Rostam Aziz now said to be `damaging` CCM reputation

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Rostam Aziz now said to be `damaging` CCM reputation

-Ruling party stalwarts asking more and more questions

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

CORRUPTION allegations surrounding business tycoon Rostam Abdulrasul Aziz, who holds senior leadership positions in Chama Cha Mapinduzi (CCM), are ’’damaging the reputation of the ruling party ahead of the 2010 general elections,’’ according to ruling party insiders.

The businessman-cum-politician currently serves as member of parliament for Igunga Constituency and member of the powerful CCM central committee, and was the party’s national treasurer for a lengthy period in the not-so-distant past.

It has however, now come to light that Rostam’s status is steadily dropping in the eyes of an increasing number of senior CCM leaders, who believe he is becoming more of an ’’electoral liability’’ for the ruling party.

’’He mainly gained influence in the ruling party because of his various fund-raising abilities during election time. But he has now actually become an electoral liability for us, especially since he still occupies top leadership positions,’’ an official close to the CCM top leadership hierarchy told THISDAY.

’’It is no secret that Rostam has been thoroughly tarnished by allegations of corruption mounting up against him. In fact, he is now damaging the reputation of the ruling party ahead of the 2010 general elections,’’ the official said.

Another ruling party insider remarked: ’’CCM can never dare ask him (Rostam) to address public rallies during election campaigns outside his Igunga Constituency. We know it would be a disaster because he is widely seen as lacking the moral authority to do so.’’

A growing number of established CCM cadres seem to agree that the Igunga legislator has managed to maintain his leadership positions within the ruling party largely thanks to his strong influence among key members of the party’s secretariat and other crucial party departments.

They point to the fact that while at least three ’heavyweight’ political heads tumbled as a result of the Richmond energy generation scandal, Rostam was left largely unscathed despite also being heavily implicated.

The scathing Richmond report led to the resignations of former prime minister Edward Lowassa, and cabinet ministers Nazir Karamagi and Dr Ibrahim Msabaha.

But despite being linked alongside them in the report, Rostam has continued to hold on to his ruling party posts regardless of National Assembly-approved recommendations that all individuals implicated in the scandal should be dropped by both party and government.

’’He became an MP in 1994 at the age of just 25. Some people now even describe him as a ’king maker’ due to the influence he apparently wields in the ruling party,’’ said another political observer.

However, his available public records are scant. According to the National Assembly website, he was born on December 31, 1969, and holds a BA degree in economics. The name of the university he attended is missing.

On Rostam’s employment history, the Bunge website says he worked at unspecified periods in the following companies:

Research on Business (managing director), Africa Trade Development (director), Africa Tanneries Limited (director), Tanzania Leather Industries Limited (director), and Caspian Construction Limited (director).

Although his official CV links him to the above-mentioned companies only, Rostam has also been associated with more than a dozen other companies with little-specified business dealings.

Allegations of his involvement in some especially shadowy companies started to emerge after he was associated with proven fraudulent companies such as Richmond Development Company and Kagoda Agriculture Limited.

Though the infamous Kagoda company was used to loot more than 40bn/- from the Bank of Tanzania’s external payment arrears (EPA) account, its owners have so far escaped indictment and prosecution by government organs.

Karatu member of parliament Dr Wilbrod Slaa, from the opposition CHADEMA party, first linked Rostam to Kagoda in 2007 when publicly unveiling the infamous ’’List of Shame.’’

And although the businessman-cum-politician denied any links with the EPA fraud, it has since been established that the contact numbers of two other companies linked to Rostam were identical to that used by Kagoda.

Afritainer Limited and Africa Trade Development, both of which are associated with Rostam, used the same Dar es Salaam-listed telephone number (2861371) and fax number (2861372) as those used by Kagoda.

Similarly, Dowans Holdings company - which inherited the dubious Richmond company - used an email address similar to Caspian Construction, yet another Rostam stronghold.

According to official government records, African Trade Development (T) Limited lists its directors as Rostom A. Sakarri, Rostam Sakarri, Rustom Aziz Sakarri, Rustam Sakarri and Rustam Sakaari.

Another name associated with Rostam, Gulam Chaka alias Gulam Chakar, also appears as one of the shareholders in the controversial Tanzania International Container Terminal Services (TICTS).

It has also emerged that while Rostam has publicly acknowledged that he is proprietor of media house New Habari Corporation which publishes Rai, Mtanzania, The African and other newspapers, his name does not appear in the company’s official shareholders’ records.

’’It is quite clear that this fellow likes to operate in a shadowy manner. Everything about him is a mystery - his birthplace, his true nationality, his education background, the number of legitimate businesses he owns, etcetera,’’ said the CCM insider.
 
KULIKONI namba 661, Alhamisi Juni 4, 2009



Zigo la tuhuma za Rostam
sasa mwiba mkali kwa CCM

*Lowassa, Msabaha, Karamagi walishawajibika
*WanaCCM wastuka yeye kukwepa ya Richmond

MWANDISHI WETU

Dar es Salaam

MBUNGE wa Igunga na mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz, anayekabiliwa na zigo la tuhuma za ufisadi na bado ameshindwa kuzikanusha, anaendelea kushikilia nyadhifa zake hatua ambayo sasa, kuelekea uchaguzi mkuu 2010 inakiweka njia panda chama hicho na Serikali yake.

Tayari CCM imejikuta ikikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi baada ya kushindwa kuchukua hatua kukabiliana na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi na hatua ya watuhumiwa hao kung’ang’ania uongozi si wa mashina au majimbo, bali hata ule wa ngazi za juu za maamuzi.

Rostam ambaye awali mwaka 1994 aliingia bungeni kutokana na uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Igunga uliotokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Chales Kabeho, ndani ya miaka michache aliibuka kuwa mbunge mwenye nguvu na ushawishi mkubwa ndani ya chama na serikali.

Katika muda wa miaka zaidi ya 15 ambayo Rostam amekuwa mbunge, amepanda chati hadi kufikia kuwa mjumbe wa CC, na almanusura aukwae uwaziri mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani, Desemba mwaka 2005, kama minong'ono iliyoenea wakati huo ilikuwa sahihi.

Lakini tatizo la Rostam ni kutajwa kumiliki kampuni zaidi ya kumi, lakini jina lake, uchunguzi wetu, umeonesha, linaonekana katika kampuni moja tu, African Trade Development (T) Limited, katika namna ambayo sasa inazidi kuibua utata juu ya biashara anazofanya mbunge huyo na malengo au mwelekeo wa biashara hizo.

Madai ya Rostam kumiliki kampuni zisizo na majina yake yalianza kujitokeza lilipozuka sakata la yeye kuhusishwa na kampuni kadhaa zenye kashfa ikiwemo ya Dowans na Kagoda.

Kwa mara ya kwanza jina la Rostam kumiliki Kagoda lilitajwa na mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa, mwaka 2007 katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Tandika, Dar es Salaam.

Dk. Slaa aliwaambia umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo, kwamba Rostam amejificha nyuma ya umiliki wa Kagoda kupitia kwa Francis William na John Kyomuhendo 'wamiliki' walioandikishwa kwenye orodha ya Msajili wa Makampuni (Brela).

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Kyomuhendo na William ni wafanyakazi wa Rostam. Hata hivyo, jina la Rostam halionekani katika ofisi za Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA). Mpaka sasa, Rostam hajakanusha madai hayo ya Dk. Slaa.

Naye Wakili wa Mahakama Kuu, Byidinka Michael Sanze alipigilia msumari katika madai kuwa Rostam ndiye mmiliki wa Kagoda baada ya kunukuliwa katika hati ya kiapo, akisema kuwa Rostam ndiye aliyemtaka kushuhudia hati za mikataba ya Kagoda.

Kampuni ya Kagoda ilichota zaidi ya bilioni 40/- katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Si kosa kisheria kumiliki kampuni nyingi nchini, lakini mwenendo wa Rostam wa kutumia watu wengine na wa ndani ya familia yake majina yao kuonekana katika kampuni alizo na maslahi nazo, ndio si tu unashangaza bali una siri nzito nyuma yake ambayo sasa Watanzania wanapaswa kuijua.

Kwa mfano katika kampuni ya Afritainer ambayo inaonekana kuwa na uhusiano na Kagoda iliyohusika na uchotaji wa fedha za EPA mwaka 2000, yamo majina ya watu wengine na/au wanafamilia yake.

Watumishi wawili tata na ambao KULIKONI linafahamu kuwa ni wasiri wakuu wa Rostam, Tabu Omari ambaye ni katibu muhtasi wake wa miaka mingi na Barati Godda ndio walioandikishwa kama Wakurugenzi wa Afritainer Limited kwa haraka haraka bila kufuata taratibu za BRELA ili waweze kufanikisha uchukuaji wa fedha za EPA.

Kampuni ya Afritainer na kampuni nyingine ya familia ya Rostam ya Africa Trade Development Limited ziliwahi kutumia pamoja namba ya simu ya mezani 2861371 na faksi 2861372, namba ambazo hatimaye baadaye ndizo zilizokuja kutumiwa na Kagoda iliyoanzishwa mwaka mmoja kabla ya kuchota bilioni 40/- za EPA.

Baada ya habari za namba hizo kufichuliwa, kina Rostam waliziachia namba hizo ili hatimaye ziweze kutumiwa na mtu mwingine. Rekodi za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) zinaonesha wazi jinsi namba hizo zilivyotumika kwa muda mrefu tangu wakati Dar es Salaam ikiwa inatumia kianzio cha namba cha 051. Sasa inatumika 022.

Rostam anatajwa tena katika tuhuma nyingine za kuchukua fedha za serikali bila ya kuwa na mkataba akidai kuagiza mahindi, lakini wakaguzi wakabaini kwamba hakukuwa na ushahidi wa yeye kuingiza mahindi nchini. Hata taarifa hizo zilipoanikwa kwa mara ya kwanza hivi karibuni, mwanasiasa huyo hakukanusha.

Kuna utata pia katika kuhusika kwa Rostam katika umiliki wa Dowans. Wakati anuani na barua pepe za kampuni yake ya Caspian Construction zilitumiwa na kampuni hiyo ya Dowans, Rostam mwenyewe alikana kuimiliki lakini walau mfanyakazi mmoja wa Dowans alipobanwa na Kamati Teule ya Bunge, alifikia karibu kidogo na uhalisia pale alipokiri mbele ya Kamati Teule ya Bunge kuwa Rostam na mwanzilishi wa Dowans huko Dubai, ni maswahiba.

Hata hivyo, taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ndani na nje ya nchi, ikiwemo kauli ya mbunge mmoja kutoka kanda ya Magharibi ambaye ni swahiba mkubwa wa Rostam, Dowans Tanzania, iliyokuja kusajili muda mfupi au wakati wa sakata la Richmond ni kampuni ya Rostam.

Eneo moja la kushangaza na kuibua maswali ni la usajili na/au majina yaliyotumika kusajili kampuni ya African Trade Development (T) Limited ambapo kuna Rostom A. Sakarri, Rostam Sakarri, Rustom Aziz Sakarri, Rustam Sakarri na Rustam Sakaari.

Ukiacha kituko hicho, kampuni nyingine zinazotajwa kumilikiwa na Rostam lakini jina lake halionekani BRELA ni pamoja na Africa Tanneries Limited, Tanzania Leather Industries Limited, Manufactures Limited, Wembere Hunting Safaris Limited na Ticts ambayo pamoja na kelele zote kutokana na kushindwa kazi bandarini, hadi sasa kila kiongozi anagwaya kutekeleza azimio la Bunge lililotaka mkataba wake usitishwe.

Katika Ticts jina linaloonekana ni la Gulam Chaka, ambaye katika kampuni ya African Trade Development (T) Limited, nako kuna jina kama hilo, lakini likiandikwa kwa Gulam Chakar.

Haijafahamika kama Gulam Chakar ambaye amejitambulisha kama mwenyekiti katika African Trade Development (T) Limited., ndiye huyohuyo wa Ticts ambaye huko amejitambulisha kama mkurugenzi.

Jambo la kushangaza kuhusu biashara za Rostam ni pale ambapo hata katika ununuzi wa magazeti ya Rai, Mtanzania, The African, Dimba, Bingwa na “Chuo” cha Uandishi wa Habari–MAMET, kutoka kampuni ya Habari Corporation Limited (HCL), hakuna jina la Rostam, hata hivyo inashangaza kuwa hivi karibuni akizungumza na waandishi wa habari Rostam alikiri kuwa yeye ni mmiliki tu wa kampuni, alipokuwa akikana tuhuma za kuagiza kuchapishwa toleo lililokuwa na lengo la kueneza propaganda zisizo na msingi.

Na ni Rostam huyo huyo ambaye haonekani kwenye majina ya kusajiliwa kampuni hiyo ambapo hivi karibuni magazeti hayo, yalitoa picha akiwa anakabidhiwa kombe mojawapo la ubingwa wa mashindano ya NSSF, ambayo moja ya timu za kampuni hiyo ziliutwaa.

Taarifa zinasema kampuni ya HCL iliuzwa kwa kampuni ya Isenegeja Company Limited, kupitia New Habari (2006) Limited (NHL), ambayo Rostam ni mmiliki.

Hata hivyo, jina la Rostam halionekani katika wakurugenzi na wamiliki wa kampuni ya Isenegeja ambayo sasa imethibitika kwamba ndiyo iliyonunua HCL.

Kwa mujibu wa watu wa karibu na Rostam, ameanza taratibu za kuhamisha uwekezaji wake toka nchini na kwenda nchi za nje ambako huko kinyume na anavyofanya nchini, huko atatumia majina yake katika umiliki wa kampuni zake.

Mojawapo ya mambo yanayotajwa ni mfano wa hilo ni kusudio lake la kutaka kuhamisha hisa alizonazo kwenye kampuni ya Vodacom jambo ambalo limekutana na upinzani kutoka kwa wasimamizi wa sekta ya mawasiliano.

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo ya kisiasa na kiuchumi wanasema, Rostam ataweza kuhamisha biashara zake iwapo atafanikiwa kuingia katika timu ya kampeni ya CCM katika uchaguzi ujao.

“Huko ndiko Rostam anakotengeneza fedha. Ndiyo maana anahaha kutaka kujisafisha hata kwa kutumia majitaka, ili ateuliwe kuwa mweka hazina wa kampeni zijazo za CCM,” alisema kada mmoja wa chama hcho anayefahamu vema mwenendo wa Rostam.

Makada mbalimbali waliozungumzia mwenendo wa mambo hayo kutoka ndani ya CCM wamekiri kuwa mwaka 2010 na hata zaidi ya hapo, miongoni mwa watu watakaoikwaza CCM ni mbunge huyo.

“Ni wazi kuwa sasa wananchi wamemuelewa, tatizo liko ndani yetu, hatuko tayari kukisafisha chama, tusubiri kuchafuka zaidi chaguzi zijazo,” alisema kada mmoja.

Baadhi ya wana CCM sasa wanahoji inakuwaje Rostam bado anashikilia nyadhifa za juu katika chama wakati ambapo wanaCCM wengine waliacha nyadhifa walizokuwa nazo Serikali baada tu ya kutuhumiwa katika sakata la Richmond.

Wakati wanaCCM kama Edward Lowassa, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha waliwajibika kwa nyadhifa zao, Rostam ambaye ushahidi uliomo kwenye Kamati ya Bunge ni mzito dhidi yake yeye anaendekea kuhudhuria Kamati Kuu ya CCM, kikao muhimu ambacho kinapojadili masuala ya msingi kiutawala na kisiasa kitaifa, Rostam moja kwa moja anakosa nguvu ya kimaadili (moral authority) kushiriki au kuamua mambo hayo kutokana na tuhuma nzito na ushahidi ambao hadi sasa hajaweza kuukana.

Swali la msingi ni nguvu zote hizo za kutogusika wala kuchukuliwa hatua anazitoa wapi na kama kwa nguvu hizo ataendelea kuendesha biashara zake namna hiyo milele?
 
Atawavuruga hao mithili ya mazezeta na nchi ikianza kuchapana yeye hyooooooo -- Iran! Ndiko huko alikokua kuanzia 1974 hadi 1988.

Na waandishi wafuatiliaji wameshindwa kui-unravel "gap" hii katika history yake. Alikuwa ana-attend an Internatioinal School of Swindling?
 
Waache awavuruge ili CCM ing'oke madarakani kirahisi. In fact kama kungekuwa na serious opposition hoja ya kuiondosha CCM madarakani ni moja tu -- kuwalinda mafisadi wanaoongozwa na kinara wao Rostam Aziz. Ni matarajio yetu kwamba kuna wanaCCM watajiondoa kwenye chama cha mafisadi ili kwa ridhaa yetu tuwape nchi waiongoze. Haki ya Mungu tukifanya makosa kuiacha CCM iendelee kuwepo madarakani hata mbwa watatucheka. Sioni dalili ya CCM kubadilika, kwani hao mafisadi papa ndio wanaoipelekesha serikali watakavyo.
 
Last edited:
CORRUPTION allegations surrounding business tycoon Rostam Abdulrasul Aziz, who holds senior leadership positions in Chama Cha Mapinduzi (CCM), are ’’damaging the reputation of the ruling party ahead of the 2010 general elections,’’ according to ruling party insiders.
"According to party insiders," which ones? Taja party insider mmoja tu kama hukutunga.

Hata mimi naweza kujiandikia "Mwanakijiji anashutumiwa kulipwa na CHADEMA." Anashutumiwa na nani? Nisipotaja, ina maana ni mimi ndio namshutumu. Magazeti ya kidaku ya Tanzania.
 
"According to party insiders," which ones? Taja party insider mmoja tu kama hukutunga.

Hata mimi naweza kujiandikia "Mwanakijiji anashutumiwa kulipwa na CHADEMA." Anashutumiwa na nani? Nisipotaja, ina maana ni mimi ndio namshutumu. Magazeti ya kidaku ya Tanzania.


Hapana mkuu, unajua kuna source nyingine za habari zinakuwa held in confidence kwa sababu za kiusalama. Hiyo ipo na itaendelea kuwepo. Wewe unafikiri documents zote za kifisadi tulizo nazo, tumezipata wapi?? Ni kwa binadamu kama mimi mwenye jina na cheo, na kwa sababu ya kiusalama hata unishikie mtutu wa bunduki sisemi source, ni YAMINI hiyo Dilunga.
 
huyu jamaa mjanja anawapumbaza watu kwa sababu ya njaa zao! kuna watu wenye heshima zao lakini wanapiga magoti kwa huyu bwana mdogo! njaa mbaya watanzania wapole, mabwege, mazezeta wa mungu! hivi nimesoma baada ya balozi ferdinand Ruhinda(ana asili ya Rwanda hana uchungu na wa tz)kumaliza muda wake wa ukurugenzi VODACOM (kuganga njaa) mafisadi wamemteua mzee peter kisumo kuwa mkurugenzi mpya ili aweze kuganga njaa zake na afunge mdomo! hawa wazee aibu hawana na ndiyo waliokuwa wanafiki wakati wa uongozi wa mwalimu!
 
"According to party insiders," which ones? Taja party insider mmoja tu kama hukutunga.

Hata mimi naweza kujiandikia "Mwanakijiji anashutumiwa kulipwa na CHADEMA." Anashutumiwa na nani? Nisipotaja, ina maana ni mimi ndio namshutumu. Magazeti ya kidaku ya Tanzania.

wangopa kuuawa, WE HUWAJUI SISIEMU
 
"according to party insiders," which ones? Taja party insider mmoja tu kama hukutunga.

Hata mimi naweza kujiandikia "mwanakijiji anashutumiwa kulipwa na chadema." anashutumiwa na nani? Nisipotaja, ina maana ni mimi ndio namshutumu. Magazeti ya kidaku ya tanzania.

makamba
 
Huyu bwana RA angetosha kabisa kuitoa CCM madarakani kutokana na haya mashutuma yote aliyonayo, ila tatizo watu wa vijijini ambao ndio wapiga kura walio wengi, hawana habari hizi, hawaelewi lolote, hawana elimu ya kuchanganua mambo na kibaya zaidi wana njaa kali. Kwahiyo uchaguzi unapokaribia ccm wanajimwaga huko na kuwapatia fulanas, kanga na pilau basi, kura zote wanazizoa. Ukichanganya na zile watakazoiba, wamemaliza biashara. BTW, I hope kwenye uchaguzi ujao JK hatakwepa midahalo (debates) kati yake na wagombea wengine kama alivyofanya last time. Nadhani watanzania wamlazimishe asilete misababu yake ya kitoto. Nina hakika kwenye mambo ya midahalo ni lazima ataangukia puwa maana mara nyingi namna yake ya kujieleza na kuelezea mambo anakuwa ovyo kabisa.
 
Hawa party insiders wanakuwa wanafiki. Mbona hawajawataja mafisadi akina Mkapa, Chenge, Makamba, Lowassa, Yona, Mramba na wengi wengineo ambao nao wana tuhuma nzito tu za ufisadi!? CCM yote sasa hivi ni chama cha mafisadi tu, kuna wachache sana ambao wanataka chama kibadilike lakini sauti zao ndani ya chama hicho hazina ngyvu hata kidogo.
 
Hawa party insiders wanakuwa wanafiki. Mbona hawajawataja mafisadi akina Mkapa, Chenge, Makamba, Lowassa, Yona, Mramba na wengi wengineo ambao nao wana tuhuma nzito tu za ufisadi!? CCM yote sasa hivi ni chama cha mafisadi tu, kuna wachache sana ambao wanataka chama kibadilike lakini sauti zao ndani ya chama hicho hazina ngyvu hata kidogo.

sio ndani ya ccm pekeyake, kuna mbuge kijana wa upinzani sasa amearibika kabisa, yeye ni kutetea maslahi ya mafisadi, mara Dowans na sasa kaingia TRL
nitamwaga nyeti zake nuikimaliza mchakato wa kukusanya data
 
Huyu bwana RA angetosha kabisa kuitoa CCM madarakani kutokana na haya mashutuma yote aliyonayo, ila tatizo watu wa vijijini ambao ndio wapiga kura walio wengi, hawana habari hizi, hawaelewi lolote, hawana elimu ya kuchanganua mambo na kibaya zaidi wana njaa kali. Kwahiyo uchaguzi unapokaribia ccm wanajimwaga huko na kuwapatia fulanas, kanga na pilau basi, kura zote wanazizoa. Ukichanganya na zile watakazoiba, wamemaliza biashara. BTW, I hope kwenye uchaguzi ujao JK hatakwepa midahalo (debates) kati yake na wagombea wengine kama alivyofanya last time. Nadhani watanzania wamlazimishe asilete misababu yake ya kitoto. Nina hakika kwenye mambo ya midahalo ni lazima ataangukia puwa maana mara nyingi namna yake ya kujieleza na kuelezea mambo anakuwa ovyo kabisa.



Mfalme!

Asante sana kwa kuliona hilo. Rostam Aziz kwa lugha ya mjini ni DIGALA au kuwadi. He operates behind the scenes kama wale Mafia wa Cicily na Parlemo.

His name doesn't appear in any transactions and this is done deliberately ili ikifika siku ya watu kunyongwa asionekane. this is crazy. Kwa Bahati mbaya ameweza kupenya mpaka kwenye System ya Ikulu na he is well informed of any moves done by the president!!

Nawapa changamoto nani atanitajia mmiliki wa kwa mfano New Africa Hotel!! Go to BRELA utaona kinyaa in the same way as RA operates Ali Hasan Mwini na Arap T. Moi ndio wamiliki hao wahindi ni agents... the list is long naweza kuweka hapa yote and if it goes to the open media CCM watakuwa kaburini by February 2009.

Ask JMK aka Matonya mbona Mkapa alitumia polisi na Mahita kumwua marehemu Amran Kombe for dissent only and can't he use the same method kuwaondoa akina Rostam Azaiz na Teddy Lowasa ambao hawampi usingizi and the rest ambao they are more a liability than an asset to CCM
 
sio ndani ya ccm pekeyake, kuna mbuge kijana wa upinzani sasa amearibika kabisa, yeye ni kutetea maslahi ya mafisadi, mara Dowans na sasa kaingia TRL
nitamwaga nyeti zake nuikimaliza mchakato wa kukusanya data
Tunazingoja....
 
Back
Top Bottom