Rostam, Bashe watangaza vita na JK, wamuita naye fisadi

katika kile kinachoonekana kuwa sasa wanatangaza vita, gazeti la mtanzania linalomilikiwa na rostam aziz na kusimamiwa na hussein bashe limemchimba jk kwa kuandika leo kwamba kikwete naye fisadi wakinukuu list of shame iliyotolewa na chadema mwembe yanga, huku wakinukuu tuhuma zotte ambazo zilielekezwa kwa jk na huku wakijifanya kuwarushia mpira nape na chiligati kuwa walisema mafisadi wote ccm wajiuzulu akiwamo jk.

Jk, mukama, chiligati na nape walizungumza wakirejea vikao vya ccm na si list of shame na kama walitambua hilo wangesema mapema si baada ya kufukuzwa.

Katika vikao vya ccm list of shame ya chadema haijajadiliwa bali walijadili richmond, dowans, kagoda na rada na waliwataja kwa majina lowassa, rostam na chenge. Hii ni sawa na mwizi kukamatwa na kusema "tuliiba na mwenzangu mbona hakamatwi?" maana yake anakiri kuwa ni mwizi.

........this is what is called the beggining of the end.........
 
Huu ni muda muafaka kwa wanamageuzi kujipanga na sio kushabikia yanayoendelea ndani ya ccm bali kutumia udhaifu huo kuwasha moto zaidi, wananchi watazidi kuona pumba zipi na ngano ipi..

Kweli kabisa. Kwetu sis hiyo ndiyo take home message!
 
Kinachowafanya chadema wapendwe na ccm ichukiwe wakati huu ni kimoja tu!-"dhamira ya dhati ya kuwaadhibu mafisadi"
 
Muda si mrefu Mwakyembe atafungua "Pandora Box" ili tujue yale mambo yaliyoachwa wakati wa Sakata la Richmond "ili kutoiumbua Serikali!"

Box linamhusu mkuu wa kaya ndio maana halifunguki. Yalikuwa makubaliano kati ya mkuu wa kaya na EL ndio maana wanalia. Raisi ana usalama wa taifa. Daraja, msabaha, ndio walianza swala la Richmonduli wakisaidiana na EL wakati huo daraja balozi USA. Baraza la mawaziri chini ya uenyekiti wa JK ulikubali kumpa tender mohamed Gire JK akijua package nzima.

JK akiwa full mikoba alimjibu DR. Slaa kuhusu Richmond kelele za mlango hazimzii mwenye nyumba kulala.

Kwa kifupi kinachotokea sasa CCM ni civil war.
Kumbuka ndege aliyokodisha EL 2005 ilivyotua dodoma akiwa yeye na JK
Kumbuka Kagoda RA alijitoa mhanga kwa ajili ya JK akachukua zambi zote
EPA ilikuwa na mwendo wa kumwingiza JK mjengoni
Buzwag ilikuwa kulipa fadhila.
Jiulize kweli JK anaweza kumtosa RA, EL, chenge, nk hawa wana siri zote za umafia wa CCM kuingia ikulu, je CCM wako tayari mchele kurushwa nje, kama Ufisadi wa unawasumbua hivi kweli wanaweza kuvumilia usaliti wa mambo yao ya ndani?

Hata wakijichubua msitegemee lolote, kina JM na Nape wakionyeshwa chungu kilivyo watakuwa kimya na kuanza kutetea mauza mauza mpaka mtawachukia. Huwezi na akili ukawa CCM, imeoza hakuna pa kusafisha labda kama unataka kuchafuka.
 
WHEN THINGS FALL APART, THE RIVER BETWEEN IS NO LONGER AT EASY!!!!!!!!!!

Haya tena kumekucha, shughuli ndio kwanza inaanza, hebu sie tukae mkao wa kula tujioonee watu wakijikaanga kwa mafuta yao.

Heheheeeeee, na bado!!!! wataona rangi zote.
 
Huu ni muda muafaka kwa wanamageuzi kujipanga na sio kushabikia yanayoendelea ndani ya ccm bali kutumia udhaifu huo kuwasha moto zaidi, wananchi watazidi kuona pumba zipi na ngano ipi..

Mkuu nimekugongea senksi wewe ni miongoni mwa wananchi mahiri wanaoitakia Tanganyika mafanikio Mola kupe uzima, nguvu na utulivu zaidi.
 
Katika kile kinachoonekana kuwa sasa wanatangaza vita, gazeti la Mtanzania linalomilikiwa na Rostam Aziz na kusimamiwa na Hussein Bashe limemchimba JK kwa kuandika leo kwamba Kikwete naye fisadi wakinukuu List of Shame iliyotolewa na Chadema Mwembe Yanga, huku wakinukuu tuhuma zotte ambazo zilielekezwa kwa JK na huku wakijifanya kuwarushia mpira Nape na Chiligati kuwa walisema mafisadi wote CCM wajiuzulu akiwamo JK.

JK, Mukama, Chiligati na Nape walizungumza wakirejea vikao vya CCM na si LIST of Shame na kama walitambua hilo wangesema mapema si baada ya kufukuzwa.



Katika vikao vya CCM List of Shame ya Chadema haijajadiliwa bali walijadili Richmond, Dowans, Kagoda na Rada na waliwataja kwa majina Lowassa, Rostam na Chenge. Hii ni sawa na mwizi kukamatwa na kusema "tuliiba na mwenzangu mbona hakamatwi?" Maana yake anakiri kuwa ni mwizi.

Kilio cha mfa maji.
 
Hawana ubavu na jeuri ya kumtangaziA vita JK. Hatua inayofuata sasa Ni kuendelea kuwazomea na kuongeza magi HUKO WALIKO. Maana wahenga walisema MFA MAJI HAACHI KUTAPATA. Wametuumiza Sana, Edward Loowasa, Rostam Aziz, Endrew Chenge na Karamagi. Wasipo ondoka ukumbini. Wataendelea kukosa amani na wote watakufa kwa Blood Pressure. ZOMEA ZOMEA KILA KONA HATA KAMA KWENYE MAJIMBO YAO YA UBUNGE WANAHESHIMIWA KAMA MIUNGU HATUWATAKI MAFISADI. FISADI NI FISADI HATA KAMA KAJIVUA GAMBA. UNAWEZA UKADHANI AMEJIVUA GAMBA KUMBE WAKATI WENZAKE WANAJIVUA MAGAMBA YEYE ALIKUWA NJE KUPOKE SIMU KAMA MITAMBO YA DOWANS IMEWASHWA.
 
Mkuu nimekugongea senksi wewe ni miongoni mwa wananchi mahiri wanaoitakia Tanganyika mafanikio Mola kupe uzima, nguvu na utulivu zaidi.
mkuu penye nyekundu hapo utafungwa mkuu! sema Tanzania! tanganyika haipo kwanza ni ubaguzi kwa sisi wazanzibar!
 
Wana JF nape na chiligati kama wamei2mia kama reference dhidi ya mafisadi ni kusema ile list of shame ni ukweli?
 
Back
Top Bottom