIVYOKUWA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO ILIYOPITA.


  INAWEZEKANA,TIMIZA WAJIBU WAKO

  KULIKONI UGHAIBUNI: Rostam Aziz na Kikwete Dhidi ya Dokta Slaa
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,381
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  UNAMSEMA ROSTAM AZIZI HUYU MSUKUMA/MNYAMWEZI WA UARABUNI...............??????
  JAMANI HAWA SI WAMEKUJA KUFANYA BIASHARA? KWA NINI TUNAWAINGIZA KWENYE MAMBO YA NCHI MPAKA WANAWAWEKA VIONGOZI DHAIFU KAMA KIKWETE MFUKONI..................KIKWETE TUNAJUA KATI YA MAKAMPUNI YA KIJAMBAZI ALIYOYASAMEHE KWA MASHARTI YA KURUDISHA HELA (MIMI NINAYESTAHILI KUJUA SIJUI KM ZIMERUDISHAWA KWELI) NA LA ROSTAMU LILIKUWEMO............
  TANZANIA YENYE NEEMA ALIYOIONA KIKWETE WAKATI ANAINGIA ikulu imekuwa neema kwa akina SALVA VIBARAKA NA AKINA LOWASA NA ROSTAMU YAANI NCHI YA KWETU.........IMEKUWA YAO
   
 3. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nikianza kuifikiria Tanzania hii ambayo baba wa Taifa alituachia huwa naumia sana,katika nchi hii maamuzi mengi kuihusu hufanywa na watu wachache au kikundi fulani chenye maslahi binafsi na kutufanya tuendelee kuwa masikini huku wao wakineemeka.
  Sitoshangaa kuona baada ya JK kuupata urais wakapata nafasi kubwa na nyeti katika serikali yake hivyo kwao kupiga debe kwa gharama yoyote sio tatizo ila wajue tu kuwa kila lililo jambo lina mwisho wake.
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135

  Rais alichaguliwa na wananchi
   
 5. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tuna kazi ngumu sana ya kuzibabilisha fikra za watanzania ili wauone ukweli huu na kumkataa JK na kundi lake la mafisadi. Iwapo wana wa nchi hii wenye uchungu na nchi yao wangeamka na kuungana, sidhani kama tungeshindwa kuuong'oolea mbali utawala huu dhalimu. Ni lazima sasa tuwe kitu kimoja ili tuweze kuipigania nchi yetu. Vizazi vijavyo vitatushangaa na kujiuliza iwapo sisi tulikuwa na akili timamu au mazezeta hadi kuruhusu wageni kuichezea nchi yetu kiasi hiki.
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Aug 26, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  umesema mzee, umesema.
   
 7. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo mafisadi papa na mafisadi nyangumi sasa wameungana; JK alikuwa anaondoka ila sasa wameshapozana; hujuma zao za kibishara zimerekebishwa; hapo ndio namuonaga Mengi kama kibaraka asiyejua anakokwenda; these differences could make something
   
 8. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  kwa ushawishi na pesa za nani???????????
   
 9. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kwa gharama ya Bil. 50...

  Huwezi kujiuliza??? Think..............
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Wa kulaumiwa ni sisi watanzania tunaofahamu fika kwamba Rostamu yupo hapa nchini kwa kazi moja tu, nayo ni kuwafundisha viongozi wa Tz namna ya kuziiba pesa zao wenyewe. Halafu tunawapa kura, Ona kura za maoni Rostamu kapita kwa kishindo ilihali hakuwahi kuzungumzia chochote bungeni kuhusu jimbo lake. Basi waweza fikiri hilo jimbo ni kama mojawapo ya majimbo ya nchi za dunia ya kwanza kumbe ni ufakiri wa kutisha umejaa kila kona ya jimbo. Wa Tz tuzinduke kuwang'oa kina Jk na kondi lake lote la mafya wa kibongo.
   
 11. M

  Malembeka Shija Member

  #11
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa wewe unasema nchi yetu wakati wote ni raia,na si ajabu wana haki zaidi kuliko wewe coz its possible haujawahi kuchangia chochote katika nchi hii kama kulipa kodi au maendeleo yoyote!
  Na hao mnao waita mafisadi hamna ushahidi wowote uliyo pelekwa mahakamani kama wanahusika na ufisadi....sasa itakuwa ni kitu cha ajabu kumdhania mtu kama anahusika na ufisadi.watu wote wangehukumiwa bila kupelekwa mahakamani!nashangaa watu wanaropoka hawajui sheria za nchi na kila mtu anataka kujifanya mwanasiasa.
  Hao unaowataka wewe waongoze nchi ni mafisadi na majambazi wa kupindukia....bora hawa tuliyokuwa nao wameshiba kuliko hao ambao itatuchukua 20 years kuwashibisha ndio washibe

  Think before you write
   
 12. M

  Malembeka Shija Member

  #12
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unasikitika nini kuhusu baba wa taifa????baba wa taifa aliacha nchi hoi....haina miundo mbinu,mashirika yote ya uma yalikufa,hata sabuni za kuogea zilikuwa hamna,there was no education,ilikuwa nchi ya ujamaa na kujitegemea,uhujumu uchumi nk. KILA MBUZI ATAKULA KWA UREFU WA KAMBA YAKE
   
 13. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Alichaguliwa na wananchi baada ya....
  1. Kumdhalilisha Salim Ahmed Salim
  2.kuiba hela nyingi tangu alipopigwa chini mwaka '95
  3.Kununua media yote Nchini Tanzania
  3.Kufanyia kampeni fedha za wizi za EPA
  4................
  5...............
  6................
   
 14. M

  Malembeka Shija Member

  #14
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao unawowasema wageni ni kama ngombe......wanachunga kutafuta majani na sisi waswahili tumekaa kama mawe,mpaka tubebwe tuhamishwe!toka lini sisi tukajiendesha wenyewe?hata hao viongozi mnaowataka waingie madarakani ni mafisadi nyangumi kama mengi coz hatukujua kuhusu ufisadi aliyoufanya hadi alipoanikwa hadharani!
   
 15. M

  Malembeka Shija Member

  #15
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usiwe kama ngo'mbe.....action speaks louder than words!wewe usifikiri kama rostam hajaongea ndio hamna maendeleo katika jimbo lake la igunga.ni wilaya inayoongoza nchi nzima kwa maendeleo. Huyu ni mbunge wa vitendo na sio maneno.kama unapenda maneno,mpigie kura mrema!wewe usifikiri wananchi wa igunga wanamng'ang'ania rostam bure.....wana akili kuliko mimi na wewe tuliyokaa dar nyuma ya laptop tunabishana!hayawani.......anakubalika mwanzo mwisho

  too much of self speaking is a sign of spiritual poverty
   
 16. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,508
  Likes Received: 1,232
  Trophy Points: 280
  Sio rostam na kikwete hata mengi naye kajiunga na ni mdau wa kikwete kaazi ipo kwa sissi makabwela kupambana na hii mijitu
   
 17. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  .
  Huyo Mengi uliyemtaja hapo tumemshuhudia akimwaga pesa nyingi tu kwenye miradi ya kimaendeleo ya taifa na vikundi vingi tu vya kujikwamua kiuchumi. Hebu taja mradi mmoja tu Rostamu aliowahi kuuchangia. Kagoda kakwapua dollar za kimarekani milioni 40. Na kilichoendelea hapo ni kuwapigia simu kina mkapa na Jk kuwajulisha kwamba mchezo umechezwa vema na kwenye account yako nimekutumbukizia asilimia 35. Hata kodi huyu mtu halipi, na hata makampuni anayomiliki hayopo direct kwani anajua jinai anayoifanya nchini na likizanda tu yeye anateleza kwenda kula na kina Ahmade najad na kumwacha mkwere akihangaika na wa-tz choka mbaya.
   
 18. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #18
  Aug 26, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
   
 19. M

  Martinez JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Unakumbuka wakati fulani ilipoibuka issue ya EPA na Richmond kupamba moto, Rostam alitoroka nchi akahamisha na baadhi ya kampuni zake na fedha zake. Baadaye nadhani JK alimtoa hofu ndio akarejea na kuanza kujibu makombora. The same to Jeetu Patel
   
 20. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2010
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,082
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Malembeka Shija ndo RA mwenyewe au? Mbona jazba sana :)
   
Loading...