Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Mkutano huu wa waandishi wa habari inabidi uwe ni juu ya Rostam. Asiachwe na ajenda yake bali waandishi ndio waamue muelekeo wa ajenda ya mazungumzo. Baadhi tu ya maswali ambayo itakuwa vizuri kupata majibu yake ni haya:
Mhe. Rostam:
a. Ulizaliwa wapi, mwaka gani, ulisoma shule ya msingi wapi, sekondari wapi na Chuo Kikuu wapi na mwaka gani?
b. Una umiliki wa makampuni mangapi ya biashara (aidha ukiwa mmiliki au mwenye hisa)?
c. Mmiliki wa Dowans Gen. Aladawi amekiri kukufahamu na kuwa mna urafiki wa karibu; je una hisa yoyote kwenye kampuni yake au yeye ana hisa zozote kwenye mojawapo ya makampuni yako?
d. Ni kwa kiasi gani ulimsaidia Gen. Al-Adawi kuweza kuanzisha kampuni ya Dowans Tanzania Ltd? Unamfahamu mmiliki wa Dowans Holdings SA ya Costa Rica?
e. Ni kwa kiasi gani ulimsaidia Salva Rweyemamu mwandishi wa mojawapo ya vyombo vyako vya habari kupata kazi Ikulu?
f. Ukiwa Meneja wa Kampuni wa Kikwete bila ya shaka ulisimamia kiasi kikubwa cha fedha na mgawanyo wa matumizi yake, (a) je unaweza kuwaambia wananchi ni kiasi gani kilitumika katika kampeni ya Kikwete (b)Je fedha za kampeni ya Kikwete zilitoka wapi?
g. Ni wabunge wangapi ambao umewasaidia kifedha katika kampeni kutoka katika mfuko wako binafsi katika uchaguzi wa 2005, unaweza kuwataja baadhi yao?
h. Kuna kiasi chochote cha fedha ambacho kampeni ya Kikwete ilipokea aidha kutoka Iran au nchi nyingine yoyote ya nje au wafanyabiashara wa nje akiwemo Gen. Al-Adawi?
i. Je una uhusiano wowote wa kibiashara na Yusuph Manji na ni uhusiano upi?
j. Je, msimamo wako kuhusu wizi mkubwa kabisa wa fedha za Watanzania kutoka akaunti ya EPA ni upi na unasema nini kuhusu kutokujulikana kwa watu waliochota fedha za Kagoda na kuzirudisha taslimu. Je wafikishwe mahakamani hata baada ya kurudisha?