Si tuleteeni basi hiyo habari? Naona haiko kwenye Internet bado.
ndiyo.. iko kwa MwanaHalisi halafu kwenye Raia Mwema kuna kachumbari yake!
wakati Rostam akitoa maneno hayo Mhe. Spika alimwambia jiuzuru sasa hivi na Mhe. Pinda ambaye kwa sasa ndiye amri jeshi mkuu akamuunga mkono Mhe. Sitta.
.[/B]
Haya ni maneno mazuri sana.
Hivi huyu RA kwani yeye anafikiri akijiuzuru kuna matanzania atakayekuwa na hasara?.
Anyway JK atahangaika sana maana ni mizigo yake, hila wananchi tungepiga filimbi, nderemo na vifijo.
Nafikiri wabunge walazimishe aende akajieleze hata na hayo makablasha yake, tunaweza kufanya kasikukuu kakubwa .
Tunaombeni mtusaidie kutuwekea hapa hiyo taarifa ili tuichambue vizuri.
"Uchunguzi wa MWANAHALISI umeonyesha kuwa wajumbe walikuwa wamekamilisha kile kinachoitwa misumari ya mwisho ya kumpigilia Rostam
Imefahamika kuwa Rostam,katika hoja yake hiyo iliyokataliwa na spika aliwaita wabunge wasanii na wababaishaji kwasababu walimshuku kwenye taarifa yao kuhusu kuhusika na mkataba wa Richmond/Dowans"
Source:Mwanahalsi
JF- We always report what they dont report
na imefahamika wazi kwamba wajumbe wa kamati teule walikuwa wamejiandaa vilivyo kulithibitishia Taifa kuwa RA ndiye mwenye Richmond na Dowans"
Fuatilia tovuti ya MwanaHalisi: http://www.halihalisi.co.tz/ yumkini watachapisha toleo la wiki hii punde. Toleo za wiki hii ni kiboko, Mambo ya Chenge Hadharaniii, yaani, waweza kulia.
Kunradhi hivi huyu RA anafikiri yeye ni nani katika nchi hii?? Yeye kama hakuhusika na Richmond/Dowans kwa nini basi hakujipeleka kutoa ushahidi wa kukana kuhusika kwake na badala yake alibakia analalamikia tume kufanya kazi nje ya muda uliopangwa!!!
Surely i hate his guts!!!! ...Fisadi RA go to hell!
Napenda kutofautiana na baadhi ya maneno ktk taarifa ya kubenea.si kweli ata kidogo kuwa kamati ya uongozi imemtaka rostam ajiuzuru bali PM ametumwa akamshawishi asijiuzuru,,,ok kwa nini anataka ajiuzuru?anajiuzuru ili aweze kutoa maelezo yake kama raia bila kufungwa na ethics za kuwa mbunge.Kwa upana maelezo yake yana annexture zenye mambo makubwa matatu...moja ni kuwa priamble ya kwanza iliopelekwa kwa spika haikuwa imemtaja spika wala rostam kuwa wanausika,hapo cha msingi ni kuwa walikaa tena kwa maelekezo ya spika nje ya muda waliopewa kwa ajili ya kuandika tena.pili kuna mawasiliano ya spika na mwaki juu ya kufanya kila wanaloweza kusudi kumwingiza pm na RA.tatu walificha makusudi wakurugenzi wa richmond na uhalali wake ili watu wafanye guesing kuwa na kina Rostam,hapo ndipo maelezo kama huu ni mradi wa bwana mkubwa na rafikie RA yakawekwa kwa madai kuwa shahidi aliongea nje ya kiapo...sasa kama wangeweka ushahidi wa mmiliki wa richmond basi usanii wake wa kuwa ni mradi wa bwana mkubwa na rafiki yake husingekuwa na maana yeyote.
Mbunge wa Igunga (CCM) Rostam Aziz, ametishia kujiuzulu ubunge kutokana na hatua ya Kamati ya Uongozi ya Bunge kumzuia kuwasilisha hoja yake bungeni, MwanaHALISI limedokezwa.
Taarifa za uhakika toka ndabi ya Kamati hiyo, zinasema Rostam alitoa tishio hilo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Uongozi ambao ni pamoja na Spika wa Bunge, Samwel Sitta na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Inaelezwa kwamba baada ya Rostam kutoa kauli hiyo, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge kwa pamoja walimtaka afanye hivyo haraka.
" Kabla Rostam hajamaliza kulalama, Spika hakumkawiza. Alisema, "Andika barua ya kujiuzulu sasa hivi. Hatuwezi kupeleka matusi haya ndani ya Bunge…," alinukuliwa na mjumbemmoja wa Kamati.
Mjumbe huyo alisema kauli ya Rostam ili waudhi wajumbe wa Kamati ya Uongozi kwani haraka Waziri Mkuu alitoa tamko la kuungana na Sitta kumtaka Rostam ajiuzulu ubunge.
Wiki iliyopita, Spika alimzuia Rostam kuwasilisha maelezo yake bungeni, baada ya kubaini kuwa aliyoyaeleza katika kile alichoi ta "hoja yake" hayakustahili kuwasilishwa bungeni.
Katika Mkutano wa Bunge uliopita (wa kumi), Bunge lilimtaka Rostam kuwasilisha maelezo yake katika mkutano unaoendelea Saga mjini Dodoma, baada ya kusikika akituhumu kwamba Kamati Teule ya Bunge iliy- ochunguza mkataba wa Richmond, "iliendelea na kazi lake hata baada ya kuwasilisha ripoti yake kwa Spika."
Rostam, kwa mujibu wa taarita, alitaka Spika, kwa kutumia hoja za Rostam, amwamuru Dk. Mwakyembe kumsafisha ndani ya Bunge. Hata hiwo. shinikizo lake hila liIikataliwa
Taarifa za ndani ya Bunge, zinasema kukataliwa kwa maelezo binafsi ya Rostam kumetokana na kuonekana yamejaa tuhuma, shutuma na dharau kwa Bunge na Kamati Teule ya Mwakyembe.
Spika wa Bunge amekiri kupokea hoja binafsi ya Rostam, lakini alisema ameshind- wa kuruhusu iwasilishwe bungeni kutokana na kwenda kinyume na Kanuni za Bunge.
Mjumbe mmoja wa Kamati ya Uongozi amemkariri Spika akisema Bunge halikujadili hoja ya Rostam, siyo kwa kumwogopa, kama baadhi ya magazeti yanavyotaka kuonyesha, bali kwa sababu hoja yenyewe inakiuka Kanuni za Bunge.
Alipopigiwa simu na gazeti hili kupata undani wa taarifa hiyo, Sitta alielekeza mwandishi awasiliane na Rostam mwenyewe ambaye, Spika alisema tayari amejulishwa uamuzi huo.
MwanaHALISI halikuweza kuwasiliana na Rostam kupata upande wake.
Katibu wa wabunge wa CCM, Ali Ameir Mohammed, alipoulizwa juu ya suala hila alisema, "Sijui kilichojadiliwa. Sifahamu Kamati ya Uongozi ya Wabunge wamesema nini. Sikuwapo Dodoma, na wala sijakutana na mwenyekiti wangu (Waziri Mkuu) wala Rostam."
Hata hivyo, imefahamika kuwa wajumbe wa Kamati Teule, walikuwa wamejiandaa vilivyo kulithibitishia Taifa kuwa Rostam ndiye mwenye Richmond na Dowans.
Uchunguzi wa MwanaHALISI umeonye- shakuwa wajumbe walikuwa wamekamilisha kile kilichoitwa "misumari ya mwisho wa kumpigilia Rostam."
Wiki iliyopita Rostam alimweleza Spika wa Bunge, nia yake ya kutoa maelezo binafsi kuhusu madai ya Kamati Teule kuwa alihusika na njama za kifisadi za kuibeba Richmond.
Taarifa za Bunge zimesema hakukubaliwa kwa mujibu wa Kanuni za 53( na 54(4) za Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la 2007 zinazingatia kuwa "Mbunge yeyote hataruhusiwa kufufua jambo lolote ambalo Bunge lilikwisha kuliamua ama katika Mkutano huo au ule uliotangulia…. "
Imefahamika kuwa Rostam, katika hoja iliyokataliwa na Spika, aliwaita wabunge kuwa ni wasanii na wababaishaji kwa sababu tu walimshuku kwenye taarifa yao kuhusika na mkataba wa kifisadi wa Richmond/Dowans.
Uchunguzi wa gazeti hili umethibitisha kuwa Rostam aligawa fedha nyingi kwa baadhi ya wabunge, hasa wa Viti Maalum (majina tunayo), ili wampigie makofi ya nguvu wakati wa kuwasilisha maelezo yake.
Kuna madai pia kuwa "aligawa fedha nzuri" kwa baadhi ya waandishi wa habari (majina tunayo), ili kuipunguza makali Ripoti ya Kamati reule.
Pamoja na jitihada hila, bado zaidi ya asilimia 95 ya wabunge wanaiunga mkono Kamati Teule na wangetaka wahusika wote katika kashfa ya Richmond wachukuliwe hatua kali.
"Hawa watu hawajui kusoma mood ya wabunge. Wengi tuna hasira naye; tungemchanachana baada ya kuwasilisha utumbo wake. Sauti za Viti Maalum zingemezwa na sauti za wabunge wazalendo," amesema mbunge kijana na machachari.
Alipoulizwa Dk. Mwakyembe kama kweli Kamati yake ilikuwa na ushahidi wa ziada unaoonesha Rostam ndiye Richmond/Dowans, alisema kwa ufupi, "Tumwombee tu mwenzetu aruhusiwe kutoa dukuduku lake. Tutakayoyasema sisi yatajulikana palepale ulingoni."
Napenda kutofautiana na baadhi ya maneno ktk taarifa ya kubenea.si kweli ata kidogo kuwa kamati ya uongozi imemtaka rostam ajiuzuru bali PM ametumwa akamshawishi asijiuzuru,,,ok kwa nini anataka ajiuzuru?anajiuzuru ili aweze kutoa maelezo yake kama raia bila kufungwa na ethics za kuwa mbunge.Kwa upana maelezo yake yana annexture zenye mambo makubwa matatu...moja ni kuwa priamble ya kwanza iliopelekwa kwa spika haikuwa imemtaja spika wala rostam kuwa wanausika,hapo cha msingi ni kuwa walikaa tena kwa maelekezo ya spika nje ya muda waliopewa kwa ajili ya kuandika tena.pili kuna mawasiliano ya spika na mwaki juu ya kufanya kila wanaloweza kusudi kumwingiza pm na RA.tatu walificha makusudi wakurugenzi wa richmond na uhalali wake ili watu wafanye guesing kuwa na kina Rostam,hapo ndipo maelezo kama huu ni mradi wa bwana mkubwa na rafikie RA yakawekwa kwa madai kuwa shahidi aliongea nje ya kiapo...sasa kama wangeweka ushahidi wa mmiliki wa richmond basi usanii wake wa kuwa ni mradi wa bwana mkubwa na rafiki yake husingekuwa na maana yeyote.