Rostam, Mara Vs Jukwaa la Wahariri

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Waandishi Mara wakosa imani na Jukwaa la Wahariri
Mwandishi Wetu
Daily News; Wednesday,August 27, 2008 @00:03


Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Mara (MRPC), imesema haina imani na tume iliyoundwa na Jukwaa la Wahariri kuchunguza kile kilichoandikwa na vyombo vya habari wakati wa maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe.

Miongoni mwa sababu zilizotolewa na klabu hiyo ni kwamba wajumbe wengi wa tume hiyo wanatoka katika mkoa mmoja ambako anatoka Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto ambaye ndiye aliyetoa malalamiko hayo mbele ya Jukwaa la Wahariri. Wajumbe wa tume hiyo ni Apolinari Tairo, Nevile Meena, Jamillah Abdallah, Saed Kubenea na Jesse Kwayu.

Taarifa iliyosainiwa na Katibu Mtendaji wa MRPC, Emmanuel Bwimbo ilieleza kuwa walitegemea kuwa tume hiyo ingehoji viongozi wa Serikali, taasisi, viongozi wa kisiasa na wananchi wa kawaida. Ilifafanua kuwa tume hiyo kwa taarifa walizo nazo, ilimhoji Kamanda wa Polisi mkoani Mara na Mkuu wa Wilaya ya Tarime na kuelekeza nguvu zao kwa viongozi wa Chadema wilayani Tarime ambao tayari walikuwa wamekwishatoa tamko lao la msimamo wa chama chao.

“Jesse Kwayu, ambaye ni mjumbe wa tume hiyo inadaiwa ni ndugu wa karibu wa Mbowe,” ilieleza taarifa hiyo. Pia ilimwelezea Kubenea kuwa tayari gazeti lake la MwanaHalisi lilishaandika makala kuwa waandishi hao wa mkoani Mara walipewa fedha kwa malengo ya kuichafua Chadema na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.

Anadai makala hiyo tayari ilishatoa hukumu kwa waandishi hao. “Gazeti la MwanaHalisi linadaiwa pia kumilikiwa na mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema…kwa sababu hiyo MRPC hatuwezi kuwa na imani na taarifa itakayotolewa na tume hiyo,” ilisema taarifa hiyo. Bwimbo alisema klabu yao inashauri kazi hiyo ingefanywa na Baraza la Habari (MCT) na sio kikundi cha watu ambacho alidai kinalenga kusafisha baadhi ya watu na kudhalillisha waandishi wa habari.

Alishangaa kwa vile kuna matukio mengi mengine yanahusu waandishi wa habari kupigwa na mauaji ya albino, lakini hayajawahi kuundiwa tume, “je ni kwa nini imekuwa Mbowe na Chadema?” MRPC imefafanua kuwa hakuna upotoshaji wa aina yoyote ile katika habari zilizoandikwa kwa vyombo va habari siku ya mapokezi ya mwili wa marehemu Wangwe wakati wa mazishi na hadi sasa.

NB: Kazi imeanza tena. RA bado yuko kwenye mkakati, ameshaona wazi kuwa ripoti ya jukwaa la wahariri itakuwa moto kwake. Tayari kitita kimeshapenyezwa Mara kupitia kwa George Maratu. Ballile ameshafanya mawasiliano na Mara, gazeti la RAI la kesho litachambua jukwaa la wahariri kama karanga. Pamoja na kuwa hii timu ya sasa ya wahariri ni mpya, ile ya mwanzo ilivunjwa ikaundwa nyingine kwa ushauri wa MCT na MISA TAN

PM
 
Kwahiyo mwanahalisi ni mali ya kiongozi wa juu wa chadema kweli tunaliwa kumbe yote wanayoyafanya ni kwa matakwa yao ya kisiasa na sio mengine
 
RA huwa hachoki ni mtu ambaye kila mara huwa anaamini kuwa anaweza kupambana hata kama mapambano yake yatakuwa hayana shabaha.

FISADI likichoka ndio mwisho walo sasa atapambana mpaka siku ya mwisho, huenda amejua kuwa ripoti itamtaja na haswa baada ya waandishi na wahariri kubanwa huenda walimtaja kwa njia moja ama nyingine.
 
Hao waandishi wa Mara wana nini kikubwa zaidi ya mabosi wao (wahariri). Ninavyofahamu wahariri walibariki kuundwa kwa chombo hiki. Mara Press Club wana mamlaka gano over Editors Forum? Kwani waandishi walioandika habari hiyo walikuwa chini ya hiyo Press Club? Hao waandishi wa Mara wanawajibika wka nani, vyombo vyao vya habari wanavyoviandikia, wahariri wao, au press club yao?
 
kwa heri rostam azizi, pesa zimekuinua sana, ukaweza kununua majimbo na waroho wa pesa, pesa ilikuaminisha mpaka wakakuchagua mweka hazina wa chama alichoasisi, mtakatifu julisu nyerere, [esa zikakuweka kule juu mawinguni, ukatuzama sisi kama siafu huku chini, ukawashangaa siafu kama akina mwakyembe wanawezaje kubishana mtu wa fweza kama wewe.

katika ikulu ya dsm, wewe ulikuwa mtu muhimu, ilikuwa kama wewe ni mwamuzi wa kila kitu

ukasahau kitu kimoja, kuwa pesa zinaweza kunnua nchi, ikiwa ni pamoja na mimea , majumba na kila kilichomo, LAKINI KAMWE PESA HAZIWEZI KUNNUA TAIFA, NA WATU WAKE NA UTASHI WAO

WALE ULIODHANI NI SIAFU, BAADA YA PESA KUKUINUA SANA, NDO LEO WATAKUTAFUNA NA KUKUMALIZIA MBALI
UMESAHAU KUWA HATA TEMBO NYIKANI HUANGAMIZWA NA SIAFU

KWA HERI FISADI NAMBARI WANI
KILICHOBAKI SASA NI HISTORIA
 
Back
Top Bottom