Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Chadema bado hawana mapesa aliyo nayo Rostum Aziz, EL na Karamagi.
Are you sure? kwani bajeti ya kutuma txt msgs na internet ni kiasi gani?

nadhani its about time CHADEMA wakaanza kuwa active na mambo haya badala ya kukaa pembeni kulalamika
 
wiki chache zilizopita nilizungumzia suala moja muhimu hasa baada ya majibizano na ofisi ya Waziri Mkuu. NIkasema mnachokishuhudia ni mapambano ya kifikra (ideological battle). CCM sasa wamegundua hilo ingawa wamechelewa kidogo, na watakuja na nguvu zote. Msingi wa mapambano hayo ni kuhusu nani anamiliki na kutoa habari, na habari hiyo inamfikia nani. Kwa hili CCM have unmatched advantage. Hata hivyo, CCM wanapungukiwa kitu kimoja, nacho ni imani. WAtu wameanza kuhoji CCM, watu wameanza kuuliza, watu wameanza kukataa majibu ya CCM.

Hivyo katika mapambano haya ni lazima fikra na hoja zenye nguzu zaidi zishinde. Kabla ya kushinda kwenye sanduku la kura ni lazima tushinde kwenye sanduku la fikra za wananchi! Na hivi sasa tuna mwanzo mzuri
 
Chadema bado hawana mapesa aliyo nayo Rostum Aziz, EL na Karamagi.

Jamani ni kweli hawa watu wana mapesa mengi machafu, lakini sidhani kama UKOMBOZI wa kweli utapatikana kwa kutumia fedha.. Walipojitokeza wananchi kwa maelfu kumpokea Zitto, hawakulipwa hata senti tano, sana sana fedha zilitumika katika maandalizi. Jambo la msingi ni kufanya maamuzi. Humu ndani watu wanajitolea na huu ni mfano tosha. Kwa kuanzia wahakikishe wanafanya kazi ya kufuatilia nyendo zote zinazoelekea kutaka kuvuruga UKOMBOZI na kujibu mapigo kwa haraka. NASIKITIKA KUSEMA HILI SI LA CHADEMA. NI LA WATANZANIA WOTE hata wa CCM. UKOMBOZI NI WA WOTE. MWALIMU ALISHIRIKIANA SANA NA WATUMISHI WA SERIKALI YA WAKOLONI NA NDIPO ALIPOFANIKIWA. TUTUMIA RASILIMALI WATU TULIZO NAZO, INAPOFUKIA KWAMBA TUNAKWAMA NDIO TUANGALIE GHARAMA ZA KIFEDHA LAKINI SASA HIZO RASILIMALI WATU NA NYINGINE ZILIZOPO NDANI YA UWEZO WETU WATANZANIA WAPAMBANAJI HATUJAZITUMIA IPASAVYO< TUZITUMIE SASA
 
Jamani ni kweli hawa watu wana mapesa mengi machafu, lakini sidhani kama UKOMBOZI wa kweli utapatikana kwa kutumia fedha..

..fedha ni muhimu sana kwenye vita yeyote,hata ya maneno!

..issue ni wapi zinatoka? na je kama unakopeshwa ni kwa masharti gani?!

..wapiganaji wanahitaji nauli,malazi,chakula,n.k bila ya hivyo hawawezi kufanya kazi kwa ufanisi!infact hamna kazi itakayofanyika!

Walipojitokeza wananchi kwa maelfu kumpokea Zitto, hawakulipwa hata senti tano, sana sana fedha zilitumika katika maandalizi.

..sawa kabisa,safari hiyo ilihitaji fedha bila ya hivyo isingefanikiwa!

Jambo la msingi ni kufanya maamuzi. Humu ndani watu wanajitolea na huu ni mfano tosha. Kwa kuanzia wahakikishe wanafanya kazi ya kufuatilia nyendo zote zinazoelekea kutaka kuvuruga UKOMBOZI na kujibu mapigo kwa haraka. NASIKITIKA KUSEMA HILI SI LA CHADEMA. NI LA WATANZANIA WOTE hata wa CCM.

..hapa umenena!si la chadema pekee,wasije kutudai baadae,wakataka kurejesha fedha zao!yakawa yaleyale!

UKOMBOZI NI WA WOTE.

..kama tutashirikiana!na kupeana mawazo yenye kujenga!
 
Inawezekana RA anahusika na baadhi au yote yaliyojengewa hoja humu lakini ukweli unabaki kwamba hela zake before 2005 alizipata kwa njia yake halai kabisa, hakuibia mtu.

Pia ni vizuri ikaeleweka kwamba spinning politics zipo kila nchi, blair alizicheza sana na brown bado anazicheza, bush anazicheza kila siku na kadhaa wa kadhaa. Kwa hiyo kinachoendelea si kitu kigeni na sio uhalifu ingawa kimsingi, kama anafanya hayo yote sio jambo la busara because it will become counterproductive.

Katika kila nchi, kila uongozi unakuja na kambi yake na tactics zake. Hata angepita malecela, salim, mwandosya, kungekua na hoja kama hizi nyingi tu, may be worse. Solution ni kwa upinzani na wao kuja na tactics zao au propaganda, hilo halikatazwi.

Kuhusu link ya Karamagi, RA na wengine waliotajwa, kuna ushahidi gani? tunauomba tafadhali ili tuzidi kuelewa nini kinaendelea. Sijaona popote kwenye magazeti kuhusu RA kuwa mwizi, mla rushwa etc. Uwezekano upo ila tunaomba ushahidi. Kuna kina thisday, mwanahalisi etc na wanaweza kabisa kutuwekea bayana majambo haya.

Kama mtu ataweza kutofautishwa between TRUTH and KNOWLEDGE in such a contezt, nitaeleweka vizuri sana kuhusu maswali yangu ya ushahidi. KNOWLEDGE vs TRUTH ndio basis ya hoja yangu ya msingi.
 
Are you sure? kwani bajeti ya kutuma txt msgs na internet ni kiasi gani?

nadhani its about time CHADEMA wakaanza kuwa active na mambo haya badala ya kukaa pembeni kulalamika

Mie nasikia wako kazini, wamewasha moto. We umesikia wanalalamika? Au ni lugha tu!
 
Jamani ni kweli hawa watu wana mapesa mengi machafu, lakini sidhani kama UKOMBOZI wa kweli utapatikana kwa kutumia fedha.. Walipojitokeza wananchi kwa maelfu kumpokea Zitto, hawakulipwa hata senti tano, sana sana fedha zilitumika katika maandalizi. Jambo la msingi ni kufanya maamuzi. Humu ndani watu wanajitolea na huu ni mfano tosha. Kwa kuanzia wahakikishe wanafanya kazi ya kufuatilia nyendo zote zinazoelekea kutaka kuvuruga UKOMBOZI na kujibu mapigo kwa haraka. NASIKITIKA KUSEMA HILI SI LA CHADEMA. NI LA WATANZANIA WOTE hata wa CCM. UKOMBOZI NI WA WOTE. MWALIMU ALISHIRIKIANA SANA NA WATUMISHI WA SERIKALI YA WAKOLONI NA NDIPO ALIPOFANIKIWA. TUTUMIA RASILIMALI WATU TULIZO NAZO, INAPOFUKIA KWAMBA TUNAKWAMA NDIO TUANGALIE GHARAMA ZA KIFEDHA LAKINI SASA HIZO RASILIMALI WATU NA NYINGINE ZILIZOPO NDANI YA UWEZO WETU WATANZANIA WAPAMBANAJI HATUJAZITUMIA IPASAVYO< TUZITUMIE SASA

Halisi,

Hapa umenena.
 
in ideal world yes lakini in the real world no. As long as nchi yoyote ile duniani imeamua kuwa na liberal democracy then pesa lazima itakuwa factor kubwa ya kutimiza malengo fulani fulani be it in the United States or United Republic of Tanzania.

Sasa its up to indiviuals ku make up what they think of it.
 
Mie nasikia wako kazini, wamewasha moto. We umesikia wanalalamika? Au ni lugha tu!
kweli? Sidhani kama PR machinery ya CHADEMA iko up to the job.Unachokiona ni NCCR-MAGEUZI /MREMA REDUX. CHADEMA at the moment wako prone na makosa ambayo waliyafanya akina MREMA in the 90's
 
Inawezekana RA anahusika na baadhi au yote yaliyojengewa hoja humu lakini ukweli unabaki kwamba hela zake before 2005 alizipata kwa njia yake halai kabisa, hakuibia mtu.

Pia ni vizuri ikaeleweka kwamba spinning politics zipo kila nchi, blair alizicheza sana na brown bado anazicheza, bush anazicheza kila siku na kadhaa wa kadhaa. Kwa hiyo kinachoendelea si kitu kigeni na sio uhalifu ingawa kimsingi, kama anafanya hayo yote sio jambo la busara because it will become counterproductive.

Katika kila nchi, kila uongozi unakuja na kambi yake na tactics zake. Hata angepita malecela, salim, mwandosya, kungekua na hoja kama hizi nyingi tu, may be worse. Solution ni kwa upinzani na wao kuja na tactics zao au propaganda, hilo halikatazwi.

Kuhusu link ya Karamagi, RA na wengine waliotajwa, kuna ushahidi gani? tunauomba tafadhali ili tuzidi kuelewa nini kinaendelea. Sijaona popote kwenye magazeti kuhusu RA kuwa mwizi, mla rushwa etc. Uwezekano upo ila tunaomba ushahidi. Kuna kina thisday, mwanahalisi etc na wanaweza kabisa kutuwekea bayana majambo haya.

Kama mtu ataweza kutofautishwa between TRUTH and KNOWLEDGE in such a contezt, nitaeleweka vizuri sana kuhusu maswali yangu ya ushahidi. KNOWLEDGE vs TRUTH ndio basis ya hoja yangu ya msingi.

Mchambuzi,

Uliyoandika hapa hayafanani kabisa na jina lako, labda kama wewe ni mgeni katika Tanzania. hapa tunazungumzia spinning, siyo kwamba ilizaliwa Tanzania, ila tunachosema ni ubaya wake, hasa pale uongozi unaosaidiwa na spin doctors unapokuwa wa hovyo kama huu wa muungwana JK.

Nisaidie tu kukuonya. Dont' do any spinning here! JF guys are quite alert!
 
kweli? Sidhani kama PR machinery ya CHADEMA iko up to the job.Unachokiona ni NCCR-MAGEUZI /MREMA REDUX. CHADEMA at the moment wako prone na makosa ambayo waliyafanya akina MREMA in the 90's

Tunachokosa hapa wana JF ni kule kudhani kwamba kila mkakati wa CHADEMA utawekwa hapa. Yapo mengi tusiyoyajua yanayoendelea, na kisiasa huo ni mkakati poa. Unapokuwa unashindana, hasa unapokuwa umeshikilia makali, yapo mengi usiyopaswa kubwabwaja in public, na unayopaswa kufanya kimya kimya.

Mi naamini nao wanajifunza katika historia, kwani hawawezi kuipuuza. Ila ukumbuke kuwa NCCR ilishakufa zamani, wapo wazungumnzaji kina Mbatia, nao chama kimewalemea, wanatafuta mahali pa kukitua. TLP vile vile. Mrema amekimbiwa na kila mtu na mtaji wa kisiasa umemkimbia, hasa baada ya kuwafukuza wasomi wote...na kuwafanyia njama makatibu wakuu ake, akabaki alivyo leo. Sasa tuna vyama viwili tu CHADEMA na CUF, ndiyo sababu CCM wanafanya kila wawezalo kubomoa hivyo.

Usidhani sisi ndio pekee tunaoona hili CHADEMA hawaoni. Kama sisi tunashinda kwenye mtandano kupiga domo, nao kuna mahali wanashinda kufanya kazi ambazo haziwi up-loaded hapa.
 
Mchambuzi,

Uliyoandika hapa hayafanani kabisa na jina lako, labda kama wewe ni mgeni katika Tanzania. hapa tunazungumzia spinning, siyo kwamba ilizaliwa Tanzania, ila tunachosema ni ubaya wake, hasa pale uongozi unaosaidiwa na spin doctors unapokuwa wa hovyo kama huu wa muungwana JK.

Nisaidie tu kukuonya. Dont' do any spinning here! JF guys are quite alert!

Nionyeshe serikali gani duniani isiyo spin? Unajua kuwa Propaganda haikuanza in the 90's? hili neno lilianza na kanisa katoliki katika karne ya 16. Hata third reich walipotwaa nchi kule Ujerumani Spinning was up and running. Actually serikali ya CCM imechelewa sana kuingia katika hii karne ya new media ambako vita viliko. wao wamengangania majukwaaa tuuu lakini wamesahau kuwa sasa hivi fitna zinaendeshwa online

Nashauri urejee kitabu kinachoitwa MANUFACTURING CONCENT: THE POLITICAL ECONOMY OF THE MASS MEDIA kilichoandikwa 1988 na NOAM CHOMSKY pamoja na S HERMAN chomsky kaelezea sana kwa kirefu jinsi propaganda inavyotumika na serikai esp ya America katika kubadilisha mawazo ya watu na kadhalika actually hicho kitabu ni compulsory kwa yoyote anayefanya media studies.

mwisho ningependa kumalizia kwa kukumbusha maneno ya mwandishi wa vitabu kwa jina la Oscar Wilde ambaye aliwahi kusema:

"The pure and simple truth is rarely pure and never simple."
 
Nadhani unatutoa nje ya mada. Hakuna mtu aliyesema kwamba kuspin kumeanzia Tanzania, wala aliyesema kwamba tunapingana na historical aspect ya spinning. Huo siyo mjadala tulionao hapa. Lililo mbele yetu sote hapa ni kwamba tumegundua wanaofanya spinning hiyo na tunatahadharishana tusitumbukie katika mtego wao, kwa sababu they are not spinning for our good cause.
 
Tunachokosa hapa wana JF ni kule kudhani kwamba kila mkakati wa CHADEMA utawekwa hapa. Yapo mengi tusiyoyajua yanayoendelea, na kisiasa huo ni mkakati poa. Unapokuwa unashindana, hasa unapokuwa umeshikilia makali, yapo mengi usiyopaswa kubwabwaja in public, na unayopaswa kufanya kimya kimya.

Mi naamini nao wanajifunza katika historia, kwani hawawezi kuipuuza. Ila ukumbuke kuwa NCCR ilishakufa zamani, wapo wazungumnzaji kina Mbatia, nao chama kimewalemea, wanatafuta mahali pa kukitua. TLP vile vile. Mrema amekimbiwa na kila mtu na mtaji wa kisiasa umemkimbia, hasa baada ya kuwafukuza wasomi wote...na kuwafanyia njama makatibu wakuu ake, akabaki alivyo leo. Sasa tuna vyama viwili tu CHADEMA na CUF, ndiyo sababu CCM wanafanya kila wawezalo kubomoa hivyo.

Usidhani sisi ndio pekee tunaoona hili CHADEMA hawaoni. Kama sisi tunashinda kwenye mtandano kupiga domo, nao kuna mahali wanashinda kufanya kazi ambazo haziwi up-loaded hapa.

unayoyasema ni kweli kabisa lakini naweza kukuhakikishia kuwa PR machine ya CHADEMA haiko as effective kama ambavyo unavyofikiria au wanavyotaka kuimply.Ni kweli wana network nzuri na haswa toka kwa watu wa kaskazini ambao wako kwenye idara nyeti za serikali hivyo kupata "MABOMU" si tatizo lakini sasa hawawezi kukaa kutegemea mabomu tuuu. Wao ilitakiwa wawe wana ikosoa serikali kupitia mawaziri vivuli walionao.Nitakupa mfano mdogo tuuu. Unakumbuka yale maneno ya Mbowe kwenye Uwanja wa mashujaa kuwa bora serikali ya mkoloni? ili ilikuwa ni political suicide na walikuwa na nafasi nzuri ya kuirekebisha ile on the next day kuwa Mheshimiwa Mbowe alikuwa quoted out of context and so on na haikuwa nia yake kusema maneno yale katika uwanja ule...

Vile vile wanaye huyu kijana ZITTO KABWE ambaye ni avarage tuuu lakini hawawezi kumtegemea ZITTO pekeyake inabidi wawe na akina ZITTO 10 lakini tatizo ni kuwa Zitto yuko prone to gaffes, Na kama ZITTO anaweza kumoutshine leader wake kwa nini CHADEMA wasimpe specia ssistants ambao watakuwa wanampa hayo MABOMU ambayo hayatopelekea kusimamishwa au kupewa onyo?

Na yule Mzee SLAA kupeleka e-mail bungeni kutaka uchunguzi ufanywe bila ya yeye kuwa na enough materials kuback up motion yake ilikuwa ni makosa makubwa kisiasa, japo inawezekana ikawa kuna dalili za ukweli kwenye ile e-mail lakini still PR MACHINE ya CHADEMA ilifail kucapitalise na waliprove kuwa hata hizo source za "MABOMU" yako haziko that effectivekama ambavyo wengi wanafikiria.

Hivi unaweza kuniambia mara ya mwisho CHADEMA kama leading opposition paty Tanzania walitoa tamko ya Foreign Policy yetu kuhusu Majeshi yetu kuwepo SADC au kupelekwa LEBANON au performance ya balozi zutu nje?
 
Nadhani unatutoa nje ya mada. Hakuna mtu aliyesema kwamba kuspin kumeanzia Tanzania, wala aliyesema kwamba tunapingana na historical aspect ya spinning. Huo siyo mjadala tulionao hapa. Lililo mbele yetu sote hapa ni kwamba tumegundua wanaofanya spinning hiyo na tunatahadharishana tusitumbukie katika mtego wao, kwa sababu they are not spinning for our good cause.

Actually niko ndani kabisa ya mada labda hujaelewa nilicho.Naomba urejee kichwa cha thread utaona issue ni Spinning ambayo inadiwa inafanya na ROSTAM AZIZ on behalf of CCM. Na haitofautiani sana na Propaganda.

Tahadhari ni sawa lakini CHADEMA au upinzani nao wasikae chini kulalama kuwa CCM wana spin wakati na wao wanayo nafasi ya ku counter spin ambayo itaonyesha ni wapi kwenye ukweli na wapi kuna spin. By the way spinning isnt always for a good cause
 
unayoyasema ni kweli kabisa lakini naweza kukuhakikishia kuwa PR machine ya CHADEMA haiko as effective kama ambavyo unavyofikiria au wanavyotaka kuimply.Ni kweli wana network nzuri na haswa toka kwa watu wa kaskazini ambao wako kwenye idara nyeti za serikali hivyo kupata "MABOMU" si tatizo lakini sasa hawawezi kukaa kutegemea mabomu tuuu. Wao ilitakiwa wawe wana ikosoa serikali kupitia mawaziri vivuli walionao.Nitakupa mfano mdogo tuuu. Unakumbuka yale maneno ya Mbowe kwenye Uwanja wa mashujaa kuwa bora serikali ya mkoloni? ili ilikuwa ni political suicide na walikuwa na nafasi nzuri ya kuirekebisha ile on the next day kuwa Mheshimiwa Mbowe alikuwa quoted out of context and so on na haikuwa nia yake kusema maneno yale katika uwanja ule...

Vile vile wanaye huyu kijana ZITTO KABWE ambaye ni avarage tuuu lakini hawawezi kumtegemea ZITTO pekeyake inabidi wawe na akina ZITTO 10 lakini tatizo ni kuwa Zitto yuko prone to gaffes, Na kama ZITTO anaweza kumoutshine leader wake kwa nini CHADEMA wasimpe specia ssistants ambao watakuwa wanampa hayo MABOMU ambayo hayatopelekea kusimamishwa au kupewa onyo?

Na yule Mzee SLAA kupeleka e-mail bungeni kutaka uchunguzi ufanywe bila ya yeye kuwa na enough materials kuback up motion yake ilikuwa ni makosa makubwa kisiasa, japo inawezekana ikawa kuna dalili za ukweli kwenye ile e-mail lakini still PR MACHINE ya CHADEMA ilifail kucapitalise na waliprove kuwa hata hizo source za "MABOMU" yako haziko that effectivekama ambavyo wengi wanafikiria.

Hivi unaweza kuniambia mara ya mwisho CHADEMA kama leading opposition paty Tanzania walitoa tamko ya Foreign Policy yetu kuhusu Majeshi yetu kuwepo SADC au kupelekwa LEBANON au performance ya balozi zutu nje?

We! we! we! we!

Nguvu ya PR machinery ya CHADEMA siwezi kuisemea kwani simo, nawe (kutokana na mtiririko wa hoja zako hapo juu) nadhani humo, ni obsever kutoka nje. NInachotaka kukueleza hapa ni kwamba CHADEMA hawafanyi kazi peke yao, kuna mtandao mkubwa unaokerwa na usanii huu na unaojua kwa kina wapi muungwana na watu wanakosea, wapi wana nguvu na wapi wana udhaifu. Upo mtandao wa watu wanaoipenmda nchi hii na walio tayari kuwekeza nguvu na akili katika kuleta mabadaliko. Hilo nalijua fika, sihisi; na ningekushauri usiidharau nguvu hiyo.

Pili, kauli ya Mbowe kuhusu serikali ya mkoloni haikuwa political suicide kam unavyodhani. Huu ni mwaka 2007 siyo 1970. Ni wananchi wangapi wanaoishi leo, wanaotegemewa, waliomuona mkoloni wakaumizwa naye kiasi cha kumuona Mbowe mbaya? Hawa anaowaaddress leo wanaishi katika mateso ambayo yanafanana na yale waliyosoma vitabuni kuhusu ukoloni. Wanaona watawala wanavyoishi kwa kutumbua na wao wanavyohangaika, na wana hasira zile zile tulizokuwa nazo dhidi ya mkoloni.

Kumbe hujajiuliza kisa cha umma kuamka sana leo na kuunga mkono hoja ya Zitto? Ni kwa sababu wananchi wanaona wanaishi maisha ya kitumwa wakatyi raslimali zao zinawatajirisha walio madarakani. Hisia zao zimejikita katika dhana ya chuki dhidi ya ukoloni mweusi, tena mbaya kuliko ule uliokuwapo - ambao hata hivyo wengi wa vijana wa leo hawakuuona. Hiyo ni political capital, sio suicide.

Kusema Zitto anamu-outshine mkubwa wake ni dhana ya ki-CCM. Katika CHADEMA wanatambua talent za watu na kuzikuza, wanajenga chama taasisi kwa nguvu ya kila mmoja, leo huyu kesho yule. Katika suala hili, aliyefukuzwa na Bunge ni Zitto kwa kile alichokisimamia, lakini alikuwa anazungumza siyo kwa ajili ya CHADEMA ila kwa niaba ya upinzani. Hamad Rashid ndiye kiongozi wa upinzani Bungeni, lakini halalamikii kuwa outshined kwa sababu hoja yao imekua. Bahati kwa CHADEMA ni kwamba hoja imesaidia kuwasha moto nchi nchi nzima na chama kinakua, hivyo njia inapatikana, na viongozi wanaitumia. Ukilitazama kwa macho ya ubinafsi, ndo utasema amemu-outshine mkubwa wake, Ni kweli kwamba kama angekuwa CCM wangeishamnyamazisha maana ndiyo system yao. Je, na sisi tujiruhusu kufikiri na kutenda kama CCM?

Tatu, kuhusu Dk. Slaa. Kumbe hujajua kinachoendelea. Hakupeleka tu internet sources bali alitumia hoja ya sources hizo kutaka serkali itoe majibu, halafu wenye sources wenyewe wakanza kufumuka. Lile likitabu limejaa documents ambazo hata kina EL wanashangaa amezipata wapi, na nyingine alikuwa hajawakabidhi anasubiri waruhusu hoja yake.

He is very well informed, na wakubwa wanajua hilo, la sivyo ndiye wangeanza naye kabla ya Zitto. Ushahidi wa hili ninao lakini sio kwa ajili ya kumwaga hapa sasa hivi. Subiri tu siku zisogee utajua ninachosema.
 
Waandishi wengi huku bongo ni kama wamenunuliwa. Nafahamu hapa JF watu wana uwezo wa kuanalyze news. Kwa mfano JK alipokwenda Seoul alipiga picha na Rais wa nchi ile baadhi ya waandishi wakaja na headline "Kikwete mwisho" what a crap!!, akifanya lolote like hata blunder anasifiwa sana. Hata kuialika timu ya "Real Madrid" kuja Tanzania alisifiwa sana, wakati mwaliko wenyewe ungetumia mamilioni ya pesa without any return, na shule kibao mkoa wa pwani zina mwalimu mmoja, hazina viti wala madarasa, even more urgent hakuna hata dawa hospitali. Sasa waandishi wa magazeti kama haya can you count on them? Sishangai kusikia kuwa kuna strong media campaign inayoendelea kuwalinda wabovu na kuwabomoa wazuri. Ni hapa JF na kwenye blogs chanche nyingine wanakutana wenye akili na kumkoma nyani giladi. Ni juzijuzi tu member mmoja alituletea post kuulizia kama ni kweli wahiriri walipewa bahasha zenye laki kadhaa, unadhani hiki ni nini? no doubt ni kuwanunua.
Issue ya BAE JK akasema anadai kilichozidi, media ikasifu lakini rushwa iliyohusika haikusemwa.......inasikitisha sana...
 
Back
Top Bottom