Rostam Aziz kugeukia Waislamu, Kuibua wengine CHADEMA

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Rostam Aziz kugeukia Waislamu, Kuibua wengine CHADEMA

Nilisema hapa miezi mingi nyuma kuwa Rostam kumtumia Chacha Wangwe kuibomoa CHADEMA. Watu wakasema nasema udaku. Leo CHADEMA ineshavikwa ukabila na ubadhirifu wa ruzuku. Ni matokeo ya kikao cha RA na Wangwe Kempinsiki Hoteli na baadaye kikao kwenye ile nyumba ya Kinondoni mitaa ya jirani na Balozi Wa Marekani hapa Tanzania.

Nilesema hapa Rostam alivyomnunua yule aliyejiita kiongozi wa CHADEMA Igunga kutoa tamko la kumwuunga mkono kugombea Ubunge 2010, lakini nikaweleza kwamba baada ya hapo mkakati utakaofuata ni wa kuwatumia viongozi wa dini. Maneno yangu yamedhihirika kwa Rostam kulitumia kanisa la KKKT Kinondoni. Sasa habari kutoka duru la wanamkakati wa Rostam ni kwamba sasa atawatumia Viongozi wa Kislamu hivi karibuni na atahamia kwa watu mashuhuri Tanzania. Na katika mkakati wake huo amefanikiwa kuwanunua hata baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi katika vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vikimuanika zaidi vya Thisday/Kulikoni na Tanzania Daima. Na vile vilivyokuwa katikati vya Mwananchi na Nipashe. Na ameongeza nguvu zaidi katika vyombo anavyovitawala vya Majira na Mtanzania.

Kwa upande mwingine, ule mkakati niliousema siku nyingi wa kumtumia Chacha Wangwe umefanyiwa marekebisho kwa kuwa malengo hayafukiwa kama ilivyopangwa. Awali ilipangwa Chacha Wangwe atumie kikao kilichofanyika Dodoma 28 Juni, 2008 kutoa hoja ya kutaka Kamati Kuu ipige kura ya kutokuwa na imani na Dr Wilbroad Slaa kama Katibu Mkuu, ili akiondolewa Slaa aondoke na Sekteratiati yake yote wakina Zitto, Tundu Lissu, Mnyika, Tumbo na wengineo; Mbowe abaki mwenyewe na iwe rahisi kummalizia.

Katika Mkakati huo ilipangwa kama kura za kutokuwa na imani hazitatosha ilikuwa Chacha Wangwe atoke nje na kusema kuwa Mbowe ametumia udikteta kuzuia hoja hiyo, na ajitokeze mbele ya umma na hoja hizi hizi ambazo ameumua kuzitoa sasa. Angefanya kama anavyofanya sasa lakini ujumbe wake ungekuwa ni kuwa Mbowe anamlinda Dr Slaa ambaye ameshindwa kazi na anaruhusu ubadhirifu. Lengo la Mkakati mzima likiwa ni Dr Slaa kupoteza imani kwa wananchi na hatimaye mjadala wa ufisadi kuonekana hauwahusu watu 11 wa CCM aliowataja kwenye list of shame bali hata yeye mwenyewe. Kwa bahati mbaya au nzuri, mtu mmoja wa Rostam ambaye ni mpenzi wa Dr Slaa akatoa siri nyingi kwa Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA.

Suala hili likaingizwa kwa Kamati ya Wazee wakina Mtei, Profesa Baregu, Balozi Ngaiza, Makani na Ndesamburo, hata hivyo wazee wakaamua yote yawekwe kama kumbukumbu na kuamua kupatanisha hasa baada ya Chacha kuonyesha urafiki na kujirudi. Nyuma ya pazia Chacha akaendelea na mpango wake kwa kwenda kumng’oa Dr Slaa Dodoma, na tayari Ballile alitumwa Dodoma na Rostam kuratibu habari hiyo. Lakini mambo yakabadilika Dodoma pale ripoti ya Kamati ya Wazee ilipowasilishwa Dodoma, Chacha akawageuka Wazee kuwa hakukubaliana nao yaishe, akatoa hoja ya kumshambulia Dr Slaa; kikao kikamgeuka yeye. Akachukia na kumtukana Baregu. Akamtukana pia Mama Chiku Abwao matusi ya nguoni kwa kutangaza kuwa pamoja na kuwa alimuunga mkono na kumpigia debe kuwa Makamu katika hilo hakubaliana nao.

Matusi yake yakamuudhi Tundu Lissu aliyetaka achukuliwe hatua za kinidhamu, Chacha akainuka na kumvamia Tundu Lissu kutaka kumpiga- Board Guard wa Mwenyekiti akapambana nae na kumzuia.

Ndio maana mtakumbuka kuwa habari ya Mtanzania iliyoandikwa kabla ya Chacha kusimamishwa, huku Ballile akijua kuwa matarajio ni Slaa kusimamishwa, wakati kikao kinaendelea mpaka usiku wa mananeo Ballile akaandika Habari ya Mambo ambayo alitarajia yangetokea kikaoni lakini hayakutokea. Alitarajia pangekuwa na mjadala mkali kuhusu hoja ya Ruzuku lakini kwa bahati mbaya suala hilo halikujadiliwa kama ilivyotarajiwa. Baaada ya Mkakati huo kushindwa, Rostam na Ballile wakaamua kutumia mkakati wa “CHADEMA yamwaga Mboga, Chacha Amwage Ugali”. Pamoja na Mkakati huo kufanikiwa kuichafua CHADEMA, bado haujaweza kutimiza malengo ya awali. Hivyo, wakabadili Mkakati na kukubaliana kwa Chacha Atangaze Wazi kuwa lengo lake ni Kugombea Uenyekiti na Kumwondoa Mbowe na Dr Slaa.

Mkakati huo umeanza ku-back fire’ kwa kuanza kuwaunganisha waCHADEMA wote makini na hata wapenzi kwa kuanika rangi halisi za Chacha Wangwe. Jana kimefanyika kikao kingine, tathmini imefanyika ya jinsi Mkakati wa kuwatumia KKKT Kinondoni ulivyofanikiwa. Kwa ujumla imeonekana Mkakati umefanikiwa lakini kuna hofu viongozi wa juu wa kanisa la KKKT hususani Askofu Malasusa wanaweza kuchukia na kutoa onyo kali kwa wenzao wa Kinondoni.

Suala hili linajengwa uzito zaidi kwa jinsi ambayo Spika Sitta amechukizwa na habari za kanisa hilo kutumika. Ili kuzuia hali hiyo, imekubaliwa Rostam afanye kwa haraka tukio na Waislamu ili Wakristu waoone dini zote zinakubaliana nae na kumuona ni mtu msafi.

Kwa upande mwingine, sasa Rostam Aziz ameamua kubadili mkakati wa jinsi ya kuwabomoa CHADEMA na sasa pamoja na Chacha Wangwe kukusudia kwenda mahakamani na kukata rufaa kwenye baraza kuu, Rostam Aziz amepanga mkakati mwingine unaoitwa “GAWA, TAWALA”, chini ya mkakati huu ‘mashujaa’ kadhaa watalipwa kujitokeza kuwa mstari wa mbele kuungana na Chacha, tayari Wangwe na Ballile wamepewa fungu la fedha kuingiza watu kuunda kundi lao. Mpaka sasa katika Orodha wako Mziray, Shilembi. Lyimo, Shilungushela. Chini ya azma hiyo, kikwazo kikubwa ni kukosa home base baada ya Tarime kutoa msimamo wa wazi wa kumpinga na kueleza wazi kuwa wao wanapokea ruzuku ya Laki Nne kila mwezi kutokana na moja ya wilaya iliyofanya vizuri zaidi katika matokeo ya uchaguzi 2005.

Baada ya Habari hiyo ya Nipashe, Chacha Wangwe alipiga simu kuwatisha viongozi hao lakini viongozi hao wakamweleza kuwa msimamo wao ni msimamo pia wa madiwani wengi wa CHADEMA na Mwenyekiti wa Halmashauri(Kama Meya) wa Tarime ikikumbukwa kuwa CHADEMA ni chama tawala huko. Baada ya Kadhia hiyo, Jana Rostam alimwelekeza Chacha Kufanya mapinduzi Tarime kwa kuwaondoa viongozi hao. Jana hiyo hiyo Chacha Wangwe akampigia simu Chacha Okong, yule aliyekuwa kampeni manager wake kwenye uchaguzi mkuu 2005 ambaye pia alikuwa katibu wa wilaya a;iyehama toka CHADEMA kwenda CCM baada ya Chacha Wangwe kushindwa kuendeleza kazi za chama na pia kuwatelekeza kabisa wapiganaji wenzake na kukaa Dar es salaam.

Chacha Wangwe amemuahidi milioni 10 kama atarejea chama chake cha awali cha CHADEMA na atahakikisha kuwa anarudi kwenye nafasi yake ya Katibu wa Wilaya na kutoa kauli ya kuumuunga mkono. Fedha hizo ni chini ya kiwango ambacho Rostam aliahidi kitolewe kwa ajili ya zoezi hilo. Kuna mengi yanaendelea hivi sasa, na tutarajie mengine zaidi wiki hii. Mkakati huu ni sehemu ndogo tu ya mpango kabambe wa Rostam wa kujisafisha na kuwaita watu wengine zaidi mafisadi ili kugeuza mjadala wa ufisadi nchini Tanzania.

PM
 
Washindwe na walegee!

Kweli CHADEMA ni chama makini,ndiyo maana nasema CHADEMA walichukua uamuzi muaafaka kumtimua huyo msaliti
 
Ona sasa mafisadi walivyoumbuka.Unajua siku zote Shetani akikutumia kutenda maovu siku ya mwisho lazima akuaibishe.

Ona alivyoaiabisha hao watumishi wake sasa.
 
Basi huyu chacha ni mtu hatari, duh anawatukana matusi ya nguoni na kutaka kuwapiga baadhi ya viongozi wenzake! Kama hii habari ni ya kweli na kweli tupu basi huyo sio kusimamishwa tu, bali anafaa kufukuzwa hata uanachama.

Hafai kuwa kiongozi wa wananchi, kiongozi mzuri haongozwi na jazba, bali ni msikivu, mvumilivu na anayeshaurika.
 
Na hata makosa mengine ni ya jinai.Watu wa aina hiyo ndiyo marafiki wa CCM na Rostam Aziz.No wonder serikali nzima ina-misbehave!
 
huyo ndo chacha wangwe! kama kweli rostam yuko nyuma ya pazia hili, ndo kwanza filamu imeanza, tujiandae
 
PM shukrani kwa taarifa hiyo, baadhi ya uliyoandika yamekwisha tokea, sasa tusubiri hayo mengine, endapo yatatokea basi Chacha si Mpinzani na si rutuba kwa CHADEMA wamfute uanachama kabisa, jimbo lake litapata tu mwakilishi mwingine. shame on you Chacha Wangwe!!!
 
tunasubiri kwa hamu kuona rostam azizi, baada ya kuingoza ikulu kwa remote, sasa anataka kuongoza vyama vya siasa, dini, mh! kwa kweli tumezidisha ubwege
 
Rostam ni mtu hatari sana, na kuendelea kusubiri ni sawa na kusubiri janga ama balaa. Hivi anatoroka lini? kama bado sana inabidi atimuliwe, ni mnafiki, mfitini, fisadi, ndumilakuwili and so on. Hivi wataallam hakuna namna yeyote legal inayoweza kumuwajibisha Rostam? anatuchezea akili watanzania na kibaya zaidi anacheza na akili ya Rais!
 
Hii habari ni ya kupikwa maana umeunganisha vipande vipande

Mimi mwenyewe ndio nilianza kuandika Lisu amwaga Ugali Chacha amwaga mboga baada ya siku kama moja mbili nikaona kichwa cha habari hichohicho ktk gazeti wamekirekebisha kidogo tu baada ya Lisu wakaandika CHADEMA.

Rejea kwenye maada ya KLHnews Lisu chacha walongwa iliyoandikwa na mwanakijiji.

Haya mambo ya uzushi ni ya nini?? Jamani

Mimi nakuhakikishia sina element na chama chochote na ni mda sasa nimetoka hapo nyumbani kama wataka uhakika +48697461457 niandikie nami nikujibu.
 
yale ya anne kilango na EPA yakumbushwa teh teh teh teh

Hapana mama
Nia si kutaka kuonyesha nani kaanzisha malengo sio hayo
ila nikutaka kuonyesha kua habari ni ya kupikwa maana huo mpango anaouuita umeandaliwa wa CHADEMA kumwaga bonga na chacha ugali si kweli maana Magazeti wanaingia humu JF na wanaandika habari zao nyingi kutoka humu JF.
Sasa kuita mkakati wakati source ya hilo jambo inaieleweka ni upotoshaji usio na msingi.
 
Sasa Chadema mnangoja nini kumfuta Wangwe uanachama? angalieni vinginevyo ataambukiza wengi.
 
Hapana mama
Nia si kutaka kuonyesha nani kaanzisha malengo sio hayo
ila nikutaka kuonyesha kua habari ni ya kupikwa maana huo mpango anaouuita umeandaliwa wa CHADEMA kumwaga bonga na chacha ugali si kweli maana Magazeti wanaingia humu JF na wanaandika habari zao nyingi kutoka humu JF.
Sasa kuita mkakati wakati source ya hilo jambo inaieleweka ni upotoshaji usio na msingi.

asante kwa maelezo yako. Una uhakika gani kama habari hii ni ya kupikwa ilihali hauko nyumbani Tz? je ukigeukiwa na kuambiwa kuwa habari uliyotoa wewe ndio ulipika?

I dont know ila kama maelezo ya PM ni kweli, basi Chacha ni mtu hatari sana, hafai kuwa kiongozi!

Hebu nipatie hiyo habari ambayo si ya kupikwa!
 
Sasa Chadema mnangoja nini kumfuta Wangwe uanachama? angalieni vinginevyo ataambukiza wengi.

hicho ndicho kinashangaza wengi ,kwa njisi Jinsi chadema wanavyoelezea vitendo vya wangwe ilikua sio tu kumfuta uanachama bali kumpeleka ktk vyombo vya sheria.
 
Hapana mama
Nia si kutaka kuonyesha nani kaanzisha malengo sio hayo
ila nikutaka kuonyesha kua habari ni ya kupikwa maana huo mpango anaouuita umeandaliwa wa CHADEMA kumwaga bonga na chacha ugali si kweli maana Magazeti wanaingia humu JF na wanaandika habari zao nyingi kutoka humu JF.
Sasa kuita mkakati wakati source ya hilo jambo inaieleweka ni upotoshaji usio na msingi.

Soma vizuri ujumbe wangu. Labda niongezee tu. Mara baada ya Mbowe kuanika sababu za Kamati Kuu kupiga kura ya kutokuwa na imani na Wangwe. Kikao kilifanyika cha kutafakari nini Chacha afanye. Ni katika kikao hicho ndipo Chacha alipashauriwa na kuambiwa kama wao wamemwaga mboga wewe mwaga ugali kabisa. Na huu ndio ukawa mkakati na Chacha akaambiwa apite kwenye vyombo mbalimbali vya habari na ujumbe aliondakiwa na Ballile. Alienda Majira na Mtanzania wakampa uzito. The Citizen wakafanya naye mahojiano lakini hawakuandika. Wengine wakaona its too much. Hawakatua kabisa. Msemo wa Mboga na ugali wewe siye mwanzilishi wake, ni msemo wa miaka mingi sana katika kiswahili. Unless kama wewe ni kikongwe

PM
 
hicho ndicho kinashangaza wengi ,kwa njisi Jinsi chadema wanavyoelezea vitendo vya wangwe ilikua sio tu kumfuta uanachama bali kumpeleka ktk vyombo vya sheria.

Kama unabisha kuwa Chacha hakuamka kutaka kumpiga Tundu Lissu au kama hakumtukuna Chiku aku kusema lugha mbaya kwa Baregu hebu waulize wahusika niliowataja. Wote hawa nimeongea nao kuthibitisha habari yangu. Chacha 0782488133, au 0713488133. Tundu Lissu 0754447323 na Baregu 0713506382. Mtu pekee ambaye sijampata ni Chiku Abwao. Mwenye namba ya Mama Chiku anipatie tafadhali

PM
 
vitu vingine vinaudhi kweli sasa kama ni chacha ni hatari si afukuzwe tu uanachama!sasa kwa nini muendelee kufuga kidonda?
 
Kama unabisha kuwa Chacha hakuamka kutaka kumpiga Tundu Lissu au kama hakumtukuna Chiku aku kusema lugha mbaya kwa Baregu hebu waulize wahusika niliowataja. Wote hawa nimeongea nao kuthibitisha habari yangu. Chacha 0782488133, au 0713488133. Tundu Lissu 0754447323 na Baregu 0713506382. Mtu pekee ambaye sijampata ni Chiku Abwao. Mwenye namba ya Mama Chiku anipatie tafadhali

PM

Mimi nimeshakubali mkuu

Lakini kwa vitendo vya CHACHA kuendelea kua mwanachama na mbunge wenu ni hatari sana ,HUyu anastahili kutimuliwa uanachama na kuchukuliwa hatua za kisheria
 
Back
Top Bottom