Rostam Aziz kugeukia Waislamu, Kuibua wengine CHADEMA

hili La Cv Limewekwa Hadharani Kabisa, Sidhani Kama Wangezianika Cv Za Wabunge Kama Zingekuwa Ni Siri Au Wabunge Wenyewe Wangeshalipinga Hili La Cv Zao Kuwekwa Hadharani. Sioni Kama Kuna Chochote Cha Kuficha Ukishakuwa Mwakilishi Wa Wananchi Toka Jimboni Kwako, Labda Utaficha Ufisadi Wako Tu Kama Mzee Wa Vijisenti...:)

Unapokuwa Na Cv Moja Unalinganisha Na Ya Mwingine. Hapa Ni Wangwe Vs Mbowe.wote Cv Zao Chafu Na Ya Mbowe Ndio Mbaya Zaidi. Amefeli Chuo Kikuu.
 
Mi nawaambia CHADEMA bado hamusikilizi ushauri na naona Wangwe anawapeleka peleka kinoma.
Ila Wangwe uliniudhi sana na issue ya UKABILA!
Na hapo ndio nashindwa kukuelewa..Kwani ni sera za kina CHENGE,ROSTAMA AZIZII NA MKAPA.
 
Kumbe Wangwe alikuwa Chadema kwanza kabla hajaenda NCCR -Mageuzi... Mhnnnn! na ni kitu gani kilichomrushisha - akapokelewa!.. na hata kufikia hapo alipo kama makamu mwenyekiti wa chama..Sababu gani hasa zilizofanya akapokelewa tena kama mtu aliyeokoka?
Na nimesikia kuwa kila upande aliokwenda chama kiliweza kupata ushindi Tarime... hii jamani nzito kwetu ku deny baadhi ya uwezo wake. As a fact sidhani kama kasema mahala popote kuwa yeye ana elimu ya Juu isipokuwa ni mwanasiasa... sidhani kama cheo cha Makamu mwenyekiti kinahitaji CV kubwa ya Udaktari na mara nyingi hawa wasomi ndio huharibu sana Uongozi wa chama kwa sababu siasa mara nyingi hazina ufumbuzi wa kitabuni... Ni swala la hekima na Busara - mjuzi wa kusema na kuunda FITNA!..
Tatizo la huyu jamaa ni pale alipouleta ndani..lakini sii Chadema waliomkaribisha huyu player hadi chambani wakamwacha na mke mwenye khanga moja!..
 
..lakini sii Chadema waliomkaribisha huyu player hadi chambani wakamwacha na mke mwenye khanga moja!..

Hili la Mke mwenye Kanga moja limeniacha hoi, lakini siendelei zaidi ili nisije vuruga haya majadiliano mazuri yanayoendelea hapa...:) Haya na tuendelee
 
Huyu Rostam anatakiwa kudhibitiwa vikali maana ataanza kupandikiza chuki ndani ya jamii na matokeo yake tutayaona baadaye na kujuta. Jana nilichangia ile thread ya Rostam kuonekana kanisani na kuchangia kwaya. Nilisema huyu mtu atasababisha wananchi wawachukie watu fulani fulani ambao hawahusiki na tabia chafu ya Rostam. Sasa kama anatumia hela kufanikisha ajenda yake ya siri ya kujisafisha huyu mtu anatakiwa kudhibitiwa. Huko Tarime bado kuna chuki kati ya kabila na kabila au koo na koo. Sasa ukija kuingiza utumbo huo anaojaribu kufanya, that means anataka kuweka au kishaweka kambi ya Wangwe na ambao hawamtaki Wangwe chamani au jimboni. Matokeo yake hawa watu watakuja kuumizana vibaya. Mie nawajua wakurya na jamii hiyo, nimeishi nao more than 5 yrs. Hii chokochoko si nzuri kabisa, watu watatoana roho.

Huyu Rostam hasipojiheshimu na kuanza kuleta mgawanyiko ndani ya jamii anaweza kushughulikiwa na wananchi wenye hasira. Yeye kishaiba pesa yetu, anatakiwa kurudisha zote na si kuanza kudanganya danganya hapa kuchangia kwaya. Amekuwa Mbunge kwa muda mrefu mbona hakuwahi kutoa misaada hiyo kwenye kwaya za Igunga, Nzega ambazo zilikuwa zinahitaji misaada kama hiyo wakati huo nami nikiwa Choir Member kule? Uchafu aliuanza zamani yeye na cousin wake Brandon wa Nzega wakati huo watu hawajui undani wa biashara za hawa jamaa.

Umefika wakati sasa wananchi kusema ENOUGH kama serikali haiwezi kumthibiti huyu muiran.
 
Mkandara,
Hivi CHADEMA walikuwa na choice gani? Wangwe ameshinda kwa kishindo kule Tarime wakati ambapo Mwungana kachukua nchi kwa ushindi wa Tsunami. Katika hali kama hii Wangwe alikuwa kama lulu kwa CHADEMA. Kwa hiyo hata kupanda kwake kuwa makamu mwenyekiti sishangai ukizingatia kwamba kulikuwa na propaganda za kukionyesha chama kama cha ukabila. Katika mazingira kama haya CHADEMA haikuweza ku afford kum "vet" Wangwe. Na ni upenyo au udhaifu huo huo ambao unatumiwa na utaendelea kutumiwa na akina Rostum Aziz kuubomoa upinzani. Ndio maana nimesema kuwa kujiunga na upinzani Tanzania lazima uwe na moyo kweli kweli wa kuipenda nchi yako.
 
Unapokuwa Na Cv Moja Unalinganisha Na Ya Mwingine. Hapa Ni Wangwe Vs Mbowe.wote Cv Zao Chafu Na Ya Mbowe Ndio Mbaya Zaidi. Amefeli Chuo Kikuu.

Mie sidhani kufeli Chuo Kikuu kinaweza kikasababisha ukashindwa kuwahudumia wananchi as long as malengo yako ni mazuri. Inawezekana akawa na matatizo yake mengine lakini unaweza ukawa na rekodi nzuri tu ya kuwahudumia wananchi wakati ukiwa ni MAIMUNA.
 
According to government officials, the Meremeta company was set up specifically to engage in gold mining activities at the Buhemba mine in Mara Region and purchase gold from artisanal miners At the same time...According to the CV of yours...You happened to be...
"Africa Mashariki Gold Mines Field Supervisor 1994 1997"
Je una maslahi ya jeshi na MEREMETA?
 
Wangwe wewe ni shushushu?
TANU Youth Chairman (Mkwawa High School) 1975 1976


Maana enzi hizo ukiwa kiongozi wa TANU huko Mkwawa basi ulikuwa unaripoti kwa Mkuu wa nini?
Jeshi ama usalama wa Taifa?
Ama direct kwa mwalimu?

NB:Chadema kama na nyie hamna lenu...Ilikuwa vipi mkampa mtu mwenye cv kama hiyo na mwenye chuki za kikabila nafasi ya kuwachungulia hovyo kiasi hicho?
Hamwezi kuona huyo kanyweshwa kitu?
Niliwapa ushauri mkadharau...Na sasa mdharau mwiba...
 
Jasusi,
sawa mkuu lakini kumbuka tu kitu kimoja kwamba dunia hii ya maskini FEDHA inachukua sana nafasi. Na ni kosa kubwa sana kusema Chadema had no choice..
Nitakupa mfano tofauti na ule uliotangulia.. nitasema hivi, ni sawa na kuoa mwanamke malaya mzuri wa sura ukitegemea kuwa kivutio fulani hali ukijua fika kwamba wenye fedha watachukua nyumba..
Kama kweli Rostam ana mkono ndani (jambo ambalo siwezi kupinga kabisa) imekuwaje afike huko? Hizi habari za huyu Jamaa na CCM hazikuanza jana wala hazikuanza Chadema alikuwa na record hiyo toka huko alikotoka, imekuwaje mnamkabidhi Mwizi mwenye record ufunguo wa chumba cha fedha!.. Chadema had no choice sio lugha kabisa jamani Chadema haiwezi kushinda uchaguzi kwa sababu ya mtu yaani Wangwe! itakuwa mnaturudisha nyuma kuanza kuuliza kuwa kinachouzwa kwa wananchi ni sera za Chadema ama sura ya Wangwe!..
Chadema kumpokea tena Wangwe huyu Player ni lazima kulikuwepo na sababu zaidi pengine naweza sema labda Chadema wajiulize kitu kimoja nani aliyempigia debe Wangwe arudi?.. Binafsi huamini vitu kama hivi hupangwa ndani yaani wizi wa Wangwe umetoka ndani ya chama, lazima kuna Kuhadi aliyempeleka mkali hadi chumbani..
Hizi habari za kilio cha mke kawa raped zina uzito mkubwa sana lakini sio ktk mazingira haya maanake inaonyesha wazi milango haikubomolewa, jamaa kaingia chumani tena amekaribishwa hadi chumabni wakati ambao sii wa kawaida kabisa!... Up to now kama raia mkuu sioni force marks ambazo Wangwe kaweza ama ameweza kuzisababisha..Sioni kabisa isipokuwa ni mambo ya ndani ambayo yhayakutakiwa kabisa yatoke nje kiasi hicho..Kumbuka tu kwa macho ya mwanamke uzuri wa mwananume sio elimu hata Mfanyakazi wako anaweza kutembea na mkeo! swala ni uwezo wake ktk maswala hayo!...hapo ndipo mnapokosea na kum under estimate Wangwe..
Rostam ni opportunist, labda kaona udshaifu fulani akautumia..Huyu jamaa ni hatari kuliko Wangwe mwenyewe na nakuhakikishia kama kweli kuna mkono wa Rostam ktk sakata hili basi wapo wengine makuhadi dani ya chama wamevaa ngozi ya kondoo... take my word for that.. Rostam hujipanga kisawasawa kabla hajarusha mapambano -Uwezo anao!
 
Mkandara.
Unaelewa vizuri na kuchambua mambo kwa pande zote uko huru.mawazo yako ni original si mgando.Wangwe ameshinda kwa kishindo hajawahi kutokea mbunge wa Chadema mwenye kupata kura nyingi kama yeye, lakini anatokea mtu hajui kitu anasema kuwa Wangwe ni mzigo bila kutathimini nyuma ya Wangwe kuna nini.mtu huyo hajawahi kushikiri chaguzi hata moja nje na ndani ya chadema,Wangwe na vigingi vyote hajawahi kushindwa chaguzi iwe ndani na nje ya Chadema, upimaji wako wa mambo nimeuhusudu bwana Mkandara.
 
Mkandara.
Unaelewa vizuri na kuchambua mambo kwa pande zote uko huru.mawazo yako ni original si mgando.Wangwe ameshinda kwa kishindo hajawahi kutokea mbunge wa Chadema mwenye kupata kura nyingi kama yeye, lakini anatokea mtu hajui kitu anasema kuwa Wangwe ni mzigo bila kutathimini nyuma ya Wangwe kuna nini.mtu huyo hajawahi kushikiri chaguzi hata moja nje na ndani ya chadema,Wangwe na vigingi vyote hajawahi kushindwa chaguzi iwe ndani na nje ya Chadema, upimaji wako wa mambo nimeuhusudu bwana Mkandara.

Hivi wewe mtu una akili nzuri kweli?
Hivi unajuwa mawazo original ya wananchi kuhusu wewe?
Na mawazo yao kuhusu wewe kwa sasa?
Mawazo ORIGINAL ambayo yaliwafanya wananchi na hata viongozi wa Chadema kufikiri kuwa na wewe ni mpinzani wa kweli?
Sasa Mkandara akikutetea wewe nani atashangaa?
Ama mtu wa ccm kama MASAKA akikutetea ama akiingilia mjadala huu na kupenyeza tujisifa twa ccm kwa style ya kufurahia maugomvi yenu...Nani atashangaa?
Acha siasa zako hizo kwani unaonekana KITUKO?
Tena hilo jina la "mgagagigikoko" Ni wazi una nia ya kikabila!
 
MUSHI.
Wakabila una wajua wamerundika wabunge wa viti maalum toka KILIMANJARO TU.
na mtu akishika nafasi ya juu ya NGO yao wanakuja juu kulinda maslahi yao.wewe kwa vile MUSHI umeamua kuwa suppoter wa chama cha wachagga wenzako-Chadema. mie unayesema kuwa mkabila niliamua kuja huko ili kuondoka kanza hii mbaya. sasa umakamu upewe wewe iwe MBOWE.MUSHI,NDESAMBURO. MTEI,MBAtIA ETC.

Ushauri mngeweka na lugha ya kichagga iwe official language ya chama chenu au kila document iwe translated kwenye kichagga ili kurahisisha kazi.
 
Last edited:
Mgagagigikoko,

Mkuu ktk hili mimi nalishikia bango haswa!.. haiwezekani huyu mtu atokee huko alikotoka awe mzigo kwetu lazima ipo kitu hapa. Labda walifikiria kwamba malaya anaweza kubadilika akipewa mapenzi ya kweli hali Umalaya sii mapenzi ni hulka ama kisu tuuu..
Nimerudia kusoma malalamiko ya huyu jamaa mkuu yanatisha!..Kwa kila mbinu inayotumika ktk kujikinga mimi naona kama wakuu wa Chadema ndio kwanza wanachemsha zaidi. Hoja zilizojibiwa kwa uhakika ni hiyo ya Ruzuku na Uteuzi wa Wabunge..lakini ktk kufukuzwa kwake hapa itakuwa ngumu sana kuwaridhisha wananchi walioko nje ya chama - Wananchi wapiga kura!
Kazi ilikuwa ndogo sana na hakika majibu ya hoja kama haya ndio yangetumiaka kumwangusha Wangwe..Nina hakika kabisa mkutano mkuu wa chama ungetengua kabisa kiti hicho maanake uongo ungeweza kuonekana wazi badala ya kurushiana madongo..
Siku zote ugonvi wa matusi na kupakana hakuwezi kumwonesha mbora na mwenye nidhamu wakati wote mnamwaga madudu ya ndani chumbani..watu watawachekeni nyote na pengine kujua siri nyingine za ndani ambazo hazikutolewa kwa nia njema.
Sasa nambie huyo Wangwe anayajua mangapi ya Chadema?..Umesikia wenyewe kina Lissu wakisema walimwamini na kumwona kama mtu mzuri sana, wakamsaidia kwa mengi, ati Wangwe yule wamjuaye sio huyu!... Leo tunakuja ambiwa mengi mabaya yanayorudi hadi wakati akiwa NCCR-Mageuzi tena akitokea Chadema!...
Tena basi huyu huyu mbaya amefikia kuwa makamu mwenyekiti wa chama KITAIFA!..something isn't right!
Mtu kama huyu binafsi ningemwogopa sana! sii kwa matusi wala kuwa kushindana naye maanake ni kupoteza utu wako na kuwa mnyama kama yeye.
 
MUSHI.
Wakabila una wajua wamerundika wabunge wa viti maalum toka KILIMANJARO TU.
na mtu akishika nafasi ya juu ya NGO yao wanakuja juu kulinda maslahi yao.wewe kwa vile MUSHI umeamua kuwa suppoter wa chama cha wachagga wenzako-Chadema. mie unayesema kuwa mkabila niliamua kuja huko ili kuondoka kanza hii mbaya. sasa umakamu upewe wewe iwe MBOWE.MUSHI,NDESAMBURO. MTEI,MBAtIA ETC.

Ushauri mngeweka na lugha ya kichagga iwe official language ya chama chenu au kila document iwe translated kwenye kichagga ili kurahisisha kazi.

Mimi sina chama na sijawahi kuwa na chama na sijawahi kuipenda ccm kwasababu nyingi tu mojawapo ni sera mbovu za Mwalimu na ujambazi wa MAHITA!
Hivi huyu naye mchagga?
Polisi ni wachagga tu?
Wakati alipopewa UIGP na MKAPA kwa kuwadhibiti wachagga na kumtowa Arusha hadi Kilimanjaro ambapo alitandika Mrema kisawasawa na mimi miongoni wakati wa kusukuma gari a MREMA NA MARANDO!
Wakati mwingine akitowa maneno ya kashfa dhidi ya wachagga?
Mkapa alikuwa akileta viongozi wasiopenda maendeleo wala haki wala hata mchagga kama mtanzania!
Mahita kamwe hakupata u IGP Simply because alifanya kazi dhidi ya majambazi...Mahita na yeye JAMBAZI!
Manyanyaso ya watu kama kina ZOMBE NA CHIKO!
Manyayaso ambayo yananikumbushia jamaa yangu mmoja aliwahi kumwuliza askari polis kama nchi imeshauzwa pale askari polisi alipomwuliza kitambulisho!
Miaka hio ya tisini tukiwa vijana wadogo na askari wana tu harass licha ya kwamba wanatufahamu fika!
Jamaa akamwuliza askari kwani umeona mimi ni mwarabu?
Askari akachukia kabisa na kumzoazoa!
Jamaa yangu ni Myakyusa!
Sasa mimi nakwambia hivi...Chuki yako ya kikabila inaweza kukubaliwa na washenzi wachache...Na mkifanya hivyo...Mulewe na sisi tutakuja na COALITION A WAZALENDO YENYE KUJALI UTANGANYIKA KWANZA...NA TUTAPAMBANA!
 
Jmushi1,
Mkuu samahani nikuulize kitu kimoja...
Wewe mchagga?.. kama ni mchagga ilikuwaje uwe Mchagga na sio Mtanzania kwanza! Uchagga huo umeupata vipi kwa baba au baba na mama!
 
Ushauri mngeweka na lugha ya kichagga iwe official language ya chama chenu au kila document iwe translated kwenye kichagga ili kurahisisha kazi.
Hapo kwenye kusema lugha ya kichagga iwe ya chadema pia bado unauonyesha huo ugagaggigikoko wako!
Mbowe ni Mmachame.
Ndesamburo nafikiri ni Marangu..Sasa lugha zipi kati ya hizo ziwe za CHADEMA?
 
Jmushi1,
Mkuu samahani nikuulize kitu kimoja...
Wewe mchagga?.. kama ni mchagga ilikuwaje uwe Mchagga na sio Mtanzania kwanza! Uchagga huo umeupata vipi kwa baba au baba na mama!

Mimi ni mchagga lakini siyo kabila moja na mbowe wala ndesamburo!
Na ndiyo maana namwambia HUYU FALA aache kusema wachagga hivi wachgga vile!
Hata Mramba ni mchagga wa ROMBO.
Lugha za makabila hayo ni tofauti.
Kwahiyo haina maana kabisa kushupalia hoja ya ukabila hapa!
Msiwapotoshe wananchi kabisa!
Hatutakubali in any means!
 
Mgagagigikoko,

Mkuu ktk hili mimi nalishikia bango haswa!.. haiwezekani huyu mtu atokee huko alikotoka awe mzigo kwetu lazima ipo kitu hapa. Labda walifikiria kwamba malaya anaweza kubadilika akipewa mapenzi ya kweli hali Umalaya sii mapenzi ni hulka ama kisu tuuu..
Nimerudia kusoma malalamiko ya huyu jamaa mkuu yanatisha!..Kwa kila mbinu inayotumika ktk kujikinga mimi naona kama wakuu wa Chadema ndio kwanza wanachemsha zaidi. Hoja zilizojibiwa kwa uhakika ni hiyo ya Ruzuku na Uteuzi wa Wabunge..lakini ktk kufukuzwa kwake hapa itakuwa ngumu sana kuwaridhisha wananchi walioko nje ya chama - Wananchi wapiga kura!
Kazi ilikuwa ndigo sana na hakika majibu kama haya ndio yangetumiak kumwangusha Wangwe..Nina hakika kabisa mkutano mkuu wa chama ungetengua kabisa kiti hicho maanake uongo ungeweza kuonekana wazi badala ya kurushiana madongo..
Siku zote ugonvi wa matusi na kupakana hakuwezi kumwonesha mbora na mwenye nidhamu..watu watawachekeni nyote na pengine kujua siri nyingine za ndani ambazo zilitolewa kwa nia njema.
Sasa nambie huyo Wangwe anayajua mangapi ya Chadema?..Umesikia wenyewe kina Lissu wakisema walimwamini na kumwona kama mtu mzuri sana, wakamsaidia kwa mengi, ati Wangwe yule wamjuaye sio huyu!... Leo tunakuja ambiwa mengi yanayorudi hadi wakati akiwa NCCR-Mageuzi tena akitokea Chadema!...Tena basi amefikia kuwa makamu mwenyekiti wa chama KITAIFA!..
Mtu kama huyu binafsi ningemwogopa sana! sii kwa matusi wala kuwa kushindana naye maanake

Mambo haya yanataka hekima na busara na uwe tayari kupokea pande zote mbili za shilingi,

tatizo wengi wenu humu mna upande wenu na majibu yenu, mnafikiri mnamuangamiza mtu kumbe ndio kwanza mnazidi kumjenga na kutufanya watu kama sisi tuliokuwa tukisita na kusema kuwa pale ni NGO ya watu fulani,kuyasadikisha maneno yetu, kwa nguvu kubwa ISIYOHITAJIKA kutumiwa kumuangamiza Wangwe, wanaofikiri wanatengeneza PR za wachagga na Chadema ndio wanakipaka mavi chama na wachagga, kutulia au kulinyamazia hili suala ilikuwa jambo zuri lakini kufungua thread za kusema CCM kuna udini kama majibu ya hoja za Wangwe sio sahihi,

Ukiulizwa kwanini unatizamia darasani huwezi kujibu kuwa hata MKANDARA alikuwa anatizamia jibu swali uliloulizwa halafu kwa wakati wako sema ulichonacho moyoni kwako, kutizamia kwa Mkandara hakukufanyi kutizamia kwako kuwe halali, hapa ndio penye kosa, na wewe kama mwanachama waambie wenzako kuwa kuna hoja huwezi kuziziba au kujaribu kukanusha tu bila kuzitafuti ufumbuzi.

wabunge wa Chadema hawakuchaguliwa na taratibu yeyote ya kidemokrasia zaidi ya kusemwa kuwa mtoto wa Ndesamburo kapewa ubunge kwa vile baba yake alitoa millioni mia moja, matokeo yake mmepeleka wabunge bungeni wanaopiga usingizi tu bungeni sijawahi kusikia wameongea bungeni zaidi ya wale waliochaguliwa na wanachi.

kama mama Clinton angekuwa chadema basi asingepigiwa kura wasemaji wa chadema wangesema alikuwa ikulu kwa muda na mume wake amechangia sana chama hivyo apite tu bila kupingwa,lakini demokrasia imefanya kazi yake hata ethinic minoroty OBAMA kama alivyokuwa Wangwe ethinic minority ndani ya Chadema lakini anabanwa amepata tiketi ya DEMOCRATIC wameonesha demokrasia halisi kwa kumpa ethinic minority tiketi wametizama merit za wanachama wa kawaida wanataka nini, wamekubali kuRISK kuweka mweusi

lakini kuhakikisha wanalinda kauli mbiu yao ya demokrasia ambayo chadema wameshindwa, kwanza kwa kuwabana wanachama kuchagua wawakilishi wao, pili wakina baba wamewasemea wanawake wa Chadema na kuwachagulia watu na zaidi kuwanyima wana chadema wenye mikoa mingine kupata wawakilishi,ukihoji unajibiwa nafasi zilikuwa sita utagawa vipi kwenye wilaya 120, walihoji watu mikoa sio wilaya, hata kama nafasi sita jibu sio kuwapa mkoa mmoja ndio iwe fair play.
 
Back
Top Bottom