Rostam, Msabaha, Kikwete and Richmond - Yes I said it again!

Hivi ile kesi ya RA kushitaki gazeti la Mwanahalisi imeishia wapi? nafikiri hapa ndo tungepata ukweli wa yote. Mmiliki wa Dowans anajulikana kabisaaa. niliambiwa kwa mdomo na mtu mwenyewe namjua. sina tu ushahidi. RA sio msafi hata chembe
 
Kwani magazeti si yameandikwa na watu kama akina mwanakijiji?

Kasheshe, recently you have been very personal with me.. do you have something you really want to say... just go ahead and say it. cheap shots ain't doing anything to me.
 
sawa kama ni utoto, lakini kwa kutuita watoto hakufanyi hoja zako kuwa na nguvu kama yule ndugu mwingine ambaye asipokubaliana na wengine anawaita wapumbavu! Rostam alikuwa na hisa kwenye RDC... he knows it na mtu yeyote ambaye angeamua kufuatilia suala hili lilipoanza 2006 angeona hivyo. Wengine tulishafanya uchunguzi mapema sana na kuestablish the following facts. (tafuta maswali yangu 10 kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU kuhusu Richmond - 2006).
Kwanza kwenye highlights hapo juu panatosha kabisa kuwa Tanzania Richmond ni ROSTAM AZIZ...N hilo linatowa nafasi nzuri kabisa kupata mahali pa kuanzia uchunguzi.
a. RDC iliingia nchini kwa ushirika wa Mhe. Msabaha (Mbunge - Waziri wa Madini)
Sasa kama unasema maneno kama haya..Kwanini huamni kuwa hawa watu wanatosha kuendeleza uchunguzi kwa kuhojiwa?
Haya yote yana KEY SUSPECTS LAKINI TUNAFANYA POLITICS HAPA!

b. RDC iliingia nchini kwa ushirika wa Jakaya Kikwete (Mbunge)

Umeshasema RA ndiye alikuwa na share kwenye kampuni ya Richmond..Na kumbe wakati huo JK alikuwa mbunge na MKAPA RAIS.

c. RDC (USA) wametoa mchango mkubwa katika kampeni ya Kikwete na Msabaha

Pointi hii pia bado swali ni kuwa wengine nao walipata nini?
Na unaposema pesa zilitolewa kwenye kampeni..Kwanini usingesema walipewa wao na bila kujali kuwa zilikuwa na misingi ya kampeni ama ni personal gift?

d. Rostam Aziz ndiye mfanyabiashara aliyetengeneza mazingira ya wao RDC kujikita kwenye biashara hiyo ya energy. Yeye mwenyewe akiwa ni shemeji ya Kikwete.
Sijuwi huo ushemeji wao ulianza lini..Lakini unaweza kuona yeye RA ndiye bosi.
e. Naeem Gire waliingia na asilimia 75 ya RDC (tanzania) na asilimia 25 zilizobakia zikigawanywa miongoni mwa wahusika wakuu.

yes I said it! RDC inahusiana na Msabaha, Kikwete, Rostam na familia ya kina Gire ambao ni wachangiaji wa kampeni za uchaguzi CCM (2005). Kupewa kwa mradi wa bomba la mafuta 2005 na miezi michache baadaye mradi wa majenereta ilikuwa ni shukrani ya CCM kwa michango ya kina Gire katika kampeni za Msabaha na Kikwete na pia kama nafasi ya kuvuna walipopanda hasa baada ya JK alipoingia madarakani kumchukua Msabaha na kumuweka kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

so, now you know
.

Kwa ujumla naomba uweke msisitizo kwenye highlights na pia kwenye point kwamba..Kama pesa za kampeni zilitolewa basi wahusika ni awamu ya tatu kwani JK alikuwa bado si Rais na mikataba hiyo ilisainiwa chini Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya Tatu amabye alishiriki kikamilifu kwenye maadalizi ya kichama ya kumweka JK madarakani ili amtumikie yeye na mashemeji zake kina Rostam
Rais huyo si mwingine bali ni BWM.

Ahsante.
 
katika maneno hayo manne angalia mawili ya mwisho, halafu angalia swali lako uliloliuliza.. utaona ni wapi ulikosea.

MMJJ naona sasa mvinyo uliochachushwa unakuzengua. Mara maneno manne ya mwanzo, mara ongeza na limao, mara tia na chumvi, kama huna jibu weka hapa wanaume wajionee kuliko kuendelea na mchezo wa jikoni.

RDC na JK bado havijaingia kichwani, weka data angalau kiduchu tukuunge mkono.
 
KJ.. nilisema "I think".. na wewe ukauliza "how do you know"! you make it too easy its not even fun!
 
Ukitoa hoja utajibiwa kwa hoja, ukiuliza swali ambalo wewe mwenyewe unaweza kulipatia jibu nitakusaidia kufanya hivyo kwani nikikupatia jibu moja kwa moja sitakuwa nimekusaidia. Ninapokuambia utafute jibu ni kwa sababu naamini kuwa ukichukua muda kidogo tu na wewe utalipata. Kwa sababu kama mimi nililipata nina uhakika na wewe ukiamua utaweza kulipata kwani ni public knowledge. Hivyo sitoi jibu si kwa sababu sitaki bali nataka nikuencourage utafute majibu.



the effect itakuwa ni ile ile, mimi kukupatia wewe jibu ambalo wewe mwenyewe unaweza pia kulipata.



Haitoshi tu kuuliza maswali, take time to research the answers. Unauliza maswali sahihi wakati mwingine the only thing is you don't want to put time to find the answers.

Kwahiyo wewe hujuwi kuwa wananchi wengi wanafuatilia hii mijadala?

Ama wewe unafikiri this is just about Jmushi, ama Nyani Ngabu na hata Kubwa Jinga?

MKJJ umeshafuatilia hata hawa presidential nominees?

Wanarudia message ile ile kwasababu wanajuwa kuna wasikilizaji wapya!

Hivi si unafuatilia the situation room?

Wolf Blitzer kila mara kabla hajaenda kwenye commercial huwa anadai.."Stay with us...I ama Wolf Blitzer...You are in A SITUATION ROOM"

Yani haina maana kwamba hajui kuwa watizamaji wake wanafahamu kuwa ile ni situation room na yeye ni WOLF BLITZER!

Kwanza hata kabla hasema maandishi yenyewe yanasema.

Ila hata hivyo bado anarudia....Sambamba na wagombea urais...Kuna ile hali ya ku assume kuwa kuna wasikilizaji wapya!

Kwa mtizamo wangu hapa jf...Kwa kweli nina ushahidi kuwa kuna mamia ya visitors wapya na jf ndio kioo cha jamii.

Hivyo basi tusikate tamaa kwani hujafungua thread ya maswali peke yake bali pia mjadala.

Na kama maswali yangu umeyaona hayana maana na pia umeweza kuyajibu ya watu wengine...Basi kweli hapo nimeshangazwa.

Ni wazi kuwa pointi yangu ni sawa na ya wengine kama vile ilivyo kwako wewe pia kwani kuna watu wanaokusapoti kwenye pointi yako.

Na hivyo mswali pande zote ni muhimu.

Kama vile alivyouliza Kidatu.

Hivyo basi...Acha niendelee na hiyo reserch yangu na mjadala nina amnini utaendelea bila mikwaruzo.

Ni hayo kwa sasa.

Ahsante.
 
Jmushi.. sayari ya dunia inazunguka jua tu... na sisi sote tunazunguka jua pamoja nayo. Kuna maswali yako ambayo naweza kuyajibu kiurahisi lakini kuna mengine ningependa wewe utafutie majibu kwa sababu kwa kufanya hivyo utagundua mengi zaidi. Kuuliza tu maswali kwa sababu yanakujia kichwani kunataka mtu mwingine ajibu, sasa jaribu kutafuta majibu wewe mwenyewe pale uliposhindwa na hakuna jinsi basi unaomba msaada. Hivyo ndivyo tunajifunza.
 
Jmushi.. sayari ya dunia inazunguka jua tu... na sisi sote tunazunguka jua pamoja nayo. Kuna maswali yako ambayo naweza kuyajibu kiurahisi lakini kuna mengine ningependa wewe utafutie majibu kwa sababu kwa kufanya hivyo utagundua mengi zaidi. Kuuliza tu maswali kwa sababu yanakujia kichwani kunataka mtu mwingine ajibu, sasa jaribu kutafuta majibu wewe mwenyewe pale uliposhindwa na hakuna jinsi basi unaomba msaada. Hivyo ndivyo tunajifunza.

MKJJ Naomba uelewe jambo moja...Sijauliza maswali kwasababu tu ya hizo quotes zako kutoka kwenye ripoti ya kamati.

Na pia nasisitiza kuwa umma wa watanzania macho yako jf.

Maswali yangu si personal...

Bali maswali yangu yanatokana na hoja unayojaribu kuijenga...Na sasa umeshindwa kuonyesha direct relation ya JK.

Hata hivyo kwa kuanzia...Naomba kwanza uwekwe wazi huo ushemeji ili tuone kama kweli JK atakuwa na UBAVU wa kufanya lolote.

Maana hapo sasa kama na undugu ushaingia ndio ugumu wenyewe na ndio maana sishangazwi na kutoamini kwako kuwa JK atafanya lolote.

Haina maana kuwa na sisi tunamwani JK.

NO!

Ila tunajuwa UZALENDO NI MGUMU!

Lakini kama tunakata issue...Tuakte issue maana hata wabongo wanakubali hapa jf anakomwa giledi.

Kuhusu pointi ya kuwa RA ana influence Kubwa sana hiko si siri!

Umeshasema wazi kabisa alikuwa na share na kampuni na kwasababu yeye alikuwa wakimwamini kwa kila kitu..Yeye ndiye responsible.

Tena wakati ambao hata JK mwenyewe hajaupata Urais!

RA alikuwa na bado ana nguvu sana tu kuliko JK!

Kwasababu nchi ilishauzwa kupitia mikataba mibovu chini ya Mkapa,Chenge,karamagi na kina msabaha.

Tunataka details zote za huyu RA kwani NI HATARI HUYU MTU!

NB:NI WAZI KUWA JK ATAKABILIWA NA EITHER USHEMEJI AMA UTANGANYIKA NA UTAIFA!
 
Rais wetu angeachwa kwanza angalau kwa sasa. Vinginevyo, sakata hili halitaishia popote. Tukumbuke pia maneno ya MWALIMU; huwezi kumtikisa RAIS nchi isitikisike. CCM na Mkapa kwa kiasi kikubwa walichangia mno kumfikisha Kikwete kuomba mapesa ya kampeni kwa watu kama akina Gire, Karamagi, RA,...
Angeyarudishaje mapesa haya machafu? Ikulu hakuna biashara ndio maana zikaundwa hizi RICHMOND.
 
Nadhani sasa wakati umefika Rais nae awajibike kwa suala hili la Richmond, maana hatujui ni nani atamfadhili tena kwa kampeni 2010 na atalipwa nini kama fadhila!! Sijui ni kwa nini viongozi wetu wanapenda kununuliwa kwa bei rahisi namna hii..
 
Rais wetu angeachwa kwanza angalau kwa sasa. Vinginevyo, sakata hili halitaishia popote. Tukumbuke pia maneno ya MWALIMU; huwezi kumtikisa RAIS nchi isitikisike. CCM na Mkapa kwa kiasi kikubwa walichangia mno kumfikisha Kikwete kuomba mapesa ya kampeni kwa watu kama akina Gire, Karamagi, RA,...
Angeyarudishaje mapesa haya machafu? Ikulu hakuna biashara ndio maana zikaundwa hizi RICHMOND.

Pesa za kampeni zilishughulikiwa na awamu ya tatu ilo liko wazi!

Na walifanya sana kama dizaini ya west wakidhani bongo ni marekani.

Yeye RA alitumia u lobbyst kwenye kanchi kama ka TZ.

Sasa jamani kwa style ya viongozi wetu ya kuomba omba...Kuna tajiri ama kampuni gani ya kimataifa itakayoshindwa kuinunuwa nchi?

Hayo mambo ya kampeni yeye aliambiwa atulie tu na ni wazi ilisukwa KIMAFIOSO!

JK HAJATAWALA BONGO KABISA!

Ni NAIVE! ANA HITAJI MSAADA!

Wamemzingira vibaya sana na pia wao wanaielewa issue vizuri sana na wao wanaongea kama viongozi sema hawana kofia ya urais na hapo ndio shida!

JK wa watu mwenyewe alikuwa yupo yupo tu hata hako ka mgogoro ka hapo Kenya ni Mkapa ailwahi huko tena kwa gharama za wananchi.

Na baadae akatupwa chini...Na JK akapewa uenyekiti wa AU.

Hata hivyo tatizo lilikuwa Bush hasa hasa kwenye issue ya Zimbabwe.

Kwa hiyo ni muhimu kutilia maanani kuwa...Pesa za kampeni za kina Gire ni kama tu za EPA kwani utaratibu ni ule ule wa kutegana.

RICHMOND TANZANIA NI ROSTAM AZIZ NA KAMA NI USHAURI WA KUTOWA PESA KWA ccm NI WAKE NA INAWEZEKANA PIA NI YEYE ALIYEZIPOKEA PESA HIZO KUTOKA KWA GIRE YEYE KAMA MWAKILISHI NA LOBBYST WA RICHMOND HAPO BONGO!

Yeye ndiye connection ya ccm-Richmond kama ilivyo kwa Iddi Simba kuwa ndiye EPA-ccm.
 
kasheshe, Recently You Have Been Very Personal With Me.. Do You Have Something You Really Want To Say... Just Go Ahead And Say It. Cheap Shots Ain't Doing Anything To Me.

No. No. No. No !!! HOJA ZAKO NDIO ZINA AGENDA ZA SIRI NDANI YAKE.... MIMI BADO NAKUHESHIMU SANA.....
 
Ushahidi wa kumuhusisha Rais wetu wa sasa na RDC bado sijauona na siamini kuwa upo wa kutosha, kwa sababu simple politics ni kwamba asingeweza kuwatosa kina Lowassa, Msabaha na Karamagi iwapo angekuwa yumo kwenye lile deal, hakuhusika ndio maana haikuwa taabu kwakwe kuwatosa, unless kuna ushahidi mwingie upo mahali haujaletwa hapa,

However, ninaamini sehemu zote ambazo ana "something" zimezibwa kabisa huwezi kuzigusa, hizi Meremeta tunazoambiwa ni za jeshi, Chenge, huko EPA na BOT kwa ujumla, nina wasi wasi kuwa ana something huko,

kwa sababu Pinda anamuogopa somebody, nani huyu? Na kwa nini?
 
However, ninaamini sehemu zote ambazo ana "something" zimezibwa kabisa huwezi kuzigusa, hizi Meremeta tunazoambiwa ni za jeshi, Chenge, huko EPA na BOT kwa ujumla, nina wasi wasi kuwa ana something huko,

kwa sababu Pinda anamuogopa somebody, nani huyu? Na kwa nini?

Field Marshall ES,

Huko nako sio kwamba anaingia yeye kama yeye! lakini ni kwa kuwa taasisi nyeti anazoziongoza ndio zina-feature... mfano mzuri ni CCM. Na inaeleweka wazi kwamba ukiweka taasisi kama CCM kwamba ndio imekwiba... hayo yatakuwa maporomoko makubwa sana.
 
Kabla ya taarifa ya Mwakyembe rais JK alihutubia na kusema kuwa 'imefika wakati wafanyanyabiashara wakaachana na Siasa', maneno hayohayo yalirudiwa na Mwakyembe wakati wa kusoma taarifa ya kamati, je yanauhusiano wa JK+Mwakyembe(kamati)-EL+Karamagi+Bangusilo+(-RA?)= Focus 2010?
 
Kuna maswali ya msingi sana ya kumuuliza Mwakyembe ambayo hayakuulizwa, likiwemo hilo hapo juu kwa sababu watu walipagaishwa na hoja yake iliyomfanya Lowasa ajiuzulu.

Kwa kuwa sasa mpagaisho huo pengine umeisha tunahitahi kurudi kwenye hali yetu ya kawaida na ku-reflect tena more critically kwenye report ya Mwakyembe na kuona kama alijibu maswali ya msingi yaliyofanya kamati iundwe.

Binafsi sijawahi kuridhika na maelezo yake juu ya kwa nini hakumhoji Lowasa, ambaye at the end of the day ndiye alikuja kuonekana kwamba ndiye aliyekuwa player mkubwa na ultimate casuality kwenye sakata zima la Richmond. Mwakyembe anapaswa pia atueleze nafasi ya Rais Kikwete kwenye Richmond hasa kwa kuzingatia utetezi mzito ambao Rais Kikwete amewahi kuujenga juu ya kampuni hii ya kitapeli. Rais Kikwete aliwahi kututhibitishia watanzania, zaidi ya mara moja, kuwa kampuni ya Richmond ilikuwa ya uhakika na kwamba ingefanya kazi yake vizuri ndani ya muda uliopangwa. Sasa ilikuwaje maelezo muhimu kama haya hayakujikeza kwenye report ya Mwakyembe?

Ni kwa sababu ya hoja hizi mimi mwenzenu hushawishika kuamini kwamba report ya Mwakyembe ilitumika kama silaha ya kumalizana na kujengana kisiasa na wala haikuwa na lengo la kutafuta ukweli kuhusu kampuni Richmond. At the end of the day, ukweli utajulikana maana hata Mtikila amejificha miaka yote hii lakini leo hii shetani amemuumbua kweupe!

Nakubaliana na wewe mkuu kwa yote uliyobainisha. Kweli watu tulichukuliwa na yaliyomo kwenye ripoti na bila kufanya tafakuri ya kina tukapitisha hukumu, na sasa tulipoanza kufikiri, tunagundua kuwa yapo mengi zaidi ya yale yaliyomo kwenye ripoti.
Lakini ukizingatia maandishi niliyohighlight, tunapaswa pia kujiuliza wka nini Lowassa na yeye hakutoa maelezo yenye kuonyesha upande wa piliw a shilingi alipopata nafasi ya kufanya hivyo>
 
Marafiki wa JMK wote ni Mafisadi, na ni watu wake wa karibu sana. Hii haimanishi JMK naye ni fisadi. Lakini kwa hoja ya MKJJ nakubaliana naye kuwa JMK atakuwa anahusika na hili deal la RDC.

Haiwezekani akose ujasiri wa kukabiliana na watu waliohusika na ufisadi huu. JK Nyerere alitofautiana na Kambona na akam fire, iweje yeye?

Sasa hivi tunachoshuhudia ni kujisafisha kwa akina RA na EL wakimvuta na Msabaha. Ukiangalia link ya Makampuni fake utagundua ni wale wale ndio wanaotajwa - Masha>Deep Green, Chenge,Mgonja, wako Meremeta na Tangold halafu JMK bado anawakumbatia.

Haiingii akilini kumsikia Salva akimtaja RA kuwa anahusika na RDC na wafanyakazi wake wa Caspian wakienda kufanya pia DOWANS, how comes?

Maswali ya kujiuliza

Ni kwa nini JMK anashikwa na Kigugumizi hata kutoa tamko tu juu ya ufisadi na mafisadi?

Ni kwa nini mafisadi wote waliotishia kwenda mahakamani kushitaki kuhusu kukashifiwa na wazalendo juu ya ufisadi wao hawajaenda?

Ni kwa nini RA ana hisa kwenye vyombo vingi vya habari?

Ni kwa nini RA aliamua kuinunua Habari Corporation?

Ni kwa nini RA bado yumo CC ya CCM?

Ni kwa nini RA anakanusha kuhusishwa na RDC bila kutuambia ni nani hasa mmiliki?


Hakika ni maswali mengi ambayo yanatupatia picha picha kuwa the Whole Govt is corrupt, ukianza na mchakato mzima wa kumfikisha JMK madarakani pamoja na wapambe wake wote. Nachelea kusema kuwa anayeulea ufisadi hapa Nchini ni CCM especially CC na NEC.

Kisidumu Chama Cha Mafisadi!!!!!!!!!!!!
 
katika kuangalia hoja zote, ushahidi wa kimazingira na kadha wa kadhalika na kupima uzito wa mambo, mimi kama mtu wa kawaida kabisa mwananchi wa nchi husika ktk yote haya ninadhani Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anayo kesi ya kujibu, sijui alisema nini au alimwambia nani hayo hayajulikani kwa umma bali kwa wachache tu, ila vitu vinavyomu implicate viko wazi, by connectin the dots unaona, ingesaidia zaidi kama walau angeweka wazi msimamo wake kwa wananchi, lakini wakati tukimngojea, ngoja tutumie yaliyopo kuonesha ni jinsi gani watanzania hatustahili kuongozwa na viongozi wa namna ya JK!
 
Hicho ndicho nilichosema nimenotice katika maelezo ya Rostam. Siyo kwamba hakuhusika, na hajawahi kukanusha hicho. Yeye anasema walichunguza na hawakuona jina lake. Vitu hivi ni viwili tofauti. Rostam hajawahi kukana kuhusika na Richmond na Dowans. Sikiliza tena majibu yake alipoulizwa hata jana.


Sasa, kama anachosema "mwanakijiji" ni utumbo kwanini watake ushahidi tena? Hivi nani mmiliki wa Richmond au Dowans? Kuna mtu anajua. Kamati ya Bunge ilishindwa kuonesha ni nani hasa mmiliki wa Richmond. Hebu nikukumbushishe kilichosemwa kuhusu Rostam kwenye ripoti ya Mwakyembe:



Na kamati hiyo hiyo teule inasema hivi:



Sasa kwa mfanyabiashara mzuri na msafi kama Rostam ambaye anasingiziwa tu mambo ya ufisadi, kufanya kazi na biashara na hata kushirikiana anuani na kampuni ya kifisadi ambayo ilishajulikana ni ya kifisadi hakumfanyi yeye fisadi? Inakuwaje kwa mfanyabiashara "msafi" ambaye familia yake imefanya biashara kuanzia 1852 kushindwa kuangalia uhalali wa kampuni anazofanya nazo biashara?

Je kweli Rostam hakuijua kabisa hii kampuni? Kwa ukaribu aliokuwa nao inapita akili kufikiria kuwa alikuwa hajui RDC ni nini au kuhusika na mambo yao.




Hakuna umbeya, Rostam alikuwa anahusika na Richmond, that is an established fact. Suala pekee ambalo halikuweza kuonekana (siyo kwamba halipo) ni kuwa halionekani.




sawa kama ni utoto, lakini kwa kutuita watoto hakufanyi hoja zako kuwa na nguvu kama yule ndugu mwingine ambaye asipokubaliana na wengine anawaita wapumbavu! Rostam alikuwa na hisa kwenye RDC... he knows it na mtu yeyote ambaye angeamua kufuatilia suala hili lilipoanza 2006 angeona hivyo. Wengine tulishafanya uchunguzi mapema sana na kuestablish the following facts. (tafuta maswali yangu 10 kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU kuhusu Richmond - 2006).

a. RDC iliingia nchini kwa ushirika wa Mhe. Msabaha (Mbunge - Waziri wa Madini)
b. RDC iliingia nchini kwa ushirika wa Jakaya Kikwete (Mbunge)
c. RDC (USA) wametoa mchango mkubwa katika kampeni ya Kikwete na Msabaha
d. Rostam Aziz ndiye mfanyabiashara aliyetengeneza mazingira ya wao RDC kujikita kwenye biashara hiyo ya energy. Yeye mwenyewe akiwa ni shemeji ya Kikwete.
e. Naeem Gire waliingia na asilimia 75 ya RDC (tanzania) na asilimia 25 zilizobakia zikigawanywa miongoni mwa wahusika wakuu.

yes I said it! RDC inahusiana na Msabaha, Kikwete, Rostam na familia ya kina Gire ambao ni wachangiaji wa kampeni za uchaguzi CCM (2005). Kupewa kwa mradi wa bomba la mafuta 2005 na miezi michache baadaye mradi wa majenereta ilikuwa ni shukrani ya CCM kwa michango ya kina Gire katika kampeni za Msabaha na Kikwete na pia kama nafasi ya kuvuna walipopanda hasa baada ya JK alipoingia madarakani kumchukua Msabaha na kumuweka kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

so, now you know.


Mwanakijiji,

Kwanini usjiunge nao..nitakupa njia ili tushinde..Nahisi wanatudharau
 
Bill na Mama Paroko..Mimi binafsi ninakubaliana na upande mwingine wa hoja yenu kuwa JK ni kweli anatakiwa kuprove beyond a resonable doubt kuwa yeye hausiki na ama ushauri aliopewa ni mbaya na hivyo ni lazima awashughulikie Mafisadi ipasavyo.

Na kwasababu kipimo chetu cha mwisho kiko hapo then ni wazi kuwa bado tuna uwezo wa kupata conclusion nzuri tu kabla ya uchaguzi wa 2010.

Na ndio maana nasisitizia juu ya umuhimu wa bunge.

Tukirudi kwene msisitizio wangu wa point...Ni kwamba wote tunajuwa kuwa sasa tuko kwenye soko huria kwa full kujiachia.

Na ndio maana nikatowa mfano wa Lobbying ambao ni mfano wa hapa USA.

Kwamba wale wanaochangia kampeni ndio wenye kupanga uongozi....I mean wale matajiri waliotowa pesa za kampeni ndiyo wenye ku call shots...Na hata mara baada ya kuingia madarakani...Kwa kutumia hao malobbysts ambao ni wawakilishi wa makampuni hayo waloko kribu na wabunge watunga sheria pamoja na uongozi wote ikiwemo Rais mwenyewe.

Na hama kwa hakika mfano mzuri ni wa Bush amabaye anauza mafuta na Chenney ambaye anauza silaha.

Kwahiyo wakati Bush ananyonya mafuta...Chenney yeye anauza silaha za kumwaga damu wakati wa upatikananji wa mafuta hayo.

Na nikatoa mfano wa Rostam Aziz....

Ndugu zangu...Hiyo system yenyewe ya lobbysts kuwa na nguvu za kuiamulia serikali maamuzi mazito ndiyo Obama anapingana nayo!

Na kamwe sikuamuwa kuwa sapota wa Obama simply eti because ana asili ya hapo Kenya.

Ni kwasababu ya msimamo wake kuwa serikali ifanye maamuzi kutegemeana na mawazo na mahitaji ya wananchi na si makampuni machache.

Na pia tukumbuke kuwa kama hiyo system ina madhara kwa federal state kama USA vipi kuhusu ka Republic ka Tanzania?

Kwasababu hata kama ni kulobby...States ni nyingi na hivyo hata kama uchumi wao ukiyumba inachukuwa muda ku feel the impact.

Mkikubali malobbyst tena kutoka nje kama ilivyo kwa Rostam ambaye alimwakilisha Gire kwenye dili lote...Then nchi si inaongozwa na RICHMOND KWA KUPITIA ROSTAM?

AMA HAMUELEWI HILO?

Msaada wa USA kwenye hili unahitajika mkubwa sana kwani la sivyo ni kweli kuna uwezekano wa machafuko.

Na hata machafuko yenyewe si lazima eti wananchi ndiyo wayaanze...NO...Wanaweza kufanya hivyo...Lakini mtizamo wangu ni kuwa even ndani ya vyombo vyetu vya usalama...Kuna wale wanaoona kuwa ni wazi nchi imeuzwa na hata wao ni wananusalama KANYABOYA TU!

Hata Bush alipokuja si mliona mambo?

Tunataka USHIRIKIANO MZURI NA WENYE MANUFAA KWA WOTE!

Si manufaa peke yake...BALI UTU, UBINADAMU, HAKI, Pamoja na maendeleo.

Na niliwahi pia kutoa mfano wa kuhusu dhahabu yetu...
Ndugu zangu...Naomba nitowe mfano...

Kama nchi yote ya Marekani...Say dolla imeshuka chini vya kutisha na imekuwa haina thamani kama ilivyo hata sasa...

Ama hata kama nchi imewaka moto na pesa zote zikaisha na labda zikawa hazina maana kama ilivyo hapo Zimbabwe kwenye iflation yao.

Utajiri wa Taifa Hupimwa kwa kutumia DHAHABU.

Hata Federal reserve si mapesa yamewekwa humo...UTAJIRI WA TAIFA HATA KAMA LA MAREKANI UNAPIMWA NA GOLD WALIYOKUSANYA NA ILE THAMANI YAKE NDIYO INATAJWA KAMA PESA.

Na ndio maana unakuta Uchumi wa nchi za mataifa ya magharibi hata uchui wao ukiyumba...Bado wana nguvu kwasababu Gold ambayo ndiyo kipimo cha utajiri wao na wao wameziifadhi...Huwa zinapanda bei na kwahiyo thamani na utajiri wa Taifa haufi moja kwa moja eti tu kwasababu dola haina nguvu.

Na kwasababu hiyo basi...Ninashtushwa sana na the fact kuwa...Sisi kizazi chetu bado tu ni kama wale mababu zetu ambao wazungu walikuwakuta wanatumia gold kucheza bao...Kipindi hicho gold zikipatikana hata kwenye river banks.

Bado hazijatunufaisha...Na sasa zinachimbwa...Na pia tunajuwa zina mwisho!

TATIZO NI KWAMBA KWA UTARATIBU HUU...NI WAZI IKO SIKU SISI NDIO TUTAKUWA TUKINUNUWA GOLD KUTOKA HUKO KWAO KAMA VILE NI ZAO.

Wamarekani wenyewe walishawahi kuwa na machimbo ya vito na dhahabu miaka ya nyuma..Na viliisha!

Lakini kabla ya kuisha kwake mnaweza kuona ni manufaa gani waliyapata.

Hata mafuta nk...Gas na kila kitu!

Vitu ambavyo waafrika tunagawa bure wao ndio walivitumia kupata maendeleo haya.

Kama pia mnafahamu nilishawahi kusema kuwaiga wamarekani kwa kila kitu ni sawa na kumwiga tembo kwani msamba unapasuka!

Ni sawa na kumlazimisha mtoto anayetaka kusimama aanze kukimbia.
This time tuamke.

Najuwa kuwa viongozi wameshasema kuhusu sisi kuanzisha processing ya raw materials zetu ili tuzipe thamani zaidi.

Ndugu zangu...Nyie hamjuwi...Lakini kama viongozi wetu kweli wangekuwa wazalendo na wenye kujali wanyonge...Basi Taifa letu lingekuwa na maendeleo na hizi picha mbovu mbovu za magonjwa na njaa na watu waliochoka zisingekuwepo.

Na ndio maana napingana sana na hayo mashirika yanayojiita ya msaada kwani misaada yao si ya kimaendeleo kabisa!

Kwasababu tumeshagunduwa kuwa misaada wanayotowa ina kuwa pia na influence za matajiri wenye nia zao na hivyo wao kupenda kutufanya sisi kuwa omba omba ili waendelee kutowa misaada yenye masharti kama vile kufanya biashara ambazo hazina usawa kwa kigezo cha mimi ni mfadhili wako!

Hilo LIKOME KABISA!

Tunataka misaada sasa in terms of vitendea kazi!

Walete matrekta...Wawezeshe kilimo cha umwaligiliaji.

Viwanda vidogo vidogo vifunguliwe na wananchi wa kiwango cha chini ili kuiwezesha jamii i move up to the middle class.

Misaada ya knowledge kama vile kuwapeleka vijana wetu wakapigwe msasa kwenye issue ya Quality Control, packaging na operation management ili kuweza kuzalisha bidhaa zitakazofikia viwango!

Msisitizo uwekwe kwenye elimu napia bajeti ya elimu ipewe kipaumbele kuliko matumbo ya viongozi mafisadi.

Kila kijiji kiwe na MAKTABA na access ya INTERNET NA VITABU VYA KUWAWEZESHA KUSOMA KUHUSU KILIMO BORA, UTUNZAJI WA MAZINGIRA,NAMNA YA KUJIEPUSHA NA MAGONJWA NK.


Hakuna kiongozi yeyote aliyeonyesha kuwajali wananchi.
Na kwasababu hiyo basi...Licha ya kwamba natowa msisitizo wa kutoona direct link ya JK kweny hii issue ya Richmond...Lakini tunajuwa ilivyotokea na tunataka uwajibishwaji kama katiba ilivunjwa!
Hilo haliwezi kupingika...!
 
Back
Top Bottom