Rostam, Bashe watangaza vita na JK, wamuita naye fisadi

Asante Mkuu! Umenikumbusha mbali sana:

When The river Between flows, Things fall Apart, people are No Longer at Ease and only A man of the People (Dr Slaa?) can right it!! :A S thumbs_up:

Or might be just the 'song of Lawino/Ocol'?
 
Nataka niwatengenezee bomu kabisa walipuane wamalizane, wachapane vibao na sisi tuanze maisha mapya, nani mwenye ujuzi wa kutengeneza bomu hapa tusaidiane??? hata la machozi tu litatosha maana ninachokiona sasa ni moto mkubwa sana utawaka ndani ya CCM, I cant even imagine, maana RA hatakaa kimya, Loo-hasa hatakubali na Broda Six akiwa na Maembe sorry membe mmmh sidhani kama watakaa kimya, naskia membe ameshaaanza kutofautiana na akina January huko bungeni leo....imekuja mapema sana!!
 
Mimi nafikiri wangebadilisha hata jina la chama na hiyo alama zao za jembe na nyundo. Watu wamechoka mambo hayo
 
Katika kile kinachoonekana kuwa sasa wanatangaza vita, gazeti la Mtanzania linalomilikiwa na Rostam Aziz na kusimamiwa na Hussein Bashe limemchimba JK kwa kuandika leo kwamba Kikwete naye fisadi wakinukuu List of Shame iliyotolewa na Chadema Mwembe Yanga, huku wakinukuu tuhuma zotte ambazo zilielekezwa kwa JK na huku wakijifanya kuwarushia mpira Nape na Chiligati kuwa walisema mafisadi wote CCM wajiuzulu akiwamo JK.

JK, Mukama, Chiligati na Nape walizungumza wakirejea vikao vya CCM na si LIST of Shame na kama walitambua hilo wangesema mapema si baada ya kufukuzwa.

Katika vikao vya CCM List of Shame ya Chadema haijajadiliwa bali walijadili Richmond, Dowans, Kagoda na Rada na waliwataja kwa majina Lowassa, Rostam na Chenge. Hii ni sawa na mwizi kukamatwa na kusema "tuliiba na mwenzangu mbona hakamatwi?" Maana yake anakiri kuwa ni mwizi.

Bado watameguka vipande vipande sana tu
 
aptanzaniaelection3nov2.jpg


 
..Origin ya neno 'Mafisadi' katika uongozi na siasa za Tanzania ni MWEMBEYANGA. Hakuna reference nyingine!poor CCM


Halafu mimi napendekeza hiyo ORODHA YA UCHAFU iwe inafanyiwa update kila mwaka ili kuiweka hai mpaka kieleweke. kwa mara ya kwanza ilitangazwa mwebeyanga, DSM, mwaka huu inaweza kutangazwa tena mahali pengine kama mwanza or arusha na kuongezea majina ya new fisadis, mwaka kesho tena mkoa mwingine - mchaka mchaka hadi wawe wanaona noma kutoka nje kwa aibu!!!


Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
Teh! Teh ! Teh kazi wacha waumbuane,hivi nani wa kumfunga paka kengele ndani ya ccm?
 
JK naye ni fisadi na kama mpango wa CCM ni kusafisha chama chao haitaleta maana iwapo watashindwa kumfukuza uanachama mwenyekiti wao. Isije ikawa tabia ya papa kuwala dagaa.
 
Hilo gamba lililovuliwa litasababisha mpasuko mkubwa sana hapo kwenye chama.....tusubiri!
 
Let us all pray that changes in CCM will go smoothly for the peace of Tanzanian
 
Back
Top Bottom