Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

KakindoMaster

JF-Expert Member
Dec 5, 2006
1,357
1,225
Kuna maswali bado mengi kuliko majibu. Spika anataka RA ajiuzuru, wakati huo huo hataki awasilishe hoja yake ambayo inaonekana ingesaidia kupata ukweli wa mambo.

Kuna kitendawili bado hakijateguka, kama kuna uwezekano wa kupata ripoti yenyewe inaweza kujibu maswali mengi.

Kama alivyosema Mtanzania watanzania wana uelewa wa kujua kama huu ni ukweli au ni uongo kama vile tulivyoona mantiki ya ripoti ya Richmond
 
taffu69

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,087
1,195
Habari ndio hiyo!

Uchunguzi wa gazeti hili umethibitisha kuwa Rostam aligawa fedha nyingi kwa baadhi ya wabunge, hasa wa Viti Maalum (majina tunayo), ili wampigie makofi ya nguvu wakati wa kuwasilisha maelezo yake.

Kuna madai pia kuwa "aligawa fedha nzuri" kwa baadhi ya waandishi wa habari (majina tunayo), ili kuipunguza makali Ripoti ya Kamati reule.

"[/SIZE]

HII NI KASHFA MBAYA NA NI AIBU KWA BUNGE KWANI HAWA WAMEJIHUSISHA NA RUSHWA NA INATAKIWA WOTE WALIOHUSIKA KATIKA KUTOA (RA) NA HAO WALIOPOKEA (WABUNGE NA WAANDISHI WA WAHABARI) WAWE DEALT ACCORDINGLY KULINGANA NA SHERIA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA.
 
Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,505
1,225
Sababu za Rostam kujiuzuru

1.Anajiuzuru ili aweze kutoa maelezo yake kama raia bila kufungwa na ethics za kuwa mbunge.
2.Kwa upana maelezo yake yana annexture zenye mambo makubwa matatu
  • a) kwa kuwa priamble ya kwanza iliopelekwa kwa spika haikuwa imemtaja spika wala rostam kuwa wanausika,hapo cha msingi ni kuwa walikaa tena kwa maelekezo ya spika nje ya muda waliopewa kwa ajili ya kuandika tena.
  • b)kuna mawasiliano ya spika na mwaki juu ya kufanya kila wanaloweza kusudi kumwingiza pm na RA.
  • c)tatu walificha makusudi wakurugenzi wa richmond na uhalali wake ili watu wafanye guesing kuwa na kina Rostam,hapo ndipo maelezo kama huu ni mradi wa bwana mkubwa na rafikie RA yakawekwa kwa madai kuwa shahidi aliongea nje ya kiapo
Nenda ukamwambie RA,Gembe amesema aache kuwa Mpumbavu na tunataka ajiuzuru kwanza na aje atuambie Uraia wa Tanzania nani alimpa
 
Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,505
1,225
Napenda kutofautiana na baadhi ya maneno ktk taarifa ya kubenea.si kweli ata kidogo kuwa kamati ya uongozi imemtaka rostam ajiuzuru bali PM ametumwa akamshawishi asijiuzuru.

Kama si kweli basi tueleze ukweli ni upi kutoka kwako ambaye unajua zaidi.tuambie usiogope
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,669
0
Aje Jangwani kwa wananchi aongee tumsikie.Vinginevyo mwambie huyo bosi wako kiama chake kimemfika tayari.

Rostam, is very good in blackmailing other leaders, huyu hana uchungu na mwananchi yoyote, sasa hivi toka girlfriend mama meghji achomolewe, anahangaika na hana cha zaidi ila kutumia what he knows best yaaani zile zile njia alizozitumia kuwapa mtandao madaraka,

Can somebody tell that man kuwa sasa sio kampeni tena za urais ziliisha, sasa ni saa ya kutawala na kwamba wa-Tanzania hatuwezi kufikia mahali pa kusumbuliwa na huyu mhindi, wakati jela zetu hazijajaa, nasikia ilifikia mahali ilikuwa kumuona mkulu mpaka upitie kwa huyu mhindi? That is low, huyu hana lolote hivi kwenye siasa zetu kazi yake hasa ni nini?

Mbona wabunge wengine hatuwasikii mpaka wakati wa bajeti, yeye tu kila kona mafisadi yumo, ripoti ya kamati ya Mwakyembe yumo, Richimonduli yumo, hela misaada Japan yumo, I mean hivi this is what Mwalimu fought uhuru wetu wa-Tanzania for? Kuja kusumbuliwa na hawa wahindi? Halafu mbona hajafungiwa kwa kutofuata sheria za bunge?

Mkapa umefika wakati lazima na wewe uambiwe ukweli, chukua wahindi wako hawa muondoke, enough! wewe Mkapa ndiye uliyetuletea hawa gabacholi kwenye serikali, wote na mulegeee!
 
Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,812
1,250
naibu Spika Anne Makinda, ameliambia Bunge kwamba Rostam Aziz aliwasilisha kwa spika maelezo ambayo yalifanana na yale aliyowasilisha kwa maandishi wakati akichangia hoja ya Kamati teule ya Dk. Harison Mwakyembe, kwa hiyo ikaonekana atakua anarudia yale yale ambayo alitakiwa ayafafanue, wakati Kanuni zinamzuia kufanya hivyo. Kukawa na malumbano na Zitto na Hamad Rashid walisimama na kutoa maelezo kupinga CCM kumeza hoja, lakini Naibu Spika alitoa maelezo na hatimaye kummaliza kabisa Rostam. Maelezo zaidi baadaye kutoka kwa walio Dodoma
 
Kitila Mkumbo

Verified Member
Feb 25, 2006
3,351
2,000
Ngoja kwanza,

i) Hii habari haitusaidii kwa yale tuliyokuwa tunasubiri. Msiniambie kwamba sisi pia hapa JF ni wepesi wa kusahau. Tulichokuwa tunasubiri ni taarifa ambayo Rostam alikuwa aitoe kuchapishwa kwenye gazeti la leo. Lakini sicho hicho ninachokisoma hapa, au siyo?

ii) Hao wabunge wa CCM wataanzia wapi kumsuta Rostam wakati inajulikana wazi kuwa zaidi ya 70% yao walipewa hela za kampeni na Rostam? Ndio tunasema kila siku ukikubali kununuliwa ujue umeliwa mpaka mwisho. Sasa hao ndugu zetu wa CCM bungeni hawana pa kujificha, hili litawaandama hadi mwisho. Hii pia ni kwa mhe Rais, yeye kukubali mahela ya Rostam kwenye kampeni zake ambayo hakujua hata yametoka wapi alikuwa anajikaanga. Haya mahela yatamfuata kwenye urais wake mpaka mwisho, atabaki kuwa na good intentions, lakini hamna atakachofanya hadi mwisho.

iii) Rais wetu inabidi aelezwe kwamba huwezi kusema unapambana na rushwa na ufisadi na wakati huohuo unawaweka mafisadi kwenye serikali yako. Kitendo cha Mhe Rais wetu kumteua Chenge na kumteua tena, tena kwenye wizara nyeti ni cha kulaaniwa,na kinafanya intentions za JK za kupambana na rushwa kuwa ni kejeli za mwaka. Na kwa hapa mkuu wangu FMES huna cha kumlaumu Mkapa maana hakuna mtu aliyemlamisha JK ambebe Rostam wala amteue Chenge kuwa waziri na tena mjumbe wa kamati ya maadili ya CCM (this is the biggest joke of JK's administration(!

iv) Hebu niwekeni sawa, hivi kuna watu humu wanashangilia Rostam kutopewa nafasi ya kusema bungeni au kuna kitu sijakielewa? Hivi, si ni spika huyuhuyu aliyesema kwamba Rostam lazima aje ajieleze bungeni, sasa nini kilitokea? So long as vyombo vyetu muhimu kama bunge vinaendelea kufanya kazi kishabikia kwa lengo la kumalizana na kujengana kisiasa, litaendelea kuwa irrelevant

.
 
Kitila Mkumbo

Verified Member
Feb 25, 2006
3,351
2,000
Haitusadii sana hii. Wenyewe ndiyo waliosema Rostam lazima ajieleze bungeni, wangemwacha atoe maelezo yake wananchi wapime pumba na mchele. Hili la kumkatalia linazidi kuchochea hisia tu kwamba kuna kitu kibaya dhidi ya wakubwa amacho Rostam alikuwa anakwenda kukisema.
 
DIKTETA

Member
Mar 28, 2008
55
0
Wewe wewe wewe wewe!!,

ebu acha njaa yako hiyo kakutuma huyu Muirani kumsemea hapa?Kama anaogopa kubanwa na "ethics" za ubunge kwa nini "asiichomoe" hoja yake hii na kuileta katika mahakama ya wananchi kama alivyofanya Dr. Slaa na wenzake pale Jangwani August 2007?Pili si ana magazeti yake (New Habari Corruption na Majira)?Kwa nini asisemee huko?

Aje Jangwani kwa wananchi aongee tumsikie.Vinginevyo mwambie huyo bosi wako kiama chake kimemfika tayari.
Nadhani tuwe objective ili tupate habari kamili hapa,sasa kama fisadi anatupa upande mwingine wa shilingi then tunaonyesha wazi kumpinga na kumwambia anamsemea muiran pamoja na kuita magazeti yake kuwa ni new habari corruption haiondoi haki yake ya kusema ukweli.....Mimi nachojua ni kuwa kwa taratibu za ccm ni ngumu sana kwa mtu kama rostam kuzungumza nje ya bunge kama Slaa kwa kuwa ule ni uamuzi wa kamati ya uongozi ambayo ni ya chama,naye ni mjumbe wa kamati kuu ya ccm.Hivyo hatua aliochukua ni sahihi...hapo msaliti ni Sita kwa nini hakupeleka kwa wabunge hoja na akaipeleka ccm.aliogopa kuumbuliwa.???????????
 
Sekenke

Senior Member
Mar 3, 2008
132
170
Rostam Taabani
Na Mwandishi Wetu
MwanaHALISI, Toleo Na. 093, Jumatano Aprili 16-22, 2008

Mbunge wa Igunga (CCM) Rostam Aziz, ametishia kujiuzulu ubunge kutokana na hatua ya Kamati ya Uongozi ya Bunge kumzuia kuwasilisha hoja yake bungeni, MwanaHALISI limedokezwa.

Taarifa za uhakika toka ndani ya Kamati hiyo, zinasema Rostam alitoa tishio hilo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Uongozi ambao ni pamoja na Spika wa Bunge, Samwel Sitta na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Inaelezwa kwamba baada ya Rostam kutoa kauli hiyo, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge kwa pamoja walimtaka afanye hivyo haraka.

“ Kabla Rostam hajamaliza kulalama, Spika hakumkawiza. Alisema, “Andika barua ya kujiuzulu sasa hivi. Hatuwezi kupeleka matusi haya ndani ya Bunge…,” alinukuliwa na mjumbemmoja wa Kamati.

Mjumbe huyo alisema kauli ya Rostam ili waudhi wajumbe wa Kamati ya Uongozi kwani haraka Waziri Mkuu alitoa tamko la kuungana na Sitta kumtaka Rostam ajiuzulu ubunge.

Wiki iliyopita, Spika alimzuia Rostam kuwasilisha maelezo yake bungeni, baada ya kubaini kuwa aliyoyaeleza katika kile alichoi ta "hoja yake" hayakustahili kuwasilishwa bungeni.

Katika Mkutano wa Bunge uliopita (wa kumi), Bunge lilimtaka Rostam kuwasilisha maelezo yake katika mkutano unaoendelea Saga mjini Dodoma, baada ya kusikika akituhumu kwamba Kamati Teule ya Bunge iliy- ochunguza mkataba wa Richmond, "iliendelea na kazi lake hata baada ya kuwasilisha ripoti yake kwa Spika."

Rostam, kwa mujibu wa taarita, alitaka Spika, kwa kutumia hoja za Rostam, amwamuru Dk. Mwakyembe kumsafisha ndani ya Bunge. Hata hiwo. shinikizo lake hila liIikataliwa

Taarifa za ndani ya Bunge, zinasema kukataliwa kwa maelezo binafsi ya Rostam kumetokana na kuonekana yamejaa tuhuma, shutuma na dharau kwa Bunge na Kamati Teule ya Mwakyembe.

Spika wa Bunge amekiri kupokea hoja binafsi ya Rostam, lakini alisema ameshind- wa kuruhusu iwasilishwe bungeni kutokana na kwenda kinyume na Kanuni za Bunge.

Mjumbe mmoja wa Kamati ya Uongozi amemkariri Spika akisema Bunge halikujadili hoja ya Rostam, siyo kwa kumwogopa, kama baadhi ya magazeti yanavyotaka kuonyesha, bali kwa sababu hoja yenyewe inakiuka Kanuni za Bunge.

Alipopigiwa simu na gazeti hili kupata undani wa taarifa hiyo, Sitta alielekeza mwandishi awasiliane na Rostam mwenyewe ambaye, Spika alisema tayari amejulishwa uamuzi huo.

MwanaHALISI halikuweza kuwasiliana na Rostam kupata upande wake.

Katibu wa wabunge wa CCM, Ali Ameir Mohammed, alipoulizwa juu ya suala hila alisema, "Sijui kilichojadiliwa. Sifahamu Kamati ya Uongozi ya Wabunge wamesema nini. Sikuwapo Dodoma, na wala sijakutana na mwenyekiti wangu (Waziri Mkuu) wala Rostam."

Hata hivyo, imefahamika kuwa wajumbe wa Kamati Teule, walikuwa wamejiandaa vilivyo kulithibitishia Taifa kuwa Rostam ndiye mwenye Richmond na Dowans.

Uchunguzi wa MwanaHALISI umeonye- shakuwa wajumbe walikuwa wamekamilisha kile kilichoitwa "misumari ya mwisho wa kumpigilia Rostam."

Wiki iliyopita Rostam alimweleza Spika wa Bunge, nia yake ya kutoa maelezo binafsi kuhusu madai ya Kamati Teule kuwa alihusika na njama za kifisadi za kuibeba Richmond.

Taarifa za Bunge zimesema hakukubaliwa kwa mujibu wa Kanuni za 53(8) na 54(4) za Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la 2007 zinazingatia kuwa "Mbunge yeyote hataruhusiwa kufufua jambo lolote ambalo Bunge lilikwisha kuliamua ama katika Mkutano huo au ule uliotangulia…. "

Imefahamika kuwa Rostam, katika hoja iliyokataliwa na Spika, aliwaita wabunge kuwa ni wasanii na wababaishaji kwa sababu tu walimshuku kwenye taarifa yao kuhusika na mkataba wa kifisadi wa Richmond/Dowans.

Uchunguzi wa gazeti hili umethibitisha kuwa Rostam aligawa fedha nyingi kwa baadhi ya wabunge, hasa wa Viti Maalum (majina tunayo), ili wampigie makofi ya nguvu wakati wa kuwasilisha maelezo yake.

Kuna madai pia kuwa "aligawa fedha nzuri" kwa baadhi ya waandishi wa habari (majina tunayo), ili kuipunguza makali Ripoti ya Kamati reule.

Pamoja na jitihada hila, bado zaidi ya asilimia 95 ya wabunge wanaiunga mkono Kamati Teule na wangetaka wahusika wote katika kashfa ya Richmond wachukuliwe hatua kali.

"Hawa watu hawajui kusoma mood ya wabunge. Wengi tuna hasira naye; tungemchanachana baada ya kuwasilisha utumbo wake. Sauti za Viti Maalum zingemezwa na sauti za wabunge wazalendo," amesema mbunge kijana na machachari.

Alipoulizwa Dk. Mwakyembe kama kweli Kamati yake ilikuwa na ushahidi wa ziada unaoonesha Rostam ndiye Richmond/Oowans, alisema kwa ufupi, "Tumwombee tu mwenzetu aruhusiwe kutoa dukuduku lake. Tutakayoyasema sisi yatajulikana palepale ulingoni."
 
DIKTETA

Member
Mar 28, 2008
55
0
Ngoja kwanza,

i) Hii habari haitusaidii kwa yale tuliyokuwa tunasubiri. Msiniambie kwamba sisi pia hapa JF ni wepesi wa kusahau. Tulichokuwa tunasubiri ni taarifa ambayo Rostam alikuwa aitoe kuchapishwa kwenye gazeti la leo. Lakini sicho hicho ninachokisoma hapa, au siyo?

ii) Hao wabunge wa CCM wataanzia wapi kumsuta Rostam wakati inajulikana wazi kuwa zaidi ya 70% yao walipewa hela za kampeni na Rostam? Ndio tunasema kila siku ukikubali kununuliwa ujue umeliwa mpaka mwisho. Sasa hao ndugu zetu wa CCM bungeni hawana pa kujificha, hili litawaandama hadi mwisho. Hii pia ni kwa mhe Rais, yeye kukubali mahela ya Rostam kwenye kampeni zake ambayo hakujua hata yametoka wapi alikuwa anajikaanga. Haya mahela yatamfuata kwenye urais wake mpaka mwisho, atabaki kuwa na good intentions, lakini hamna atakachofanya hadi mwisho.

iii) Rais wetu inabidi aelezwe kwamba huwezi kusema unapambana na rushwa na ufisadi na wakati huohuo unawaweka mafisadi kwenye serikali yako. Kitendo cha Mhe Rais wetu kumteua Chenge na kumteua tena, tena kwenye wizara nyeti ni cha kulaaniwa,na kinafanya intentions za JK za kupambana na rushwa kuwa ni kejeli za mwaka. Na kwa hapa mkuu wangu FMES huna cha kumlaumu Mkapa maana hakuna mtu aliyemlamisha JK ambebe Rostam wala amteue Chenge kuwa waziri na tena mjumbe wa kamati ya maadili ya CCM (this is the biggest joke of JK's administration(!

iv) Hebu niwekeni sawa, hivi kuna watu humu wanashangilia Rostam kutopewa nafasi ya kusema bungeni au kuna kitu sijakielewa? Hivi, si ni spika huyuhuyu aliyesema kwamba Rostam lazima aje ajieleze bungeni, sasa nini kilitokea? So long as vyombo vyetu muhimu kama bunge vinaendelea kufanya kazi kishabikia kwa lengo la kumalizana na kujengana kisiasa, litaendelea kuwa irrelevant

.
KITILA UNA AKILI SANA NA NDIO MAANA KILA SIKU NAWAZA KWA NINI HAUKO NYUMBANI,NATUMAINI SIKU MOJA UTARUDI NYUMBANI KWAKO,NYUMBA YA WENZAKO WENYE AKILI,NYUMBA YA WAZAZI WAKO...CCM.HAPA HATUKUWA TUNATAKA MAWAZO YA KUBENEA WALA MWANANZILA.TULIKUWA TUNATAKA MAELEZO YA RA KWA SPIKA.TUSOME WENYEWE NA KUYACHAMBUA.ZAIDI YA HAPO NI KICHEKESHO TU.
 
DIKTETA

Member
Mar 28, 2008
55
0
Rostam, is very good in blackmailing other leaders, huyu hana uchungu na mwananchi yoyote, sasa hivi toka girlfriend mama meghji achomolewe, anahangaika na hana cha zaidi ila kutumia what he knows best yaaani zile zile njia alizozitumia kuwapa mtandao madaraka,

Can somebody tell that man kuwa sasa sio kampeni tena za urais ziliisha, sasa ni saa ya kutawala na kwamba wa-Tanzania hatuwezi kufikia mahali pa kusumbuliwa na huyu mhindi, wakati jela zetu hazijajaa, nasikia ilifikia mahali ilikuwa kumuona mkulu mpaka upitie kwa huyu mhindi? That is low, huyu hana lolote hivi kwenye siasa zetu kazi yake hasa ni nini?

Mbona wabunge wengine hatuwasikii mpaka wakati wa bajeti, yeye tu kila kona mafisadi yumo, ripoti ya kamati ya Mwakyembe yumo, Richimonduli yumo, hela misaada Japan yumo, I mean hivi this is what Mwalimu fought uhuru wetu wa-Tanzania for? Kuja kusumbuliwa na hawa wahindi? Halafu mbona hajafungiwa kwa kutofuata sheria za bunge?

Mkapa umefika wakati lazima na wewe uambiwe ukweli, chukua wahindi wako hawa muondoke, enough! wewe Mkapa ndiye uliyetuletea hawa gabacholi kwenye serikali, wote na mulegeee!
jenga hoja na acha siasa za kinaguzi hapa.huwezi just kusema wahindi aondoke.wewe huko unakokaa ni kwenu???onyesha umesoma kidogo walau,Mukheshi wa Haki Elimu ni muhindi,kwa hio wahindi wote ni wabaya ata kama Mukheshi kafanya mambo mazuri.Naja wewe ni kibaraka wa Malechela lazima umchukie ninafsi RA ata kama afanyaje na mshauri wako niAnne Kilango.
 
Fisadi Mtoto

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
639
195
[/LIST]Nenda ukamwambie RA,Gembe amesema aache kuwa Mpumbavu na tunataka ajiuzuru kwanza na aje atuambie Uraia wa Tanzania nani alimpa

SIWEZI MWAMBIA KWA KUWA KWANZA ATASHANGAA SISIMIZI KAMA WEWE KUJIPA JUKUMU LA UHAMIAJI,PILI ANAAMINI MIMI NINA AKILI WALAU AVARAGE SASA NIKIMPELEKEA UJUMBE WAKO ANAWEZA ZANIA HUWA NAKAA CLUB YA VICHAA....RA HAKUPEWA URAIA BALI NA HAKI YAKE YA KUZALIWA,KAZALIWA NZEGA NA MPAKA ZAHANATI ALIOZALIWA IPO NA WANA RECORDS ZOTE....KAMALIZA SHULE YA MSINGI IGUNGA NA NENDA KWA AFISA ELIMU WA MKOA ATAKWAMBIA ALIKUWA WA KWANZA MKOA DARASA LA SABA....ANAZUNGUMZA KINYAMWEZI NA KISUKUMA FASAHA.
 
DMussa

JF-Expert Member
Sep 24, 2007
1,314
1,500
Nadhani tuwe objective ili tupate habari kamili hapa,sasa kama fisadi anatupa upande mwingine wa shilingi then tunaonyesha wazi kumpinga na kumwambia anamsemea muiran pamoja na kuita magazeti yake kuwa ni new habari corruption haiondoi haki yake ya kusema ukweli.....Mimi nachojua ni kuwa kwa taratibu za ccm ni ngumu sana kwa mtu kama rostam kuzungumza nje ya bunge kama Slaa kwa kuwa ule ni uamuzi wa kamati ya uongozi ambayo ni ya chama,naye ni mjumbe wa kamati kuu ya ccm.Hivyo hatua aliochukua ni sahihi...hapo msaliti ni Sita kwa nini hakupeleka kwa wabunge hoja na akaipeleka ccm.aliogopa kuumbuliwa.???????????

Which side of the shilling....!!
 
Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,952
2,000
[QUOTE=ishengoma;175699]baada ya hapo kitakachofuata ni kuuana ndani ya sisiem na kutuambia ni mshtuko.[/QUOTE]

[FONT="Garamond"]ISHENGOMA hapo umenena, maana mtu aweza kuondolewa hivi hivi mkaelezwa ni SHINIKIZO, AJALI MBAYA, etc. Ushauri wa BURE kwa RA ni kuwa WANANCHI HAWANA IMANI NAYE TENA, ATAFUTE UTARATIBU WA KUONGEA NA WANANCHI AWAELEZE UKWELI WOTE NA UKWELI TUPU KUHUSU RICHMOND, jinsi na katika mazingira gani DOWANS alimrithi RICHMOND, ikawaje kampuni yake ya CASPIAN ikawa mshirika wa DOWANS tangu alipoingia na hapo baadaye;na kwa nini yeye alikuwa kiranja wa DOWANS kufuatilia malipo/michuzi kule HAZINA (kwa mama Meghji) kila ambapo hundi ikichelewa kutoka na na kwa nini hakuenda kujieleza kwenye tume ya MWAKYEMBE??? MAMBO!!!Nawasilisha. [/FONT]
 
TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
9,838
2,000
baada ya hapo kitakachofuata ni kuuana ndani ya sisiem na kutuambia ni mshtuko.

Tatizo letu siyo kuuana ili kushibisha matumbo yao wenyewe bali tunataka maendeleo ya kiuchumi nchini kwa kutumia rasilimali nyingi tu tulizojaliwa na Mwenyenzi na zinazoliwa na Washenzi wachache.

Tena nadhani wakiuana tutakuwa tunapungukiwa na mzigo wa mafisadi waliojaa kila penye maslahi nchini.

Anyway, hilo siliombei kwa usalama wa amani isie vurugwa.
 
a.9784

Senior Member
Feb 19, 2008
146
0
wewe anna makinda kwanini umetunyima huo utamu?ungemuacha ajikanyagekanyage kwanza,sasa utasababisha ajidai.So what next about Rostam
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom