Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
Rostam Aziz kugeukia Waislamu, Kuibua wengine CHADEMA
Nilisema hapa miezi mingi nyuma kuwa Rostam kumtumia Chacha Wangwe kuibomoa CHADEMA. Watu wakasema nasema udaku. Leo CHADEMA ineshavikwa ukabila na ubadhirifu wa ruzuku. Ni matokeo ya kikao cha RA na Wangwe Kempinsiki Hoteli na baadaye kikao kwenye ile nyumba ya Kinondoni mitaa ya jirani na Balozi Wa Marekani hapa Tanzania.
Nilesema hapa Rostam alivyomnunua yule aliyejiita kiongozi wa CHADEMA Igunga kutoa tamko la kumwuunga mkono kugombea Ubunge 2010, lakini nikaweleza kwamba baada ya hapo mkakati utakaofuata ni wa kuwatumia viongozi wa dini. Maneno yangu yamedhihirika kwa Rostam kulitumia kanisa la KKKT Kinondoni. Sasa habari kutoka duru la wanamkakati wa Rostam ni kwamba sasa atawatumia Viongozi wa Kislamu hivi karibuni na atahamia kwa watu mashuhuri Tanzania. Na katika mkakati wake huo amefanikiwa kuwanunua hata baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi katika vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vikimuanika zaidi vya Thisday/Kulikoni na Tanzania Daima. Na vile vilivyokuwa katikati vya Mwananchi na Nipashe. Na ameongeza nguvu zaidi katika vyombo anavyovitawala vya Majira na Mtanzania.
Kwa upande mwingine, ule mkakati niliousema siku nyingi wa kumtumia Chacha Wangwe umefanyiwa marekebisho kwa kuwa malengo hayafukiwa kama ilivyopangwa. Awali ilipangwa Chacha Wangwe atumie kikao kilichofanyika Dodoma 28 Juni, 2008 kutoa hoja ya kutaka Kamati Kuu ipige kura ya kutokuwa na imani na Dr Wilbroad Slaa kama Katibu Mkuu, ili akiondolewa Slaa aondoke na Sekteratiati yake yote wakina Zitto, Tundu Lissu, Mnyika, Tumbo na wengineo; Mbowe abaki mwenyewe na iwe rahisi kummalizia.
Katika Mkakati huo ilipangwa kama kura za kutokuwa na imani hazitatosha ilikuwa Chacha Wangwe atoke nje na kusema kuwa Mbowe ametumia udikteta kuzuia hoja hiyo, na ajitokeze mbele ya umma na hoja hizi hizi ambazo ameumua kuzitoa sasa. Angefanya kama anavyofanya sasa lakini ujumbe wake ungekuwa ni kuwa Mbowe anamlinda Dr Slaa ambaye ameshindwa kazi na anaruhusu ubadhirifu. Lengo la Mkakati mzima likiwa ni Dr Slaa kupoteza imani kwa wananchi na hatimaye mjadala wa ufisadi kuonekana hauwahusu watu 11 wa CCM aliowataja kwenye list of shame bali hata yeye mwenyewe. Kwa bahati mbaya au nzuri, mtu mmoja wa Rostam ambaye ni mpenzi wa Dr Slaa akatoa siri nyingi kwa Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA.
Suala hili likaingizwa kwa Kamati ya Wazee wakina Mtei, Profesa Baregu, Balozi Ngaiza, Makani na Ndesamburo, hata hivyo wazee wakaamua yote yawekwe kama kumbukumbu na kuamua kupatanisha hasa baada ya Chacha kuonyesha urafiki na kujirudi. Nyuma ya pazia Chacha akaendelea na mpango wake kwa kwenda kumngoa Dr Slaa Dodoma, na tayari Ballile alitumwa Dodoma na Rostam kuratibu habari hiyo. Lakini mambo yakabadilika Dodoma pale ripoti ya Kamati ya Wazee ilipowasilishwa Dodoma, Chacha akawageuka Wazee kuwa hakukubaliana nao yaishe, akatoa hoja ya kumshambulia Dr Slaa; kikao kikamgeuka yeye. Akachukia na kumtukana Baregu. Akamtukana pia Mama Chiku Abwao matusi ya nguoni kwa kutangaza kuwa pamoja na kuwa alimuunga mkono na kumpigia debe kuwa Makamu katika hilo hakubaliana nao.
Matusi yake yakamuudhi Tundu Lissu aliyetaka achukuliwe hatua za kinidhamu, Chacha akainuka na kumvamia Tundu Lissu kutaka kumpiga- Board Guard wa Mwenyekiti akapambana nae na kumzuia.
Ndio maana mtakumbuka kuwa habari ya Mtanzania iliyoandikwa kabla ya Chacha kusimamishwa, huku Ballile akijua kuwa matarajio ni Slaa kusimamishwa, wakati kikao kinaendelea mpaka usiku wa mananeo Ballile akaandika Habari ya Mambo ambayo alitarajia yangetokea kikaoni lakini hayakutokea. Alitarajia pangekuwa na mjadala mkali kuhusu hoja ya Ruzuku lakini kwa bahati mbaya suala hilo halikujadiliwa kama ilivyotarajiwa. Baaada ya Mkakati huo kushindwa, Rostam na Ballile wakaamua kutumia mkakati wa CHADEMA yamwaga Mboga, Chacha Amwage Ugali. Pamoja na Mkakati huo kufanikiwa kuichafua CHADEMA, bado haujaweza kutimiza malengo ya awali. Hivyo, wakabadili Mkakati na kukubaliana kwa Chacha Atangaze Wazi kuwa lengo lake ni Kugombea Uenyekiti na Kumwondoa Mbowe na Dr Slaa.
Mkakati huo umeanza ku-back fire kwa kuanza kuwaunganisha waCHADEMA wote makini na hata wapenzi kwa kuanika rangi halisi za Chacha Wangwe. Jana kimefanyika kikao kingine, tathmini imefanyika ya jinsi Mkakati wa kuwatumia KKKT Kinondoni ulivyofanikiwa. Kwa ujumla imeonekana Mkakati umefanikiwa lakini kuna hofu viongozi wa juu wa kanisa la KKKT hususani Askofu Malasusa wanaweza kuchukia na kutoa onyo kali kwa wenzao wa Kinondoni.
Suala hili linajengwa uzito zaidi kwa jinsi ambayo Spika Sitta amechukizwa na habari za kanisa hilo kutumika. Ili kuzuia hali hiyo, imekubaliwa Rostam afanye kwa haraka tukio na Waislamu ili Wakristu waoone dini zote zinakubaliana nae na kumuona ni mtu msafi.
Kwa upande mwingine, sasa Rostam Aziz ameamua kubadili mkakati wa jinsi ya kuwabomoa CHADEMA na sasa pamoja na Chacha Wangwe kukusudia kwenda mahakamani na kukata rufaa kwenye baraza kuu, Rostam Aziz amepanga mkakati mwingine unaoitwa GAWA, TAWALA, chini ya mkakati huu mashujaa kadhaa watalipwa kujitokeza kuwa mstari wa mbele kuungana na Chacha, tayari Wangwe na Ballile wamepewa fungu la fedha kuingiza watu kuunda kundi lao. Mpaka sasa katika Orodha wako Mziray, Shilembi. Lyimo, Shilungushela. Chini ya azma hiyo, kikwazo kikubwa ni kukosa home base baada ya Tarime kutoa msimamo wa wazi wa kumpinga na kueleza wazi kuwa wao wanapokea ruzuku ya Laki Nne kila mwezi kutokana na moja ya wilaya iliyofanya vizuri zaidi katika matokeo ya uchaguzi 2005.
Baada ya Habari hiyo ya Nipashe, Chacha Wangwe alipiga simu kuwatisha viongozi hao lakini viongozi hao wakamweleza kuwa msimamo wao ni msimamo pia wa madiwani wengi wa CHADEMA na Mwenyekiti wa Halmashauri(Kama Meya) wa Tarime ikikumbukwa kuwa CHADEMA ni chama tawala huko. Baada ya Kadhia hiyo, Jana Rostam alimwelekeza Chacha Kufanya mapinduzi Tarime kwa kuwaondoa viongozi hao. Jana hiyo hiyo Chacha Wangwe akampigia simu Chacha Okong, yule aliyekuwa kampeni manager wake kwenye uchaguzi mkuu 2005 ambaye pia alikuwa katibu wa wilaya a;iyehama toka CHADEMA kwenda CCM baada ya Chacha Wangwe kushindwa kuendeleza kazi za chama na pia kuwatelekeza kabisa wapiganaji wenzake na kukaa Dar es salaam.
Chacha Wangwe amemuahidi milioni 10 kama atarejea chama chake cha awali cha CHADEMA na atahakikisha kuwa anarudi kwenye nafasi yake ya Katibu wa Wilaya na kutoa kauli ya kuumuunga mkono. Fedha hizo ni chini ya kiwango ambacho Rostam aliahidi kitolewe kwa ajili ya zoezi hilo. Kuna mengi yanaendelea hivi sasa, na tutarajie mengine zaidi wiki hii. Mkakati huu ni sehemu ndogo tu ya mpango kabambe wa Rostam wa kujisafisha na kuwaita watu wengine zaidi mafisadi ili kugeuza mjadala wa ufisadi nchini Tanzania.
PM