Rostam kukutana na waandishi wa habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam kukutana na waandishi wa habari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, May 2, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Rostam kukutana na waandishi wa habari

  Kuna habari kwamba kesho (Jumapili) saa 5 mchana Rostam Aziz atakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Kempinski.
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  May 2, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Hoteli ambayo ilimtoa mengi pangoni
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  *************************

  Atawaalika wale wa IPP? Au atachagua mamluki wake watakaomwandika vizuri?
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Labda atatangaza kuondoka CCM na kuhamia CUF. Si unajua tena mambo yanavyokwenda baina ya maswahiba -- Rostam -- Jussa -- Lipumba na huenda wakachotwa akina Zitto, Serukamba, Makamba etc.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,544
  Likes Received: 18,184
  Trophy Points: 280
  Akialika waandishi, ataalika wote bila ubaguzi tatizo la press com za RA, huja na karatasi, litahusu kumburuza Mangi kwa pilato, atalisoma, its over, no maswali, no ufafanuzi, baada ya hapo ni waandishi kukirimiwa lunch ya Kempinski, followed by fat brown envelopes its all over.
   
 6. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  '...Alternatively he is it to apologize to me personally within 48 hours, failing all of which, I reserve the right to exercise any appropriate actions in order to expose his wrongdoings"

  Oké! Labda anataka kutuhabarisha 'mabaya' ya Mengi!
   
 7. DDT

  DDT Member

  #7
  May 2, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii biashara ya kukutana na waandishi inalipa sana...mwisho wa yote anayefaidi ni nani? Kempiski, waandishi na RA anajipatia burudisho la nafsi kuwa na yeye kidume ametoa mpya zaidi ya mwenzie one shilling aka Manji
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nionavyo mimi ndicho kitakachotokea...tusubili hiyo saa 5 ya J2
   
 9. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Waandishi wa habari wa nini? masaa 48 yalisha isha mi nilidhani kaisha elekea kisutu Kumshitaki mengi. Wacha tusubili.
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Safi saana RA kwa kutoka pangoni!
  Waandishi independent tafadhali maswali yafuatayo:

  -kwa nini alitoka uweka hazina ccm, na aliingiaje huko?
  -kama ana uhusianao na Richmond ana uchungu gani na nchi
  -ukweli kama anaijua Kagoda
  -je anahusikaje na TRL(Reli)

  Wadau tupate dondoo tu!
   
 11. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Ni vyema akaulizwa pia anahusikaje na Kagoda. Wakili Sanze anathibitisha kwa kiapo kuhusu kusaini nyaraka za Kagoda ofisini kwa Rostam, anajitoaje hapo?
   
 12. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sidhani kama atakuwa na jipya maana..... ila naunga mkono kusiwe na ubaguzi wa waandishi wa habari. Na atuambie ni lini atafungua kesi dhidi ya Mh Mengi ili sasa Mengi atue mzigo wa makabrasha ya MAFISADI PAPA.
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kadhalika aulizwe na autueleze, bila kutafuna maneno, kwa nini imekuwa kawaida yake kuandikisha makampuni yake bila ya kuwamo jina lake popote pale katika nyaraka husika na badala yake hutumia majina ya watu wengine ambao ni feki.

  Atueleze maana yake nini hasa kufanya hivyo kama siyo namna ya kufanya utapeli, kama vile kukwepa kodi, kukwepa mashitaka n.k. Atupe mwanga kwa hilo.
   
 14. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 667
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80
  Kwa waandishi wetu ikiwezekana aondoe utata uliojitokeza kuhusu uraia wake na shule alizosoma kama ni hapa TZ au nje. Isije ikawa ni geresha ya mambo tu!
   
 15. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,644
  Likes Received: 21,855
  Trophy Points: 280
  Humu jamvini najua wapo waandishi ambao watapata nafasi ya kuwepo katika hiyo conference. Please msituangushe, yale maswali ambayo tunayo hapa kijiweni kwetu basi muulizeni ili tujiridhishe kwa majibu yake,pengine tunamhukumu isivyo.
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  ***************************

  Counterpunch:

  Kuna thread yako ya juzi kwamba gazeti la Rai halijui nani mmiliki wake -- yaani halijui kama Rostam ndiyo mmiliki wa kampuni inayolichapisha -- New Habari. Hii ni kampuni nyingine tena ambayo Rostam hakutaka kutumia jina lake na inasemekana ina matatizo makubwa pamoja na kudaiwa kodi na TRA na michango ya NSSF.
   
 17. Ndanda to Lomwe

  Ndanda to Lomwe Member

  #17
  May 2, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni strategy yake tu ambayo kaanza toka juzi nadhani anafikiri watanzania ni wajinga unaweza ukawaibia na ukawanunua baadhi ukawatumia kuwadanganya wengine,kawalipia wenyeviti wa UVCCM ticket za kuja Dar kusoma waraka alioandikiwa na Lowasa,by the way baadhi wamekusudia kusema ukweli na kulaumu wenzao kuwasukuma kufanya wasiyo yajua,kwa mfano mmoja wa wenyeviti niliyeongea nae kaniambia walilipwa shs laki 3 kila mmoja na wamelipiwa ticket na gharama za kuishi Dar na wakapelekwa Maelezo kusoma waraka ambao hawajui nani aliyeuandiaka.
   
 18. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #18
  May 2, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asalaam Alaeikum wana Ukumbi,
  Mie si mgeni katika ukumbi huu, ni msomaji mzuri na mfuatiliaji wa mijadala iliyomo humu. Leo nimeona nami nichangie kidogo.

  Niliposoma kwamba RA atakutana na waandishi wa habari Kempiski nikakumbuka niliwahi kusikia kwamba bwana huyu huko nyuma alikuwa akiranda kwenye mahoteli yote makubwa makubwa kama Movenpick n.k. akiwa na wapambe wanaomzunguka na kuandamana naye. Lakini baada ya scandals zinazomuhusu kuanza kufumuka, amekuwa akikwepa watu, sehemu anayoonekana, tena mara chache, ni Kempiski! Kama haya ni ya kweli kwamba anawakwepa Watanzania wenziwe basi ni dhahiri dhamira yake inamwambia kuwa anayo kesi ya kujibu!

  Twasuburi kusikia atawaambia nini Watanzania ili wasiendelee kuamini kwamba amelikosea Taifa kwa kutangazwa na kuandikwa mara nyingi kwamba yeye ni FISADI. Hata kama atatoa hadharani madhambi yote anayoyajua ama anayoweza kutunga kuhusu Mengi ama wengine wanaomshutumu, haitabadilisha ukweli kwamba anatuhumiwa kwa ufisadi, na Watanzania walio wengi wamekwishaamini hivyo. Kwa maoni yangu, suluhisho kwake yeye na kwa wengine wenye kutuhumiwa ni kuwa jasiri wa roho, kutubu na kuwaomba radhi Wananchi kwa kuwahujumu na kuficha ukweli kwa muda mrefu na kuwa tayari kupokea hukumu inayostahili.

  RA et al kama kweli walitenda, wapige moyo konde na kuutangazia Umma kwamba ni kweli ibilisi aliwakamata wakafanya hayo yote waliyoyafanya, na kwamba watarejesha 'masenti' yote wanayodaiwa kufisadi na kuahidi kwamba wao, watoto na ndugu zao, marafiki zao na wapambe wao hawatarudia tena kulihujumu Taifa letu. Kwa kufanya hivyo watakuwa wamesalimisha silaha zao na bila shaka hata mafisadi wengine wengi watashindwa ama kuogopa kuendelea na ufisadi wao.

  Kama hayo yanaweza kutokea, basi huo utakuwa ni mwanzo wa ukurasa mpya wa kuweza kuvishinda kabisa na kuvitokomeza vitendo vya kifisadi pamoja na rushwa kubwa na hata ndogo. Taifa litakuwa limezaliwa upya!!!

  Mungu Ibariki nchi yetu!
   
 19. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #19
  May 2, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,695
  Trophy Points: 280
  Issue zinaanza kubumbuluka.

  Strategies zimepangwa visivyo! Watoto wanaanza kuharibu, itabidi wanyang'anywe mgawo waliopewa na ikiwezekana waongezewe waweze 'kula buyu'
   
 20. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #20
  May 2, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Waandishi wa habari wa bongo bwana, sijui taaluma yao wameipatia wapi ?........samahanini waungwana.......lakini ndio ukweli huo............
  Jamaa anaitisha conference utasiki .......sema tu uayotaka kusema muungwana........kamaliza hapo.
  Hamna swali hamna cha nini......
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...