Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

tibwilitibwili

Senior Member
Sep 12, 2006
184
10
Hii ndiyo halisi ya habari Tanzania . Naleta makala hii japokuwa ni ya muda kidogo ili iweze kuingia kweney record. Je ni kwa sababu hii ndiyo maana waandishi wanalamba viatu vya JK ?


HEADLINE: CCM magnates in the media

The treasurer of the Chama cha Mapinduzi (CCM) and advisor to the government party on economic and financial issues, the businessman and MP Rostam Aziz has recently acquired a significant stake in the largest press company in the country, Habari Corporation Ltd (HCL).

And yet he is not a newcomer in the Tanzanian press sector, since during the 1990s he had launched the company Mwananchi Communications Ltd (MCL) in partnership with Ferdinand Ruhinda, a former ambassador turned businessman and close ally to former President Benjamin Mkapa.

Aziz and Ruhinda subsequently joined forces with the Aga Khan's Nation Media Group to launch a daily English language newspaper, The Citizen.

They later disagreed with their Kenyan partners over the coverage of Jikaya Kikwete's election campaign last year. A few months ago Aziz therefore sold a large proportion of his shares in MCL and purchased the stakes held by several journalists (Salva Rweyemamu, Jenerali Ulimwengu and William Shoo) in HCL. Since then this press group which was quite virulent under the previous regime has calmed down considerably with the present government. Other CCM dignitaries also have interests in the media. This is so in the case of Minister of Livestock, Anthony Diallo the owner of Sahara Communications Ltd which operates Star Television and Radio Free Africa as well as publishing the weekly magazine Msanii Afrika.

For its part, the IPP Media group (The Guardian Ltd, Media Solutions Ltd, Independent Television and Radio One Ltd) owned by the magnate Reginald Mengi has always been able to butter up successive governments. However, today he is in the line of sight of several CCM executives due to some of his news stories.


URL: www.IndianOceanNewsletter.com

LOAD-DATE: October 27, 2006
 
sidhani kama kuna sheria inamkataza kununua hayo makampuni na of course lengo ni kupata profit

sasa labda issue iliopo mkononi ni kama kuna conlict of interest zozote na kama zipo je kuna maelezo au evidence yoyote kussuport hizo data?
 
Nakubaliana nawe hakuna sheria lakini matokeo yake ndiyo haya sasa kwamba habari za kweli na makelele ya kweli yanatokea jambo na si media za hapa nyumbani ambazo zinawafikiwa wengi ili wajue Nchi yao iko vipi .
 
Hivi ile sheria ya kutoruhusiwa kucover habari zaidi ya 25% ya eneo la Tanzania bado ipo?
 
kuna ukweli ulio Dhahiri kwamba ukimudu kuvituliza vyombo vya habari utatawala utakavyo,kwani maovu yako hayatosikika kwa umma.Sasa kwa mtazamo wangu naona awamu hii hilo ndilo lengo lao.Wanajaribu kwa kila mbinu kuwakumbatia waandishi ili mabovu yao yasisemwe.Si unaona hii issue ya RDC itakufa hivi hivi kwa sababu tu haisemwi sana kwenye vyombo vya habari vya nyumbani,na nataka kukuthibitishia tu,ya kwamba wananchi walio wengi hawajui Mkataba huu mbovu kati ya serikali yao na akina Gire!
 
Mwawado, right on... kwa sababu watanzania wanapenda kugereshwa sana.. Hakuna anayeuliza iweje tukodi mtambo kwa gharama ya juu ambapo tungeweza kupata mtambo huo huo na kuumiliki kwa gharama ya chini sana kuliko hiyo ya kukodi? Iweje uamue kukodi kwa gharama ya juu badala ya kumiliki kwa gharama ya chini. Ni sawa na mtu anaamua kukodi gari na analipia shilingi milioni 20, wakati gari hilo hilo tena jipya lina gharibu shilingi milioni 10!! IT DOESN'T MAKE ANY SENSE!!
 
Brother MKJJ,
You'll never, ever get an explanation from the Gov't on this, trust me. Same like SONGAS (You sell your house to become a tenant to that house), Radar (which I heard worked for a couple of months only and now it is kaput!!), IPTL, Military L/R Discoveries (refer BCS discussion), and many, many more issues like these. It only happens in TZ.
 
ndiyo maana Rostam kaamua kuvimaliza si mambo ya biashara hapana na haya mambo JK na Rostam waliya anza mapema sana . Iko kazi sana kweney kampeni sijui itakuwaje .Halafu wanalalama kwamba wanatukanwa na watu wa Kenya juu ya kulamnba viatu .Lakini Jk na Rostam na kundi lako mjue kwamba haya ya mwisho sana .Ni wakati wa kujenga senta za habari Nchini watu wengi wawezeku access mitandao ili kupambana na waandishi wajinga na ndiyo maana hata umeme unakuwa shida ili watu wasiweze kukaa online kwa muda mwingi .
 
Defacto leader wa Tanzania sasa hivi ni Rostam Aziz...sasa katika kuhakikisha anajilinda na mambo yake machafu katika kuangamiza nchi........ameteka magazeti yaliyokuwa yanaheshimika sana katika utoaji wa habari zilizofanyiwa utafiti..
Ndio sio mbaya kununua gazeti, lakini lazima sisi wa TZ tuelewe madhara ya ununuzi huu hasa hasa kwenye swala la transparency and good governance
 
Watanzania maisha yao hawajui kwamba yana amliwa na Chama siasa kinacho kuwa madarakani bali wanaleta mchezo kwa kuweka ushabiki wa Simba na Yanga matokeo yake watu wanaleta mikataba kama ya Richmond na hakuna wa kusema magazeti kimya na wasomi mitini na watu tunalia na Upinzani sasa kesho wakiomba kura kuwa nguvcu Bungeni ku balance issues tunasema wana tamaa tamaa ya madaraka .
 
watu kama rostam na mengi wanatuharibia uhuru wetu wa kikatiba wa kupata habari[za kweli] kuhusu nchi yetu,,huyu rostam na jk historia itawahukumu kwa kununua wana habari,,tena nasikia na kada wa chama manji kanunua shea majira ,,je ni kweli wana lengo na faida??
 
Kuna habari za kuaminika kuwa Mhe Rostam Aziz maarufu humu kama RA amekuwa akihaha katika vyumba vya habari na kufanya vikao mbalimbali na baadhi ya wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kumtengenezea mabomu Zitto Kabwe ili jamii iache kuamini kile ambacho amekuwa akikisimamia katika siku za hivi karibuni.

Kumbukeni kuwa RA ndiye alikuwa mmoja wa wakuu wa idara ya propaganda wakati wa kampeni za urais ndani ya CCM mwaka 2005. Kwa kutumia waandishi mbalimbali ambao wengi wao tayari wameshatajwa hadharani huyu jamaa ndiye alikuwa chanzo cha habari nyingi nyeti za serikali ambazo zilipelekea kuanguka kisiasa kwa mawaziri kadhaa wa serikali ya tatu ambao walikuwa wakonekana tishio kwa JK ambaye walitegemea kupata ride yake kuneemesha maslahi yao binafsi.

Huyu jamaa ambaye kwa sasa ndio anaonekana kama KING MAKER nchini mwetu na kiongozi wa pili katika kundi la MTANDAO MASLAHI akifuatiwa na mshirika wake kibiashara na tajiri mwenzake Nizar Karamagi amekuwa mwiba mkubwa kwa JK kutokana na uroho wake wa kutaka awe katika kila deal inayoendelea nchini. Rostam ni mtu mwenye upeo mkubwa sana wa kiakili na mjanja kibiashara na asiye na simile katika kulinda maslahi yake. Mbinu chafu ndio jina lake la pili na unafiki ndio middle name yake.

Katika hali inayojitokeza sasa inaelekea RA anapigania maslahi ya kundi ziima la MTANDAO MASLAHI kutokana na dalili kuwa limekuwa mzigo mzito kwa JK kufikia mahala kuonyesha dalili zote za kushukiwa na nyundo kali hata kabla ya uchaguzi wa ndani wa chama kufanyika.

Pamoja na kuwa maslahi katika makampuni mbalimbali miliki ya vyombo vya habari kama Habari Corporation ambayo hutoa magazeti ya RAI, MTANZANIA na vilevile share ndogo katika umiliki wa gazeti la MWANANCHI na THE CITIZEN ambako amekuwa akizidiwa nguvu na Wakenya, RA anaushawishi mkubwa kwa waandishi wengi wa magazeti yetu kufikia wakati fulani kuwa akiwalipa mishahara tena mikubwa kuliko wapatayo kutoka kwa waajiri zao.

Moja ya kazi inayoendelea ni uandishi wa makala mbalimbali za kuwahadaa watanzania kutomuamini Zitto kabwe akiwatumi watu kaka Dr Gideon Shoo na Muhingo Rweyemamu ambao kwa miaka mingi sasa wamekuwa watumishi wake waaminifu katika kazi ya UHANDISI WA HABARI. Hawa ni vinara tu lakini wapo wengi wengine. ngome yake nyingine ni Gazeti la MAJIRA.

Kwa hali inayoendelea ni wazi mtasikia mengi kuhusu Zitto Kabwe lakini kuweni makini na kujaribu kujua vyanzo vya habari hizo. cha ajabu ni kuwa huyu jamii wakati wote hupenda kujifanya ni rafiki wa Zitto na kujigamba kuwa anamkubali na misimamo yake lakini ukweli ni kuwa akipata nafasi tu hataacha kummaliza ndugu yetu na kijana mwenzetu Zitto Kabwe. Ukweli ni kuwa RA ameshiriki hata kupanga njamaa za kuwaundermine baadhi ya wanamtandao wenzake ambao wanonekana kuelemea kundi la MTANDAO MATUMAINI linaloongozwa na Waziri MMoja mwandamizi Nchini ambalo liliweka imani ya matumaini ya watanzania kwa JK ambaye anaonekana kuelemewa nguvu na mafisadi waliojikita katika mpango wa kula hadi kusaza utajiri wa watanzania.

Zaidi sintashangaa kuwa hili likawa kosa la mwisho la RA ambalo sio tu litamrudi yeye binafsi lakini pia lina hatari ya kuzua hasira za watanzania wengine dhidi ya watanzania wenzao wenye asili ya asia (mnapenda waita wahindi) ambao RA anaonekana kama kinara wa maslahi yao katika ngazi ya kisiasa ingawa yyeye ni Muiran (mbulushi)zaidi ya uhindi.

Tanzanianjema
 
TanzaniaNjema:

Ahsante sana kwa taarifa. Unajua, vita yetu hii ya kuiokoa nchi yetu ambayo sasa inaelekea kung'ang'aniwa na mafisadi, ukiwa unatupa tu risasi gizani bila kujua adui yupo wapi ni kazi bure.

Michango ya namna hii inayowatoa nje mahasimu wetu ni mhimu sana katika mapambano haya.
 
Kalamu na wananchi wenzangu, mi nadhani from now onwords, tuanze kufikiria si tuu kuwaidentify hawa wanaotuhujumu. Tuanze kustrategize kipi tunaweza kufanya katika hizi harakati. Kila mtu akitimiza wajibu wake. Hakika, mambo yatabadilika. Maana hawa mafisadi wameshakula vya kutosha mno. we cant afford any other minute of waiting. Tupeane mawazo katika hili.
 
Mtu akitaka kuujua ukweli kabisa atakubaliana na mimi kwamba Rostam Aziz ndiye hasa rais wa Jamhuri ya Muungano.Maana si king Maker pekee pia final decision maker . Kitendo cha Uslama wa Taifa kumwachia mtu wa Iran kuwa na nguvu kubwa za namna kama alivyo kuwa Kinana those days kuna risk usalama wa Nchi hii .Siasa chafu na hata kutumia pesa na vyombo vya habari kwa manufaa ya wizi wao na kuwaacha watanzania wengi katika dimbwi la umasikini haikubaliki na mwisho wake ni mbaya sana .RA tuachie Nchi yetu bakia na CCM yenu .
 
Back
Top Bottom