Rostam Aziz, kwanini siku hizi Kubenea na CHADEMA hawamgusi?

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,223
4,681
Ilikuwa ni kawaida kwa magazeti ya CHADEMA na wanasiasa wa CHADEMA kutaja jina la Rostam Aziz kulihusisha na ufisadi wa kutisha wa nchi hii.

Kinachotia shaka tangia kipindi cha uchaguzi uliopita CHADEMA wamekuwa kimya kuhusu huyu mtu. Hawamtaji tena kwenye ufisadi na wapo radhi kumtetea.

Swali :

Rostam kwa nini haitwi tena fisadi na CHADEMA?

Ni sababu Rostam ni rafiki wa damu wa Lowassa?

Au ni sababu alifadhili harakati za 4 U kupitia Ukawa?

Bado CHADEMA wana nguvu ya kumnyooshea kidole Rostam?

Wafuasi wa CHADEMA wameshafutiwa kwenye vichwa vyao kuhusu Rostam na sasa wanamezeshwa wimbo mpya?
 
Wakati CHADEMA na KUBENEA wanamsema Rostam kipindi hicho kama unavyodai wewe ulikuwa unajisikiaje na ss ambapo hawamtaji kama unavyodai unajisikiaje?
 
CHADEMA wameshapoteza nguvu yao ya asili, wameshapoteza lengo kuu la uwepo wao. Kurudi katika mstari inahitaji kuibuka kwa kizazi kingine chenye kutaka kweli mabadiliko.

Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru alizunguka nchi nzima na landrover, alikuwa mtu rahisi sana kwa maana ya ule ukaribu wa kuongea naye, kumshauri, hakujikweza wakati akiwa vitani katika kutafuta upatikanaji wa Uhuru. Na hata aliokuwa nao katika vita ya kudai uhuru walikuwa na ile simplicity.

CHADEMA wamepoteza simplicity, wamepoteza ile hali ya mtu kuwaachia kitu na kutegemea kukikuta kesho asubuhi kikiwa vile vile kama kilivyoachwa jana usiku.

Mwanasiasa ambaye atakuwa na mvuto utakaowafanya watu waweze kuisahau CCM kwa haraka sana, bado yupo kwenye michakato ya kuandaliwa. Labda 2020 anaweza kuonekana, labda 2025, kwani inategemea na jinsi gani vyama vya siasa vya upinzani vinajitazama na kujiandaa kwa ajili ya mapambano ya kweli ya kuiondoa CCM madarakani, nasema mapambano ya kweli na sio hizi sanaa za majukwaani.
 
Wakati CHADEMA na KUBENEA wanamsema Rostam kipindi hicho kama unavyodai wewe ulikuwa unajisikiaje na ss ambapo hawamtaji kama unavyodai unajisikiaje?

Najihisi kusalitiwa kwenye mapambano ya mafisadi... Pesa sio mwenzio.
 
Unauliza na kujibu mwenyewe,kwanini? Waache uliowauliza wakujibu. Chura!

Mzee Tupatupa

Mkuu haya mambo yaliwatokea vinega misukule ya mr Sugu walijifanya wana uchungu na muziki.. Basi Sugu alipopewa pesa yake na Ruge na kelele zikaishia hapo akawakimbia wenzake anasema kashakomboa muziki.

Vinega sasa hivi wengine wanaosha magari wengine wakata mkaa Tanga huko, Sugu akiwaona njiani anafunga vioo.

CHADEMA kazi yao kuwatumia wajinga.
 
Katika watu wa ajabu ni wana CCM, wanawaza mambo ya kijinga tu.Rostam Aziz ni mmiliki wa gazeti la Raia Tanzania kila andiko inatukana CHADEMA sasa nashangaa ila hamna shida labda wana CCM wanaamini watanzania wako karne ya 20.
 
Katika watu wa ajabu ni wana ccm, wanawaza mambo ya kijinga tu.Rostam Aziz ni mmiliki wa gazeti la Raia Tanzania kila andiko inatukana Chadema sasa nashangaa ila hamna shida labda wana ccm wanaamini watanzania wako karne ya 20.
Raia Tanzania na Raia Mwema ni magazeti ya mzalendo Jen Ulimwengu.
 
Ilikuwa ni kawaida kwa magazeti ya Chadema na wanasiasa wa Chadema kutaja jina la Rostam Aziz kulihusisha na ufisadi wa kutisha wa nchi hii.

Kinachotia shaka tangia kipindi cha uchaguzi uliopita Chadema wamekuwa kimya kuhusu huyu mtu. Hawamtaji tena kwenye ufisadi na wapo radhi kumtetea.

Swali :

Rostam kwa nini haitwi tena fisadi na Chadema?

Ni sababu Rostam ni rafiki wa damu wa Lowassa?

Au ni sababu alifadhili harakati za 4 U kupitia Ukawa?

Bado Chadema wana nguvu ya kumnyooshea kidole Rostam?

Wafuasi wa chadema wameshafutiwa kwenye vichwa vyao kuhusu rostam na sasa wanamezeshwa wimbo mpya?
Kubenea anatajirika.
 
hizi siasa zimebadlisha watu na fikra zao wanahrakati wamekua wateteaji wa wakosaji. ngoja nizungushe mikono
 
Back
Top Bottom