Rostam Aziz ahusishwa ufisadi mabilioni ya Japan

Rostam Aziz ahusishwa ufisadi mabilioni ya Japan

Ni za Mfuko wa Chakula
Zilizochotwa ni bilioni 200
Toleo Na. 090
Rostam Aziz ahusishwa ufisadi mabilioni ya Japan

Na Waandishi Wetu
Mwanahalisi

MBUNGE wa Igunga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz, ni miongoni mwa wafanyabiashara kadhaa wanaotajwa kufilisi Mfuko wa Chakula (FACF) baada ya kuchotewa na serikali zaidi ya Sh. 200 bilioni.

Taarifa za ukakika zilizothibitishwa na Serikali, zinasema Rostam alichotewa mabilioni hayo ya shilingi kupitia kampuni yake ya African Trade Development.

Mfuko huo unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Japan.

MwanaHALISI imeelezwa kwamba Rostam, pamoja na wafanyabiashara wenzake kadhaa wameshindwa kurejesha fedha hizo kama walivyotakiwa na serikali.

Kampuni ya Rostam ilichotewa zaidi ya Sh. 2.012 bilioni Novemba 1999, lakini hadi mwishoni mwa mwaka jana, fedha hizo hazikufanya kazi iliyokusudiwa.

Aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Chakula katika serikali ya rais mstaafu Benjamin Mkapa, Charles Keenja, ameithibitishia gazeti hili kutolewa fedha hizo.

Alisema, "ni kweli wapo wafanyabiashara ambao walipewa fedha kutoka katika mifuko hiyo. Na hadi naondoka ofisini (mwaka 2005), nyingi ya fedha hizo zilikuwa hazirudishwa."

Hata hivyo, Keenja aliongeza kwamba "fedha za Mfuko wa Chakula huwa hazikopeshwi, bali mhitaji hutakiwa aandae mradi wa maendeleo wenye manufaa kwa jamii. Akishindwa kuendesha mradi, anatakiwa kurudisha fedha mara moja."

Mbali na Rostam, wakurugenzi wengine wa African Trade Development, ni Gulam A. Chakaar na Bahram A. Chakaar.

Makampuni mengine yaliyochotewa fedha, ni Tanganyika Farmers Association Limited (TFA) ambayo wakurugenzi wake ni Ndesario K. Shangali, Elia R.K. Mshiu, C.J Bannister, Elisamia I. Swai, Eric Jorgensen na Charles D.J. Mungai.

Mengine ni Ramwigema General Suppl ambayo inamilikiwa na G. Mwinuka na wenzake na Sales Point Company Limited, inayomilikiwa na Matunda Abdulrahman na Abdallah S. Hassan.

Makampuni mengine yaliyochotewa fedha ni VIP Engineering inayomilikiwa na James B. Rugemalira, Mathias Mutabirwa, Suleiman A. Abubakar, Gwalugano Mwamukonda na Mohamed B. Somji.

Mengine ni TANTI Co. Ltd., inayomilikiwa na Nuru A. Kihiyo na Twaha Y. Kaujanja; BCS Limited ikimilikiwa na Jackson V. Kaale, Kandaga J. Muhangwa, Edmund Mkwawa, Flavian I. Gowele, Judith M. Juma, Abdul Nuru Suleiman, Fatuma B. Mikidadi na Salome J. Mbatia.

Ipo pia Agro – Impex inayomilikiwa na Parvez Vira na Azmina Vira.

Wakurugenzi wengine ni makampuni yao kwenye mabano, ni Juma Ngalema na wenzake (Kiswele Salt Works Ltd); Bupen S. Tank na wenzake (Shivlal Tank & Co) na W.C. Marwa na wenzake (Tanzania Fertilizer Company).

Mbali na Mfuko wa Chakula, pia fedha hizo zilitolewa katika Mfuko wa Pembejeo.

Mifuko hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuiwezesha Serikali kupata uhakika wa chakula kwa wananchi wake pamoja na kusukuma mbele miradi ya maendeleo katika sekta ya afya, elimu na maji.

Mfuko wa Chakula ulikuwa ukitoa ruzuku kwa wafanyabiashara wakati Mfuko wa Pembejeo ulitoa mikopo ya pembejeo za kilimo ambayo ililazimu mkopaji kurejesha.

Taarifa kutoka Ubalozi wa Japan nchini, zimesema kwamba hatua ya serikali kutoa fedha hizo bila ya kufanyiwa kazi iliyokusudiwa, imechangia kuzorotesha madhumuni ya mifuko hiyo.

MwanaHALISI lilipowasiliana na Afisa Mtendaji Mkuu wa mifuko hiyo, Dk. Lorri Willibald, alithibitisha kuwapo kwa wafanyabiashara waliochotewa fedha hizo lakini wakashindwa kuzitumia kama ilivyotarajiwa.

Hata hivyo, Dk. Lorri alisema kwa sasa hayuko katika nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hilo kwa vile yuko nje ya ofisi.

Juhudi za kumpata Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Peter Msolla, hazikuzaa matunda kwani simu yake haikupatikana kwa muda mrefu.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula ambaye sasa ni Naibu wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Christopher Chiza, alisema ingawa walifanya jitihada kubwa kuhakikisha fedha hizo zinarudishwa, hadi anaondoka, kiasi kikubwa kilikuwa bado hakijapatikana.

Tukio hilo linaendelea kuthibitisha namna fedha za umma, zikiwemo zile zinazotolewa na washirika wa maendeleo, zinavyotafunwa na wajanja wachache kwa maslahi yao binafsi.

Aidha, taarifa hizi zinakuja wakati Watanzania wakisubiri hatma ya wakwapuaji wengine waliotafuna mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA).

Wajanja wametafuna zaidi ya Sh. 133 bilioni za fedha hizo zilizochotewa makampuni kadhaa kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Wizara ya Fedha katika kipindi cha mwaka 2005/06.

Wizi wa fedha hizo uligunduliwa na maodita, kampuni ya Ernst & Young walioelekezwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini (CAG) baada ya kubainika upotevu wa fedha katika akaunti hiyo.

Vilevile, sakata hili linaibuka sasa wakati ambapo haijajulikana hatma ya watendaji serikalini waliongiza nchi katika mkataba wa kinyonyaji wa Richmond.

Katika mkataba huo, shirika la umeme Tanesco linailipa kampuni hiyo kupitia dada yake Dowans, Sh. 152 milioni kwa siku.
Duh!Hii mutu imetafuna inji!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Fupa hilo limetushinda, tutaendelea kupiga kelele humu weeee, yeye anapeta tu hao ndo CCM na serikali yao legelege
 
Mkuu naona leo umeamua kufanya kazi ya kufukunyua 'sredi' za miaka iliyopita, hongera zako.
Mkuu,bado zina make sense kwasababu haki bado haijapatikana...Case aint closed yet, sema tunasahau mapema sana.
 
Mkuu,bado zina make sense kwasababu haki bado haijapatikana...Case aint closed yet, sema tunasahau mapema sana.

Umenena ukweli kabisa na hii ndio sababu kubwa ya Watanzania wengi kukata tamaa na hii Serikali taahira iliyopo madarakani. Ufisadi wa zaidi ya shilingi Trillioni moja lakini hakuna hata mmoja aliyewajibishwa wote bado wanapeta na mapesa yao waliokwapua toka kwa walipa kodi wa Tanzania.
 
Huyu Rostam Aziz naona wazi kwamba mnamuonea kumtupia lawama zote pekee yake.

Yeye ni mfanya biashara kama walivyo wafanya biashara wengine. Kapewa pesa ya kufanyia biashara baada ya kufuata taratibu zote kama walivyofanya wengine. Kwanini wengine hawatupiwi lawama kama yeye?, ama sababu yeye ni mwarabu?.

Maelezo yanaonesha kwamba ni makampuni mengi yamechotewa pesa hizo na kuna majina ya watu wazito mengi tu, mbona hawaandikwi hapa ila Roastam Aziz peke yake?.

Kitu cha maana ni kuwaauliza wote waliopewa pesa hizo wamezifanyia nini?, na kama hawakufanya kile walichopaswa kukifanyia basi tuwadai wazirudishe bila ya kumwoga mtu ama sheria ifuate mkondo wake, lakini si vyema kumtupia lawama mtu mmoja.

Tuache chuki binafsi.
Kwa taarifa yako kampuni zote ni Zake RA ila katumia majina tofauti kusajiri.
 
aah mmenikumbusha kweli mwanahalisi ya ukweli enzi hizo,mwanahalisi ngangari,siku hizi mwanahalisi nyoro nyoro kama cuf sio ngangari tena!!!wala haina ubavu wa kuandika story kama hizi tena!
 
Daah! Kweli sie watanzania vilaza yani mngese wa kiindi anachota pesa za maendeleo ya wananchi tunanyamaza kuna kila sababu ya kuingia street.
 
Back
Top Bottom