Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Si tuleteeni basi hiyo habari? Naona haiko kwenye Internet bado.

leo jioni unaweza ipata katika Tovuti ya Raia Mwema.kuhusu hii ya Mwanahalisi. check na saed kubenea katika e-mail yake atakupa copy coz yeye ndiyo ameiandika.ila kwa kifupi habari niliyotoa hapo juu ndio iko hivyo hivyo,mie niliipata kwa ufupi tu.
 
ndiyo.. iko kwa MwanaHalisi halafu kwenye Raia Mwema kuna kachumbari yake!

Mwanakijiji,

Watu tumesubiri wee, mpaka na kuamka mapema ili tuwahi utamu. Sasa utamu mpaka utaisha ili baadaye tule makombo? Mwenye nayo naomba hata kama ni kwenye PM yangu kama hairuhusiwi kuiweka hapa.
 
wakati Rostam akitoa maneno hayo Mhe. Spika alimwambia jiuzuru sasa hivi na Mhe. Pinda ambaye kwa sasa ndiye amri jeshi mkuu akamuunga mkono Mhe. Sitta.

.[/B]

Haya ni maneno mazuri sana.

Hivi huyu RA kwani yeye anafikiri akijiuzuru kuna matanzania atakayekuwa na hasara?.

Anyway JK atahangaika sana maana ni mizigo yake, hila wananchi tungepiga filimbi, nderemo na vifijo.

Nafikiri wabunge walazimishe aende akajieleze hata na hayo makablasha yake, tunaweza kufanya kasikukuu kakubwa .
 
Na Lula Ndali Mwananzela.
Raia mwema.

Kama kuna kitu ambacho kimenikera wiki iliyopita ni habari ya kuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Abdurasul Aziz (CCM), amelazimishwa kunyamaza baada ya kutishia kusema "Kitu" bungeni.

Kwamba mbunge ambaye ameapa kulinda katiba ya Tanzania ambayo ndani yake inasemwa wazi kuwa hakuna mtu ambaye mawasiliano yake yanaweza kuingiliwa kati au uhuru wake kuwekewa mipaka pasipo sheria anakubali kukaa kimya kwa ajiri ya chama chake.

Wazo hili si ti limatisha linatetemesha pia. Sikubali na siwezi kulikubali na hakika halistahili kukubliwa na Mtanzania mwingine yoyote yule.

Lakini ni kitu gain hasa kilifanyika bungeni kiasi cha kusababisha mbunge huyo kushindwa kuleta maeleze yake aliyotakiwa ayalete kufuatia mapendekezo ya bunge yaliyotokana na ripoti ya kamati teule ya Bunge ikongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe?

Ni kitu gain hasa alitaka kusema kiasi kwamba kwa nyakati tofauti imeonekana kana kwamba ana "Jambo" kubwa ambalo lingeweza kuleta vurugu bungeni?

Kwanza kabisa tuliambiwa kuwa Rostam ataleta maelezo yake hasa baada ya wakati ule wa kiko cha Richmond kudai ameonewa kuhusishwa kwake na kampuni hiyo hadi ilipofikia mbuge mmoja kumtaja kuwa yeye ndiye mmiliki wa kampuni hiyo na pili ni pale alipodai kuwa ripoti iliyotolewa si yenyewe au imebadilishwa na iliandaliwa hata baada ya muda wake kwisha. Hayo na lile la yeye kushidwa kujitokeza kuhojiwa na Kamati hiyo yamechangia kufanya watu waulize swali la kwanza la msingi huyu Rostam anadhani yeye ni nani?

Sitaki kujaribu kujibu sehemu ya swali hilo.

Kinachonigusa mimi leo hasa baada ya matukio haya ya juzi ku kujaribu kufuta jawabu la ni kitu gani mbunge huyu alitaka kusema bungeni kiasi kwamba kusababisha spika wa bunge, Samuel Sitta kugwaya mbele mbele yake kama mianzi iplizwayo na upepo? Je alikuwa na kitu gania ambacho spika Sitta na CCM wasingependa hadhaara ya Watanzania isikie.

Kwa mtu yeyote ambaye anajua kujumlisha si kazi kuweza kujua ni nini Rostam alitaka kusema na kujaribu kuchanganua na kuchambua yele ambayo Rostam angeweza kusema na mabayo yangeweza kuwa tishio kwa CCM na mishikamano wa Wabunge wa CCM bungeni.

Kwanza kabisa lazima turudi kwenye mjadala wa Richmond ambo ulisababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa waziri Mkuu, Edward Rowasa na mawaziri wengine wawili , Naziri Karamagi na Dr. Ibrahim Musabaha (Siwezi kueleza kama kisheia hilo linawezekana kwani waziri mkuu alijiuzulu na Baraza la Mawaziri nalo linavunkika isipokuwa kama msabaha na karamagi wangemtangulia Lowasa).

Katika mjadala ule kama kuna kitu ambacho kilikuwa dhahiri ni hasira za wabunge ambao walionyesha msimamo mkali na mabo uliwauma waliotajwa kuhusika na Richmond ni Anne Kilango Malecela ambaye kwa uthabiti wa maneono na pasipo kugugumizi alitangazia umma mzima kuwa hata kama ingekuwa ni mzee malecela ametajwa kuhusika na ufisadi wa Richmond angemtosa vile vile!!

KWA habari zaidi tafuteni Raia Mwema.
 
Haya ni maneno mazuri sana.

Hivi huyu RA kwani yeye anafikiri akijiuzuru kuna matanzania atakayekuwa na hasara?.

Anyway JK atahangaika sana maana ni mizigo yake, hila wananchi tungepiga filimbi, nderemo na vifijo.

Nafikiri wabunge walazimishe aende akajieleze hata na hayo makablasha yake, tunaweza kufanya kasikukuu kakubwa .

"Uchunguzi wa MWANAHALISI umeonyesha kuwa wajumbe walikuwa wamekamilisha kile kinachoitwa misumari ya mwisho ya kumpigilia Rostam

Imefahamika kuwa Rostam,katika hoja yake hiyo iliyokataliwa na spika aliwaita wabunge wasanii na wababaishaji kwasababu walimshuku kwenye taarifa yao kuhusu kuhusika na mkataba wa Richmond/Dowans"

Source:Mwanahalsi

JF- We always report what they dont report
 
Tunaombeni mtusaidie kutuwekea hapa hiyo taarifa ili tuichambue vizuri.

Inaelezwa kwamba baada ya RA kutoa kauli hiyo,Waziri mkuu na Spika kwa pamoja walimtaka afanye hivyo haraka.

"kabla Rostama hajamaliza kulalama,Spika hakumkawiza.Alsisema,"Andika Barua ya kujiuzuru sasa hivi.Hatuwezi kupeleka matusi haya ndani ya bunge..."

na imefahamika wazi kwamba wajumbe wa kamati teule walikuwa wamejiandaa vilivyo kulithibitishia Taifa kuwa RA ndiye mwenye Richmond na Dowans"
 
"Uchunguzi wa MWANAHALISI umeonyesha kuwa wajumbe walikuwa wamekamilisha kile kinachoitwa misumari ya mwisho ya kumpigilia Rostam

Imefahamika kuwa Rostam,katika hoja yake hiyo iliyokataliwa na spika aliwaita wabunge wasanii na wababaishaji kwasababu walimshuku kwenye taarifa yao kuhusu kuhusika na mkataba wa Richmond/Dowans"

Source:Mwanahalsi

JF- We always report what they dont report

Kunradhi hivi huyu RA anafikiri yeye ni nani katika nchi hii?? Yeye kama hakuhusika na Richmond/Dowans kwa nini basi hakujipeleka kutoa ushahidi wa kukana kuhusika kwake na badala yake alibakia analalamikia tume kufanya kazi nje ya muda uliopangwa!!!
Surely i hate his guts!!!! ...Fisadi RA go to hell!
 
Domo Kaya, ingawa mada yako ni mwafaka, lakini mkuu tubadilishie hizo font (ondo rangi nyekundu na uzikuze kidogo); font ulizotumia zatuumiza macho, wana JF wengine umri wetu umekwenda, twaomba mutujali. Nawakilisha
 
na imefahamika wazi kwamba wajumbe wa kamati teule walikuwa wamejiandaa vilivyo kulithibitishia Taifa kuwa RA ndiye mwenye Richmond na Dowans"

Hapa nafikiri walimuepushia mengi maana kidogo tu arudishwe Irani, Sasa spika naona anampenda sana huyu FISADI
 
Tabia ya siri huwa inaweza kutoka yenyewe ikizuiwa sana,Tusubiri kidogo hiyo siri itatoka tuu hata kama ikizuiwa
 
mimi simpendi sana RA lakini kama amefikia hatua ya kutaka kuwaambia aliwatumia kufanikisha mamabo yake bungeni kuwa ni wababaishaji ningefurahi sana angepewa nafasi hiyo maana ingekuwa bora sana kama wabunge wangekubali kuwa kikulacho ki....., maana sisi tukiwaambia wabunge wa CCM ni wababaishaji na wenye siasa za chumia tumbo wanatudharau.

ningefurahi sana huyu RA angepewa awasilishe hayo anayoita spika matusi ili sitta mwenyewe awe wa kwanza kuanguka maana kuna habari ambayo haijathibitishwa kuwa RA anataka kumwaga upuuzi wote wa Sitta na hata kile kilichofichwa na Mwakyembe kumuhusu JK na Luhanjo.

hii ndio sababau kubwa ya jeuri ya RA na hata huyu mizengwe anajikomba kumlinda bosi wake nakwambieni mtashangaa siku ikilipuka hili pia.

mizengwe sina imani naye sana maana ameingia kumlinda mkapa na tuhuma zake mtakuja kulibaini siku sio nyingi katika reshufle za kazi za watendaji serikalini. .
 
Nafikiri hapa tusishangilie kuzuiwa kwa Rostam kuongea bungeni. Lengo la spika na PM ni kuficha ukweli na sio vinginevyo.

Wangemwacha aseme analojua na hapo ndio ingetusaidia kujua yote kwenye hiyo Richmond.

Wananchi tuna uwezo wa kutosha kuchambua uongo na ukweli. Kitendo cha kumzuia kinaleta hisia kwamba walikuwa wanailinda serikali ya CCM zaidi kuliko kutetea maslahi ya taifa.

Mwacheni Rostam aongee anavyoweza na kama ni kujimaliza basi atajimaliza mwenyewe kwa maneno yake.
 
Fuatilia tovuti ya MwanaHalisi: http://www.halihalisi.co.tz/ yumkini watachapisha toleo la wiki hii punde. Toleo za wiki hii ni kiboko, Mambo ya Chenge Hadharaniii, yaani, waweza kulia.

Asante Sekenke nilikuwa naitafuta website ya mwanahalisi, nimefurahi kuipata. Ila toleo la leo naona bado halipo hewani. Naomba mwenye hiyo makala anirushie kwenye PM yangu tafadhali.
 
Kunradhi hivi huyu RA anafikiri yeye ni nani katika nchi hii?? Yeye kama hakuhusika na Richmond/Dowans kwa nini basi hakujipeleka kutoa ushahidi wa kukana kuhusika kwake na badala yake alibakia analalamikia tume kufanya kazi nje ya muda uliopangwa!!!
Surely i hate his guts!!!! ...Fisadi RA go to hell!

Napenda kutofautiana na baadhi ya maneno ktk taarifa ya kubenea.si kweli ata kidogo kuwa kamati ya uongozi imemtaka rostam ajiuzuru bali PM ametumwa akamshawishi asijiuzuru,,,ok kwa nini anataka ajiuzuru?anajiuzuru ili aweze kutoa maelezo yake kama raia bila kufungwa na ethics za kuwa mbunge.Kwa upana maelezo yake yana annexture zenye mambo makubwa matatu...moja ni kuwa priamble ya kwanza iliopelekwa kwa spika haikuwa imemtaja spika wala rostam kuwa wanausika,hapo cha msingi ni kuwa walikaa tena kwa maelekezo ya spika nje ya muda waliopewa kwa ajili ya kuandika tena.pili kuna mawasiliano ya spika na mwaki juu ya kufanya kila wanaloweza kusudi kumwingiza pm na RA.tatu walificha makusudi wakurugenzi wa richmond na uhalali wake ili watu wafanye guesing kuwa na kina Rostam,hapo ndipo maelezo kama huu ni mradi wa bwana mkubwa na rafikie RA yakawekwa kwa madai kuwa shahidi aliongea nje ya kiapo...sasa kama wangeweka ushahidi wa mmiliki wa richmond basi usanii wake wa kuwa ni mradi wa bwana mkubwa na rafiki yake husingekuwa na maana yeyote.
 
Naona FISADI una information unaweza kutusaidia.

HIvi Richmond ni ya nani?

Je mazingaombwe yote tuliyosoma katika kupata Kampuni Richmond ni kweli au si kweli?

Unaweza kutusaidia kubandika nakala halisi ya source ya information zako hata sisi tujionee mwenyewe?

Maana sisi tutamalizia kwa uchambuzi wa mwanahalisi.
 
Habari ndio hiyo!

Kuna kitu kinaitwa OCR kwenye kifaa kinachokutumika kutengeneza vivuli na kuvihifadhi kwenye Kompyuta, Scanner! OCR kwa kirefu ni Optical Character Recognition... Sina maelezo mengi, ila moja ya kazi zake ni kama hii hapa chini:

Rostam Taabani
Na Mwandishi Wetu
MwanaHALISI, Toleo Na. 093, Jumatano Aprili 16-22, 2008

Mbunge wa Igunga (CCM) Rostam Aziz, ametishia kujiuzulu ubunge kutokana na hatua ya Kamati ya Uongozi ya Bunge kumzuia kuwasilisha hoja yake bungeni, MwanaHALISI limedokezwa.

Taarifa za uhakika toka ndabi ya Kamati hiyo, zinasema Rostam alitoa tishio hilo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Uongozi ambao ni pamoja na Spika wa Bunge, Samwel Sitta na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Inaelezwa kwamba baada ya Rostam kutoa kauli hiyo, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge kwa pamoja walimtaka afanye hivyo haraka.

" Kabla Rostam hajamaliza kulalama, Spika hakumkawiza. Alisema, "Andika barua ya kujiuzulu sasa hivi. Hatuwezi kupeleka matusi haya ndani ya Bunge…," alinukuliwa na mjumbemmoja wa Kamati.

Mjumbe huyo alisema kauli ya Rostam ili waudhi wajumbe wa Kamati ya Uongozi kwani haraka Waziri Mkuu alitoa tamko la kuungana na Sitta kumtaka Rostam ajiuzulu ubunge.

Wiki iliyopita, Spika alimzuia Rostam kuwasilisha maelezo yake bungeni, baada ya kubaini kuwa aliyoyaeleza katika kile alichoi ta "hoja yake" hayakustahili kuwasilishwa bungeni.

Katika Mkutano wa Bunge uliopita (wa kumi), Bunge lilimtaka Rostam kuwasilisha maelezo yake katika mkutano unaoendelea Saga mjini Dodoma, baada ya kusikika akituhumu kwamba Kamati Teule ya Bunge iliy- ochunguza mkataba wa Richmond, "iliendelea na kazi lake hata baada ya kuwasilisha ripoti yake kwa Spika."

Rostam, kwa mujibu wa taarita, alitaka Spika, kwa kutumia hoja za Rostam, amwamuru Dk. Mwakyembe kumsafisha ndani ya Bunge. Hata hiwo. shinikizo lake hila liIikataliwa

Taarifa za ndani ya Bunge, zinasema kukataliwa kwa maelezo binafsi ya Rostam kumetokana na kuonekana yamejaa tuhuma, shutuma na dharau kwa Bunge na Kamati Teule ya Mwakyembe.

Spika wa Bunge amekiri kupokea hoja binafsi ya Rostam, lakini alisema ameshind- wa kuruhusu iwasilishwe bungeni kutokana na kwenda kinyume na Kanuni za Bunge.

Mjumbe mmoja wa Kamati ya Uongozi amemkariri Spika akisema Bunge halikujadili hoja ya Rostam, siyo kwa kumwogopa, kama baadhi ya magazeti yanavyotaka kuonyesha, bali kwa sababu hoja yenyewe inakiuka Kanuni za Bunge.

Alipopigiwa simu na gazeti hili kupata undani wa taarifa hiyo, Sitta alielekeza mwandishi awasiliane na Rostam mwenyewe ambaye, Spika alisema tayari amejulishwa uamuzi huo.

MwanaHALISI halikuweza kuwasiliana na Rostam kupata upande wake.

Katibu wa wabunge wa CCM, Ali Ameir Mohammed, alipoulizwa juu ya suala hila alisema, "Sijui kilichojadiliwa. Sifahamu Kamati ya Uongozi ya Wabunge wamesema nini. Sikuwapo Dodoma, na wala sijakutana na mwenyekiti wangu (Waziri Mkuu) wala Rostam."

Hata hivyo, imefahamika kuwa wajumbe wa Kamati Teule, walikuwa wamejiandaa vilivyo kulithibitishia Taifa kuwa Rostam ndiye mwenye Richmond na Dowans.

Uchunguzi wa MwanaHALISI umeonye- shakuwa wajumbe walikuwa wamekamilisha kile kilichoitwa "misumari ya mwisho wa kumpigilia Rostam."

Wiki iliyopita Rostam alimweleza Spika wa Bunge, nia yake ya kutoa maelezo binafsi kuhusu madai ya Kamati Teule kuwa alihusika na njama za kifisadi za kuibeba Richmond.

Taarifa za Bunge zimesema hakukubaliwa kwa mujibu wa Kanuni za 53( na 54(4) za Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la 2007 zinazingatia kuwa "Mbunge yeyote hataruhusiwa kufufua jambo lolote ambalo Bunge lilikwisha kuliamua ama katika Mkutano huo au ule uliotangulia…. "

Imefahamika kuwa Rostam, katika hoja iliyokataliwa na Spika, aliwaita wabunge kuwa ni wasanii na wababaishaji kwa sababu tu walimshuku kwenye taarifa yao kuhusika na mkataba wa kifisadi wa Richmond/Dowans.

Uchunguzi wa gazeti hili umethibitisha kuwa Rostam aligawa fedha nyingi kwa baadhi ya wabunge, hasa wa Viti Maalum (majina tunayo), ili wampigie makofi ya nguvu wakati wa kuwasilisha maelezo yake.

Kuna madai pia kuwa "aligawa fedha nzuri" kwa baadhi ya waandishi wa habari (majina tunayo), ili kuipunguza makali Ripoti ya Kamati reule.

Pamoja na jitihada hila, bado zaidi ya asilimia 95 ya wabunge wanaiunga mkono Kamati Teule na wangetaka wahusika wote katika kashfa ya Richmond wachukuliwe hatua kali.

"Hawa watu hawajui kusoma mood ya wabunge. Wengi tuna hasira naye; tungemchanachana baada ya kuwasilisha utumbo wake. Sauti za Viti Maalum zingemezwa na sauti za wabunge wazalendo," amesema mbunge kijana na machachari.

Alipoulizwa Dk. Mwakyembe kama kweli Kamati yake ilikuwa na ushahidi wa ziada unaoonesha Rostam ndiye Richmond/Dowans, alisema kwa ufupi, "Tumwombee tu mwenzetu aruhusiwe kutoa dukuduku lake. Tutakayoyasema sisi yatajulikana palepale ulingoni."
 
Napenda kutofautiana na baadhi ya maneno ktk taarifa ya kubenea.si kweli ata kidogo kuwa kamati ya uongozi imemtaka rostam ajiuzuru bali PM ametumwa akamshawishi asijiuzuru,,,ok kwa nini anataka ajiuzuru?anajiuzuru ili aweze kutoa maelezo yake kama raia bila kufungwa na ethics za kuwa mbunge.Kwa upana maelezo yake yana annexture zenye mambo makubwa matatu...moja ni kuwa priamble ya kwanza iliopelekwa kwa spika haikuwa imemtaja spika wala rostam kuwa wanausika,hapo cha msingi ni kuwa walikaa tena kwa maelekezo ya spika nje ya muda waliopewa kwa ajili ya kuandika tena.pili kuna mawasiliano ya spika na mwaki juu ya kufanya kila wanaloweza kusudi kumwingiza pm na RA.tatu walificha makusudi wakurugenzi wa richmond na uhalali wake ili watu wafanye guesing kuwa na kina Rostam,hapo ndipo maelezo kama huu ni mradi wa bwana mkubwa na rafikie RA yakawekwa kwa madai kuwa shahidi aliongea nje ya kiapo...sasa kama wangeweka ushahidi wa mmiliki wa richmond basi usanii wake wa kuwa ni mradi wa bwana mkubwa na rafiki yake husingekuwa na maana yeyote.

Wewe wewe wewe wewe!!,

ebu acha njaa yako hiyo kakutuma huyu Muirani kumsemea hapa?Kama anaogopa kubanwa na "ethics" za ubunge kwa nini "asiichomoe" hoja yake hii na kuileta katika mahakama ya wananchi kama alivyofanya Dr. Slaa na wenzake pale Jangwani August 2007?Pili si ana magazeti yake (New Habari Corruption na Majira)?Kwa nini asisemee huko?

Aje Jangwani kwa wananchi aongee tumsikie.Vinginevyo mwambie huyo bosi wako kiama chake kimemfika tayari.
 
Back
Top Bottom