Rostam kuapishwa Jumapili!

Zyansiku

Member
Jul 27, 2009
49
10
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (MNEC) CCM anaeuwakilisha mkoa wa Tabora na Mbunge wa Igunga Mh Rostam Aziz Jumapili hii ataapishwa rasmi kuwa kamanda wa Uvccm wilaya ya Igunga katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Rostam Aziz ataapishwa na mjumbe wa NEC kupitia vijana kutoka Zanzibar Mh Bundalla! aidha sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika katika kata ya Ndembezi mahali ambapo pia anatoka mkiti wa halmshauri ya wilaya ya Igunga, sherehe hizo zitahudhuriwa na viongozi wote wa vijana wa mkoa wa Tabora ambapo kila wilaya itawakilishwa na viongozi wawili ambapo upande wa chama katibu wa CCM mkoa waTabora Mh Ame Idd (Mpemba) atahudhuria.

Taarifa zaidi zinasema kuwa viongozi wa CCM mikoa jirani ikiwemo kigoma shinyanga na mwanza wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo zitakazo hitimishwa kwa Mh Rostam Aziz jioni kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa albam ya kwaya ya Nkinga (Nkinga hospital)
 
Haki ya nani hatutafika tuendako kwa mwendo huu...Duu,kelele zote tulizopiga wenzetu wameziba masikio..Kweli hii nchi imabakwa na wenye nazo.....Duu,sina hamu kabisaaaaaaaaaaaaaa...Kweli money can buy everything asikudanganye mtu..
 
Upon all wizi wote na makelele ya Watanzania lkn jamaa anazidi kupaa tu,je kweli mafisadi bongo watafungwa?sidhani...
 
Kwa mujibu wa chama chao, anaqualify kuwa kamanda wao kuongoza na kuendeleza yale waaaminiyo wao ya kwamba ni yenye kuwafaa. Kazi ipo!!
 
Ulitegemea watu wa aina tofauti na hao?

By the way, ATASIMIKWA na sio KUAPISHWA
 
Haki ya nani hatutafika tuendako kwa mwendo huu...Duu,kelele zote tulizopiga wenzetu wameziba masikio..Kweli hii nchi imabakwa na wenye nazo.....Duu,sina hamu kabisaaaaaaaaaaaaaa...Kweli money can buy everything asikudanganye mtu..

ndo hapo muone kuwa makelele yenu hayana maana...na mtapiga sana kelele mwaka huu
 
Ooh Tanzania,nakupenda sana nchi yangu. Amani imejaa tele. Ukiibia serikali wewe shujaa na unafanyiwa sherehe kubwa na kutukuzwa. Mungu atujaalie uhai tuendelea kushuhudia upuuzi huu. Swali ni 'je hali hii itaendelea hadi lini ?' Jibu unalo mpiga kura,hii ni 2010.
 
Hawa jamaa siwaelewi, pamoja natuhuma zote hizi bado tu wanambeba? Hivi viapo vya kisiasa siviamini mie. Sasa anaapa ili atende kwa uadilifu au anaapa kuendelea kuwa fisadi? Lakini sipaswi kushangaa sana manake huyu ni miongoni wa wafadhili wa CCM hasa kwenye kampeni za kitaifa wanamwaga pesa kwenye chama kama mchanga!
 
Back
Top Bottom