M
MegaPyne
Guest
Mbunge Wa Igunga Ingefaa Aondolewe Safari Hii
(ninafahamu nguvu ya fedha)
Ng'wana Ngosha (raia mwema)Napenda kuipongeza sana serikali ya ya Awamu ya Tatu, ya Chama Cha Mapinduzi ikiongozwa na Mheshimiwa Rais Benjamin William Mkapa kwa mambo mengi yaliyofanyika hususan maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo:
• Elimu ya msingi chini ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM), uliofanikiwa sana kote nchini.
• Mpango we Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) unaoendelea.
• Huduma za Afya
• Ujenzi wa barabara chini ya uongozi wa Mheshimiwa Magufuli
• Ubinafsishaji na matunda yaliyoletwa na wawekezaji: ikiwemo ajira zaidi, ukuaji wa kasi wa uchumi wetu na miundombinu mbalimbali ukiwemo umeme na maji kwa wananchi walio karibu na miradi ya uwekezaji (kama vile wachimbaji madini wa Kanda ya Ziwa na kwingineko).
• Jitihahada za kuleta utawala wa sheria kwa misingi ya uwazi na ukweli
• Vita dhidi ya rushwa
Nikitaja machache tu (orodha ya mafanikio ni ndefu)
Katika kipindi cha serikali yetu hii ya Awamu ya Tatu, zipo pia wilaya nyngi za nchi yetu zilizobahatika kuteuliwa kufanyiwa miradi ya maendeleo (pilot projects) kwa fadhila za vyombo vya ki-mataifa kama vile Benki ya Dunia n.k. Niliyoyataja hapo juu ni mafanikio yaliyotokana kwa juhudi za serikali kitaifa, si kwa sababu Mheshimiwa Mbunge fulani "Kayaleta yeye kwa juhudi zake binafsi". Nasema hivyo kwa sababu wapo wabunge wanaowahadaa wapiga kura katika majimbo yao kwa kuvizia kila serikali itendapo jema husema "angalia, nimewaletea mimi". Tena, mara nyingine wanadai wametoa pesa zao wenyewe.
MMEM ikijenga shule za msingi jimboni kwake: "Angalieni shule za msingi… Nimewaletea mimi"
Mpango wa MMES ukitekelezwa kidogo kwenye jimbo lake: Angalieni shule za sekondari … Nimewaletea mimi" Mheshimiwa Magufuli akipitisha barabara kwenye jimbo lake: "Angalieni barabara… Nimewaletea mimi"
Wawekezaji wakitoa huduma ya umeme kwenye jumbo lake: "Angalieni umeme… Nimewaletea mimi"
Kwa mfano, Mheshimiwa sana Rostam Aziz, aliyekuwa Mbunge Igunga hadi bunge lilipovunjwa hivi majuzi(2005). Yeye ana kipindi kinachozidi miaka 10 bungeni, lakini hajawahi kusikia hata siku moja akiuliza swali, kuchangia hoja au kutetea jimbo lake (ambalo likio nyuma kabisa kimaendeleo katika nyanja zote). Lakini kila aonapo jema limefanyika "Angalieni … Nimewaletea mimi"
Nemebahatika kuona na kusoma Taarifa ya Maendeleo ya jimbo hilo, iliyotolewa Julai 2005 na mheshimwa Rostam akiwa kwenye kivuli cha mwavuli wa Serikali makini ya CCM. Kataka taarifa hiyo, nadhani hata mvua kama zingekuwa zimenyesha vizuri mheshimiwa huyu angesema: "Angalieni mvua… Nimewaletea mimi" Mheshimiwa huyu katika taarifa hiyo amedai kutumia fedha yake binafsi jumla ya shilingi za Tanzania zaidi ya milioni mia sita kwa ajili ya miradi ya maendeleo jimboni kwake.
Mtu mwenye akili lazima kutilia mashaka tarakimu zilizotajwa na mheshimiwa huyo. Kisha kujiuliza maswali kadhaa: je, kazi ya mbunge ni kukaa kimya bungeni muda wote na kuleta maendeleo kwa ktumia mamilioni ya fedha yake mwenyewe? Na yeye (kama mfanyabiashara) atazirudshaje fedha hzo?
Katika Mkutano Mkuu huo wa Julai 2005 (wilayani), mheshimiwa Rostam aligawa bahasha kwa wajumbe – na kila mmoja alipofungua alikuta TSH 20,000. Mungu ampe nini mjumbe huyu masikini? (na amchague nanikwa ajali ya kinyang'anyiro cha Oktoba mwaka 2005)?
Ni kawaida ya mheshimiwa huyu kugawa "misaada" ya chumvi kidogo, pea za kanga, sukari kidogo (ukiwa mjanja, baiskeli) n.k. kwa wakulima masikini hawa (kwa wale walio karibu na makao ya wilaya) nyakati za karibu na uchaguzi Ndugu zangui, wagombea wa namna hiyo wanatumia hali ya kutofahamu (ignorance) ya wananchi na kuendelea na mchezo mchafu ili waendelee kuchaguliwa, na "mambo yao" (ya biashara) yawanyokee.
Mimi ni mwanachama na mpenzi wa Chama Cha Mapindizi, tena waweza kuniiita wa siasa kali. Nadhani, nionavyo ni kwamba chama chetu kinahitaji kuteua wagombea makini katika hatua za mwamzo kwa kudhibiti mbinu chafu-chafu. Vinginevyo, labda tuombe wananchi waendelee kulala; la wakiamka kuna hatari chama kikapakwa matope na watu wa aina ya mheshimiwa "Nimewaletea Mimi"
Cha kusikitisha amechaguliwa tena!
Nimetuma makala hii Radio Tanzania/TUT (mara mbili) haikusikika, Tume ya kuzuia Rushwa (TAKURU) – e-mail address yao ina matatizo. Hivyo naomba ikiwezekana itoke kwenye vyombo vingine. Mwenye mashaka juu ya yaliyoandikwa anaweza kuhakiki na wananchi hapa Igunga na pia anayekanusha atoe ushahidi kama mtajwa alishasikika Bungeni katika kipindi husika
(ninafahamu nguvu ya fedha)