Rostam Aziz anavyochezea akili za Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam Aziz anavyochezea akili za Watanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ntemi Kazwile, Sep 7, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mwanzoni mwa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM mwaka 2005, wengi walitarajia Dr Salim Ahmed Salim angelichaguliwa kwa kura nyingi kutokana na ukweli kwamba yeye ndiye alikuwa anaonekana kuwa na sifa zote - hakuwa na makundi, hakuwa na kashifa nyuma yake, utendaji kazi wake kwa ujumla ulimuainisha kama Rais mtarajiwa baada ya Benjamin Mkapa.

  Hata hivyo, magenge ya majasusi yakiongozwa na Jangili Rostam yalijua kama hilo lingelitokea wangelijikuta ama wanakimbia nchi au wanapata vyumba katika magereza yetu. Hawakutaka vyote viwili na walijua kuwa mtu waliyemtaka achukue Urais hakuwa na sifa za kiutendaji, kwa wengi Kikwete alionekana kama brother man fulani ambaye mahala pake ilikuwa ni vijiwe vya mjini na kwenye kumbi za starehe, haiba yake na utendaji wake wa kazi wa nyuma haukuonyesha kuwa huyu alikuwa rais mtarajiwa.

  Wafuasi wake walilitambua hilo vyema na wakabuni mbinu ambazo zingelimuuza huyu kwa wapiga kura (walinunua vyombo vya habari na kuwalipa wanahabari kulifanikisha hili), lakini pia walibuni mbinu za kuwaengua wagombea wengine wote waliokuwa na sifa stahili na ambao walionekana kuwa ni kikwazo kwa mgombea wao. Katika wagombea wote wa kura za maoni, Dr Salmin ndiye alikuwa tishio kubwa na walifanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha kuwa wanamchafua ipasavyo.

  Wahariri wa magazeti walilipwa kuhakikisha kuwa habari za wagombea zilimsifia mgombea wao, Kikwete, propaganda za chini chini zilipenyezwa na kutuaminisha kuwa Salmin alishiriki kumuua Karume Snr na alikuwa hafai kupewa nchi. Tukaambiwa kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu, akina sisi tulijua tunapotoshwa na tuliwapuuza waliokuwa wakimsifia, lakini walifanikiwa kuwavuna wengi na wakafanikiwa kumuweka Kikwete madarakani kwa kura nyingi.

  Kwa sababu Dr Salmin hakujiandaa kwa siasa za kihuni namna hii, aliangushwa vibaya na matokeo yake wote tunayafahamu.

  Baada ya kuingia Ikulu walibuni mbinu mbalimbali za kuhakikisha kuwa wanavuna ipasavyo, wakaja na Richmond (baada ya kufanikiwa kuchota za EPA).

  UCHAGUZI wa 2010 umeleta changamoto zinazofanana na zile za 2005 lakini sasa wamekuja na mbinu mpya.

  Baada ya kuikagua CV ya Mh Slaa wasione mawaa wala dosari yoyote katika utendaji kazi wake wamempata akiishi na mama aliyeolewa na kuachana na mme wake wa awali na kulifanya kuwa mtaji wao mkubwa.

  Wamewahamisha watanzania kutoka kwenye mijadala ya muhimu na ya msingi ya kuangalia ni nini wagombea wanataka kuifanyia Tanzania na wanaweza kiasi gani, wametuhamisha kutoka kwenye mijadala ya je haya anayosema Kikwete na CCM watayafanya wanaweza na wanaoutashi wa kuyafanya? Je ni kwa nini hawakuyafanya au hata kuonyesha jitihada za kutaka kuyafanya kwa kipindi walichokuwa madarakani miaka mitano inayomalizika? Wametukosesha fursa ya kutafakari na kujadili ni yupi kati ya wagombea wa upinzani anaweza kuyatekeleza yale anayoyasema? Je Dr Slaa ataweza kulishughulikia suala la ufisadi kwa nguvu zile zile alizolishughulikia akiwa mbunge wa upinzani? Je anao utashi na uwezo kuzitatua kero zilizoishinda serikali ya CCM?

  Badala yake wametupeleka kwenye mijadala ya kitoto na isiyotusaidia kupata kiongozi atakaye shughulikia kero zetu, sasa tunajadili ndoa mfu iliyofufuliwa na tamaa ya pesa, ndoa ambayo haitusaidii kupambana na umasikini wa taifa letu, tunajadili mambo yanayojaza kurasa za magazeti ya UDAKU!

  Kama taifa tumejishusha na tunajidhalilisha tunapoacha kujadili mstakabali wa uchumi wetu, tunajidhalilisha tunaposhindwa kujadili hoja za wagombea na ilani za vyama vyao, tumekuwa dampo la siasa za maji taka na tunachekelea. Kuna wengi wetu wanafurahia namna ambavyo Dr Slaa amebanwa wasijue kuwa wanaoleta hizi habari wanataka waendelee kutunyonya na kutuibia, tumekuwa kama mazuzu na bado hatujaligundua hili.

  Tanzania inasifika nje ya nchi kwa nchi yenye wasomi kuliko majirani zao lakini ikiwa ni nchi iliyo nyuma kuliko wote hao kiuchumi (hata Msumbiji itatupita muda si muda) licha ya kuwa na rasilimali lukuki.

  Tunaongoza kwa mataifa yanayopokea misaada katika nchi zinazoendelea na tunajisifu kwa hilo, tunajisifu tunaposema kuwa Wamarekani wameshaizinisha pesa kwa ajiri ya kutatua kero zetu, tunafurahia huku bajeti yetu ikiendelea kutegemea hisani ya wafadhili.

  Tumeshindwa hata kuwa na vitu vya kujivunia (Kenya wanajivunia Katiba yao mpya na shirika lao la Kenya Airways) sisi tunajivunia kuyauza mashirika yaliyotuletea heshima kama taifa na tumeridhika, tunataka kuirudisha madarakani serikali hiyo hiyo iliyoshindwa kuzitatua changamoto za taifa hili, tunakubali kutumika kama mifagio ya choo ambayo haiwezi hata kutunzwa sebuleni, sehemu yetu ni huko huko ****** na tunafurahia!

  Wakati Rais Clinton akikabiliwa na tuhuma za ufusika akiwa Ikulu, wananchi waliowengi wa Marekani walimuangalia Clinton kama mtendaji mkuu wa nchi na si kama mwanaume aliyeisaliti ndoa yake. Waliangalia ameifanyia nini Marekani kabla ya kuangalia maisha yake ya ndoa. Mwisho wa siku walizipuuza tuhuma zile na kumuunga mkono Rais wao.

  Ninawasihi watanzania wote tuzipuuze tuhuma hizi za maisha binafsi ya Slaa na tuangalie utendaji wake wa kazi. Tusijishushe kiasi kile na kuwaruhusu maadui wetu watushinde kwa kututupia pipi, tunastahili zaidi ya hapo!
   
 2. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  linasaidiwa na haramia lilokubuhu - Kinana
   
 3. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,819
  Trophy Points: 280
  Lord have mercy!
  Yaani mtu mmoja anatuchezea akili sisi watu milioni 40!!
  Wabongo tuna matatizo ya akili:becky:
   
 4. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  This time wameula wa chuya, waTZ hatudanganyiki kirahisi tena hivyo.
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Kwa mtizamo wa Rostam Aziz, Watanzania ni Wapumbavu wanaoweza kusikilizishwa upumbavu na wakauzikiliza huo upumbavu na wakaendelea kuishi na upumbavu wao wakati yeye na genge lake wakila pepo.
   
 6. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Huu ndo ukweli. Yaani jamaa anatuona WaTZ mazezeta wenye kudanganywa na kupewa sahani ya pilau ya kula mlo mmoja wakati yeye na mafisadi wenzake wakiendelea kuuhujumu uchumi wa taifa letu. Hatudanganyiki.
   
 7. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kama ni suala la kuchafuana kwa mtindo huu basi CCM wakubali tuanze kuanika uozo wa viongozi wetu akiwemo, JK, Lowasa n.k wanavyotembea na wake za watu. Data tunazo. JK akiwa waziri wa madini alishawahi kumpa mtu scholarship ya kwenda kusoma nje ya nchi ili achukue mke wake na alifanikiwa kufanya hivyo. Lowasa naye kafanya hivyo na hivi sasa anatembea na wake za watu wengi tuu tunayajua yote haya.
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Bangi za watawala
   
 9. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  jk, lowasa, na wengine pia wamechezewa na rostam, wakati jk, lowasa wakichapa maisha na akina chifupa, na wengine na huenda kudatishwa mdudu rostam anavuma kwa kwenda mbele, ngoja waanze vikohozi na kunaguka kifafa
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Chadema ni wasaliti wa maendeleo ya nchi hii ,ilikuwaje Slaa akafanya Uturn kuurudia Uraisi wakati tayari alikwisha kutangaza kugombea ubunge na wananchi walikuwa wameshajipanga kuiangusha CCM kama mgombea Lipumba angeachiwa awe mgombea pekee ? Sasa wacha Slaa abebe price ya undumila kuwili ,na kwa kikwetu tunasema mtaka yote hukosa yote au mtaka yote moja humponyoka ila kwa hili Slaa yamemponyoka yote ,ubunge ndio hana na Uraisi haupati ,na sio haupati haukaribii kabisa.

  Hiyo mada hapo juu ni sawa kabisa lakini ndani yetu kuna watu kama akina Slaa ,unafikiri tutavuka kwa karibu ? No way to get out of this prism.
   
 11. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM does not trumpet xenophobia like other political parties!
  Rostam has done a lot of good both for his electoral district-Ingunga and this country. He deserves appreciation and respect. He's one of the most hard working local businessmen in Tanzania. He's is clean and very smart, contrary to the allegations of grand corruption that the opposition leaders have been voicing about. The people of Ingunga like him and that's the reason why he's been elected year in year out. Tanzania needs people like Rostam in order to take this ailing economy to the next level. Chadema and CUF stop being anti-business and hate Tanzanians of Asian origin. You can file charges to the court of law and not during the campaigns
  Vote CCM!! Long live JK !!!!!!!!!!!!!!!!
   
 12. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM does not trumpet xenophobia like other political parties!
  Rostam has done a lot of good both for his electoral district-Ingunga and this country. He deserves appreciation and respect. He's one of the most hard working local businessmen in Tanzania. He's is clean and very smart, contrary to the allegations of grand corruption that the opposition leaders have been voicing about. The people of Ingunga like him and that's the reason why he's been elected year in year out. Tanzania needs people like Rostam in order to take this ailing economy to the next level. Chadema and CUF stop being anti-business and hate Tanzanians of Asian origin. You can file charges to the court of law and not during the campaigns
  Vote CCM!! Long live JK !!!!!!!!!!!!!!!!
   
 13. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  pamoja na hayo yote tunasema sasa hivi watanzania hatudanganyiki, cha muhimu kama wengi walivyoshauri sehemu mbali mbali (kama Rev Kishoka) ni kuwa kwa sasa Dr Slaa a-concentrate na sera na mapungufu ya CCM kama chama na JK kama mgombea wake, hizo propaganda za akina Makamba amwachie Marando, Shibuda, Mpendazoe na Tindu lissu najua hapo JK atapata mchecheto mpaka aanguke tena, na ukizingatia sasa hivi CCM wamempa JK ratiba tight bila kupumzika hapo lazima pressure ipande ishuke. Kanyaga twende Dr Slaa hakuna kulala mpaka kieleweke, manyang'au mpaka yashindwe 31 octoba. Go Slaa go.
   
 14. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Wandugu watanzania wameshtuka issue hii ya Majangili.

  Wengi sasa wanatumiana message kupitia simu zao za kukataa CCM; mwanga unaanza kuonekana.

  Tuhamasishane kupinga CCM;

  Siku hizi nawatumia marafiki na jamaa zangu message ya kuipigia CHADEMA na DR Slaa kura
   
 15. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  wewe Mhindi andika Kiswahili, it's not even Ingunga, it's Igunga. mmtuibia muda mrefu, ndiyo huwa mnakimbia wakati wa uchaguzi! You know you are guilty, but your days are numbered! Kodi hamlipi, ndiyo maana kazi yenu ni kuipigia debe CCM at the expense of bonafide Tanzanians! Why are u always foot loose if you are Tanzanians, kumbuka mali zetu zitarudi! Kwa nini hamuishi kwenye makazi ya wazawa, mnaopgopa nini? Angalia sana, wengine tuna bifu na nyie pia!
   
 16. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,501
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  shigongo kawaambuiza watanzania udaku badala ya kula daku sasa wanakula udaku
   
 17. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  nikipewa ujaji wa mahakama kuu naanza na kazi hii,
  1. ROSTAM AZIZI, KIFUNGO CHA MAISHA JELA NA VIBOKO 2 KILA SIKU KWA UHUJUMU UCHMI
  2. ABDURLAHAMAN KINANA, KIFUNGO MIAKA 90 JELA KWA UJANGILI
  3. JK, KIFUNGO GEREZANI MIAKA 25 KWA KUTOWAJIBIKA KWA MADARAKA YAKE
  4. EDWARD LOWASSA , KUNYONGWA HADI KUFA
  5. PATEL NA SOMAIYA, KUYONGWA HADI KUFA
  6. ANDREW CHENGE NA BEN MKAPA, KIFUNGO CHA MAISHA JELA
  7. endelezeni list

  haya yote yatafanyika kama tu Watanzania tutaruhusu mabadiliko ya kweli kwa uongozi wa Taifa letu.
   
 18. Charles Mtekateka

  Charles Mtekateka Verified User

  #18
  Sep 8, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 310
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Punguzen hasira !
   
 19. M

  MathewMssw Member

  #19
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku moja nchi itakuwa huru na mafisadi!
   
 20. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  PhD, pamoja na kuwa sipendi siasa za maji taka na kuchafuana, ila comment za hapo juu halahala. Huwezi kuhukumu kifungo cha maisha jela au kifo bila kuwa na kesi za msingi.

  Labda useme, nikipewa nafasi ya kuwa Jaji Mahakama Kuu; nitahakikisha kesi zote za uhujumu uchumi kwa taifa hili zinafufuliwa na kuchunguzwa upya ili HAKI ipatikane.
   
Loading...