Rostam mdeni mkubwa wa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam mdeni mkubwa wa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Radi, Sep 13, 2010.

 1. R

  Radi Member

  #1
  Sep 13, 2010
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wana JF Hii ndio hali halisi ya kwetu hapa nyumbani?Mishahara ya wafakazi haiwezi kuongenzwa hata kama wakigoma ,,Miaka nane"Mungu ibarika hiii Nchi"

  TOFAUTI na alivyojigamba kwamba ni mlipaji mzuri wa madeni anayodaiwa na serikali, Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi anadaiwa Sh. 2,576,583,013 tokea mwaka 1993, MwanaHALISI limegundua.

  Alikopeshwa Sh. 2 bilioni (2,025,739,660) mwaka 1993 na 1997 na Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa (CIS) uliokuwa ukifadhiliwa na serikali ya Japan na kusimamiwa na Wizara ya Fedha na Uchumi.

  Alitumia makampuni ya Africa Tanneries Ltd, Tanzania Leather Industries Ltd na Africa Trade Development.
  Fedha nyingine alizokopeshwa ni Sh. 1,516,024,125. Hizi alikopeshwa na serikali ili kuagiza mchele kupitia mpango wa Counterpart Fund. Alitumia Kampuni ya African Trade Development.

  Imethibitika kwamba Rostam ameshindwa au hataki kulipa deni hilo lililodumu kwa miaka 16 sasa.
  Akizungumza na vyombo vya habari 3 Mei 2009, siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam, Rostam alitamba kuwa ni mlipaji mzuri wa madeni yake kwa serikali.

  Alikuwa akijibu tuhuma mbalimbali za ufisadi anaodaiwa kufanya kwa kutumia makampuni yake mbalimbali. Gazeti hili lina kumbukumbu za jinsi alichukua fedha hizo, zilizokusudiwa kuboresha biashara nchini.

  Uchunguzi umebaini kuwa mwaka 1993 alichukua Sh. 280 milioni kupitia Kampuni ya African Tanneries Limited. Mwaka 1997 alitumia Kampuni ya Tanzania Leather Industries Limited kuchukua Sh. 725,943,120.

  Mwaka huohuo Rostam alitumia Kampuni yake nyingine ya African Trade Development kubeba Sh. 1,019,796,540 kutoka mfuko huo.
  Mwishoni mwa mwaka jana, baada ya ‘mshike mshike nguo kuchanika,' Rostam alilipa Sh. 500 milioni akikusudia kupunguza deni la "mchele."
  Lakini kutokana na kuwepo deni jingine la zaidi ya Sh. 1bilioni katika mfuko wa CIS, mamlaka husika zikaamua kutumia kiasi hicho kupunguza madeni hayo.

  Kwa sasa anadaiwa na mfuko huo Sh. 1.060,558,888. Deni hilo likijumlishwa na deni alilokopa kuagiza mchele, Rostam anadaiwa jumla ya Sh. 2,576,583,013. Katika mazungumzo yake na serikali kwa nyakati tofauti, alikiri na kuahidi kulipa ingawa hadi sasa ameendelea kukaidi kulipa.

  MwanaHALISI limebaini kuwa tayari mmoja wa wanasheria jijini Dar es Salaam, anayeshughulikia suala la kukusanya madeni hayo anaandaa taarifa ya kisheria itakayokabidhiwa kwa wadeni sugu wakati wowote kuanzia sasa.

  Jukumu jingine analotekeleza mtaalamu huyo wa sheria ni kumshauri Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kufanya mpango wa kutumia mamlaka ya Kamishna Mkuu wa TRA ili kutekeleza azma ya kufilisi mali za Rostam na vigogo wenzake wanaodaiwa.

  Pamoja na Rostam, wadeni sugu wengine ambao walizungumza na serikali, wakakiri kudaiwa na wakaahidi kulipa madeni kwa kadri walivyoomba lakini badala ya kulipa wakaingia ‘mitini' ni pamoja na Mbunge wa Temeke, Abass Mtemvu (CCM).

  Mbunge huyo mwaka 1998 alitumia Kampuni ya A.M. General Agency kukopa Yen 20,000,000 sawa na Sh. 280 milioni. Ingawa alikiri kudaiwa na kuahidi kulipa deni, hadi sasa hajalipa hata shilingi moja.

  Aliyewahi kuwa Waziri wa Utumishi na Mbunge wa Mlangege, Zanzibar, Fatma Said Ali (CCM), mwaka 1998 alitumia Kampuni ya Tanzania Save Way Co. Ltd., kukopa Yen 20,000,000 lakini akakopeshwa Yen 10,000,000 sawa na Sh.140 milioni. Aliwahi kupunguza Sh. 23,400,000 tu.

  Aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wakati wa serikali ya awamu ya pili na ya tatu, ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Henry Shekiffu, mwaka 2000.

  Alitumia kampuni ya Shemshi & Sons Limited kukopa Sh. 399,560,000. Amewahi kupunguza Sh. 65,340,051. Hadi sasa anadaiwa Sh. 279,653,794.

  Nicodemas Banduka, mwaka 2000 alitumia kampuni ya Kadolo Investment kukopa Yen 105,210045 sawa na Sh. 147,294,630. Aliwahi kulipa Sh. 22,500,000. Hadi sasa anadaiwa Sh.124,794,630.

  Mwingine ambaye arobaini zake zimekaribia ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka, aliyetumia kampuni ya Petmon Investment, mwaka 2000. Alikopa Sh. 140 milioni, aliwahi kupunguza Sh. 24,712,200. Hadi sasa anadaiwa Sh. 115.287,800.

  Ufuatiliaji unabainisha kuwa idadi kubwa ya makampuni yaliyotumiwa na vigogo hao yalianzishwa kwa lengo la kuchota fedha hizo. Mengi kati ya hayo hayapo tena.

  Vigogo wengine waliobainika kukopeshwa na CIS lakini taarifa hazielezi kama mali wanazomiliki pia zitafilisiwa, ni aliyekuwa mbunge wa Sengerema, Dk. William Shija ambaye sasa ni Katibu wa Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola.

  Alikopa Sh. 140 milioni kwa kutumia kampuni ya Pyramid Investments Limited, mwaka 2000. Amewahi kupunguza Sh. 22,650,000.
  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wassira, naye jina lake limo kwenye orodha ya wanaodaiwa ingawa taarifa muhimu, mathalani alikopa kiasi gani, lini na amelipa au bado hazionyeshwi katika kumbukumbu hizo.

  Ingawa serikali inaelezwa kuwa kwenye hatua za kukamilisha mipango ya kufilisi mali za wadeni wake hao na wengine, bado inasuasua.
  Mkataba wa kufanikisha mikopo hiyo unaruhusu serikali kupitia kwa Kamishna Mkuu wa TRA kufilisi mali za asiyetekeleza mkataba katika kipengele cha kulipa, tena bila kulazimika kwenda mahakamani. Haijafahamika kwa nini TRA haijachukua hatua hiyo.

  Dhana inajengeka kwamba huenda "kigugumizi" hicho katika kukusanya madeni ya walipa kodi wa Tanzania, kinatokana na wadaiwa wengi kuwa vigogo ambao miongoni mwao bado wapo kwenye nyadhifa za juu serikalini.

  CIS ilianzishwa kwa nia njema ya kukuza sekta ya biashara nchini, kwa kuwasaidia wafanyabiashara kufanya biashara za kimataifa. Kuagiza bidhaa mbalimbali kutoka nchi tofauti, zilizofadhili mpango huo.

  Mpango huo ulikuwa ukitekelezwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Fedha na Uchumi. Hata hivyo taarifa zinaonyesha kuwa jumla ya Sh. 44 bilioni zilichotwa na wizara nane katika mazingira ambayo hadi sasa serikali haijafafanua.
   
 2. c

  chama JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Raj Patel ona dugu yako RA
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145

  Wadaiwa wote hao ni wanachama wa ccm na wengi wao ni viongozi wa serikali ya ccm.
  Ama kweli rushwa na ufisadi ni sera ya kudumu ya ccm.
  Ole wao mafisadi mwaka huu mtakiona cha moto, ngoja Dr. Slaa aingie ikulu, mtajuuuuta kumfahamu.
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Sep 14, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  dDoctor akipenya ikulu itabidi magereza yaongezwe, 4 sure hayatatosha kuhifadhi wafungwa.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mjomba,
  MaDokta wapo wengi siku hizi...kuna udocta huu wa kupewa wa Saint Claus!
  Unatakiwa u'specify docta yupi!...huh!
   
 6. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  kama tunawaze kuwaua ndugu zetu kwa sababu za kuiba simu au kuku

  tunashindwa nn kwa huyo gabachori...!

  tusitegemee serikali...manake kaiweka mfukoni..ana mfuko mpana saana huyo..! akiona wananchi tunakuwa personal na yeye ataogopa na ataondoka ktk nchi hii..!

  LETS DO IT...! YES WE CAN..!
   
 7. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  kama Mchungaji Mtikila aliswekwa lupango kwa kutolipa Deni Kwa nini isiwe hivyo hivyo kwa wasiolipa?
   
 8. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Una uhakika anaweza kufanya kweli. Hivi huko upinzani ni kusafi kiasi hicho cha yeye kuweza kuwa na utashi wa kulishughulikia hilo ipasavyo?
   
 9. M

  Mndamba Member

  #9
  Sep 14, 2010
  Joined: Jun 22, 2007
  Messages: 50
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hizo sheria uchwara ndizo zinazowapa mianya hawa watu kuendeleza wizi wao. Yawezekana hizi kampuni zilishakufa siku nyingi. Ama kweli TZ ni shamba la bibi.
   
 10. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  1.Serikali ilibinafisisha Viwanda vyake ili kuongeza uzalishaji na kutoa bidhaa bora .
  2.Serikali hiyo hiyo inawakopa walionunua viwanda ili viwe imara zaidi??

  3.Sasa hii African Tannaries (nadhani iko mwanza)ilinunuliwa kwa shilingi ngapi? Imeajiri watanzania wangapi? Inazalisha nini? Inazalisha kiasi gani? Inalipa Kodi kiasi gani?

  Sitashangaa kusikia hiki kinachoitwa kiwanda wala sio kiwanda ni kituo tu cha kukusanyia na kukausha ngozi kabla hazijapelekwa.
   
 11. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Navyozidi kujua mengi zaidi na ndiyo hivyo roho inavyozidi kuniuma.
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kama vile atajisafisha....
   
 13. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,468
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Ukiona watu wanagangania ungozi licha ya kuwa na kasoro nyingi katika maadili ya uongozi,ni kinga ya kuficha madhambi yao.Siku tukiamka usingizini watakuwa wameishakimbilia Canada na Uingereza.Hayo madeni watalipa watoto wa wanyonge ambao hata hawajui hizo deal za wizi wa mchana.Kweli kasi mpya,hari mpya,damu mpya ya maendeleo ni ndoto kwa miaka 50 ijayo.
   
 14. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ndugu na jamaa zao wanashabikia ccm ishinde uchaguzi ili kukwepa hukumu zitakazowapata. Angalia posts zao wanavyohaha !
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Pole ndugu yangu......unaweza kuua!!
   
 16. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Maumivu ya kichwa huanza polepole
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mdai -- kwa maana ya Serikali, kama ina ubavu wa kumshitaki Rostam -- inaweza na kwa kuomba kumuodolea hiyo corporate veil ambayo anajificha nayo, na anaweza kutinga gerezani kama Mtikila tu. Lakini serikali ya rushwa ya JK (ya CCM) haina ubavu kabisa kumshughulikia fisadi huyu.
   
 18. J

  JAY2da4 JF-Expert Member

  #18
  Sep 15, 2010
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  kumbe ndo maana kila mtu anataka kuwa mwanasiasa.wadeni wote ni wanasiasa,kazi bado ipo,hapa bila dictator nchi hii haiwezi kwenda mbele maana wajinga wengi mno.Hivi huwa hakuna riba ,maana kama mtu alikopa billion 2 tsh,mwaka 1993 ,si ajabu tukamdai riba zaidi ya mamilioni ya hela shilingi.
   
 19. F

  Froida JF-Expert Member

  #19
  Sep 15, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Anatakiwa kupigwa risasi kwenye viwanja vya jangwani tunawattoto millioni 4.1 ambao hawajui watakula nini na wataishi wapi hii ni takwimu za serikali
   
 20. M

  Maka Kassimoto Member

  #20
  Sep 15, 2010
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini asiweze? Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno. Aliwatimua watendaji wa vijiji na kuwafungulia mashitaka walipokwapua fedha za maendeleo Karatu, aliwalipua waliotumia misamaha ya kodi kupitia makanisa (wakwepa kodi), aliwalipua hata makada wenzie walipoleta ufisadi katika chama chao (kumbuka ya kafulila na mwenzake, na uchaguzi wa umoja wa vijana wa CHADEMA).

  On the other side, jamaa alituambia anayo orodha ya wauza unga na kwamba dawa yao ipo jikoni. Ask him hiyo dawa bado inachemka tu, ama anatumia mkaa wa migomba?
   
Loading...