Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
Waandishi Mara wakosa imani na Jukwaa la Wahariri
Mwandishi Wetu
Daily News; Wednesday,August 27, 2008 @00:03
Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Mara (MRPC), imesema haina imani na tume iliyoundwa na Jukwaa la Wahariri kuchunguza kile kilichoandikwa na vyombo vya habari wakati wa maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe.
Miongoni mwa sababu zilizotolewa na klabu hiyo ni kwamba wajumbe wengi wa tume hiyo wanatoka katika mkoa mmoja ambako anatoka Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto ambaye ndiye aliyetoa malalamiko hayo mbele ya Jukwaa la Wahariri. Wajumbe wa tume hiyo ni Apolinari Tairo, Nevile Meena, Jamillah Abdallah, Saed Kubenea na Jesse Kwayu.
Taarifa iliyosainiwa na Katibu Mtendaji wa MRPC, Emmanuel Bwimbo ilieleza kuwa walitegemea kuwa tume hiyo ingehoji viongozi wa Serikali, taasisi, viongozi wa kisiasa na wananchi wa kawaida. Ilifafanua kuwa tume hiyo kwa taarifa walizo nazo, ilimhoji Kamanda wa Polisi mkoani Mara na Mkuu wa Wilaya ya Tarime na kuelekeza nguvu zao kwa viongozi wa Chadema wilayani Tarime ambao tayari walikuwa wamekwishatoa tamko lao la msimamo wa chama chao.
Jesse Kwayu, ambaye ni mjumbe wa tume hiyo inadaiwa ni ndugu wa karibu wa Mbowe, ilieleza taarifa hiyo. Pia ilimwelezea Kubenea kuwa tayari gazeti lake la MwanaHalisi lilishaandika makala kuwa waandishi hao wa mkoani Mara walipewa fedha kwa malengo ya kuichafua Chadema na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.
Anadai makala hiyo tayari ilishatoa hukumu kwa waandishi hao. Gazeti la MwanaHalisi linadaiwa pia kumilikiwa na mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema kwa sababu hiyo MRPC hatuwezi kuwa na imani na taarifa itakayotolewa na tume hiyo, ilisema taarifa hiyo. Bwimbo alisema klabu yao inashauri kazi hiyo ingefanywa na Baraza la Habari (MCT) na sio kikundi cha watu ambacho alidai kinalenga kusafisha baadhi ya watu na kudhalillisha waandishi wa habari.
Alishangaa kwa vile kuna matukio mengi mengine yanahusu waandishi wa habari kupigwa na mauaji ya albino, lakini hayajawahi kuundiwa tume, je ni kwa nini imekuwa Mbowe na Chadema? MRPC imefafanua kuwa hakuna upotoshaji wa aina yoyote ile katika habari zilizoandikwa kwa vyombo va habari siku ya mapokezi ya mwili wa marehemu Wangwe wakati wa mazishi na hadi sasa.
NB: Kazi imeanza tena. RA bado yuko kwenye mkakati, ameshaona wazi kuwa ripoti ya jukwaa la wahariri itakuwa moto kwake. Tayari kitita kimeshapenyezwa Mara kupitia kwa George Maratu. Ballile ameshafanya mawasiliano na Mara, gazeti la RAI la kesho litachambua jukwaa la wahariri kama karanga. Pamoja na kuwa hii timu ya sasa ya wahariri ni mpya, ile ya mwanzo ilivunjwa ikaundwa nyingine kwa ushauri wa MCT na MISA TAN
PM