Rostam Aziz/Reginald Mengi na Simuliziya Mpiga Filimbi wa Amelin | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam Aziz/Reginald Mengi na Simuliziya Mpiga Filimbi wa Amelin

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, May 13, 2009.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Ni bahati mbaya sana Rostam Aziz hana ubavu wa kumshinda Mzee Reginald Mengi katika uwezo wa kuwateka wananchi kiakili! Uwezo huo anao Reginald Mengi ambapo umwangiliapo tu wakati anapoongea, sura yake inatoa ujumbe wa mtu safi, mpole, mkarimu na ambae watu hupenda kumuonea kutokana na upole wake! Hata hivyo, kwa upande wa Rostam Aziz hutachelewa kuiona jeuri ya pesa na majivuno wakati wa maongezi yake! Labda kinachoonekana kutoka kwa wote, hususani kwa yule asiyetaka kuumiza kichwa, ni uchungu walionao watu hawa kwa ndugu zao watanzania!

  Kwangu mimi, si Rostam wala Mengi ambae tuhuma zake zimetokana na uchungu alionao kwa nchi hii! Hawa wote hawana tofauti yoyote na Mpiga Filimbi wa Amelini aliyekusudia kuwatokomeza panya na ambapo mwisho wa mchezo na watoto wa vijiji vile nao wakapotelea kusikojulikana walipokuwa wanamfuata mpiga filimbi wa Amelini!

  Kama nilivyosema awali, Rostam keshazidiwa kete na Mzee Mengi tangu zamani hizo! Wakati Rostam alijikita zaidi kuwashika viongozi na watendaji mbalimbali wa serikali, Mzee Mengi alijikita zaidi katika kuziteka hisia za watu, hususani wanyonge! Mengi alishafanikiwa tangu zama hizo kujionesha kuwa yeye ni mtu safi, mpole, mnyonge, muonewa wivu, na kubwa zaidi ni mpenda maskini na watanzania kwa ujumla!

  Hata hivyo, nasikitika kwamba si Rostam Aziz wala Reginald Mengi aliyefanikiwa kunipata kwenye tundu lake.

  Hata hivyo, kwavile naamini kati yao ni Reginald Mengi ndie aliyefanikiwa kubeba ipasavyo mikoba wa Mpiga Filimbi wa Amelini, basi nahisi kusononeka kutokuwamo kwenye msafara wake! Sina shaka yoyote kwamba mpiga filimbi huyu alipopita mtaani kwetu, mimi nilijumuika na watoto wenzangu kumfuata nyumanyuma huku tukifaidi utamu wa muziki kutoka kwenye filimbi yake! Sifahamu ni nini kilinitokea, lakini kabla hajakata kona kiasi cha kutoweka kwenye upeo wa macho kutoka nyumbani kwetu, nilishituka na kurudi mbio nyumbani huku nikihema!Pamoja na yote hayo, hivi sasa nahisi kama najutia maamuzi yangu ya kumuacha Mpiga Filimbi wa Amelini aende zake! Rafiki zangu wote ambao nilikuwa nao awali kwenye msafara wa mpiga filimbi; bado hawajarejea! Siamini kama wamepotea, bali nahisi wanaendelea kufaidi muziki wa filimbi, na ndio maana hawataki kurejea nyumbani! Kwani si wapo wanaoamini kwamba hata wafu nao kuna kitu wanafaidi huko kuzimu na ndio maana hawataki kurejea duniani!? Sio siri, naowaonea wivu watoto wenzangu, nahisi wanafaidi muziki wa mpiga filimbi!
  Good! Nimeikumbuka sababu iliyonifanya nimshiti Mpiga Filimbi wa Amelini aende zake na mimi kurejea nyumbani, haijalishi hata kama hivi sasa najilaumu! Pamoja na ala tamu za filimbi, lakini mashairi yalikuwa ni yaleyale ya akina Marijan Rajabu, TX Moshi William, Muhidini Ngurumo na wengineo wengi kama hao! Ni mashairi ambayo nahisi yalishayachosha masikio yangu! Lakini kwavile natamani kwenda kuungana na watoto wenzangu ili tuserebuke wote na ala za filimbi yake, basi namshauri angalau aweke chorus (kibwagizo) ya muziki wa kizazi kipya!

  Ngoja kwanza nijaribu kutengeneza theory kama ita-fullfil:
  First Law:
  “To every grand corruption action there must be two dependent bonds responsible for completing the corruption circuit, these are business people and decision makers bonds!”

  Second Law: “For any corruption circuit to be disconnected and allow no more electrons to pass through,there must be a committed techinician who’s able to expose both bonds from a connected terminal”

  Mzee Mengi bado hajanishawishi kwamba yeye ni committed technician kwavile haja-expose both bonds! Mbaya zaidi ni kwamba napata mashaka zaidi na commitment yake kwavile bonds alizozi-expose ni zile tu zinazowafanya watu wahisi kuwepo kwa conflicting objectives! Kama tunakubaliana angalau kwa 50% na theory zangu basi wale ambao Mzee Mengi hajawataja ni Decision Makers, ambao wengi wao kama sio wote ni wanasiasa na watendaji wakuu wa serikali au taasisi za umma!

  Binafsi, hawa watu kwangu ndio muhimu zaidi kuliko hao akina Jeetul Patel! Si kwamba wakina Rostam si watu muhimu katika hili, ninachosema ni kwamba watu ambao hawajatajwa ni wale waliowekwa sehemu walizopo ili kulinda maslahi ya watanzania! Jeetul Patel na wenzake hawafanyi biashara kwa maslahi ya watanzania, bali wanafanya kwa maslahi yao binafsi na ndio maana hawaoni aibu kuwahujumu watanzania walio wengi. Endapo ningepewa nafasi ya kuulizwa ni bond ipi itajwe na ipi isitajwe, basi sina shaka ningeitaka bond ya decision makers ndio itajwe. Hii ni kwavile muda si mrefu bond hii itajinadi mbele yetu kwamba wao ni watu safi hivyo wangependa kutuongoza na kuendelea kulinda maslahi yetu kumbe ndio wala rushwa wakubwa!

  Mzee Reginald Mengi alikaririwa kwamba kuna mafisadi kama kumi hivi nchini, miongoni mwao watano ni mafisadi papa ambao wote ni wafanyabiashara! Sasa kama nia yake si kuwamaliza washindani wenzake wa kibiashara ni kwanini asiwataje hao mafisadi wengine ambao bila shaka ni wanasiasa hata kama ni mafisadi sangara au vibua?! Kama kweli aliwataja mafisadi papa kwa ajili ya uchungu alionao nao kwa watanzania basi hana budi kuwataja na mafisadi sangara kwavile ndio hasa tuliowaweka ili wayalinde maslahi ya watanzania wote! Asipowataja, basi nitahisi wale aliowataja amesukumwa zaidi na:
  1. Maslahi Binafsi ya Kibiashara,
  2. Inawezekana kweli Mzee Mengi ana ndoto za kugombea urais wa nchi hii hivyo asingependa kujiundia maadui wa kisiasa ambao bila shaka wengi wao kama sio wote watakuwa ndio wajumbe wa NEC
  3. Kama kweli Mzee Mengi anakwepa kodi basi anaogopa kuwaumbua wanasiasa ambao ndio wadau wakuu katika kuwezesha ukwepaji kodi wa wafanyabiashara wakubwa. Maana yangu ni kwamba anawaogopa kwavile anajuwa ameshawahi kuwatumia katika kukwepa kodi!

  Kama nilivyoeleza hapo awali, natamani kumfuata mpiga filimbi huyu wa Amelini, lakini aweke kibwagizo cha Bongo Flavor kwa kuwataja na mafisadi sangara,na haidhuru hata kama ni vibua wa hapa kitaani kwetu!
   
 2. H

  Hongasuta Member

  #2
  May 13, 2009
  Joined: Sep 10, 2006
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umetumia effort kubwa sana kuelezea hilo la mpiga filimbi wa amelini lakini huna hoja ya maana.
   
 3. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hamelin
   
 4. B

  Baba Ubaya Senior Member

  #4
  May 13, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu hueleweki mbona
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Anahitaji Fisadi Nyangumi awataje wafisadi wa serikalini(watendaji) na wanasiasa ambao kwa namna moja ama nyingine wanahusika na ufisadi wa Mafisadi Papa
   
 6. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Bila shaka mleta hoja ameeleweka vyema pamoja na kwamba ameweka vikorombwezo vingi ili kutia utamu. GOOD PIECE OF WORK
   
Loading...