Rostam Aziz ahusishwa ufisadi mabilioni ya Japan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam Aziz ahusishwa ufisadi mabilioni ya Japan

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Jun 16, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,806
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  Rostam Aziz ahusishwa ufisadi mabilioni ya Japan

  Ni za Mfuko wa Chakula
  Zilizochotwa ni bilioni 200
  Toleo Na. 090
  Rostam Aziz ahusishwa ufisadi mabilioni ya Japan

  Na Waandishi Wetu
  Mwanahalisi

  MBUNGE wa Igunga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz, ni miongoni mwa wafanyabiashara kadhaa wanaotajwa kufilisi Mfuko wa Chakula (FACF) baada ya kuchotewa na serikali zaidi ya Sh. 200 bilioni.

  Taarifa za ukakika zilizothibitishwa na Serikali, zinasema Rostam alichotewa mabilioni hayo ya shilingi kupitia kampuni yake ya African Trade Development.

  Mfuko huo unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Japan.

  MwanaHALISI imeelezwa kwamba Rostam, pamoja na wafanyabiashara wenzake kadhaa wameshindwa kurejesha fedha hizo kama walivyotakiwa na serikali.

  Kampuni ya Rostam ilichotewa zaidi ya Sh. 2.012 bilioni Novemba 1999, lakini hadi mwishoni mwa mwaka jana, fedha hizo hazikufanya kazi iliyokusudiwa.

  Aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Chakula katika serikali ya rais mstaafu Benjamin Mkapa, Charles Keenja, ameithibitishia gazeti hili kutolewa fedha hizo.

  Alisema, “ni kweli wapo wafanyabiashara ambao walipewa fedha kutoka katika mifuko hiyo. Na hadi naondoka ofisini (mwaka 2005), nyingi ya fedha hizo zilikuwa hazirudishwa.”

  Hata hivyo, Keenja aliongeza kwamba “fedha za Mfuko wa Chakula huwa hazikopeshwi, bali mhitaji hutakiwa aandae mradi wa maendeleo wenye manufaa kwa jamii. Akishindwa kuendesha mradi, anatakiwa kurudisha fedha mara moja.”

  Mbali na Rostam, wakurugenzi wengine wa African Trade Development, ni Gulam A. Chakaar na Bahram A. Chakaar.

  Makampuni mengine yaliyochotewa fedha, ni Tanganyika Farmers Association Limited (TFA) ambayo wakurugenzi wake ni Ndesario K. Shangali, Elia R.K. Mshiu, C.J Bannister, Elisamia I. Swai, Eric Jorgensen na Charles D.J. Mungai.

  Mengine ni Ramwigema General Suppl ambayo inamilikiwa na G. Mwinuka na wenzake na Sales Point Company Limited, inayomilikiwa na Matunda Abdulrahman na Abdallah S. Hassan.

  Makampuni mengine yaliyochotewa fedha ni VIP Engineering inayomilikiwa na James B. Rugemalira, Mathias Mutabirwa, Suleiman A. Abubakar, Gwalugano Mwamukonda na Mohamed B. Somji.

  Mengine ni TANTI Co. Ltd., inayomilikiwa na Nuru A. Kihiyo na Twaha Y. Kaujanja; BCS Limited ikimilikiwa na Jackson V. Kaale, Kandaga J. Muhangwa, Edmund Mkwawa, Flavian I. Gowele, Judith M. Juma, Abdul Nuru Suleiman, Fatuma B. Mikidadi na Salome J. Mbatia.

  Ipo pia Agro – Impex inayomilikiwa na Parvez Vira na Azmina Vira.

  Wakurugenzi wengine ni makampuni yao kwenye mabano, ni Juma Ngalema na wenzake (Kiswele Salt Works Ltd); Bupen S. Tank na wenzake (Shivlal Tank & Co) na W.C. Marwa na wenzake (Tanzania Fertilizer Company).

  Mbali na Mfuko wa Chakula, pia fedha hizo zilitolewa katika Mfuko wa Pembejeo.

  Mifuko hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuiwezesha Serikali kupata uhakika wa chakula kwa wananchi wake pamoja na kusukuma mbele miradi ya maendeleo katika sekta ya afya, elimu na maji.

  Mfuko wa Chakula ulikuwa ukitoa ruzuku kwa wafanyabiashara wakati Mfuko wa Pembejeo ulitoa mikopo ya pembejeo za kilimo ambayo ililazimu mkopaji kurejesha.

  Taarifa kutoka Ubalozi wa Japan nchini, zimesema kwamba hatua ya serikali kutoa fedha hizo bila ya kufanyiwa kazi iliyokusudiwa, imechangia kuzorotesha madhumuni ya mifuko hiyo.

  MwanaHALISI lilipowasiliana na Afisa Mtendaji Mkuu wa mifuko hiyo, Dk. Lorri Willibald, alithibitisha kuwapo kwa wafanyabiashara waliochotewa fedha hizo lakini wakashindwa kuzitumia kama ilivyotarajiwa.

  Hata hivyo, Dk. Lorri alisema kwa sasa hayuko katika nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hilo kwa vile yuko nje ya ofisi.

  Juhudi za kumpata Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Peter Msolla, hazikuzaa matunda kwani simu yake haikupatikana kwa muda mrefu.

  Aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula ambaye sasa ni Naibu wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Christopher Chiza, alisema ingawa walifanya jitihada kubwa kuhakikisha fedha hizo zinarudishwa, hadi anaondoka, kiasi kikubwa kilikuwa bado hakijapatikana.

  Tukio hilo linaendelea kuthibitisha namna fedha za umma, zikiwemo zile zinazotolewa na washirika wa maendeleo, zinavyotafunwa na wajanja wachache kwa maslahi yao binafsi.

  Aidha, taarifa hizi zinakuja wakati Watanzania wakisubiri hatma ya wakwapuaji wengine waliotafuna mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA).

  Wajanja wametafuna zaidi ya Sh. 133 bilioni za fedha hizo zilizochotewa makampuni kadhaa kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Wizara ya Fedha katika kipindi cha mwaka 2005/06.

  Wizi wa fedha hizo uligunduliwa na maodita, kampuni ya Ernst & Young walioelekezwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini (CAG) baada ya kubainika upotevu wa fedha katika akaunti hiyo.

  Vilevile, sakata hili linaibuka sasa wakati ambapo haijajulikana hatma ya watendaji serikalini waliongiza nchi katika mkataba wa kinyonyaji wa Richmond.

  Katika mkataba huo, shirika la umeme Tanesco linailipa kampuni hiyo kupitia dada yake Dowans, Sh. 152 milioni kwa siku.
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  wache wagawane pesa ....wapo wanahasara gani? kwani njaa haiwaaathiri hata kidogo
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Rostam kaiweka serikali yooote mfukoni
   
 4. I

  Ipole JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2008
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa mtaji huo kama ni kweli huyo Rostam anastahili kuchinjwa
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2008
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hivi hakuna vichaa snipers bongo? If its true, sijui tunasali wapi siku hizi!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2008
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Na watendelea kufanya hivyo......unless tuamue kitu cha kuafanya ...Insurgent anasema ".....kutumia ULIMI umepitwa na wakati what we need is VITENDO"

  Hili jamaa mimi naona ndilo linatawala nchi behind the scene....inaonekana anacheza ile staili ya Hoover wa FBI...ana dataz za vigogo wote ndio maana Richmond.EPA...n.k.... zitazimwa
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa ana nguvu gani ya kuwashindwa watu zaid ya milio ni 35?
   
 8. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Tulishalisema hili hapa kitambo.

  Kwa mara nyingine tuko mbele ya magazeti yetu.
   
 9. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ... kawaweka mfukoni watu tuliowapa nguvu juu yetu, tabaka tawala.

  Nguvu haiko kwenye namba
   
 10. T

  Tujisenti JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2008
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waswahili wanasema siku za mwizi ni 40. Na wakristu wanasema mshahara wa dhambi ni mauti. Siku ya Rostam na wenzake inakuja.
   
 11. Typical

  Typical JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 261
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Hakuna chuo unachokijua tupeleke vijana???????
   
 12. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  You can tell from his name ROAST THEM ... the best label for fisads
   
 13. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2008
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi nina kampuni yangu. Hivi hizo pesa nitazipata vipi?
   
 14. F

  FundiUmeme New Member

  #14
  Jul 10, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inavyoonekana sasa Rostam amefika pahala pabaya! Ananuka hapa nchini na ni wazi kuwa hana amani rohoni mwake>>>Atafia jela na Maafisa Magereza yatashindania apelekwe kwao.... Hivi sheria ya Uhujumu uchumi imefutwa?
   
 15. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Rostam in the state of panic.............
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,966
  Trophy Points: 280
  Kama dola ikimlinda thats a different case na hapo ndipo kwenye possibility ya INSURGENCY!
   
 17. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,966
  Trophy Points: 280
  Talking about SNIPERS?
  Wako wengi tu...Wengi wao ndio wanawalinda.
  Umesahau USALAMA WA.....!?
   
 18. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2008
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  FISADI ni fisadi tu. Mwaka huu kama utaisha salama then CCM watatawala milele!!! Muiran ananitia kichefuchefu mimi basi tu!!!
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kila kitu kina mwisho ndugu zangu. Ukiona hata aliowahonga 7m siku chache zilizopita wanatamani kuzirudisha baada ya outcry ya wananji, basi ujue mwisho u karibu.
   
 20. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyu Rostam Aziz naona wazi kwamba mnamuonea kumtupia lawama zote pekee yake.

  Yeye ni mfanya biashara kama walivyo wafanya biashara wengine. Kapewa pesa ya kufanyia biashara baada ya kufuata taratibu zote kama walivyofanya wengine. Kwanini wengine hawatupiwi lawama kama yeye?, ama sababu yeye ni mwarabu?.

  Maelezo yanaonesha kwamba ni makampuni mengi yamechotewa pesa hizo na kuna majina ya watu wazito mengi tu, mbona hawaandikwi hapa ila Roastam Aziz peke yake?.

  Kitu cha maana ni kuwaauliza wote waliopewa pesa hizo wamezifanyia nini?, na kama hawakufanya kile walichopaswa kukifanyia basi tuwadai wazirudishe bila ya kumwoga mtu ama sheria ifuate mkondo wake, lakini si vyema kumtupia lawama mtu mmoja.

  Tuache chuki binafsi.
   
Loading...